Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mazoezi-ya-kibinadamu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mazoezi-ya-kibinadamu. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 16 Machi 2018

Umeme wa Mashariki | Kazi na Kuingia (10)

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, kumjua Mungu,
Kazi na Kuingia (10)

Kazi na Kuingia (10)


Mwenyezi Mungu alisema, Kwa wanadamu kuendelea mbele kiasi hiki ni hali isiyo na kigezo. Kazi ya Mungu na kuingia kwa mwanadamu vinaendelea bega kwa bega, na hivyo kazi ya Mungu, pia, ni tukio kubwa lisilo na kifani. Kuingia kwa mwanadamu hadi sasa ni ajabu ambayo kamwe haijawahi kufikiriwa na mwanadamu. Kazi ya Mungu imefikia upeo wake—na, kufuatia, "kuingia" kwa mwanadamu[1] pia kumefikia kilele chake. Mungu amejishusha kwa kadiri Anavyoweza, na kamwe Hajawahi kuwalalamikia wanadamu au vitu vyote katika ulimwengu.