Jumatatu, 7 Oktoba 2019

1. Kuna tofauti ipi kati ya maneno yaliyoonyeshwa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema na maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu katika Enzi ya Ufalme?

V. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Tofauti Kati ya Kazi ya Mungu ya Hukumu Katika Siku za Mwisho na Kazi Yake ya Ukombozi Katika Enzi ya Neema

1. Kuna tofauti ipi kati ya maneno yaliyoonyeshwa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema na maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu katika Enzi ya Ufalme?

Aya za Biblia za Kurejelea:
Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu” (Mathayo 4:17).
Na kwamba toba na msamaha wa dhambi vinapaswa kuhubiriwa katika jina lake miongoni mwa mataifa yote, kuanzia Yerusalemu” (Luka 24:47).
Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo” (Yohana 16:12-13).

Jumapili, 6 Oktoba 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV Utakatifu wa Mungu I” Sehemu ya Pili


Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV Utakatifu wa Mungu (I)” Sehemu ya Pili
Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu anafanya kazi, Mungu anamtunza mtu, anamwangalia mtu, na Shetani anafuata hatua Yake yote. Yeyote anayefadhiliwa na Mungu, Shetani pia anatazama, akifuata nyuma. Iwapo Mungu anamtaka mtu huyu, Shetani atafanya kila kitu kwa uwezo wake kumzuia Mungu, akitumia mbinu mbalimbali mbovu kujaribu, kusumbua na kuharibu kazi anayofanya Mungu ili kufikia lengo lake lililofichwa. Lengo lake ni nini? Hataki Mungu awe na mtu yeyote; anataka wale wote ambao Mungu anataka, kuwamiliki, kuwatawala, kuwaelekeza ili wamwabudu, ili watende maovu pamoja naye. Je, hii siyo nia ya husuda ya Shetani?... Shetani yuko vitani na Mungu, akifuata nyuma Yake. Lengo lake ni kubomoa kazi yote ambayo Mungu anataka Kufanya, kuwamiliki na kudhibiti wale wote ambao Mungu anawataka, kuwafisha kabisa wale ambao Mungu anataka. Kama hawajafishwa, basi wanakuja kwa milki ya Shetani kutumiwa naye—hili ndilo lengo lake.”

Zaidi: Tokeo Lililofikiwa kwa Kumjua Mungu
Tazama Video: Wimbo wa Kuabudu | "Tabia ya Haki ya Mungu ni ya Pekee" | How to Know God

Jumamosi, 5 Oktoba 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Uendelezo wa Sehemu ya Nne



Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Uendelezo wa Sehemu ya Nne
Mwenyezi Mungu anasema, “Wakati Ayubu alipopitia majaribio yake kwa mara ya kwanza, alinyang’anywa mali yake yote na watoto wake wote, lakini hakujisujudia na kusema chochote ambacho kilikuwa dhambi dhidi ya Mungu kutokana na hayo. ... Kwenye jaribio la pili, Shetani aliunyosha mbele mkono wake ili kumdhuru Ayubu, na ingawaje Ayubu alipitia maumivu yaliyokuwa makubwa zaidi kuliko yale aliyokuwa amepitia awali, bado ushuhuda wake ulikuwa wa kutosha wa kuacha watu wakiwa wameshangazwa. Alitumia ujasiri wake, imani yake, na utiifu kwa Mungu, pamoja na kumcha Mungu kwake, kwa mara nyingine tena kumshinda Shetani, na mwenendo wake na ushuhuda wake viliweza kwa mara nyingine tena kuidhinishwa na kupata kibali cha Mungu.

Ijumaa, 4 Oktoba 2019

Mwanadamu Anaweza Kuokolewa tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kazi ya Mungu

Kila mtu anahisi kuwa usimamizi wa Mungu ni wa ajabu, kwa sababu watu wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu hauna uhusiano wowote na mwanadamu. Wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu ni kazi ya Mungu pekee, shughuli za Mungu, na hivyo wanadamu hawajali kuhusu usimamizi wa Mungu. Kwa njia hii, kuokolewa kwa wanadamu kumekuwa kusiko yakini na kusiko dhahiri, na kumebaki tu maneno matupu. Hata kama mwanadamu anamfuata Mungu ili aokolewe na aingie katika hatima inayopendeza, mwanadamu hajishughulishi na jinsi ambavyo Mungu Hutekeleza kazi Yake. Mwanadamu hashughulishwi na Anachokipanga Mungu na anachopaswa kufanya ili aokolewe.

Alhamisi, 3 Oktoba 2019

Kutanafusi kwa Mwenye Uweza

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki, Mapenzi ya Mungu

Kunayo siri kubwa moyoni mwako. Huifahamu kamwe kwa sababu umekuwa ukiishi katika ulimwengu usio na mwanga unaoangaza. Moyo wako na roho yako vimechukuliwa mateka na yule mwovu. Macho yako yamefunikwa na giza; huwezi kuliona jua angani, wala nyota ikimetameta wakati wa usiku. Masikio yako yamezibwa na maneno ya udanganyifu na husikii sauti ya Yehova ingurumayo kama radi, wala sauti ya maji yatiririkayo kutoka katika kiti cha enzi. Umepoteza kila kitu ambacho kilipaswa kuwa chako na kila kitu ambacho mwenye Uweza alikupa. Umeingia katika bahari ya uchungu isiyokuwa na mwisho, pasipo uwezo wa kukuokoa, hukuna matumaini ya kuishi, umeachwa ukipambana na kuzunguka zunguka tu.…

Jumatano, 2 Oktoba 2019

Maneno ya Mungu | Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki, neno la Mungu,

Kulingana na vitendo na matendo katika maisha yenu, nyote mnahitaji kurasa za maneno ya kuwajaza na kuwajenga kila siku, kwani mko na upungufu mno, na ujuzi na maarifa yenu ya kupokea ni ya hali ya chini sana. Katika maisha yenu ya kila siku, mnaishi katika hali na mazingira yasiyo na ukweli ama fahamu nzuri. Hamna rasilimali ya uwepo na pia hamna msingi wa Kunijua au kujua ukweli. Imani yenu imejengwa tu juu ya ujasiri usio dhahiri au kwenye ibada za kidini na ujuzi kulingana na mafundisho ya kidini kabisa. Kila siku Ninatazama mienendo yenu na kuchunguza nia yenu na matunda yenu maovu.

Jumanne, 1 Oktoba 2019

Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki, Kumjua Mungu,

Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani


Nyinyi nyote mna furaha kupokea tuzo mbele ya Mungu na kutambuliwa na Mungu. Haya ni matakwa ya kila mtu baada ya yeye kuanza kuwa na imani kwa Mungu, kwani mwanadamu kwa moyo wake wote hutafuta mambo yaliyo juu na hakuna aliye tayari kubaki nyuma ya wengine. Hii ndiyo njia ya mwanadamu. Kwa sababu hii, wengi kati yenu wanajaribu daima kupata neema ya Mungu mbinguni, lakini kwa kweli, uaminifu wenu na uwazi kwa Mungu ni wa kiasi kidogo sana ukilinganishwa na uaminifu na uwazi wenu kwenu wenyewe. Mbona Nasema hivi? Kwa sababu Sikiri uaminifu wenu kwa Mungu kabisa, na zaidi Nakana kuwepo kwa Mungu ndani ya mioyo yenu.