Ijumaa, 31 Mei 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake"



Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake"

Mwenyezi Mungu anasema, “Hakuna mtu mbali na Yeye anayeweza kujua mawazo yetu yote, au kufahamu asili yetu na kiini chetu kwa dhahiri na ukamilifu, ama kuhukumu uasi na upotovu wa binadamu, ama kusema nasi na kufanya kazi kati yetu kama hivi kwa niaba ya Mungu aliye mbinguni. Hakuna mtu isipokuwa Yeye ambaye amepewa mamlaka, hekima, na heshima ya Mungu; tabia ya Mungu na kile Mungu Anacho na alicho yanatoka, kwa ukamilifu wao, ndani Yake. Hakuna mtu mbali na Yeye ambaye anaweza kutuonyesha njia na kutuletea mwangaza. Hakuna yeyote ila Yeye anayeweza kutufichulia siri ambazo Mungu hajatufunulia tangu uumbaji hadi leo.

Alhamisi, 30 Mei 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu II Sehemu ya Tatu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Uhuru: Awamu ya Tatu
Mwenyezi Mungu anasema, Baada ya mtu kupita utoto na wakati wake wa kubaleghe na kwa utaratibu bila kuzuilika kufikia ukomavu, hatua inayofuata ni kwake yeye kuuaga kabisa ule ujana wake, kuwaaga wazazi wake, na kukabiliana na barabara iliyo mbele yake akiwa mtu mzima huru. Wakati huo[c] lazima wakabiliane na watu, matukio na mambo yote ambayo mtu mzima lazima apitie, na kukabiliana na viungo mbalimbali katika msururu wa hatima yake. Hii ndiyo awamu ya tatu ambayo lazima mtu apitie.
1. Baada ya Kuwa Huru, Mtu Huanza Kupitia Ukuu wa Muumba
Kama kuzaliwa kwa mtu na kulelewa kwake ni "kipindi cha matayarisho" katika safari ya mtu maishani, kuweka lile jiwe la msingi katika hatima ya mtu, basi uhuru wa mtu ndio mazungumzo nafsi ya kufungua hatima ya maisha ya mtu.

Jumatano, 29 Mei 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II) Sehemu ya Pili

Maneno ya Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II) Sehemu ya Pili

Awamu Sita katika Maisha ya Binadamu
Katika mkondo wa maisha ya mtu, kila mtu hufikia kwenye misururu ya awamu muhimu. Hizi ni hatua za kimsingi zaidi, na muhimu zaidi, zinazoamua hatima ya maisha ya mtu. Kile kinachofuata ni ufafanuzi mfupi kuhusu mafanikio haya ambayo kila mtu lazima apitie kwenye mkondo wa maisha yake.
Kuzaliwa: Awamu ya Kwanza
Mahali ambapo mtu amezaliwa, amezaliwa katika familia ya aina gani, jinsia ya mtu, umbo la mtu, na wakati wa kuzaliwa: haya ndiyo maelezo ya awamu ya kwanza ya maisha ya binadamu.
Hakuna yeyote aliye na chaguo kuhusu sehemu hizi za awamu hii; zote ziliamuliwa kabla, mapema kabisa na Muumba.

Jumanne, 28 Mei 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu II Sehemu ya Kwanza

Leo tutaendelea na ushirika wetu kuhusu mada ya "Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee." Tayari tumekuwa na ushirika mara mbili katika mada hii, wa kwanza kuhusiana na mamlaka ya Mungu na wa pili kuhusiana na tabia ya haki ya Mungu. Baada ya kusikiliza ushirika huu mara mbili, je, mmepata ufahamu mpya wa utambulisho wa Mungu, hadhi, na hali halisi? Je, maono haya yamewasaidia kufikia maarifa mazito zaidi na uhakika wa ukweli kuuhusu uwepo wa Mungu? Leo Ninapanga kufafanua mada hii ya "Mamlaka ya Mungu."

Kuelewa Mamlaka ya Mungu Kutoka kwa Mitazamo Mikubwa na Midogo
Mamlaka ya Mungu ni ya kipekee. Ndiyo maonyesho ya sifa ya, na hali halisi maalum ya, utambulisho wa Mungu Mwenyewe. Hakuna kiumbe ambacho kiliumbwa wala kile ambacho hakikuumbwa kinachomiliki maonyesho ya sifa kama hizi na hali halisi maalum; Muumba tu ndiye anayemiliki aina hii ya mamlaka.

Jumatatu, 27 Mei 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemi ya Tatu



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemi ya Tatu

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”. Maudhui ya video hii: Uhuru: Awamu ya Tatu 1. Baada ya Kuwa Huru, Mtu Huanza Kupitia Ukuu wa Muumba 2. Kuwaacha Wazazi wa Mtu na Kuanza kwa Bidii Kuendeleza Wajibu Wako Kwenye Ukumbi wa Sanaa wa Maisha Ndoa: Awamu ya Nne 1. Mtu Hana Chaguo Kuhusu Ndoa 2. Ndoa Inazaliwa Kutokana na Hatima ya Wandani Wawili


Tazama Video: Neno la Mungu | “Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu

Kujua zaidi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Jumapili, 26 Mei 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Kuhusu Majina na Utambulisho" (Sehemu ya Kwanza)



Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Kuhusu Majina na Utambulisho" (Sehemu ya Kwanza)


Mwenyezi Mungu anasema, "Yesu aliwakilisha Roho wa Mungu, na Alikuwa Roho wa Mungu Akifanya kazi moja kwa moja. Alifanya kazi ya enzi mpya, kazi ambayo hakuna aliyekuwa amefanya mbeleni. Yeye Alifungua njia mpya, Alimwakilisha Yehova, na Alimwakilisha Mungu Mwenyewe. Ilhali kwa Petro, Paulo na Daudi, bila kujali walichoitwa, waliwakilisha tu utambulisho wa kiumbe wa Mungu, ama walitumwa na Yesu na Yehova.

Jumamosi, 25 Mei 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu Sehemu ya Tano


Aina Tano za Watu
Kwa sasa, Nitaacha ushirika wetu kuhusu tabia ya haki ya Mungu umalizikie hapo. Kinachofuata Nitaainisha wafuasi wa Mungu katika kategoria mbalimbali, kulingana na ufahamu wao wa Mungu na ufahamu wao na kile wamepitia kuhusiana na tabia ya haki Yake, ili muweze kujua awamu ambayo kwa sasa mnapatikana ndani pamoja na kimo chenu cha sasa. Kuhusiana na maarifa yao ya Mungu na ufahamu wao wa tabia Yake ya haki, awamu na kimo tofauti ambavyo watu huwa navyo vinaweza kugawanywa katika aina tano.