Umeme wa Mashariki | Tamko la Ishirini
Mwenyezi Mungu alisema, Utajiri wa jumba Langu ni bila idadi na usioeleweka, lakini mwanadamu hajawahi kuja Kwangu kuufurahia. Hana uwezo wa kuufurahia mwenyewe, wala wa kujilinda mwenyewe kwa kutumia juhudi zake mwenyewe; badala yake, yeye daima huweka imani yake kwa wengine. Kwa wale wote Ninaowatazamia, hakuna mtu aliyewahi kunitafuta kwa makusudi na moja kwa moja. Wao wote huja mbele Zangu kwa kushawishiwa na wengine, wakifuata halaiki ya watu, na hawana nia ya kulipa gharama au kutumia muda kuimarisha maisha yao. Kwa hivyo, miongoni mwa watu hakuna mtu aliyewahi kuishi katika hali halisi, na watu wote huishi maisha yasiyo na maana.
