Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kijito-Kidogo. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kijito-Kidogo. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 16 Februari 2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII | (II) Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote | Hadithi ya 2. Mlima Mkubwa, Kijito Kidogo, Upepo Mkali, na Wimbi Kubwa

Hadithi ya 2. Mlima Mkubwa, Kijito Kidogo, Upepo Mkali, na Wimbi Kubwa

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mungu,

Mlima Mkubwa, Kijito Kidogo, Upepo Mkali, na Wimbi Kubwa


Mwenyezi Mungu alisema, Kulikuwa na kijito kidogo kilichotiririka kwa kuzungukazunguka, hatimaye kikawasili chini ya mlima mkubwa. Mlima ulikuwa unazuia njia ya kijito hiki, hivyo kijito kikauomba mlima kwa sauti yake dhaifu na ndogo, “Tafadhali naomba kupita, umesimama kwenye njia yangu na umenizibia njia yangu kuendelea mbele.” Basi mlima ukauliza, “Unakwenda wapi?” Swali ambalo kijito kililijibu, “Ninatafuta makazi yangu.” Mlima ukasema, “Sawa, endelea na tiririkia juu yangu!”