Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Haki-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Haki-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote

Jumatano, 2 Oktoba 2019

Maneno ya Mungu | Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki, neno la Mungu,

Kulingana na vitendo na matendo katika maisha yenu, nyote mnahitaji kurasa za maneno ya kuwajaza na kuwajenga kila siku, kwani mko na upungufu mno, na ujuzi na maarifa yenu ya kupokea ni ya hali ya chini sana. Katika maisha yenu ya kila siku, mnaishi katika hali na mazingira yasiyo na ukweli ama fahamu nzuri. Hamna rasilimali ya uwepo na pia hamna msingi wa Kunijua au kujua ukweli. Imani yenu imejengwa tu juu ya ujasiri usio dhahiri au kwenye ibada za kidini na ujuzi kulingana na mafundisho ya kidini kabisa. Kila siku Ninatazama mienendo yenu na kuchunguza nia yenu na matunda yenu maovu.

Jumamosi, 28 Septemba 2019

Maonyo Matatu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Kama muumini wa Mungu, hamfai kuwa watiifu kwa yeyote mwingine isipokuwa Yeye katika mambo yote na mjilinganishe na moyo Wake katika mambo yote. Hata hivyo, ingawa wote huelewa mafundisho haya, ukweli huu wa kimsingi ulio wazi kabisa kwa binadamu hauwezi kuonekana kuwa kujumuishwa kwao kikamilifu, kutokana na ugumu wao, kama vile hali yao ya kutojua, upuzi, au ufisadi. Kwa hivyo, kabla mwisho wenu haujaamuliwa, Ninafaa kuwaambia kwanza baadhi ya mambo, ambayo ni yenye umuhimu mkubwa sana kwenu. Kabla Sijaendelea, mnafaa kwanza kuelewa yafuatayo: Maneno Ninayoongea ni ukweli unaoelekezwa kwa wanadamu wote, na wala si kwa mtu mahususi au aina fulani ya mtu.

Alhamisi, 26 Septemba 2019

Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki, Tabia ya Haki ya Mungu

Nimefanya kazi nyingi miongoni mwenu na, ni wazi kwamba, Nimezungumza vizuri pia. Hata hivyo, Nahisi kwamba maneno na kazi Yangu havijatimiza lengo la kazi Yangu ya siku za mwisho. Maana, katika siku za mwisho, kazi Yangu si kwa ajili ya mtu au watu fulani bali ni kwa manufaa ya kufafanua tabia Yangu asilia. Hata hivyo, kutokana na sababu nyingi—pengine ukosefu wa muda au shughuli nyingi za kazi—tabia Yangu haijamwezesha binadamu kunijua hata kidogo. Kwa hivyo, Ninasonga mbele na katika mpango Wangu mpya, kazi Yangu ya mwisho, kufungua ukurasa mpya ili wale ambao wataniona watajipiga kifuani na kuulilia uwepo Wangu bila kukoma.

Jumanne, 24 Septemba 2019

Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Kazi ya siku za mwisho ni kutenganisha vitu vyote kulingana na jinsi yavyo, kuhitimisha mpango wa usimamizi wa Mungu, kwa maana muda u karibu na siku ya Mungu imewadia. Mungu huwaleta wote ambao wameingia katika ufalme Wake, yaani, wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake mpaka mwisho, katika enzi ya Mungu Mwenyewe. Hata hivyo, kabla ya kuja kwa enzi ya Mungu Mwenyewe, kazi Atakayofanya Mungu si kutazama matendo ya mwanadamu wala kuchunguza maisha ya wanadamu, ila ni kuhukumu uasi wake, kwa maana Mungu atawatakasa wale wote wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi.

Jumamosi, 21 Septemba 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu” Sehemu ya Pili



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu” Sehemu ya Pili

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Ingawaje Hasira ya Mungu ni Fiche na Haijulikani kwa Binadamu, Haivumilii Kosa Lolote
Hasira ya Mungu Ni Usalama wa Nguvu Zote za Haki na Mambo Yote Mazuri
Mtu Hafai Kutegemea Uzoefu na Fikira Ili Kujua Tabia ya Haki ya Mungu
Ingawa Shetani Anaonekana Mwenye Utu, Haki na Maadili, Ni Mkatili na Mwovu katika Kiini Chake

Jumapili, 18 Agosti 2019

Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku ya Ghadhabu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Leo, Nawaonya hivi kwa ajili ya kupona kwenu wenyewe, ili kazi Yangu iendelee vizuri, na ili kazi Yangu ya uzinduzi kote ulimwenguni iweze kufanyika kwa njia inayofaa na kikamilifu, ikifichua maneno Yangu, mamlaka, adhama na hukumu kwa watu wa nchi zote na mataifa. Kazi Ninayoifanya miongoni mwenu ni mwanzo wa kazi Yangu katika ulimwengu wote. Ingawa sasa ni siku za mwisho tayari, jua kwamba "siku za mwisho" ni jina tu la enzi: Kama tu vile Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema, linaashiria enzi, na linaashiria enzi nzima, badala ya mwisho wa miaka au miezi michache. Hata hivyo siku za mwisho ni tofauti kabisa na Enzi ya Neema na Enzi ya Sheria.

Ijumaa, 16 Agosti 2019

Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu (Sehemu ya Pili)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Petro

Maisha yote ya mwanadamu yamekuwa chini ya himaya ya Shetani, na hakuna mtu yeyote anayeweza kujitoa kutoka katika ushawishi wa Shetani yeye mwenyewe. Wote wanaishi katika dunia chafu, kwa upotovu na utupu, bila maana yoyote au thamani; wanaishi maisha ya kutojali kwa ajili ya mwili, tamaa, na kwa ajili ya Shetani. Hakuna maana yoyote kwa kuwepo kwao. Mwanadamu hana uwezo wa kupata ukweli utakaomweka huru kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Ingawa mwanadamu anaamini katika Mungu na anasoma Biblia haelewi jinsi ya kujitoa kutoka kwa ushawishi wa Shetani.

Jumamosi, 10 Agosti 2019

Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Tabia ya Haki ya Mungu

Baada ya miaka elfu kadhaa ya upotovu, mwanadamu amekuwa asiyehisi na mpumbavu, pepo anayempinga Mungu, kwa kiasi kwamba uasi wa mwanadamu kwa Mungu umeandikwa katika vitabu vya historia, na hata mwanadamu mwenyewe hana uwezo wa kutoa ripoti kamili ya tabia zake za uasi wake—kwa kuwa mwanadamu amepotoshwa sana na Shetani, na amehadaiwa na Shetani kiasi kwamba hajui ni wapi pa kugeukia. Hata wa leo, mwanadamu bado anamsaliti Mungu: Wakati mwanadamu anamwona Mungu, anamsaliti, na wakati yeye hawezi kumwona Mungu, bado anamsaliti. Kuna hata wale ambao, baada ya kushuhudia laana ya Mungu na ghadhabu ya Mungu, bado wanamsaliti.

Jumamosi, 13 Julai 2019

Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake Sehemu ya Tano


Majaliwa ya Binadamu Yanaamuliwa na Mwelekeo Wake Kwa Mungu
Mungu ni Mungu aliye hai, na kama vile tu watu wanavyotenda tofauti katika hali tofauti, ndivyo mwelekeo wa Mungu ulivyo katika utendakazi huu na unavyotofautiana kwa sababu Yeye si kikaragosi, wala Yeye si hewa tupu. Kupata kuujua mwelekeo wa Mungu ni jambo lenye thamani kwa wanadamu. Watu wanafaa kujifunza vipi, kwa kuujua mwelekeo wa Mungu, wanaweza kuijua tabia ya Mungu na kuuelewa moyo Wake kidogo kidogo. Unapouelewa moyo wa Mungu kidogo kidogo hutahisi kwamba kumcha Mungu na kujiepusha na maovu ni jambo gumu la kutimiza.

Jumamosi, 22 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Sehemu ya Kwanza Mhutasari wa Mamlaka ya Mungu, Tabia ya Haki ya Mungu, na Utakatifu wa Mungu


Mhutasari wa Mamlaka ya Mungu, Tabia ya Haki ya Mungu, na Utakatifu wa Mungu

Mnapomaliza maombi yenu, je, mioyo yenu inahisi utulivu katika uwepo wa Mungu? (Ndiyo.) Ikiwa moyo wa mtu unaweza kutulizwa, ataweza kusikia na kuelewa neno la Mungu na ataweza kusikia na kuuelewa ukweli. Ikiwa moyo wako hauwezi kutulizwa, ikiwa moyo wako siku zote unayoyoma, au siku zote unafikiria juu ya mambo mengine, utaathiri kuja kwako pamoja kusikia neno la Mungu. Sasa, ni kitu gani cha msingi tunachokijadili wakati huu? Hebu sote turudi nyuma kidogo katika hoja kuu.

Jumatano, 12 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V Utakatifu wa Mungu II Sehemu ya Kwanza


Leo, kaka na dada, hebu tuimbe wimbo. Tafuta mmoja ambao mnapenda na ambao mmeimba mara nyingi kabla. (Tungependa kuimba wimbo wa neno la Mungu "Upendo Safi Bila dosari.")
1. "Upendo" unarejelea hisia ambayo ni safi na bila dosari, ambapo mnatumia mioyo yenu kupenda, kuhisi, na kuwa wa kufikiri. Katika upendo hakuna masharti, hakuna vizuizi, na hakuna umbali. Katika upendo hakuna tuhuma, hakuna udanganyifu, na hakuna ujanja. Katika upendo hakuna umbali na hakuna chochote kichafu. Iwapo una upendo, basi hautadanganya, kulalamika, kusaliti, kuasi, kushurutisha, au kutafuta kupata kitu au kupata kiasi fulani.

Ijumaa, 1 Desemba 2017

Umeme wa Mashariki | Mbingu Mpya na Nchi Mpya | Tamthilia ya Jukwaa "Kwaya ya Injili ya Kichina 13"

   
 1. WANADAMU WAMEUPATA TENA UTAKATIFU WAO WALIOKUWA NAO AWALI

La … la … la … la …

    Wakati huu wa shangwe, wakati huu wa nderemo (du ba du ba), haki ya Mungu na utakatifu wa Mungu vimeenda ugenini kote ulimwenguni (ba ba ba …), na binadamu wote wanavisifu bila kikomo. (Du … ba … ba la ba ba) Miji ya mbingu inacheka kwa furaha (du ba du ba), na falme za nchi zinacheza kwa shangwe (Ba ba ba …) Ni nani wakati huu ambaye haonyeshi furaha? Na ni nani wakati huu ambaye halii? (Du … ba … ba la ba ba) Nchi ni miliki ya mbingu, na mbingu imeungana na nchi. Mwanadamu ni ugwe unaounganisha mbingu na nchi, na kwa sababu ya utakatifu wake, kwa sababu ya mwanadamu kufanywa upya, mbingu haijafichwa tena kwa nchi, na nchi haiko kimya tena kwa mbingu.