Jumanne, 9 Oktoba 2018

211. Mungu Katika Mwili Hufanya Kazi Kimya ili Kuwaokoa Wanadamu

I
Mungu alipata mwili, akabaki kujificha miongoni mwa wanadamu
ili kufanya kazi mpya, kutuokoa kutoka katika upotovu.
Anahifadhi maelezo.
Kwa mipango Aliyoifanya, Yeye hufanya kazi Yake hatua kwa hatua.
Maneno Yake yanaongezeka kila siku,
yakifariji, kukumbusha, kushutumu, na kuonya.

Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Aliyepata Mwili na Wanadamu Wanaotumiwa na Mungu

Smiley face


Kwa miaka mingi Roho wa Mungu Amekuwa akitafuta bila kikomo Akifanya kazi duniani. Kwa enzi nyingi Mungu Ametumia wanadamu wengi kufanya kazi Yake. Hata hivyo Roho wa Mungu bado hana mahali pazuri pa kupumzika. Kwa hivyo Mungu hupitia wanadamu mbalimbali kufanya kazi Yake na kwa kiasi kikubwa hutumia wanadamu kufanya hivyo. Yaani, katika miaka hii yote mingi, kazi ya Mungu haijawahi kusimama. Inaendelezwa mbele kupitia mwanadamu, bila kikomo mpaka siku ya leo. Ingawa Mungu Amesema na Ametenda mengi, mwanadamu bado hamjui Mungu, hii ni kwa sababu Mungu hajawahi kuonekana na mwanadamu na Yeye Hana umbo.

Jumatatu, 8 Oktoba 2018

nyimbo za kusifu na kuabudu | Anga Hapa ni Samawati Sana

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, nyimbo za sifa


Hii hapa anga,
anga iliyo tofauti sana!
I
Harufu ya kupendeza inasambazwa kote kwenye nchi, na hewa ni safi.
Mwenyezi Mungu alikuwa mwili na anaishi miongoni mwetu,
Akionyesha ukweli na kuanza hukumu ya siku za mwisho.
Maneno ya Mungu yanaweka wazi ukweli wa upotovu wetu,
tunatakaswa na kukamilishwa na kila aina ya jaribio na usafishaji.
Tunayaaga maisha yetu maovu na kubadilisha sura yetu ya zamani kuwa sura mpya.

Dondoo za Filamu za Injili "Sauti Nzuri Ajabu" (1) - Je, Ni Vipi Unabii wa Kurudi kwa Bwana Yesu Unatimia?


Utambulisho

Dondoo za Filamu za Injili "Sauti Nzuri Ajabu" (1) - Je, Ni Vipi Unabii wa Kurudi kwa Bwana Yesu Unatimia?
Watu wengi katika ulimwengu wa kidini hufuata unabii unaosema kwamba Bwana atashuka akiwa juu ya wingu na wanamsubiria Yeye kuja kwa njia hiyo kisha kuwanyakua hadi kwenye ufalme wa mbinguni, lakini wanapuuza unabii mbalimbali wa Bwana kuhusu kuja kwa siri: "Tazama, mimi nakuja kama mwizi" (Ufunuo 16:15). "Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha" (Mathayo 25:6). Hivyo unabii huu mbalimbali wa kurudi kwa Bwana unatimizwa vipi? Na tunafaa kuwa vipi wanawali wenye hekima ambao wanakaribisha kurudi kwa Bwana?
Tazama Video: Msifuni Mwenyezi Mungu (MV) ,Utongoaji wa Neno la Mungu 

Jumapili, 7 Oktoba 2018

Tunaweza Kunyakuliwa Hadi Ufalme wa Mbinguni Baada ya Kukubali Ukombozi Kutoka kwa Bwana Yesu?

Kwa msingi wa maneno ya Bwana Yesu akiwa msalabani "Imekwisha," wachungaji na wazee wa kanisa wa jamii ya dini kwa kawaida huhitimisha kwamba kazi ya Mungu ya wokovu wa wanadamu ilikuwa basi imekamilika. Bwana aliporudi, waumini wangepokelewa kwenye ufalme wa mbinguni, bila ya haja ya kazi yoyote ya utakaso na uokoaji wa watu. Je, mtazamo huu wa wachungaji na wazee wa kanisa unalingana na maneno ya Mungu? Bwana Yesu alikuwa akirejelea nini hatimaye, Aliposema "Imekwisha" akiwa msalabani? Kwa nini Mungu atake kuuonyesha ukweli wakati wa siku za mwisho, akiifanya kazi ya kuhukumu na kuwatakasa watu?

Tazama Video: Umeme wa Mashariki Sinema za Injili

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Jinsi ya Kuujua Uhalisi

Smiley face


Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Jinsi ya Kuujua Uhalisi

Mungu ni Mungu wa uhalisi: kazi Zake zote ni halisi, maneno yote Anayoyanena ni halisi, na ukweli wote Anaouonyesha ni halisi. Kila kisicho maneno Yake ni kitupu, kisichokuwepo, na kisicho timamu. Leo, Roho Mtakatifu yupo kwa ajili ya kuwaongoza watu katika maneno ya Mungu. Ikiwa watu wanatafuta kuingia katika uhalisi, basi ni lazima wauandame uhalisi, na waujue uhalisi, baadaye ni lazima wapitie uhalisi, na kuishi kwa kudhihirisha uhalisi.

Jumamosi, 6 Oktoba 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Thelathini

Matamshi ya Mwenyezi MunguTamko la Thelathini

Kati ya binadamu, wakati mmoja Nilifanya muhtasari wa ukaidi na udhaifu wa mwanadamu, na hivyo Nilielewa udhaifu wa binadamu na Nikafahamu vema ukaidi wake. Kabla ya kuwasili kati ya binadamu, Nilikuwa nimekuja kuelewa kitambo furaha na huzuni kati ya binadamu—na kwa sababu ya hili, Ninaweza kufanya kile ambacho binadamu hawezi, na kusema kile ambacho binadamu hawezi, na Mimi hufanya hivyo kwa urahisi sana.