Swahili Gospel Movie "Ndoto Yangu ya Ufalme wa Kibinguni"
Utambulisho
![]() |
| Ndoto Yangu ya Ufalme wa Kibinguni |
Song Ruiming ni mchungaji wa kanisa huko Korea Kusini. Kama mfuasi wa dhati wa Bwana kwa miaka mingi, amekuwa akifuatilia imani yake kwa bidii sana na kumfanyia kazi Bwana huku akisubiri kuinuliwa hadi katika ufalme wa mbinguni Bwana atakaporudi. Katika miaka ya hivi karibuni, amekuwa akihisi kuchanganyikiwa sana na mwenye udhaifu anapokuwa akiona kwamba Kanisa halina kazi ya Roho Mtakatifu na linazidi kuwa na ukiwa. Hapo ndipo aliposikia kuhusu dhehebu kwa jina la Umeme wa Mashariki linaloibuka nchini China ambalo linashuhudia kurudi kwa Bwana Yesu—Mwenyezi Mungu, ambaye Anafanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho kwa kuonyesha ukweli. Hivyo Song Ruiming na mhubiri Cui Cheng'en walisafiri kwenda China kujifunza Umeme wa Mashariki, ambapo hatimaye waliyasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, na kugundua kwamba maneno yote ya Mwenyezi Mungu ni ukweli, sauti ya Mungu! Mwenyezi Mungu huenda ndiye Bwana Yesu aliyerejea!
