1. Utofautishaji Kati ya Kazi ya Mungu na Ile ya Mwanadamu
Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya Mungu Mwenyewe inahusisha kazi ya wanadamu wote, na pia inawakilisha kazi ya enzi nzima. Hii ni kusema kwamba, kazi ya Mungu mwenyewe inawakilisha harakati na mwelekeo wa kazi yote ya Roho Mtakatifu, ilhali kazi ya mitume inafuata kazi ya Mungu na wala haiongozi enzi, na wala haiwakilishi mwelekeo wa kufanya kazi wa Roho Mtakatifu katika enzi nzima.