Jumamosi, 30 Juni 2018

Kutatua Asili na Kutenda Ukweli

Kutatua Asili na Kutenda Ukweli

1. Uhusiano Kati ya Ubinadamu na Uwezo wa Kutenda Ukweli
Mwenyezi Mungu alisema, Watu husema kuwa kutenda ukweli ni vigumu kabisa. Basi mbona watu wengine wanaweza kutenda ukweli? Watu wengine husema ni kwa sababu kwa asili wanaipokea kazi ya Roho Mtakatifu ikifanya kazi juu yao, na pia kwa sababu ni wazuri kiasili. Hoja hii ina kiwango fulani cha mantiki. Watu wengine ni wazuri kiasili; wana uwezo wa kutenda ukweli. Ubinadamu wa watu wengine ni mnyonge, hivyo ni vigumu kwao kutenda ukweli; hii inamaanisha kuwa watakumbana na matatizo fulani. Je, mnaweza kusema kuwa yule ambaye hatendi ukweli amewahi kuutafuta ukweli? Hajautafuta kabisa! Fikira zake binafsi hutokea: “Njia hii ni nzuri, ni kwa faida yangu.” Mwishowe, bado anatenda kulingana na mawazo yake binafsi. Hatafuti ukweli kwa sababu kuna kitu kisicho sawa na moyo wake, moyo wake hauko sawa.

Swahili Christian Movie | Nyendo za Mateso ya Kidini | "Kukaribia Hatari na Kurudi"


Swahili Christian Movie | Nyendo za Mateso ya Kidini | "Kukaribia Hatari na Kurudi"


Utambulisho


Christian Movie Video Swahili | Nyendo za Mateso ya Kidini Nchini China | "Kukaribia Hatari na Kurudi"
Tangu kilipokuja mamlakani katika China Bara mnamo mwaka wa 1949, Chama Cha Kikomunisti cha China kimekuwa hakikomi katika mateso yake kwa imani ya kidini. Kwa wayowayo kimewashika na kuwaua Wakristo, kuwafukuza na kuwadhulumu wamishonari wanaofanya kazi nchini China, wakachukua ngawira na kuchoma nakala nyingi za Biblia, wakafunga kabisa na kubomoa majengo ya kanisa, na bila mafanikio wakajaribu kukomesha makanisa yote ya nyumbani.

Ijumaa, 29 Juni 2018

Jinsi ya Kufahamu Tabia Yenye Haki ya Mungu

Jinsi ya Kufahamu Tabia Yenye Haki ya Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Watu wanaweza kupangwa kwa makundi, ambayo hubainishwa kwa roho zao. Watu wengine wana roho za binadamu, na wao huchaguliwa kwa njia iliyoamuliwa kabla. Ndani ya roho ya binadamu kuna sehemu iliyoamuliwa kabla. Watu wengine hawana roho; wao ni pepo ambao wamepenyeza. Hawajaamuliwa kabla na kuchaguliwa na Mungu. Ingawa wamekuja ndani, hawawezi kuokolewa, na hatimaye wataondolewa na pepo. Inaamuliwa na asili ya ndani ya mtu huyo iwapo ataikubali kazi ya Mungu, au njia ipi atakayochukua au iwapo ataweza kubadilika baada ya kuikubali. Watu wengine hawana la kufanya ila kupotea. Roho zao huamua kwamba wao ni aina hii ya kitu; hawawezi kubadilika. Kuna watu ambao Roho Mtakatifu hukoma kufanya kazi kwa sababu watu hawa hawajachagua njia sahihi. Wakirudi Roho Mtakatifu huenda bado akafanya kazi Yake, lakini wakishikilia kutorudi basi wamemalizika kabisa.

Umuhimu na Mazoezi ya Sala

Umuhimu na Mazoezi ya Sala

Mwenyezi Mungu alisema, Je, mnaomba vipi kwa sasa? Ni maendeleo kwa sala za kidini jinsi gani? Mnaelewa nini hasa kuhusu umuhimu wa sala? Je mmechunguza maswali haya? Kila mtu ambaye hafanyi sala ako mbali na Mungu, kila mtu ambaye hasali anafuata mapenzi yake; Kukosekana kwa sala kunaashiria kwenda mbali na Mungu na usaliti wa Mungu. Ni nini uzoefu wenu hasa na sala? Sasa hivi, kazi ya Mungu tayari inakaribia mwisho na uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu unaweza kuonekana kutoka kwa maombi ya mwanadamu. Je wewe hutenda vipi wakati watu walio chini yako wanakurai na kukupa sifa kwa matokeo unayozalisha katika kazi yako? Je wewe hutenda vipi wakati watu wanakupa mapendekezo? Je, wewe huomba mbele ya Mungu? Mnasali wakati mna mambo na matatizo, lakini je, mnasali wakati hali zenu ni nzuri, au wakati mnahisi mmekuwa na mkutano wa mafanikio? Kwa hivyo wengi wenu huwa hamsali!

Alhamisi, 28 Juni 2018

Kupitia Aina Tofauti Za Mazingira Kuna Manufaa Kwa ukuaji Wa Maisha Ya Binadamu

Kupitia Aina Tofauti Za Mazingira Kuna Manufaa Kwa ukuaji Wa Maisha Ya Binadamu

Ni vyema kupitia mazingira ya aina tofauti. Mungu hakupangii mazingira haya bila sababu. Yeye hakuongozi popote pale bila makusudi, bali Yeye huandaa mazingira fulani spesheli kwa kila mmoja—mazingira ya kifamilia, mazingira ya kimaisha, mazingira uliyokulia, na mazingira unatekeleza majukumu yako punde utakapo mwamini. Yeye hutayarisha hali au mazingira fulani spesheli kwako wewe kuzipitia. Iwapo umetambua jinsi ya kupata uzoefu katika hali zote, muktadha na mazingira, bila kushindwa hata kwenye mazingira ya kuchukiza zaidi, na iwapo katika mazingira mazuri kabisa na ya kustarehesha kabisa na katika hali za majaribu makubwa kabisa, haupotoshwi au kudanganyika na katu hauanguki, basi utakuwa umepiga hatua na kuzidisha kimo. Je, yote haya yaweza kuchukuliwa kama wokovu? Kwa hakika, bado haujaokolewa. Lakini angalau, mazingira yako hayawezi kushawishi imani yako kwa Mungu au kusadiki kwako kwa Mungu, na unao msingi.

jinsi Mungu alitayarisha chakula kilicho muhimu kwa maisha ya mwanadamu ya kila siku


📚Mungu alisema, "Nafaka, matunda na mboga, na kila aina ya njugu vyote ni vyakula vya wala mboga. Hata kama ni vyakula...
ç”± Kanisa la Mwenyezi Mungu 發佈於 2018å¹´6月26日星期二

Mwenyezi Mungu alisema, "Nafaka, matunda na mboga, na kila aina ya njugu vyote ni vyakula vya wala mboga. Hata kama ni vyakula vya wala mboga, vina lishe za kutosha kuridhisha mahitaji ya mwili wa mwanadamu. Kwa hali yoyote, Mungu hakusema: “Kuwapa wanadamu hiki kunatosha. Wanadamu wanaweza tu kula vitu hivi.” Mungu hakuachia hapo na badala yake aliwatayarishia wanadamu vitu vyenye ladha nzuri zaidi. Vitu hivi ni gani? Ni aina mbalimbali ya nyama na samaki mnaopenda kuona juu ya meza zenu na kula kila siku. Kuna aina nyingi sana za nyama na samaki.

Jumatano, 27 Juni 2018

"Njia ya Kwenda katika Ufalme wa Mbinguni ni Yenye Hatari" (1) - Umeme wa Mashariki Laitikisa Dunia ya Kidini


"Njia ya Kwenda katika Ufalme wa Mbinguni ni Yenye Hatari" (1) - Umeme wa Mashariki Laitikisa Dunia ya Kidini


Utambulisho


Umeme wa Mashariki—kuonekana na kazi ya Mungu katika siku za mwisho limetikisa makundi na madhehebu yote, na kila aina ya wanadamu wamefichuliwa. Kondoo wengi wazuri katika kanisa wangependelea kuteseka kukamatwa kusikodhibitiwa na kuteswa na Chama cha Kikomunisti cha China ili tu kutafuta na kuchunguza Umeme wa Mashariki. Watu wengine, hata hivyo, wanaamini maneno ya wachungaji na wazee wa kanisa na wanasisitiza kutochunguza Umeme wa Mashariki, huku wengine, licha ya kujua kikamilifu kwamba Umeme wa Mashariki linashuhudia ukweli, hawathubutu kutafuta wala kulichunguza kwa hofu ya kuteswa na Chama cha Kikomunisti cha China. Kwa nini kondoo wazuri kanisani wanaweza kuchunguza Umeme wa Mashariki? Je, wale watu ambao hawawezi kutafuta na kuchunguza kazi ya Mungu katika siku za mwisho wanaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni hata hivyo? Video hii fupi inakuletea msukumo.