Jumanne, 14 Mei 2019

Neno la Mwenyezi Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I) Uendelezo wa Sehemu ya Pili

Neno la Mwenyezi Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu  (I) Uendelezo wa Sehemu ya Pili

Kwenye Siku ya Sita, Muumba Aongea, na Kila Aina ya Kiumbe Hai Akilini Mwake Chajitokeza, Kimoja Baada ya Kingine
Bila kuchoka, kazi ya Muumba ya kuumba viumbe vyote ilikuwa imeendelea kwa siku tano, na punde tu baada ya hapo ndipo Muumba alipokaribisha siku ya sita ya uumbaji Wake wa viumbe vyote. Siku hii ilikuwa mwanzo mwingine mpya, na siku nyingine isiyo ya kawaida. Nini, basi, kilikuwa mpango wa Muumba mkesha wa siku hii mpya?

Jumatatu, 13 Mei 2019

Neno la Mungu | “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” Sehemu ya Pili



Neno la Mungu | “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” Sehemu ya Pili

Mwenyezi Mungu anasema, “Hatua tatu za kazi ndizo kiini cha usimamizi mzima wa Mungu, na ndani yazo zimeelezwa tabia ya Mungu na kile Alicho. Wale wasiojua kuhusu hatua tatu za kazi ya Mungu hawana uwezo wa kutambua jinsi Mungu anavyoonyesha tabia Yake, wala hawajui hekima ya kazi ya Mungu, na wanasalia kutojua njia nyingi Anazomwokoa mwanadamu, na mapenzi Yake kwa wanadamu wote. Hatua tatu za kazi ndizo maonyesho kamili ya kazi ya kumwokoa mwanadamu.

Jumapili, 12 Mei 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I) Sehemu ya Pili


Kwenye Siku ya Nne, Misimu, Siku, na Miaka ya Mwanadamu Iliumbika Huku Mungu Akionyesha Mamlaka Yake kwa Mara Nyingine Tena
Muumba alitumia matamshi Yake kutimiza mpango Wake, na kwa njia hii Alipitisha siku tatu zake za kwanza kwenye mpango Wake. Kwenye siku hizi tatu, Mungu hakuonekana kushughulika kila pahali, au kujichosha Yeye Mwenyewe; kinyume cha mambo ni kwamba, Alikuwa na siku tatu za kwanza nzuri katika mpango Wake na Alitimiza utekelezaji mkubwa wa mabadiliko makubwa ya ulimwengu.

Jumamosi, 11 Mei 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I) Sehemu ya Kwanza

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Vikao vyangu mbalimbali vya ushirika vilivyopita vilikuwa vinahusu kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Baada ya kuvisikiliza vikao hivi vya ushirika, je, unahisi kuwa umefaidi na kupata ufahamu na maarifa kuhusu tabia ya Mungu? Ufahamu wako na maarifa ni mkubwa kiwango gani? Je, unaweza kuweka nambari katika kiwango hicho? Je, vikao hivi vya ushirika vilikupa ufahamu wa kina kuhusu Mungu? Inaweza kusemwa ufahamu huu ni maarifa ya kweli ya Mungu? Inaweza kusemwa kwamba maarifa na ufahamu huu wa Mungu ni maarifa ya hali halisi nzima ya Mungu, na kila kitu Anacho na alicho? La, bila shaka haiwezi kusemwa hivyo!

Ijumaa, 10 Mei 2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III (Sehemu ya Saba)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Sasa hebu tusome dondoo za maandiko zilizo hapa chini.
12. Maneno ya Bwana Yesu kwa Wanafunzi Wake Baada ya Kufufuka Kwake
Yohana 20:26-29 Na kufuatia siku nane tena wanafunzi wake walikuwa ndani, naye Tomaso alikuwa nao: kisha Yesu akaja, milango ikiwa imefungwa, na kusimama katikati, na kuema, Amani iwe nanyi. Kisha akasema kwa Tomaso, nyoosha kidole chako hapa, na uitazame mikono yangu, nyoosha mkono wako hapa, na uusongeshe mbavuni mwangu: na usiwe bila imani, ila mwenye imani.

Alhamisi, 9 Mei 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V Utakatifu wa Mungu II” Sehemu ya Nne



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V Utakatifu wa Mungu (II)” Sehemu ya Nne

Mwenyezi Mungu anasema, “Kuelewa kiini cha Mungu na kujua kiini cha Mungu kinapeana msaada usioweza kupimika kwa kuingia kwa watu katika maisha. Natumai kwamba hamtapuuza haya ama kuyaona kama mchezo; kwa sababu kumjua Mungu ni msingi muhimu na msingi wa imani ya mwanadamu kwa Mungu na ufuatiliaji wa mwanadamu wa ukweli na wokovu na kitu ambacho hakifai kuachiliwa.

Jumatano, 8 Mei 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Pili



Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Pili

Mwenyezi Mungu anasema, “Hakuna kizuizi chochote katika kazi Yake na kile Anachokifanya, na haitawekewa kizuizi chochote na binadamu yeyote, kitu chochote, au kifaa chochote, na haitakatizwa na nguvu zozote za kikatili. Katika kazi Yake mpya, Yeye ni Mfalme anayeshinda daima, na nguvu zozote za kikatili na uvumi wote na hoja za uwongo zote kutoka kwa mwanadamu zimekanyagiwa chini ya kibao Chake cha kuwekea miguu.