Jumanne, 4 Desemba 2018

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu katika Mwili na Wajibu wa Mwanadamu"

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu katika Mwili na Wajibu wa Mwanadamu"
Mwenyezi Mungu anasema, "Hata kama Mungu mwenye mwili hunena, kufanya kazi, au kutenda miujiza, Anafanya kazi kubwa katika usimamizi Wake, kazi ambayo haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kazi ya mwanadamu ni kufanya tu wajibu wake kama kiumbe katika hatua fulani ya usimamizi wa Mungu. Bila usimamizi kama huo, yaani, ikiwa huduma ya Mungu kuwa mwili itapotea, pia wajibu wa viumbe utapotea. Kazi ya Mungu kuendeleza huduma Yake ni kumsimamia mwanadamu, ilhali mwanadamu afanyapo wajibu wake ni kutimiza wajibu wake ili kuafikia masharti ya Muumba na haiwezi kwa vyovyote vile kuchukuliwa kwamba ameendeleza huduma ya mtu yeyote. Kwa nafsi asili ya Mungu, yaani, Roho, kazi ya Mungu ni usimamizi wake, bali kwa Mungu kuwa mwili akiwa na umbile la nje la kiumbe, kazi yake ni kuendeleza huduma Yake. Kazi yoyote Aifanyayo Mungu ni ya kuendeleza huduma Yake, na mwanadamu anaweza tu kufanya awezalo ndani ya upeo Wake wa usimamizi na chini ya uongozi Wake."
Tazama Video: Utongoaji wa Neno la Mungu

Jumatatu, 3 Desemba 2018

Umuhimu wa Kuukoa Uzao wa Moabu

Katika miaka hii miwili hadi mitatu ya kazi, kile kilichopaswa kutimizwa katika kazi ya hukumu iliyofanyika juu yenu kimetimizwa kimsingi. Watu wengi wamesahau matarajio na kudura yao ya baadaye. Hata hivyo, inapotajwa kuwa ninyi ni uzao wa Moabu, wengi wenu huchukizwa sana—nyuso zenu hubadilika, vinywa vyenu hupinda, na macho yenu hukodolea. Hamuwezi kabisa kuamini kwamba ninyi ni uzao wa Moabu. Moabu ilifukuzwa hadi nchi hii baada ya kulaaniwa. Ukoo wa wana wa Moabu umerithishwa mpaka leo, na ninyi nyote ni uzao wake. Hakuna kitu ambacho Ninaweza kufanya—nani aliyekusababisha uzaliwe katika nyumba ya Moabu? Ninakuhurumia na Siko radhi uwe hivi, lakini ukweli hauwezi kubadilishwa na watu.

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu" (Sehemu ya Pili)


Maneno ya Roho Mtakatifu | "Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu" (Sehemu ya Pili)

Mwenyezi Mungu anasema, "Katika kila aina ya kazi ya Mungu kuna maono yanayofahamika na mwanadamu; maono yanayofuatwa na matarajio mwafaka ya Mungu kwa mwanadamu. Bila haya maono kama msingi, mwanadamu hawezi kuwa na uwezo wa utendaji na pia hangeweza kumfuata Mungu bila kuyumbayumba. Ikiwa mwanadamu hamjui Mungu au hayaelewi mapenzi ya Mungu, basi yote ayafanyayo ni bure na yasiyoweza kukubalika na Mungu. Hata mwanadamu awe na vipawa vingi kiasi gani, bado hawezi kujitenga na kazi ya Mungu na uongozi wa Mungu. Bila kujali uzuri na wingi wa matendo ya mwanadamu, bado hayawezi kuchukua nafasi ya kazi ya Mungu. Kwa hivyo basi, utendaji wa mwanadamu hauwezi kutenganishwa na maono katika hali yoyote ile. Wale ambao hawakubali maono mapya hawana vitendo vipya. Vitendo vyao havina uhusiano na ukweli kwani wanajifunga katika mafundisho ya dini na kufuata sheria zilizokufa; hawana maono mapya kabisa na kwa sababu hiyo hawatendi kulingana na enzi mpya. Wamepoteza maono na kwa kufanya hivyo wamepoteza kazi ya Roho Mtakatifu, hivyo basi kupoteza ukweli pia."
Tazama Video: Filamu za Injili

Jumapili, 2 Desemba 2018

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani"

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani"

Mwenyezi Mungu anasema, "Mnachukulia matendo yote ya Kristo kwa upande wa wasio wema na kuhukumu kazi Yake yote na utambulisho Wake na kiini Chake kwa mtazamo wa waovu. Mmefanya kosa kubwa sana na kufanya kile ambacho hakijawahi kufanywa na wale kabla yenu. Hiyo ni, mnamtumikia tu Mungu mkuu aliye mbinguni na taji juu ya kichwa Chake na hammshughulikii kamwe Mungu mnayemchukulia kuwa asiye na maana kabisa na hivyo kuwa ghaibu. Hii siyo dhambi yenu? Huu sio mfano halisi wa kosa lenu dhidi ya tabia ya Mungu? Mnamwabudu sana Mungu aliye mbinguni. Mnapenda sana takwimu wakuu na kuheshimu walio na ufasaha mkubwa.

Ufafanuzi wa Matamko ya Ishirini na Mbili na Ishirini na Tatu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu
Mwenyezi Mungu anasema, Leo, wote wako tayari kuelewa mapenzi ya Mungu na kujua tabia ya Mungu, lakini hakuna anayejua kwa nini hawezi kufuata matamanio yake, hajui kwa nini moyo wake daima humsaliti, na kwa nini hawezi kutimiza kile anachotaka. Kwa hiyo, yeye anakabiliwa tena na hali mbaya ya kukata tamaa, lakini pia anaogopa. Asiweze kuonyesha hisia hizi zinazopingana, anaweza tu kuonyesha huzuni na kuendelea kujiuliza: Je, inaweza kuwa Mungu hajanipa nuru? Inaweza kuwa Mungu ameniacha kwa siri? Pengine wengine wote wako sawa, na Mungu amewapa wote nuru isipokuwa mimi. Kwa nini daima mimi husikia kusumbuliwa wakati ninasoma maneno ya Mungu, kwa nini siwezi kuelewa chochote? Ingawa akili za watu hufikiri mambo haya, hakuna mtu anayethubutu kuyaonyesha; wao huendelea tu kupambana kwa ndani. Kwa kweli, hakuna mtu ila Mungu anayeweza kuelewa maneno Yake au kufahamu mapenzi Yake ya kweli.

Jumamosi, 1 Desemba 2018

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | "Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli"


Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | "Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli"

Mwenyezi Mungu anasema, "Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu.

Majani Yaangukayo Yatakaporudi kwa Mizizi Yake Utajuta Maovu Yote Ambayo Umefanya

Nyote mmeshuhudia wenyewe kazi ambayo Nimefanya miongoni mwenu, ninyi wenyewe mmesikia maneno ambayo Nimenena, nanyi mnajua mtazamo Wangu kuelekea kwenu, kwa hiyo mnapaswa kujua kwa nini Ninafanya kazi hii miongoni mwenu. Nitawaambia ukweli—ninyi ni vifaa tu vya kazi Yangu ya ushindi katika siku za mwisho; ninyi ni vyombo vya kupanua kazi Yangu miongoni mwa nchi za Mataifa. Mimi huzungumza kupitia kwa udhalimu wenu, uchafu wenu, upinzani na uasi wenu ili kupanua bora zaidi kazi Yangu ili jina Langu lienee miongoni mwa nchi za Mataifa, yaani, kuenea miongoni mwa nchi yoyote nje ya Israeli. Ni kusudi kwamba jina Langu, vitendo Vyangu, na sauti Yangu viweze kusambaza kotekote katika nchi za Mataifa, hivyo nchi hizo zote ambazo si za Israeli ziweze kushindwa na Mimi na ziweze kuniabudu Mimi, kuwa nchi Zangu takatifu nje ya nchi za Israeli na Misri.