![]() |
| Umeme wa Mashariki | Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu |
Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu
Mwenyezi Mungu alisema,Leo, tutawasiliana hasa jinsi watu wanavyostahili kumhudumia Mungu katika imani yao Mungu, masharti yanayopaswa kutimizwa na kinachopaswa kufahamika na watu wanaomhudumia Mungu, na mikengeuko ipi iliyoko katika huduma yako. Unapaswa kufahamu haya yote. Masuala haya yanagusia jinsi unavyomwamini Mungu, jinsi unavyotembea katika njia ya kuongozwa na Roho Mtakatifu, na jinsi mambo yako yote yanavyopangwa na Mungu, na yatakuwezesha kujua kila hatua ya kazi ya Mungu ndani yako.
