Jumanne, 3 Desemba 2019

Sura ya 15

Mwanadamu ni kiumbe asiyejifahamu. Hata ingawa hawezi kujijua mwenyewe, yeye hata hivyo anajua kila mwanadamu mwingine kama kiganja cha mkono wake, kana kwamba watu wengine wote wamepitia ukaguzi wake na kupokea kibali chake kabla waseme au kufanya chochote, na hivyo ionekane kama yeye amewapima kikamilifu wengine wote mpaka katika hali yao ya kisaikolojia. Binadamu wote wako namna hii. Mwanadamu ameingia katika Enzi ya Ufalme leo hii, lakini asili yake bado haijabadilika. Yeye bado anafanya kama Ninavyofanya akiwa mbele Yangu, lakini nyuma Yangu anaanza kufanya “shughuli” zake mwenyewe za kipekee. Hata hivyo, mara hiyo inapokamilika na anarudi mbele Yangu tena, yeye huwa kama mwanadamu tofauti, akiwa na hali ya utulivu safihi, hali yake ni shwari, na mpigo wa moyo wake ni mtulivu. Je, si hili ndilo hasa hufanya mwanadamu kudharauliwa? Ni watu wangapi huvaa sura mbili tofauti kabisa, moja mbele Yangu na nyingine nyuma Yangu? Wangapi kati yao ni kama wanakondoo wachanga mbele Yangu lakini nyuma Yangu hugeuka na kuwa chui wabaya wenye milia wakali kinyama, na kisha kugeuka ndege wadogo wanaorukarukakwa furaha milimani? Ni wangapi huonyesha lengo na uamuzi mbele Yangu? Ni wangapi huja mbele Zangu, kutafuta maneno Yangu kwa kiu na hamu lakini, nyuma Yangu, kukerwa nayo na kuyaacha, kana kwamba maneno Yangu ni mzigo unaosumbua? Mara nyingi, Nikiona jamii ya binadamu ikipotoshwa na adui Yangu, Mimi Nimeacha kuweka matumaini Yangu katika mwanadamu. Mara nyingi, Nikiona mwanadamu akija mbele Zangu kwa machozi akiomba msamaha, lakini kwa sababu ya kutojiheshimu kwake, utundu wake usiorekebika, Nimefunga macho Yangu kwa vitendo vyake kwa hasira, hata wakati moyo wake ni wa kweli na nia yake ni ya dhati. Mara nyingi, Naona mwanadamu akiwa na uwezo wa kuwa na imani ya kushirikiana na Mimi, na jinsi, mbele Yangu, anaonekana kuwa amekaa katika kumbatio Langu, akionja joto la kumbatio Langu. Mara nyingi, kwa kuona upole, uchangamfu, na uzuri wa watu Wangu Niliowachagua, katika Moyo wangu Mimi daima Nimekuwa na furaha kwa sababu ya mambo haya. Binadamu hawajui jinsi ya kufurahia baraka Nilizowaamulia kabla katika mikono Yangu, kwa sababu wao hawajui ni nini hasa maana ya baraka au mateso. Kwa sababu hii, wanadamu wako mbali na kweli katika jitihada zao za kunitafuta. Kama hakungekuwa na kesho, nani kati yenu, mlio mbele Yangu, angekuwa mweupe kama theluji inayoendeshwa, bila doa kama jiwe safi la thamani? Hakika upendo wako Kwangu si kitu ambacho kinaweza kubadilishwa kwa mlo wenye ladha, au suti yenye ufahari, au ofisi ya juu na mishahara mikubwa? Au inaweza kubadilishwa na upendo ambao wengine wako nao kwako? Hakika, kupitia majaribu hakutawafukuza wanadamu waache upendo wao Kwangu? Hakika, mateso na dhiki hayatasababisha mwanadamu alalamike dhidi ya kile Nimepanga? Hakuna mwanadamu aliyewahi kweli kufahamu upanga ulio katika kinywa Changu: Yeye anajua maana yake ya juu bila kufahamu undani wake. Kama binadamu wangeweza kufahamu kwa kweli ukali wa upanga wangu, wangetoroka kwa uoga kama vile panya wanavyokimbilia mashimo yao. Kwa sababu ya kutokuwa kwao na hisia, wanadamu hawaelewi kitu chochote cha maana halisi ya maneno Yangu, na hivyo wao hawana kidokezo kuhusu jinsi maneno Yangu ni yenye kuogofya, au kiasi gani asili yao imefichuliwa, na ni kiasi gani cha upotovu wao umepokea hukumu, ndani ya maneno hayo. Kwa sababu hii, kulingana na mawazo yao yasiyo kamili kuhusu maneno Yangu, watu wengi wamechukua msimamo vuguvugu na usio wa kuwajibika.
Ndani ya ufalme, matamshi hayatoki tu kwenye kinywa Changu, lakini miguu Yangu inakanyaga kila mahali juu ya ardhi kwa utaratibu. Kwa njia hii, Mimi Nimepata ushindi juu ya maeneo yote yasiyo safi na yenye uchafu sana, ili kwamba isiwe tu ni mbinguni inabadilika, lakini pia dunia iwe katika mchakato wa mabadiliko, ili ifanywe mpya muda mfupi baadaye. Ndani ya ulimwengu, kila kitu kinakuwa kipya katika mng’ao wa utukufu Wangu, kikiwasilisha kipengele chenye upendo kinachochangamsha akili na kuinua roho, kana kwamba sasa kiko katika mbingu zaidi ya mbingu, kama inavyoonekana katika mawazo ya binadamu, ambayo hayajachafuliwa na Shetani, ambayo hayajapata mashambulizi ya adui kutoka nje. Juu ulimwenguni, nyota lukuki zinachukua maeneo yao mateule kwa amri Yangu, zikitoa mwanga wao kupitia sehemu za nyota katika wakati wa giza. Hakuna kiumbe hata mmoja anathubutu kuwa na mawazo ya ukaidi, na hivyo, kwa mujibu wa kiini cha amri za utawala Wangu, ulimwengu mzima umedhibitiwa vizuri na kwa utaratibu mzuri: Hakuna usumbufu ambao umewahi kutokea, wala umoja wa ulimwengu haujapata kuvunjwa. Mimi Naruka juu ya nyota, na wakati jua linachomoza mionzi yake, Ninalizuia joto la miale hiyo, Nikituma mabonge ya chembe za theluji kama manyoya ya bata yakianguka chini kutoka katika mikono Yangu. Lakini Nikibadili mawazo Yangu, theluji yote inayeyuka na kuwa mto. Kwa muda mfupi, majira ya kuchipia yameibuka kila mahali chini ya anga, na zamaradi ya kijani inageuza mazingira yote juu ya nchi. Mimi Naenda kuzunguka juu ya anga, na mara moja, nchi nzima imefunikwa katika giza jeusi tititi kwa sababu ya umbo Langu: Bila ya onyo, “usiku” umewadia, na duniani kote ni giza mpaka hakuna anayeweza kuona mkono ulio mbele ya uso wake. Na kutoweka kwa mwanga, mwanadamu anachukua fursa ya kuanza uharibifu wa wenyewe kwa wenyewe, kunyakua na kuporana wenyewe. Mataifa ya dunia, kuingia katika hali ya mafarakano ya vurugu, yanaingia katika hali ya ghasia yenye matope, mpaka nafasi ambayo hawawezi kupata ukombozi. Wanadamu wanapambana katika machungu makubwa ya maumivu, kulia kwa uchungu katikati ya mateso, kuanza kuomboleza kwa hali ya kuhurumika katika mateso yao, wakitamani mwanga urejee kati yao kwa mara nyingine tena na hivyo kumaliza siku za giza na kurejesha uzima uliokuwepo. Lakini Mimi kwa muda mrefu Nimemwacha mwanadamu kwa kupapasa mkono wa vazi Langu, kamwe tena Nisimwonee huruma kwa sababu ya makosa ya dunia: Kwa muda mrefu Mimi nimechukizwa na kuwakataa watu wa dunia nzima, kufumba macho Yangu kwa hali duniani, kugeuza uso Wangu mbali na kila hatua ya mwanadamu, kila ishara zake, na kuacha kufurahiakutoridhishwa na uana wake na kutokua na hatia kwake. Mimi Nimeanza mpango mwingine wa kufanya dunia upya, ili dunia hii mpya iweze kupata kuzaliwa upya mapema na isizame tena. Miongoni mwa binadamu, mataifa mangapi ya kigeni yanasubiri Niyaweke kwenye haki, makosa mangapi ili Nije mwenyewe kuyazuia yasitendeke, ni vumbi kiasi gani ndio Mimi nije kufagia, ni siri ngapi za kufunuliwa Nami: binadamu wote wananingoja, na wanatamani kuja Kwangu.
Duniani, Mimi ni Mungu wa vitendo Mwenyewe katika mioyo ya watu; mbinguni, Mimi Ndiye Mkuu wa viumbe vyote. Nimepanda milima na kuvuka mito, na Nimeingia na kutoka katikati ya binadamu. Nani anathubutu kwa uwazi kumpinga Mungu wa vitendo Mwenyewe? Nani anathubutu kutoka kati ya ukuu wa Mwenyezi? Nani anayethubutu kudai kuwa Mimi, bila shaka, Niko mbinguni? Tena, nani ambaye anathubutu kudai kuwa Mimi, bila kukosea, Niko duniani? Hakuna binadamu kati ya wote anayeweza kujieleza kwa ufasaha na undani mahali ambapo Mimi Naishi. Inawezekana kuwa kwamba, wakati Mimi niko mbinguni, Mimi ni Mungu Mwenyewe asiye wa kawaida? Inawezekana kuwa kwamba, wakati Mimi niko hapa duniani, Ninakuwa Mungu wa vitendo Mwenyewe? Kwamba Mimi ni Mtawala wa viumbe vyote, au kwamba Mimi ninapitia mateso ya ulimwengu wa mwanadamu—hakika hivi haviwezi kuamua iwapo Mimi ni Mungu wa vitendo Mwenyewe? Kama mwanadamu anadhani hivyo[a], si yeye ni mpumbavu asiye na matumaini ya kubadilika? Mimi niko mbinguni; Mimi pia Niko duniani; Niko miongoni mwa mambo idadi kubwa ya viumbe, na pia katikati ya idadi kubwa ya watu. Mwanadamu anaweza kunigusa kila siku; zaidi ya hayo, anaweza kuniona kila siku. Kulingana na binadamu, Mimi huonekana kuwa wakati mwingine Nimejificha na wakati mwingine Naonekana; Mimi Naonekana kuwa na maisha halisi, na hata hivyo Naonekana pia kutokuwa na nafsi. Ndani Mwangu kuna siri kubwa sana zisizoweza kufahamika na binadamu. Ni kana kwamba watu wote wananitazama kwa njia ya hadubini ili kugundua siri hata zaidi ndani Mwangu, wakiwa na matumaini ya kuondoa hisia za wasiwasi katika nyoyo zao. Lakini hata watumie darubini ya nguvu kivipi, binadamu watawezaje kuziweka wazi siri zilizo ndani Mwangu?
Wakati watu Wangu, kupitia kwa kazi Yangu, wanatukuzwa pamoja na Mimi, wakati huo maficho ya joka kubwa jekundu yatafichuliwa, matope yote na uchafu kufagiliwa mbali, na maji machafu, yaliyokusanyika kwa miaka mingi, kukaushwa na moto Wangu unaochoma, yasikuwepo tena. Hapo joka kubwa jekundu litaangamia katika ziwa la moto wa jehanamu. Je, kweli unayo nia ya kusalia chini ya ulinzi Wangu ili usinyakuliwe na joka? Je, kweli unachukia mbinu yake ya udanganyifu ? Nani ambaye anaweza kuwa shahidi Wangu wa dhati? Kwa ajili ya jina Langu, kwa ajili ya Roho Wangu, kwa ajili ya mpango Wangu mzima wa usimamizi—nani ambaye anaweza kutoa nguvu zake zote katika mwili wake? Leo, wakati ufalme uko katika ulimwengu wa watu, ndio wakati ambao Nimekuja binafsi katika ulimwengu wa wanadamu. Kama haingekuwa hivyo, je, yupo ambaye angeweza, kwa ujasiri, kwenda katika uwanja wa vita kwa niaba Yangu? Ndipo ufalme uweze kuchukua mkondo, ili moyo Wangu uweze kuridhika, na tena, ili siku Yangu iweze kuja, ili wakati uweze kuja ambapo mambo mengiya uumbaji yamezaliwa upya na kukua kwa wingi, ili kwamba mwanadamu aweze kuokolewa kutoka kwenye bahari ya mateso, ili siku inayofuata iweze kuja, na ili iwe ni ya ajabu, yenye kutoa maua na kushamiri, na tena, ili starehe ya siku za usoni itimizwe, binadamu wote wanajitahidi kwa nguvu zao zote, bila kuwacha chochote katika kujitoa sadaka wenyewe kwa ajili Yangu. Je, hii si ishara kwamba ushindi tayari ni Wangu, na alama ya kukamilika kwa mpango Wangu?
Wanadamu wanavyozidi kukaa katika siku za mwisho, ndivyo watakavyozidi kuhisi utupu wa dunia na ndivyo watakavyopungukiwa na ujasiri wa jinsi ya kuishi. Kwa sababu hii, watu wasiohesabika wamekufa katika hali ya kuvunja matumaini, wengine wengi wamevunjwa matumaini katika jitihada zao, na wengine wengi kuteseka wenyewe kuwa kunyanyaswa katika mikono ya shetani. Mimi Nimewaokoa watu wengi, Nimewapa wengi msaada, na mara nyingi, wakati binadamu wamepoteza mwanga, Mimi Nimewaongoza kurudi katika nafasi ya mwanga, ili wapate kunijua wakiwa kwenye mwanga, na kunifurahia katika furaha. Kwa sababu ya ujio wa mwanga Wangu, kuabudu hukuzwa katika mioyo ya watu wanaokaa katika ufalme Wangu, kwa maana Mimi ni Mungu wa kupendwa na binadamu, Mungu ambaye binadamu unajishika katika hali ya upendo, na mwanadamu anajazwa na maono ya kudumu ya umbo Langu. Lakini, hatimaye, hakuna yeyote ambaye anaelewa kama hii ni kazi ya Roho, au ni kutokana na mwili. Hili jambo moja pekee linatosha kumfanya mwanadamu kupitia mwendo wa maisha kwa undani. Mwanadamu hajawahi kunichukia katika undani wa moyo wake kabisa; badala yake, yeye huambatana na Mimi katika kina cha roho yake. Hekima yangu inaibua upendezewaji wake, maajabu Ninayotenda ni ukuu machoni pake, maneno Yangu yanastaajabisha akili yake, na bado yeye ana mapenzi tele kwayo. Ukweli Wangu humfanya mwanadamu asijue la kusema, aduwae na kushtuka, na bado yeye yuko tayari kukubali hayo yote. Je, hiki si kipimo cha mwanadamu jinsi alivyo hasa?
Machi 13, 1992

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni