Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Matamshi-ya-Mwenyezi-Mungu-(Njia-ya-Kumjua-Mungu). Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Matamshi-ya-Mwenyezi-Mungu-(Njia-ya-Kumjua-Mungu). Onyesha machapisho yote

Jumamosi, 13 Julai 2019

Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake Sehemu ya Tano


Majaliwa ya Binadamu Yanaamuliwa na Mwelekeo Wake Kwa Mungu
Mungu ni Mungu aliye hai, na kama vile tu watu wanavyotenda tofauti katika hali tofauti, ndivyo mwelekeo wa Mungu ulivyo katika utendakazi huu na unavyotofautiana kwa sababu Yeye si kikaragosi, wala Yeye si hewa tupu. Kupata kuujua mwelekeo wa Mungu ni jambo lenye thamani kwa wanadamu. Watu wanafaa kujifunza vipi, kwa kuujua mwelekeo wa Mungu, wanaweza kuijua tabia ya Mungu na kuuelewa moyo Wake kidogo kidogo. Unapouelewa moyo wa Mungu kidogo kidogo hutahisi kwamba kumcha Mungu na kujiepusha na maovu ni jambo gumu la kutimiza.

Ijumaa, 12 Julai 2019

Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake Sehemu ya Nne


Elewa Mwelekeo wa Mungu na Utupilie Mbali Dhana zote Potovu Kumhusu Mungu
Mungu huyu ambaye kwa sasa mnasadiki, mmewahi kufikiria kuhusu Yeye ni Mungu wa aina gani? Anapomwona mtu mwovu akifanya mambo maovu, je Anayachukia? (Anayachukia.) Anapoona makosa ya mtu asiyejua, mwelekeo Wake ni upi? (Huzuni.) Anapowaona watu wakiiba sadaka Yake, mwelekeo Wake ni upi? (Anawachukia.) Haya yote yako wazi, sivyo? Anapoona mtu akiwa mzembe katika kusadiki kwake Mungu, na mtu huyo akikosa kufuatilia ukweli kwa namna yoyote, mwelekeo wa Mungu ni upi? Bado hamjaelewa jambo hili, sivyo?

Alhamisi, 11 Julai 2019

Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake Sehemu ya Tatu


Namna Ambavyo Mungu Huanzisha Matokeo Ya Binadamu na Kiwango Ambacho Hutumia Kuasisi Matokeo ya Binadamu
Kabla ya kuwa na mitazamo au hitimisho zako binafsi, unafaa kwanza kuelewa mwelekeo wa Mungu kwako, kile ambacho Mungu anafikiria, na kuamua kama kufikiria kwako ni sahihi au la. Mungu hajawahi kutumia vipimo vya muda katika kuasisi matokeo ya mtu, na Hajawahi kutumia kiwango cha mateso yaliyovumiliwa na mtu katika kuasisi matokeo yake.

Jumatano, 10 Julai 2019

Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake Sehemu ya Kwanza


Kwanza, hebu tuuimbe wimbo wa kumsifu Mungu: Wimbo wa Ufalme (I) Ufalme Umeshuka katika Ulimwengu.
Kiambata: Watu wanamshangilia Mungu, watu wanamsifu Mungu; vinywa vyote vinamwita Mungu mmoja wa kweli. Mfalme unashuka ulimwenguni.
I. Watu wanamshangilia Mungu, watu wanamsifu Mungu; vinywa vyote vinamwita Mungu mmoja wa kweli, watu wote wanainua macho yao kuyatazama matendo ya Mungu. Ufalme unashuka ulimwenguni, nafsi ya Mungu yu tajiri na mwenye ukarimu, tajiri na mwenye ukarimu. Ni nani ambaye hangeshangilia kwa ajili ya haya? (Ni nani ambaye hangeshangilia kwa ajili ya haya?) (Ni nani ambaye hangecheza kwa furaha kwa ajili ya haya?) Oo, Zayuni! (Oo, Zayuni!) Oo, Zayuni! (Oo, Zayuni!) Inua bango lako la shangwe ili kusherehekea Mungu! Imba wimbo wako wa shangwe wa ushindi na kueneza jina takatifu la Mungu!

Jumanne, 9 Julai 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote IV Sehemu ya Nne


Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV) Sehemu ya Nne
Mahitaji ya Mungu kwa Wanadamu
1. Utambulisho na Hadhi ya Mungu Mwenyewe
Tumefikia mwisho wa mada ya "Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote," vilevile na ile ya "Mungu ni wa kipekee Mungu Mwenyewe." Baada ya kufanya hivyo, tunahitaji kufanya muhtasari. Muhtasari wa aina gani? Unaomhusu Mungu Mwenyewe. Kwa kuwa ni kumhusu Mungu Mwenyewe, basi lazima ugusie kila kipengele cha Mungu, vilevile aina ya imani ya watu kwa Mungu. Na kwa hiyo, kwanza lazima Niwaulize: Baada ya kusikia mahubiri, Mungu ni nani katika jicho la mawazo yako? (Muumbaji).

Jumatatu, 8 Julai 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote IV Sehemu ya Tatu


Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV) Sehemu ya Tatu
Jinsi Mungu Anavyotawala na Kuongoza Ulimwengu wa Kiroho
3. Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Watu Wanaomfuata Mungu
Baada ya hayo, hebu tuzungumzie mzunguko wa uhai na mauti wa wale wanaomfuata Mungu. Hili linawahusu, hivyo kuweni makini. Kwanza, fikiria kuhusu ni makundi gani ambamo watu wanaomfuata Mungu wanaweza kugawika. (Wateule wa Mungu na watendaji huduma.) Kuna mawili: wateule wa Mungu na watendaji huduma. Kwanza tutazungumza kuhusu wateule wa Mungu, ambao ni wachache.

Jumamosi, 6 Julai 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote IV Sehemu ya Pili


Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV) Sehemu ya Pili
Jinsi Mungu Anavyotawala na Kuongoza Ulimwengu wa Kiroho
1. Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Wasioamini
Kwa roho yoyote, kupata kwake mwili mpya na nafasi anayochukua—nafasi yake ni ipi katika haya maisha—atazaliwa katika familia gani, na maisha yake yatakuwaje vinahusiana kwa karibu na maisha yake ya zamani. Kila aina ya watu huja katika dunia ya wanadamu, na nafasi zao ni tofauti, kama zilivyo kazi wazifanyazo.

Ijumaa, 5 Julai 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote IV Sehemu ya Kwanza


Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV) Sehemu ya Kwanza
Leo, tunafanya ushirika juu ya mada maalum. Kwa kila mmoja wenu, kuna vitu viwili vikuu tu ambavyo mnapaswa kujua, kuvipitia na kuvielewa—na vitu hivi viwili ni vipi? Cha kwanza ni kuingia binafsi kwa watu katika maisha, na cha pili kinahusu kumjua Mungu. Leo Nawapa uchaguzi: Chagua kimoja. Mngependa kusikia kuhusu mada inayouhusu uzoefu wa maisha ya kibinafsi ya watu, au mngependa kusikia inayohusu kumjua Mungu Mwenyewe? Na kwa nini Ninawapa uchaguzi huu? Kwa sababu leo Ninafikiria kufanya ushirika nanyi juu ya mambo mapya kuhusu kumjua Mungu.

Alhamisi, 4 Julai 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote III Sehemu ya Tatu


Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III) Sehemu ya Tatu

Mungu anaweka Uwiano Kati ya Vitu Vyote ili Kumpatia Binadamu Mazingira Imara kwa ajili ya Kuendelea Kuishi
Mungu anadhihirisha matendo Yake miongoni mwa vitu vyote na miongoni mwa vitu vyote Anavyovitawala na Anashikilia sheria za vitu vyote. Tumemaliza kusema juu ya jinsi ambavyo Mungu anatawala sheria za vitu vyote vilevile jinsi ambavyo Anawakimu na kuwalea binadamu wote ndani ya sheria hizo. Hiki ni kipengele kimoja. Kinachofuata, tutazungumza juu ya kipengele kingine, ambacho ni njia moja ambayo Mungu ana udhibiti wa kila kitu.

Jumatano, 3 Julai 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote III Sehemu ya Pili


Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III) Sehemu ya Pili
Ikiwa viumbe vyote vingepoteza sheria zao, visingeishi tena; ikiwa sheria za viumbe vyote zingekuwa zimepotea, basi viumbe hai miongoni mwa viumbe vyote visingeweza kuendelea. Binadamu pia wangepoteza mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo wanayategemea kwa ajili ya kuendelea kuishi. Ikiwa binadamu wamepoteza hiyo yote, wasingeweza kuendelea kuishi na kuongezeka kizazi baada ya kizazi. Sababu ya binadamu kuendelea kuishi mpaka sasa ni kwa sababu Mungu amewapatia binadamu viumbe vyote kuwalea, kuwalea binadamu kwa namna tofauti.

Jumanne, 2 Julai 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote III Sehemu ya Kwanza


Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote III Sehemu ya Kwanza

Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III) Sehemu ya Kwanza
Kwa kipindi hiki chote, tumezungumza juu ya mambo mengi yanayohusiana na kumjua Mungu na hivi karibuni tulizungumza kuhusu kitu fulani muhimu sana juu ya hii. Ni mada gani? (Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote.) Inaonekana yale mambo na mada niliyoyazungumzia yaliwachia kila mtu wazo dhahiri. Wakati uliopita tulizungumza juu ya vipengele vichache vya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliyatengeneza kwa ajili ya binadamu, vilevile Mungu kuandaa kila aina ya riziki ya lazima kwa ajili ya watu katika maisha yao.

Jumatatu, 1 Julai 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa”



Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa”


Mwenyezi Mungu anasema, “Wale watakaokamilishwa na Mungu ni wale watakaopokea baraka za Mungu na urithi Wake. Yaani, wanasikia na kuelewa kile Mungu Alicho nacho na Alicho, ili kiwe kile ambacho walicho nacho ndani yao; wanayo maneno yote ya Mungu ndani yao; haijalishi ni vipi nafsi ya Mungu ilivyo, mnaweza kusikia na kuelewa kila kitu Anachokuambia vile kilivyo, na hivyo kuishi kwa kudhihirisha ukweli. Huyu ndiye aina ya binadamu aliyekamilishwa na Mungu na aliyepatwa na Mungu.”




Jumapili, 30 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote II Sehemu ya Nne


Chakula na Kinywaji cha Kila Siku Ambavyo Mungu Anawatayarishia Wanadamu
Kuna chochote ambacho Mungu hufanya, bila kujali iwapo kitu hicho ni kikubwa au kidogo, kisicho na thamani au maana? Kila kitu Afanyacho kina thamani na maana. Tujadili hili kutoka kwa swali ambalo watu mara nyingi hulizungumzia. Watu wengi huuliza: Ni kipi kilitangulia, kuku au yai? (Kuku.) Je, utajibuje hili? Kuku alitangulia, hilo ni hakika! Kwa nini kuku alitangulia? Kwa nini yai halingetangulia? Je, kuku haanguliwi kutoka kwa yai? Mayai huangua kuku, kuku huatamiza mayai. Baada ya kuatamiza mayai kwa siku 21, kuku huangua. Kisha kuku huyo hutaga mayai, na kuku huanguliwa tena kutoka kwa mayai.

Jumamosi, 29 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote II Sehemu ya Tatu


Neno la Mwenyezi Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote II Sehemu ya Tatu

Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II) Sehemu ya Tatu
Chakula na Kinywaji cha Kila Siku Ambavyo Mungu Anawatayarishia Wanadamu
Tulikuwa tumezungumza sasa hivi kuhusu sehemu ya mazingira ya jumla, yaani, hali zilizo muhimu kwa kuendelea kuishi kwa wanadamu ambazo Mungu aliwatayarishia wanadamu tangu Alipoumba ulimwengu. Tumezungumza sasa hivi kuhusu vitu vitano, na vitu hivi vitano ndivyo mazingira ya jumla. Tunachoenda kuzungumzia baada ya hapo kinahusiana kwa karibu na kila maisha ya wanadamu katika mwili. Ni hali muhimu inayolingana zaidi na inayokubaliana zaidi na maisha ya mtu katika mwili. Kitu hiki ni chakula.

Ijumaa, 28 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote II Sehemu ya Pili


Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II) Sehemu ya Pili

Mazingira ya Kuishi ya Msingi Ambayo Mungu Anawaumbia Wanadamu
3. Sauti
Kitu cha tatu ni nini? Ni kitu ambacho mazingira ya kuishi ya kawaida ya wanadamu yanatakiwa kuwa nacho. Ni kitu ambacho Mungu alishughulikia alipoumba vitu vyote. Hiki ni kitu muhimu sana kwa Mungu na pia kwa kila mtu. Kama Mungu hakushughulikia suala hilo, ingekuwa kizuizi kikubwa kwa kuendelea kuishi kwa wanadamu. Hiyo ni kusema kwamba ingekuwa na athari yenye maana sana kwa mwili na maisha ya mwanadamu, kiasi kwamba wanadamu hawangeweza kuendelea kuishi katika mazingira kama hayo.

Alhamisi, 27 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II) Sehemu ya Kwanza


Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II) Sehemu ya Kwanza

Tuendelee na mada ya mawasiliano ya wakati uliopita. Je, mnaweza kukumbuka ni mada gani tuliwasiliana wakati uliopita? (Mungu Ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote.) Je, “Mungu Ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote” ni mada mnayohisi ikiwa mbali sana nanyi? Je, una ufahamu wowote wa juujuu kuhusu jambo hilo? Mtu fulani anaweza kuniambia wazo kuu la mada hii tuliyowasiliana wakati uliopita? (Kupitia kwa uumbaji wa Mungu wa vitu vyote, ninaona kwamba Mungu hulea vitu vyote na hulea wanadamu. Katika siku zilizopita, kila mara nilifikiria kwamba Mungu anapompa mwanadamu, Anawapa tu watu Wake waliochaguliwa neno Lake, lakini kamwe sikuona, kupitia kwa sheria za vitu vyote, kwamba Mungu anawalea wanadamu.

Jumatano, 26 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Sehemu ya Nne Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu VyoteI



Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote(I)
Kusudi la mjadala wetu wa haya mambo ni nini? Je, ni ili kwamba watu waweze kutafiti kanuni zilizopo kwenye uumbaji wa Mungu wa ulimwengu? Je, ni ili kwamba watu wavutiwe na falaki na jiografia? (Hapana.) Sasa ni nini? Ni ili kwamba watu wataelewa matendo ya Mungu. Katika matendo ya Mungu, watu wanaweza kukubali na kuthibitisha kwamba Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote. Kama unaweza kuielewa hoja hii, basi utaweza kuthibitisha kweli nafasi ya moyoni mwako na utaweza kuthibitisha kwamba Mungu ni Mungu Mwenyewe wa kipekee, Muumbaji wa mbingu na nchi na vitu vyote.

Jumatatu, 24 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Sehemu ya Tatu Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu VyoteI


Kwa mara nyingine tena Nitatumia njia ya kusimulia hadithi, ambayo ninyi nyote mnaweza kusikiliza mkiwa kimya na kutafakari juu ya kile Ninachokizungumzia. Baada ya kumaliza kusimulia hadithi, nitawauliza maswali kuona mmeelewa kiasi gani. Wahusika wakuu katika hadithi ni mlima mkubwa, kijito kidogo, upepo mkali, na wimbi kubwa.

Hadithi ya 2. Mlima Mkubwa, Kijito Kidogo, Upepo Mkali, na Wimbi Kubwa
Kulikuwa na kijito kidogo kilichotiririka kwa kuzungukazunguka, hatimaye kikawasili chini ya mlima mkubwa.

Jumapili, 23 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Sehemu ya Pili Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu VyoteI


Leo Nitashiriki nawe mada mpya. Mada itakuwa ni nini? Kichwa cha mada kitakuwa "Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote." Je, hii siyo mada kubwa kidogo kuweza kuijadili? Je, inaonekana kama kitu ambacho kidogo hakiwezi kufikika? Mungu kuwa chanzo cha uhai kwa vitu vyote inaweza kuonekana ni mada ambayo watu wanahisi kutohusika nayo, lakini wote wanaomfuata Mungu wanapaswa kuielewa. Hii ni kwa sababu mada hii haihusiani kwa kuchanganulika na kila mtu anayemjua Mungu, kuweza kumridhisha na kumheshimu. Hivyo, mada hii inapaswa kuwasilishwa. Awali, pengine baadhi ya watu walikuwa na ufahamu wa msingi wa mada hii, au pengine baadhi ya watu waliifahamu.

Jumamosi, 22 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Sehemu ya Kwanza Mhutasari wa Mamlaka ya Mungu, Tabia ya Haki ya Mungu, na Utakatifu wa Mungu


Mhutasari wa Mamlaka ya Mungu, Tabia ya Haki ya Mungu, na Utakatifu wa Mungu

Mnapomaliza maombi yenu, je, mioyo yenu inahisi utulivu katika uwepo wa Mungu? (Ndiyo.) Ikiwa moyo wa mtu unaweza kutulizwa, ataweza kusikia na kuelewa neno la Mungu na ataweza kusikia na kuuelewa ukweli. Ikiwa moyo wako hauwezi kutulizwa, ikiwa moyo wako siku zote unayoyoma, au siku zote unafikiria juu ya mambo mengine, utaathiri kuja kwako pamoja kusikia neno la Mungu. Sasa, ni kitu gani cha msingi tunachokijadili wakati huu? Hebu sote turudi nyuma kidogo katika hoja kuu.