![]() |
| Neno Laonekana Katika Mwili |
Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia
Mwenyezi Mungu alisema,Je, ungependa kumwona Yesu? Je, ungependa kuishi na Yesu? Je, ungependa kusikia maneno yaliyonenwa na Yesu? Iwapo ni hivyo, basi utakaribishaje, kurudi kwa Yesu? Je, uko tayari kabisa? Utakaribisha kurudi kwa Yesu kwa namna gani? Nafikiri kuwa kila ndugu na dada wanaomfuata Yesu wangependa kumpa Yesu makaribisho mazuri. Lakini Je, mmewaza iwapo utamjua Yesu Atakaporejea? Je, mtaelewa kila kitu Atakachosema? Je, mtakubali bila masharti, kila kazi ambayo Anafanya? Wale wote ambao wamesoma Biblia wanajua kuhusu kurudi kwa Yesu, na wale wote ambao wamesoma Biblia wanangoja kwa makini kuja Kwake.
