Christian Video Swahili "Bahati na Bahati Mbaya" | Mshukuru Mungu kwa Neema Yake ya Ajabu
Utambulisho
Kwa sababu yeye alitoka katika familia iliyo masikini, tangu akiwa na umri mdogo Du Juan alikusudia kutengeneza pesa nyingi sana apate kuishi maisha mazuri. Ili kufikia lengo hili, aliacha shule mapema zaidi kwenda kufanya kazi ya mikono, chochote angeweza kufanya ili apate pesa. Yeye hakulalamika wakati kazi ilikuwa ngumu na ya kuchokesha. Hata hivyo, yeye hakupata matokeo aliyotaka. Bila kujali jinsi alivyofanya kazi kwa bidii, hakuweza kupata yale maisha aliyojitakia mwenyewe. Mwaka wa 2008, bado akiwa na ndoto ya kutengeneza pesa nyingi, yeye na mumewe walikwenda Japan kufanya kazi.