Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Maudhui-ya-hewa. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Maudhui-ya-hewa. Onyesha machapisho yote

Jumamosi, 17 Februari 2018

Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II) | 1. Mazingira ya Kuishi ya Msingi Ambayo Mungu Anawaumbia Wanadamu | (1) Hewa

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mungu,
Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)

1. Mazingira ya Kuishi ya Msingi Ambayo Mungu Anawaumbia Wanadamu

Mwenyezi Mungu alisema, Tumejadili mada nyingi na maudhui yanayohusiana na kirai hiki “Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote,” lakini mnajua ndani ya mioyo yenu ni vitu vipi Mungu anatoa kwa wanadamu mbali na kuwapa ninyi neno Lake na kutenda kazi Yake ya kuadibu na hukumu kwenu? Watu wengine huenda wakasema, “Mungu hunipa neema na baraka, na kunipa nidhamu, faraja, na utunzaji na ulinzi kwa kila njia iwezekanayo.” Wengine watasema, “Mungu hunipa chakula cha kila siku na kinywaji,” ilhali wengine hata watasema, “Mungu hunipa kila kitu.” Kuhusu vitu hivi ambavyo watu wanaweza kukutana navyo katika maisha yao ya kila siku, nyote mnaweza kuwa na majibu yanayohusiana na matukio mnayopitia katika maisha yenu ya kimwili.