Hukumu Ni Mwanga (II)
Zhao Xia Mkoa wa Shandong
Baada ya kupitia adabu na hukumu ya Mungu wakati huu, nilipata ujuzi fulani juu ya mwelekeo wangu wa kuzingatia heshima na hadhi, na nilikuwa radhi kuachana na mwili wangu na kumwamini Mungu na kutekeleza wajibu wangu kulingana na mahitaji Yake. Hata hivyo, uchafu wangu uliotokana na sumu za Shetani zilikuwa zimezama sana. Kina cha nafsi yangu bado kilikuwa kinatawaliwa na ushawishi wa Shetani.
Ili kuniokoa vyema kutoka kwa madhara ya Shetani, Mungu aliinyoosha mikono Yake ya wokovu kwangu tena. Siku moja, niliambiwa kuwa kulikuwa na dada katika kanisa ambaye hakuwa katika hali nzuri, kwa hiyo nilishauriana na dada niliyeshirikishwa naye kuhusu jinsi ya kutatua shida hii. Kwa sababu dada niliyeshiriki naye hakuhisi vizuri, nilikwenda peke yangu kutatua tatizo hilo baada ya majadiliano yetu. Nilimtafuta dada huyo usiku uo huo ili kuwasiliana naye, na tatizo hilo lilitatuliwa haraka sana. Moyo wangu ulibubujikwa kwa furaha wakati huo, nikifikiri kuwa kiongozi wa ngazi ya juu angenisifu kwa hakika kwa sababu nilikuwa nimetia jitihada nyingi sana. Hata hivyo, wakati tu nilipokuwa nikisubiria habari njema, kiongozi wa ngazi ya juu aliandika barua akitaka kuelewa hali ya dada huyo. Nilifikiria ilikuwa ni kunisifu, kwa hiyo niliifungua kwa furaha na kuisoma. Lakini nilipoona kuwa kile kilichokuwa ndani ya barua kilikuwa hasa cha kuuliza dada mwenzi vile alivyoshughulikia tatizo hilo, mara moja nikawa mwenye uchungu: Kwa uwazi ni mimi niliyeshughulikia suala hilo. Mbona usiniandikie kuniuliza juu ya hilo? Inaonekana mimi sina nafasi katika moyo wa kiongozi na ninadharauliwa. Mimi ni msichana wa kibaraka tu. Haijalishi jinsi ninavyofanya vyema sipati sifa njema yoyote kwa sababu hakuna mtu anayelizingatia kwa makini. Nilivyofikiria zaidi juu ya hilo, ndivyo nilihisi zaidi nilikuwa nimekosewa na kuhuzunika. Nilihisi nimefedheheshwa. Wakati huu, dada yangu mwenzi alikuwa na barua mkononi mwake na alikuwa karibu kuzungumza nami. Singeweza kuzuia hisia zilizokuwa ndani yangu na nikampigia kelele: "Kiongozi wa ngazi ya juu hajui jinsi suala hili lilivyotatuliwa. Hujaelewa haya? Nililifanya kazi kwa bidii kwa muda mrefu lakini hakuna hata mmoja aliyesema neno jema kulihusu, na hatimaye wewe bado ulipata sifa zote. Mbele ya kila mtu, mimi ni mtu tu wa kutumwa na kusaidia. Haijalishi ninaliwekea jitihada gani, hakuna mtu atakayelifurahia." Baada ya kusema haya, nilihisi mwenye kudhulumiwa sana hadi nikaangua kilio. Wakati huo, maneno ya Mungu yalirudiarudia katika masikio yangu: “3. Kama ulitumia juhudi nyingi lakini bado Sikuchangamkii, je, utaweza kuendelea kunifanyia kazi katika uvunguvungu? 4. Ikiwa, baada ya wewe kutumia vitu fulani kwa ajili Yangu, Sijatimiza mahitaji yako madogomadogo, je, utavunjika moyo na kusikitishwa na Mimi au hata kuwa na ghadhabu na kunitusi?” (“Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya kushutumu ya Mungu yalinituliza polepole, na mawazo yangu yalifumbuka sana pia. Tukio ambalo lilikuwa limetoka kutokea liliendelea kucheza tena katika mawazo yangu kama sinema. Ufunuo wa Mungu ulinifanya kuona kwamba asili yangu ni ya kutisha na ya hatari sana, na kwamba imani yangu kwa Mungu na kutekeleza kwa wajibu wangu haukuwa wa kuridhisha Mungu au kupokea idhini Yake, mbali kupokea sifa na taadhimu kutoka kwa watu wengine. Mara tu matamanio yangu hayakuwa yakitoshelezwa, ningekuwa mwenye kujaa chuki; asili yangu ya unyama ungejitokeza, na kumsaliti Mungu ikawa jambo rahisi sana kufanya hata zaidi. Wakati huu, niliona kuwa nimevuka mipaka sana na kwamba nilikuwa mkatili. Maumivu niliyoyahisi yalikuwa ya kuhuzunisha sana. Nilipotubu, nikamwomba Mungu: "Ewe Mungu, nilifikiri nilikuwa nimebadilika na sikuwa ninaishi tena kwa sababu ya heshima na hadhi, na pia ningeweza kushirikiana na dada huyo. Lakini katika ufunuo Wako leo, kwa mara nyingine tena nimeweza kufunua ubaya wangu wa kishetani, daima nikihisi kuwa sikuwa na hadhi kati ya watu na kuteseka kwa sababu jitihada zangu hazikusifiwa na wengine. Ee Mungu, Shetani kweli alikuwa amenidhuru sana. Hadhi, sifa, na majivuno yote yakawa pingu zangu. Ninaomba kuwa Unaweza kuniongoza kutoka kwa ushawishi wa Shetani tena." Baadaye, niliona kati ya maneno ya Mungu yafuatayo: “Kila mmoja wenu amepanda vilele vya juu zaidi vya umati; ninyi mmepanda kuwa mababu wa umati. Ninyi ni wadhalimu mno, na mnacharuka miongoni mwa mabuu wote kutafuta mahali salama, mkijaribu kuwameza mabuu walio wadogo kuwaliko ninyi. Ninyi ni wenye kijicho na wa husuda katika mioyo yenu, kuwashinda wale pepo ambao wamezama chini ya bahari. Mnaishi chini ya samadi, mkiwasumbua mabuu kutoka juu hadi chini ili wasiwe na amani, mkipigana wenyewe kwa wenyewe kwa muda mfupi na kisha kutulia. Ninyi hamjui hali yenu wenyewe, ihali bado ninyi hupigana wenyewe kwa wenyewe ndani ya samadi. Ni nini ambacho mnaweza kupata kutokana na mapambano hayo? Kama ninyi kweli mngekuwa na moyo wa kunicha Mimi, mngewezaje kupigana wenyewe kwa wenyewe bila Mimi kujua? Haijalishi vile hali yako ilivyo juu, je, bado wewe si mnyoo mdogo mwenye uvundo ndani ya samadi? Utaweza kuota mbawa na kuwa njiwa angani?” (“Majani Yaangukayo Yatakaporudi kwa Mizizi Yake Utajuta Maovu Yote Ambayo Umefanya” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kila neno la hukumu ya Mungu lilinidunga kwa uchungu ndani ya moyo wangu kama upanga mkali, likichangamsha roho yangu na kunifanya kutambua kwamba nilitekeleza wajibu wangu sio ili kumtukuza Mungu na kumshuhudia, lakini kwa sababu daima nilitaka kujionyesha, kujishuhudia mwenyewe, na nilikuwa na ndoto ya kuwa bora kuliko watu ili waweze kunienzi na kuniheshimu. Kulikuwa na uchaji wowote wa Mungu ndani ya moyo wangu? Nilichofuatilia hakikuwa sawa na kile cha malaika mkuu aliyemsaliti Mungu? Mimi ni kiumbe kilichoumbwa kilichopotoshwa kabisa na Shetani. Mbele ya Mungu, mimi ni kama uchafu, funza. Ninatakiwa kuwa ninamwabudu Mungu na kutimiza wajibu wangu nikiwa na uchaji moyoni mwangu wakati wote, lakini sikushughulika na kazi ya uaminifu, na nilitaka daima kutumia kutekeleza wajibu wangu kama fursa ya kujionyesha na kujishuhudia mwenyewe. Mungu angewezaje kutochukia na kusinywa na haya? Mungu ni mtakatifu sana na mkuu, amejaa mamlaka na uongozi, na bado anabaki kuwa mnyenyekevu na kujisetiri, hafichui utambulisho Wake kamwe ili kuwafanya watu kumtazamia na kumstahi. Badala yake, Anaendelea kwa ukimya kujitolea Kwake kwote ili kuwaokoa wanadamu, kamwe hajitetei Mwenyewe au kudai sifa njema, na kamwe hadai chochote kutoka kwa wanadamu. Unyenyekevu, uadilifu, na kutokuwa na ubinafsi kwa Mungu kumenifanya nione kiburi, kuwa duni, na ubinafsi wangu, kumenifanya nihisi kuwa nimepotoshwa sana na Shetani na ninahitaji sana wokovu wa hukumu, adabu, jaribio na usafishaji wa Mungu. Kwa hivyo nilianguka tena mbele ya Mungu: "Ewe, Mwenyezi Mungu! Kupitia uadibu na hukumu Yako ninaweza kuona uasi wangu hata wazi zaidi, pamoja na uadilifu Wako na ukuu. Kuanzia sasa kuendelea, wakati ninapotekeleza wajibu wangu ninatumaini tu kutenda kama mwanadamu wa adabu aliye na moyo unaokuogopa Wewe, na kutupa tabia yangu ya kishetani kwa kutegemea maneno Yako."
Baada ya kupitia adabu na hukumu ya Mungu mara kwa mara tena, maoni yangu juu ya ufuatiliaji yamebadilika hatua kwa hatua, lakini tabia ya maisha yangu haikuwa bado imepata mabadiliko kweli. Ili kunitakasa kabisa zaidi na kunisababisha kutembea kwenye njia ya sahihi ya uzima, Mungu mara nyingine tena alinipa wokovu Wake. Baadaye, nilichaguliwa kuwa kiongozi wa kanisa, nikishirikiana na dada mwingine kutekeleza wajibu wetu. Kutokana na kushindwa kwangu kwa awali, niliendelea kujikumbusha kila wakati kwamba nilihitaji kukubaliana na dada huyo ili kufanya kazi ya kanisa vizuri. Mwanzoni, ningekuwa nikijadili kila kitu na dada huyo na kufuatilia mwongozo wa Mungu pamoja, kwa hivyo tulifanikisha matokeo katika vipengele vyote vya kazi. Lakini baada ya muda fulani, niligundua kuwa dada huyo alikuwa na tabia nzuri za asili, mawasiliano yake ya ukweli yalikuwa wazi na ya kuangaza, na uwezo wake wa kikazi ulikuwa sawa kuliko wangu. Wakati wa mikutano, ndugu walikuwa wote radhi kusikiliza mawasiliano yake na wote walitafuta ushauri wake walipopatwa na shida. Nilipokabiliwa na mazingira kama hayo, nilikuwa tena nimetegwa katika mtego wa Shetani na kupumbazwa nayo: Dada huyo ni bora zaidi kuliko mimi kwa kila namna na anapendwa na ndugu bila kujali mahali anaenda. Hapana! Ni lazima nimpite kwa vyovyote vile, na niache ndugu waone kwamba mimi niko chini yake. Kwa sababu hii, nilijishughulisha kanisani kila siku mtawalia, nikipanga mikutano ya ndugu na haijalishi ni nani aliyepata matatizo ningekimbia kwao kuwasaidia kutatua suala hilo. ... Inawezekana kuwa nilionekana kuwa mwaminifu na mtiifu kutoka nje, lakini malengo yangu ya ndani ingewezaje kuepuka macho ya Mungu? Uasi wangu ulifufua hasira ya Mungu, na kama matokeo nilianguka katika giza. Sikupata nuru niliposoma maneno ya Mungu, sikuwa na cha kusema wakati wa kuomba, niliwasiliana bila kusisimua wakati wa mikutano, na hata niliogopa mikutano na ndugu zangu. Nilikuwa nimefungwa kabisa na heshima na hadhi. Nilipitia kila siku bila kidokezo, ni kama nilikuwa nimebeba mzigo mkubwa mgongoni mwangu na singeweza kupumua kutokana na kubanwa. Singeweza pia kubaini tena baadhi ya masuala ya kanisa, na utendaji bora wangu wa kazi yangu ukashuka kwa kasi. Nilipokabiliwa na ufunuo kama huo kutoka kwa Mungu, sikujaribu kujijua na pia sikuwa radhi kuzungumza kwa nyofu kwa ndugu kuhusu hali yangu na kutafuta ukweli ili kuutatua, kwa hofu kuwa wangenidharau. Baadaye, kuadibu na nidhamu ya Mungu ikaniangukia. Tumbo yangu ilianza kwa ghafla kuniuma sana hadi singeweza kukaa au kusimama kwa amani. Mateso ya magonjwa na kutoridhika kutokana na kutopata hadhi kuliniacha nikizungukazunguka katikati ya maisha na kifo. Kutokana na kukataa kwangu kuyakubali matatizo yangu na kushindwa kwangu kushirikiana kwa kazi ya kanisa, kanisa halikuwa na budi ila kunibadilisha na kunituma nyumbani ili ibada ya kiroho na kujitafakari. Baada ya kupoteza hadhi yangu, nilihisi kama nilikuwa nimehukumiwa jehanamu. Kihisia, nilizama hadi katika kiwango changu cha chini kabisa na kuhisi kuwa nilikuwa nimeaibika kabisa. Niliteseka hata zaidi ndani hasa wakati nilipowaona ndugu wote wakitekeleza kikamilifu wajibu wao, wakati nilikuwa nimepoteza kazi ya Roho Mtakatifu na sikuwa na uwezo wa kutekeleza wajibu wowote. Kwa uchungu, sikuweza kujisaidia ila kujiuliza: Mbona kuna wengine wanaamini Mungu na wanaelewa ukweli zaidi na zaidi, ilhali ninaendelea kumuasi na kumpinga Mungu mara kwa mara tena kwa sababu ya heshima na hadhi? Nilimsihi Mungu mara nyingi anielekeze nipate chanzo cha kufeli kwangu. Siku moja, niliona yafuatayo kati ya maneno ya Mungu: “… watu wengine hususan humpenda Paulo sana: Wanapenda kuhutubu na kufanya kazi nje. Wanapenda kukutana pamoja na kuongea; wanapenda watu wanapowasikiliza, kuwaabudu, kuwazingira. Wanapenda kuwa na kimo katika mawazo ya watu wengine na kufurahia wakati wengine wanathamini mfano wao. Je, tunagundua nini kuhusu asili ya mtu kutokana na aina hii ya mwenendo? Hebu tuchanganue asili yake: Je, mtu wa aina hii aliye na tabia kama hii ana asili ya aina gani? Je, ingewezaje kusemwa kwa ufupi? Watu wa kawaida hawawezi kuelewa hili lakini wanaweza tu kuona mwenendo. Uhusiano kati ya tabia na asili ya mtu ni upi? Je, asili yake ni gani? Huwezi kuitambua, sivyo? Kama kweli anatennda kwa njia hii, basi hilo linatosha kuonyesha kuwa yeye ni mfidhuli na mwenye majivuno. Yeye hamwambudu Mungu kamwe; yeye hutafuta hadhi ya juu, na anataka kuwa na mamlaka juu ya wengine, kuwamiliki, kuwa na kimo akilini mwao. Huu ni mfano bora wa Shetani” (“Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Kwa kuongezea, inasema katika "Mahubiri na Ushirika kuhusu Kuingia Katika Maisha": "Kiini na asili ya Shetani ni usaliti. alimsaliti Mungu tangu mwanzo kabisa, na baada ya kumsaliti Mungu alidanganya, akapotosha, akachezea, na akatawala wanadamu duniani walioumbwa na Mungu, akijaribu kuwa sawa na Mungu kama na kuanzisha ufalme tofauti. ... Unaona, asili ya Shetani sio ile inayosaliti Mungu? Kutoka kwa yote ambayo Shetani amefanyia wanadamu, tunaweza kuona wazi kwamba Shetani ni kwa kweli pepo mbaya anayepinga Mungu na kwamba asili ya Shetani ni ile inayomsaliti Mungu. Haya yote ni kamili" ("Jinsi ya Kupata Ujuzi wa Asili Yako Potovu" katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha (I)). Nikizingatia haya maneno, singeweza kujizuia kutetemeka na hofu. Niliona kwamba yale niliyoyaishi kwa kudhihirisha yalikuwa kwa sura ya Shetani kabisa, na nilikuwa mfano halisi wa Shetani—mwenye kiburi na mwenye majivuno, na asiyemwabudu Mungu hata kidogo. Mungu aliniinua ili nitekeleze wajibu wangu kanisani, ili nipate kuwaleta ndugu mbele za Mungu nikiwa na uchaji Kwake moyoni mwangu, na kuwafanya watu wawe na nafasi ya Mungu katika mioyo yao, na pia kuwa na uchaji na kumtii Mungu. Lakini nilipokabiliwa na kuinuliwa na Mungu, sikutia maanani nia ya Mungu katika kutekeleza wajibu wangu, na sikuhisi mzigo kuwasaidia ndugu kuingia katika maisha. Badala yake, nilitaka kila mara kuwafanya watu waniangalie kwa makini na kunisikiliza, na kwa ajili ya matamanio yangu, nilijaribu kila mara kujiinua bila kujalisha popote nilipoenda. Nilikuwa hata mwenye wivu kwa waliokuwa wazuri na mwenye husuda kwa wakakamavu, na nilishindana kwa ukaidi na wengine kwa ajili ya ukuu. Kutoka nje, nilikuwa ninashindana na wanadamu, lakini kwa kweli nilikuwa nikipigana dhidi ya Mungu na nilikuwa nikishindana na Mungu kupata hadhi na uwezo. Hili ni jambo ambalo huudhi sana tabia ya Mungu na ni mwenendo ambao unapaswa kuadhibiwa na Mungu! Hata hivyo, Mungu hakunishughulikia kulingana na kile nilichokuwa nimekifanya. Alinihukumu na kuniadibu tu, kunirudia na kunifundisha nidhamu, na kuninyang’anya hadhi ili kunifanya nijitafakari na kutubu. Niliona kwamba mapenzi ya Mungu kwangu yalikuwa ya kina sana na makubwa sana! Singeweza kujizuia kuhisi majuto na kujilaumu ndani, na hata zaidi nilichukia ya kwamba upotovu wangu ulikuwa wa kina sana. Nilifuata Mungu lakini sikufuatilia ukweli, na badala yake nilifanya kazi kwa bidii bila kufikiri tu kwa sababu ya hadhi na heshima. Nilikuwa nimeshindwa kabisa kuishi kulingana na mapenzi na wokovu wa Mungu. Kadri nilivyojichungua, ndivyo nilivyoona wazi zaidi kuwa misemo niliyoishi kulingana nayo, kama vile “Kama vile mti huishi kwa sababu ya ganda lake, mtu huishi kwa sababu ya uso wake,” na “Mtu huacha jina lake nyuma popote akaapo, kama vile bata bukini hutetea popote arukapo,” yalikuwa uongo yaliyotumiwa na Shetani ili kuwapotosha na kuwadhuru wanadamu. Nilitambua kwamba Shetani alitumia mambo haya kuduwaza nafsi za watu, kupotosha mawazo yao, na kuwafanya kukuza mitazamo mbaya kuhusu maisha, kuwafanya wajitahidi kwa vyovyote vile kufuatilia vitu bure kama vile hadhi, umaarufu, utajiri na heshima, na hatimaye kupotea kutoka kwa na kumsaliti Mungu, ili waweze wote kuzingatia uwongo wake na kuifanyia kazi na kuangamizwa na kudhuruiwa kwa hiari. Nilikuwa mmoja wa watu hao ambao walikuza mtazamo mbaya wa maisha kwa msingi wa udanganyifu wa Shetani, nikawa mwenye kiburi, majivuno, dharau, na asiyekuwa na mahali pa Mungu moyoni mwangu. Niliishi katika upotovu na kumtendea Mungu kama adui. Sasa, sipaswi tena kuenda kinyume na Mungu wakati ninafurahia rehema Yake. Nitajirekebisha kabisa, nitaacha Shetani kabisa, nitampa Mungu moyo wangu kabisa, na kuishi kwa kudhihirisha mtu wa kweli ili kufariji moyo wa Mungu. Baada ya hapo, nilitaka kujua jinsi ya kuendelea na njia yangu ya baadaye, na jinsi ya kufuatilia ukweli ili kukidhi mapenzi ya Mungu. Asante kwa Mungu kwa kuniongoza tena. Kisha niliona maneno ya Mungu: “Leo, hata kama wewe si mfanyikazi, unapaswa kuwa na uwezo wa kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu, na kutafuta kujiwasilisha kwa mipango yote ya Mungu. Unapaswa kuwa na uwezo wa kutii chochote Mungu anachosema, na upitie kila aina ya madhila na usafishaji, na ingawa wewe ni dhaifu, moyoni mwako unapaswa bado uwe na uwezo wa kumpenda Mungu. Wale ambao huchukua jukumu katika maisha yao wako tayari kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu, na mtazamo wa watu kama hawa kuhusu harakati ni ule sahihi. Hawa ndio watu ambao Mungu anahitaji. … Kama kiumbe wa Mungu, mwanadamu anapaswa kutafuta kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu, na kutafuta kumpenda Mungu bila kufanya chaguo lingine kwa kuwa Mungu anastahiki upendo wa mwanadamu. Wale ambao wanatafuta kumpenda Mungu hawapaswi kutafuta faida zozote za kibinafsi au lile ambalo wanatamani binafsi; hii ndiyo njia sahihi kabisa ya ufuatiliaji” (“Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kama kioleza, maneno ya Mungu yalinipa nuru moyoni mwangu, yakinionyesha njia ambayo ninapaswa kuchukua. Mungu anatarajia kuwa watu, bila kujali kama wana hadhi na wamefikwa na hali gani, wanaweza kufanya kila wawezavyo kufuatilia ukweli, na wanaweza kutii upangaji na utaratibu wa Mungu na kutafuta kupenda na kumtosheleza Mungu. Hii ndiyo njia sahihi zaidi ya ufuatiliaji na pia ni njia ya ukweli ya uzima ambayo kiumbe kilichoumbwa kinapaswa kupitia. Hivyo basi niliamua mbele ya Mungu: Ee Mungu, asante kwa kunionyeshea njia ya ukweli ya uzima. Hadhi yangu ya awali ilikuwa kutokana na kuinuliwa na Wewe. Kutokuwa na hadhi leo pia ni kwa sababu ya haki Yako. Mimi ni kiumbe kidogo tu kilichoumbwa. Kuanzia sasa kuendelea, ninataka tu kufuatilia ukweli na kutii mipango Yako yote.
Baadaye, hali yangu ikarudi kawaida haraka kutokana na kusoma maneno ya Mungu na kuishi maisha ya kanisa. Kanisa tena lilinipangia kazi linalonifaa. Pia, nilizingatia kufuatilia ukweli katika kutekeleza wajibu wangu, wakati wowote kitu kilifanyika ningetafuta nia ya Mungu, ningejaribu kujijua mwenyewe, na kupata maneno yanayoambatana na ya Mungu ili kukitatua. Nilipokabiliwa na vitu vilivyohusisha heshima na hadhi, hata ingawa ningekuwa na mawazo fulani katika akili yangu, kwa kupitia maombi na neno la Mungu ningetafuta ukweli na kujitelekeza mwenyewe, na polepole niliweza kuwa na uwezo wa kutodhibitiwa na mambo haya na ningetekeleza wajibu wangu nikiwa na utulivu wa akili. Wakati niliona baadhi ya ndugu ambao hawakuwa wamemwamini Mungu kwa muda mrefu kama mimi wakiaminishwa na agizo, ningeweza, kwa kutafuta ukweli, kuelewa kwamba wajibu ambao unatekelezwa na mtu umejaaliwa na Mungu, na kwamba ninapaswa kutii mipango ya Mungu. Matokeo yake yakawa, niliweza kuwa na uwezo wa kuichukulia kwa njia sawa. Wakati ndugu walinishughulikia na kufichua asili yangu na kiini, ingawa nilihisi nimepoteza heshima, niliweza kuwa mtiifu kutumia sala. Hii ni kwa sababu upendo wa Mungu umeniangukia, na umefaidika sana katika kubadilisha tabia yangu ya maisha. Hapo awali, nilitia maanani katika heshima yangu sana kupindukia na sikuwa radhi kufichulia yeyote, kwa hofu kwamba wengine wangenidharau. Sasa, ninafanya mazoezi ya kuwa mtu mwaminifu kwa mujibu wa mahitaji ya Mungu, na kama nina shida yoyote nitafungua roho yangu kwa ndugu, jambo ambalo hunifanya kuhisi hasa nimefarijika na mwenye furaha katika kina cha roho yangu. Nikiyaona haya mabadiliko ndani yangu, singeweza kujisaidia ila kumshukuru na kumsifu Mungu, kwa maana mabadiliko haya yanaletwa kwangu na kazi ya adabu na hukumu ya Mungu ya siku za mwisho.
Nimemfuata Mwenyezi Mungu kwa miaka kadhaa sasa. Nikifikiria awali, ilikuwa ni sumu za Shetani ambazo zilikuwa zimemomonyoa nafsi yangu. Nilikuwa nimeishi chini ya miliki ya Shetani na niliangamizwa na kupumbazwa naye kwa miaka mingi. Sikujua thamani na maana ya maisha. Sikuweza kuona mwanga, wala sikuweza kupata furaha ya ukweli na shangwe. Nilizama katika dimbwi la simanzi na sikuweza kujinasua. Sasa, ni kupitia adhabu na hukumu ya mara kwa mara niliweza kuachana na madhara ya Shetani na kufikia faraja na uhuru. Nimepata tena dhamiri na mantiki yangu, na pia nina lengo sahihi la kufuatilia, kufuata Mungu katika njia ya ukweli na yenye kung’aa ya uzima. Kupitia adabu na hukumu ya Mungu, kwa kweli nilipitia upendo wa Mungu usio na ubinafsi na wa kweli, na kufurahia baraka na kupokea upendo ambao ulimwengu wa mwanadamu hauwezi kufurahia. Ni Mungu pekee anayeweza kumwokoa mwanadamu kutokana na bahari ya mateso ya Shetani, na ni kazi ya adabu na hukumu tu ya Mungu inayoweza kuwatakasa wanadamu kutokana na sumu za Shetani ndani yao na kuwafanya waishi kulingana na mfano wa mtu wa kweli na watembee katika njia ya ukweli ya uzima. Adabu na hukumu ya Mungu ni nuru. Ni rehema kubwa kabisa, ulinzi bora kabisa, na utajiri wenye thamani zaidi ya maisha ambayo Mungu amewapa watu. Kama vile maneno ya Mwenyezi Mungu yanasema: “… adabu na hukumu ya Mungu ndio uliokuwa ulinzi bora zaidi wa mwanadamu na neema kubwa. Ni kwa njia ya adabu na hukumu ya Mungu ndipo mwanadamu angeweza kugutuka, na kuchukia mwili, na kumchukia Shetani. Nidhamu kali ya Mungu inamweka huru kutokana na ushawishi wa Shetani, inamweka huru kutokana na dunia yake ndogo, na inamruhusu kuishi katika mwanga wa uwepo wa Mungu. Hakuna wokovu bora zaidi kuliko adabu na hukumu!” (“Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Asante kwa adhabu na hukumu ya Mungu kwa kuniokoa na kuniruhusu kuzaliwa upya! Katika njia yangu ya baadaye ya kumwamini Mungu, nitajizatiti kufuatilia ukweli, kupokea zaidi adhabu na hukumu zaidi ya Mungu, na kutoa kabisa sumu za Shetani ili kupata utakaso, kupata ujuzi wa kweli wa Mungu, na kuwa mtu ambaye kwa kweli anampenda Mungu. Utukufu wote uwe kwa Mungu. Amina!
Tanbihi:
a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kivilinganisha.
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Tazama zaidi: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni