Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Wanapenda-Ukweli. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Wanapenda-Ukweli. Onyesha machapisho yote

Jumapili, 22 Aprili 2018

Wale Wanaopenda Ukweli Wana Njia ya Kufuata

Wale Wanaopenda Ukweli Wana Njia ya Kufuata

1. Kama hali ya Watu Ni Ya Kawaida Inategemea na Kama Wanapenda Ukweli au La
Mwenyezi Mungu alisema, Watu wengi wameibua suala lifuatalo: Baada ya ushirika wa juu, wanahisi wazi kabisa, wanakuwa na nguvu zaidi, na hawana hisia hasi—lakini hali kama hiyo inabaki tu kwa karibu siku kumi, ambapo baadaye hawawezi kudumisha hali ya kawaida. Suala ni nini? Je mmewahi kujiuliza kinachosababisha hili? Mbona hali zenu ni nzuri sana katika siku hizo takriban kumi za kwanza? Wengine wanasema kuwa hili ni tokeo la kutolenga ukweli. Lakini hivyo ungeweza vipi kufikia kiwango hiki cha kawaida baada ya kusikia ushirika? Mbona ulikuwa na furaha sana baada ya kuusikia ukweli? Wengine wanasema ni kwa sababu ya kazi ya Roho Mtakatifu. Mbona basi kazi ya Roho Mtakatifu inakoma baada ya takriban siku kumi? Wengine husema ni kwa sababu wanakuwa wazembe na kuacha kusonga mbele na juu. Mbona basi hili linafanyika hata wakati watu wanapojaribu kufanya maendeleo? Mbona Roho Mtakatifu pia hafanyi kazi? Je, hukuwa unajaribu kusonga mbele na juu? Basi mbona Roho Mtakatifu hayuko kazini?