Mwenyezi Mungu alisema, Katika nyumba Yangu, kulikuwapo wakati mmoja wale waliolisifu jina Langu takatifu, ambao walifanya kazi bila kuchoka ili utukufu Wangu duniani ungejaza anga. Kwa sababu ya hili, Nilifurahi sana, moyo Wangu ulijawa na furaha—lakini nani angeweza kufanya kazi badala Yangu, akiacha usingizi usiku na mchana? Azimio la mwanadamu mbele Yangu hunipa raha, lakini uasi wake huchochea hasira Yangu, na hivyo, kwa sababu mwanadamu hawezi kamwe kuzingatia wajibu wake, huzuni Yangu kwa ajili yake inakua kubwa zaidi. Kwa nini watu daima hawawezi kujitolea Kwangu? Kwa nini daima wao hujaribu kubishana na Mimi? Mimi ni msimamizi mkuu wa kituo cha biashara? Kwa nini Mimi hutimiza kwa moyo kamili kile ambacho watu hudai kutoka Kwangu, lakini Nitakacho kutoka kwa mwanadamu hakitimii?" Inawezekana kuwa mimi Sina maarifa katika njia za biashara, lakini mwanadamu anayo? Kwa nini watu daima hunidanganya kwa mazungumzo ya ushawishi na ya kusifu mno?Kwa nini watu kila mara huja wakibeba "zawadi," wakiomba njia ya kurudi ndani? Je, hili ndilo Nililomfundisha mwanadamu kufanya?