Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kipindi-cha-hukumu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kipindi-cha-hukumu. Onyesha machapisho yote

Jumapili, 11 Machi 2018

Umeme wa Mashariki | Tamko la Ishirini na Nane

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, hukumu,
Tamko la Ishirini na Nane

Umeme wa Mashariki | Tamko la Ishirini na Nane

Mwenyezi Mungu alisema, Nilipokuja kutoka Zayuni, vitu vyote vilikuwa vimenisubiri, na Niliporudi Zayuni, Nilisalimiwa na wanadamu wote. Nilipokuja na kwenda, hatua Zangu hazikuwahi zuiliwa na vitu vilivyokuwa na uadui Kwangu, na kwa hivyo kazi Yangu iliendelea kwa utaratibu. Leo, Ninapokuja miongoni mwa viumbe vyote, vitu vyote vinanisalimu kwa kimya, kwa uoga mkuu kuwa Nitaondoka tena na Niondoe usaidizi kwao. Vitu vyote vinafuata uongozi Wangu, na vyote vinaangalia upande ulioashiriwa na mkono Wangu. Maneno ya kinywa Changu yamefanya kamili viumbe vingi na kuwaadibu wana wengi wa uasi Kwa hivyo, wanadamu wote wanaangalia maneno Yangu kwa makini, na kusikiza kwa karibu maneno ya kinywa Changu, na wanaogopa sana kupitwa na fursa hii nzuri.