![]() |
| Tabia ya Mungu ni Haki na, Hata Zaidi, Upendo |
Tabia ya Mungu ni Haki na, Hata Zaidi, Upendo
Fang Xin, Beijing
Agosti 15, mwaka wa 2012
Tangu mwaka wa 2007, nilipoikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, ingawa nimeonekana juu juu kuwa na kazi nyingi sana kutekeleza majukumu yangu, sijaupa moyo wangu kwa Mungu, na mara nyingi nimehisi kufungwa kiasi cha msongo wa pumzi na masuala madogo ya familia. Kila wakati ninapowaza kuhusu ukweli kwamba binti yangu tayari ana umri wa miaka thelathini, na angali bado hajapata mwenzi wa kufaa, mimi hulalamika kwa Mungu; mwanangu wa kiume hujali tu kuhusu kujifurahisha, na licha ya kutokuwa na mapato yoyote, yeye hutumia pesa kwa ubadhirifu, kwa hiyo mimi hulalamika; na mme wangu mzee huenda kazini, lakini msimamizi wake huwa hamlipi–na mimi hulalamika kuhusu hili pia .... Mimi hulalamika kwa pande zote, na mara nyingi humwelewa Mungu visivyo.
