Jumatano, 20 Novemba 2019

Wimbo Mpya wa Kuabudu 2019 | “Kristo wa Siku za Mwisho Ameleta Enzi ya Ufalme” (Swahili Gospel Song)

Wimbo Mpya wa Kuabudu 2019 | “Kristo wa Siku za Mwisho Ameleta Enzi ya Ufalme” (Swahili Gospel Song)


Yesu alipokuja katika ulimwengu wa mwanadamu,
Akatamatisha Enzi ya Sheria,
Alileta Enzi ya Neema.
Mungu mara nyingine akakuwa mwili katika siku za mwisho.
Akitamatisha Enzi ya Neema,
Alileta Enzi ya Ufalme.
Wote wanaokubali kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili
wataongozwa katika Enzi ya Ufalme na kupokea uongozi Wake.
Baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake,
Mungu alirudi mwilini kumwongoza.
Atamwongoza mwanadamu kuingia katika enzi mpya.
Ameanza kazi ya hukumu
ili kumleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi.
Wote wanaotii utawala Wake
watavuna ukweli wa juu na baraka kuu.
Ee wataishi katika mwangaza!
Na kupata njia, ukweli, na uzima!

Yesu alifanya kazi nyingi kati ya wanadamu.
Ukombozi wa wanadamu wote ndio kazi aliyomaliza pekee.
Aligeuka sadaka ya mwanadamu ya dhambi,
lakini hakumwondolea mwanadamu
tabia yake yote potovu, upotovu wote wa mwanadamu.
Kumwokoa mwanadamu kutoka kwa Shetani kulimaanisha
Yesu alilazimika kuchukua dhambi za mwanadamu,
lakini kazi kubwa zaidi ya Mungu ilihitaji
kumwondolea mwanadamu upotovu wa Shetani.
Baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake,
Mungu alirudi mwilini kumwongoza.
Atamwongoza mwanadamu kuingia katika enzi mpya.
Ameanza kazi ya hukumu
ili kumleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi.
Wote wanaotii utawala Wake
watavuna ukweli wa juu na baraka kuu.
Ee wataishi katika mwangaza!
Na kupata njia, ukweli, na uzima!

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni