Jumatano, 6 Novemba 2019

Matamshi ya Mungu | "Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (I)" Sehemu ya Nne

Mwenyezi Mungu anasema, “Kwamba Mungu anakimu ulimwengu ina maana na matumizi mapana sana. Mungu hawakimu tu watu kwa kuwapatia mahitaji yao ya kila siku ya chakula na kinywaji, Anawapatia wanadamu kila kitu wanachohitaji, ikiwa ni pamoja na kila kitu ambacho watu wanakiona na vitu ambavyo haviwezi kuonekana. Mungu anatetea, anasimamia na anatawala mazingira ya kuishi ambayo binadamu anahitaji.
 Mazingira yoyote ambayo binadamu anayataka katika msimu wowote, Mungu ameyaandaa. Angahewa au halijoto yoyote ambayo inafaa kwa ajili ya uwepo wa binadamu pia ipo chini ya udhibiti wa Mungu na hakuna kati ya kanuni hizi ambayo inatokea yenyewe tu au bila utaratibu; ni matokeo ya kanuni ya Mungu na matendo Yake. Mungu Mwenyewe ni chanzo cha kanuni zote hizi na ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote. Huu ni ukweli uliothibitishwa na usioweza kushambuliwa na haijalishi unauamini au huuamini, haijalishi unaweza kuuona au huwezi kuuona, au haijalishi unaweza kuuelewa au huwezi kuuelewa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni