![]() |
| Umeme wa Mashariki | Unajua Nini Kuhusu Imani? |
Umeme wa Mashariki | Unajua Nini Kuhusu Imani?
Mwenyezi Mungu alisema, Ndani ya binadamu, kunalo neno lisilokuwa la uhakika, ilhali binadamu hajui imani inajumuisha nini, na vilevile hajui ni kwa nini anayo imani. Binadamu huelewa kidogo sana, na binadamumwenyewe amepungukiwa sana; yeye anakuwa tu na imani ndani Yangu bila kujali na bila kujua. Ingawa hajui imani ni nini wala ni kwa nini anayo imani ndani Yangu, anaendelea kufanya hivyo kwa shauku mno. Kile Ninachomwomba binadamu, si tu yeye kuniita Mimi kwa shauku kwa njia hii au kuniamini Mimi kwa mtindo huu wa kukosa mwelekeo. Kwani kazi Ninayoifanya ni yake binadamu kunijia Mimi na kunijia Mimi, wala si kwa binadamu kuvutiwa na kuniangalia Mimi kwa njia mpya kwa sababu ya kazi Yangu. Awali Nilijionyesha katika ishara na maajabu mengi na kufanya miujiza mingi. Waisraeli wakati huo waliniangalia Mimi kwa tamanio kuu na walistahi pakubwa uwezo Wangu wa kipekee wa kuponya wagonjwa na kupunga mapepo. Wakati huo, Wayahudi walifikiri nguvu Zangu za uponyaji zilikuwa za kistadi na zisizo za kawaida. Kwa matendo Yangu mengi kama hayo, wote walinichukulia Mimi kwa heshima; waliweza kuhisi tamanio kuu katika nguvu Zangu zote. Kwa hiyo yeyote aliyeniona Mimi nikifanya miujiza alinifuatilia Mimi kwa karibu kiasi kwamba maelfu ya watu walinizunguka ili kunitazama nikiwaponya wagonjwa.
