Ijumaa, 26 Januari 2018

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II | 4. Ayubu Amesikia Kuhusu Mungu kwa Kusikiliza juu ya Sikio

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Biblia,
Ayubu wa kati aliona Mungu chini ya mti

4. Ayubu Amesikia Kuhusu Mungu kwa Kusikiliza juu ya Sikio

(Ayubu 9:11) “Tazama, anapita karibu nami, na mimi simwoni: Tena anapita kwenda mbele, lakini mimi simtambui.”
(Ayubu 23:8-9) “Tazama, naenda mbele, lakini hayuko huko; narudi nyuma, lakini siwezi kumwona; Katika mkono wa kushoto, anapofanya kazi, lakini siwezi kumwona: anajificha katika upande wa mkono wa kuume, hata siwezi kumwona.”
(Ayubu 42:2-6) “Najua ya kwamba unaweza kufanya mambo yote, na ya kuwa hakuna kusudi lako linaloweza kuzuilika. Ni nani yeye anayeficha ushauri bila maarifa? Hivyo, nimesema maneno nisiyoyafahamu; mambo ya ajabu kwangu nisiyoyajua. Sikiliza, nakusihi, nami nitazungumza: Nitauliza kutoka kwako, nawe ujiweke wazi kwangu. Nimesikia habari zako, kwa kusikia kwa masikio: Lakini sasa jicho langu linakuona. Ndiyo sababu najichukia nafsi yangu, na kutubu kwenye vumbi na jivu.”

Ingawaje Mungu Hajajifichua kwa Ayubu, Ayubu Anasadiki Mamlaka Ya Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Ni nini Nguvu za maneno haya? Je, Yupo yeyote aliyetambua kwamba kunayo ukweli hapa? Kwanza, ni vipi ambavyo Ayubu alijua kwamba Mungu yupo? Na ni vipi alivyojua kwamba mbingu na ardhi na mambo yote yanatawaliwa na Mungu? Kunayo kifungu kinachojibu maswali haya mawili: Nimesikia habari zako, kwa kusikia kwa masikio: Lakini sasa jicho langu linakuona. Ndiyo sababu najichukia nafsi yangu, na kutubu kwenye vumbi na jivu (Ayubu 42:5-6). Kutokana na maneno haya tunajifunza kwamba, badala ya kuwa kwamba alimwona Mungu kwa macho yake mwenyewe, Ayubu alikuwa amejifunza kuhusu Mungu kutoka kwa hekaya. Ni katika hali hizi ndipo alipoanza kutembea njia ya kumfuata Mungu, na baadaye akathibitisha uwepo wa Mungu katika Maisha yake, na miongoni mwa mambo yote. Kunayo ukweli usiopingika hapa—nayo ni gani? Licha ya kuweza kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu. Katika haya, hakuwa sawa na watu wa leo? Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu, matokeo yake ni kwamba ingawaje alikuwa amewahi kumsikia Mungu, hakujua ni wapi Mungu alikuwa, au ni vipi Mungu alifanana, au ni nini Mungu alikuwa akifanya, mambo ambayo ni ya kibinafsi; tukiongea bila mapendeleo, ingawaje alimfuata Mungu, Mungu alikuwa hajawahi kumwonekania yeye au kumzungumzia yeye. Je, huu si ukweli? Ingawaje Mungu alikuwa hajaongea na Ayubu au kumpa amri zozote, Ayubu alikuwa ameuona uwepo wa Mungu, na kutazama ukuu Wake miongoni mwa mambo yote na katika hekaya ambazo Ayubu alikuwa amesikia kumhusu Mungu kwa kusikia kwa sikio, na baadaye alianza maisha ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Hizi ndizo zilizokuwa asili na mchakato ambao Ayubu alimfuata Mungu. Lakini haikujalisha ni vipi alivyomcha Mungu na kujiepusha na maovu, ni vipi ambavyo alishikilia uadilifu wake, bado Mungu alikuwa hajawahi kujitokeza kwake. Hebu tuisome kifungu hiki. Alisema, “Tazama, anapita karibu nami, na mimi simwoni: Tena anapita kwenda mbele, lakini mimi simtambui.” (Ayubu 9:11). Yale ambayo maneno haya yanasema ni kwamba Ayubu huenda alihisi Mungu karibu naye au pengine hakuhisi— lakini alikuwa hajawahi kuweza kumwona Mungu. Kunazo nyakati ambapo alifikiria Mungu akipita mbele yake au akitenda, au akimwongoza binadamu, lakini alikuwa hajawahi kujua. Mungu humjia binadamu wakati hatarajii; binadamu hajui ni lini Mungu atamjia, au ni wapi anapomjia yeye, kwa sababu binadamu hawezi kumwona Mungu, kwa hivyo, kwa binadamu Mungu amefichwa kutoka kwake.
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Biblia,
Ayubu anaelewa kazi za Mungu katika vitu vyote

Imani ya Ayubu Katika Mungu Haitikisiki kwa Sababu Mungu Amefichwa Kutoka Kwake

Katika kifungu kifuatacho ya maandiko, Ayubu anasema, “Tazama, naenda mbele, lakini hayuko huko; narudi nyuma, lakini siwezi kumwona; Katika mkono wa kushoto, anapofanya kazi, lakini siwezi kumwona: anajificha katika upande wa mkono wa kuume, hata siwezi” (Ayubu 23:8-9). Katika simulizi hii, tunajifunza kwamba katika hali alizopitia Ayubu, Mungu alikuwa amefichwa kutoka kwake wakati wote huo; Mungu alikuwa hajajitokeza waziwazi kwake yeye, na alikuwa hajamzungumzia waziwazi maneno yoyote kwake yeye, lakini katika moyo wake Ayubu alikuwa na ujasiri wa uwepo wa Mungu. Alikuwa siku zote amesadiki kwamba Mungu huenda anatembea na yeye au huenda Anatenda akiwa kando yake, na kwamba ingawaje hakuweza kumwona Mungu, Mungu alikuwa kando yake yeye akitawala mambo yake yote. Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu, lakini aliweza kuwa mkweli katika imani yake, jambo ambalo hakuna mtu yeyote aliwahi kuweza kufanya. Na kwa nini watu hawakuweza kufanya hivyo? Kwa sababu Mungu hakuongea na Ayubu, au kujitokeza kwake yeye, na kama asingekuwa amesadiki kwa kweli, asingeweza kuendelea, wala asingeweza kushikilia njia hiyo ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Je, huu si ukweli? Unahisi vipi unaposoma kumhusu Ayubu akisema maneno haya? Unahisi kwamba utimilifu na unyofu wa Ayubu, na haki yake mbele ya Mungu, ni kweli, na wala si kupiga chuku kwa upande wa Mungu? Ingawaje Mungu alimshughulikia Ayubu kwa njia sawa na watu wengine, na hakujitokeza wala kuongea na yeye, Ayubu bado alishikilia ubinadamu wake, bado alisadiki ukuu wa Mungu, na, isitoshe, mara kwa mara alitoa sadaka za kuteketezwa na kuomba mbele ya Mungu kutokana na hofu yake ya kumkosea Mungu. Katika uwezo wa Ayubu wa kumcha Mungu bila ya kuwahi kumwona Mungu, tunaona ni kiasi kipi alichopenda mambo mazuri na ni vipi imani yake ilivyokuwa thabiti na ya kweli. Hakukataa uwepo wa Mungu kwa sababu Mungu alikuwa amefichwa kutoka kwake, wala hakupoteza imani yake na kumkataa Mungu kwa sababu hakuwahi kumwona Yeye. Badala yake, katikati ya kazi fiche ya Mungu ya kutawala mambo yote, alikuwa ametambua uwepo wa Mungu na akahisi ukuu wa Mungu na Nguvu za Mungu. Hakukata tamaa katika kuwa mnyofu kwa sababu Mungu alikuwa amefichwa, wala hakuiacha njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu kwa sababu Mungu alikuwa hajawahi kujitokeza kwake yeye. Ayubu alikuwa hajawahi kuuliza kwamba Mungu aonekane waziwazi kwake ili kuthibitisha uwepo Wake, kwani alikuwa tayari ametangaza ukuu wa Mungu miongoni mwa mambo yote na alisadiki kwamba alikuwa amepata baraka na neema ambazo wengine hawakuwa wamepata. Ingawaje Mungu alibakia fiche kwake yeye, imani ya Ayubu kwa Mungu haikuwahi kutikisika. Hivyo, alivuna kile ambacho hakuna yeyote aliwahi kuvuna. Idhini ya Mungu na baraka za Mungu.

Ayubu Abariki Jina la Mungu na Wala Hafikirii Baraka au Janga

Kunayo ukweli ambao haurejelewi katu kwenye hadithi za maandiko kuhusu Ayubu, ambayo ndio itakayokuwa zingatio letu leo. Ingawaje Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu au kusikia maneno ya Mungu kwa masikio yake mwenyewe, Mungu alikuwa na nafasi katika moyo wa Ayubu. Na mwelekeo wa Ayubu kwa Mungu ulikuwa upi? Ulikuwa, kama ulivyorejelewa awali, “libarikiwe jina la Bwana.” Baraka yake kwa jina la Mungu haikuwa ya masharti, wala isiyofuzu, na bila ya sababu. Tunaona kwamba Ayubu alikuwa ameukabidhi moyo wake kwa Mungu, na kuuruhusu kudhibitiwa na Mungu; kila kitu alichofikiria, kila kitu alichoamua, na kila kitu alichopangilia katika moyo wake kilikuwa wazi kwa Mungu na wala moyo wake haukuwa umefungwa kuzuia Mungu. Moyo wake haukumpinga Mungu, na hakuwahi kuuliza Mungu kumfanyia chochote au kumpa chochote yeye, na wala hakuwa na matamanio yasiyo ya kawaida ambayo angepata chochote kutoka kwa kumwabudu Mungu. Ayubu hakuzungumzia biashara na Mungu, na wala hakutoa ombi lolote au madai yoyote kwa Mungu. Hali yake ya kusifia jina la Mungu ilikuwa kwa sababu ya nguvu kuu na mamlaka ya Mungu katika kutawala mambo yote, na haikutegemea kama alipata baraka au alipigwa na janga. Aliamini kwamba haijalishi kama Mungu anawabariki watu au analeta janga kwao, mamlaka na nguvu vyote havitabadilika, na hivyo, haikujalisha hali za mtu, jina la Mungu linafaa kusifiwa. Kwamba binadamu amebarikiwa na Mungu ni kwa sababu ya ukuu wa Mungu, na wakati janga lilipompata binadamu, hivyo, pia ni kwa sababu ya ukuu wa Mungu. Nguvu na mamlaka ya Mungu vyote vinatawala na kupangilia kila kitu cha binadamu; matukio yasiyo ya kawaida kuhusu utajiri wa binadamu ni maonyesho ya nguvu na mamlaka ya Mungu, na licha ya maoni yake mtu, jina la Mungu linafaa kusifiwa. Haya ndiyo ambayo Ayubu alipitia na kuishia kujua katika miaka ya maisha yake. Fikira na matendo yote ya Ayubu vyote vilifikia masikio ya Mungu na vikawasili mbele ya Mungu, na vikaonekana kuwa muhimu na Mungu. Mungu aliyapenda sana maarifa haya ya Ayubu na akathamini sana Ayubu kwa kuwa na moyo kama huo. Moyo huu ulisubiria amri ya Mungu siku zote, na pahali pote, na haijalishi ni muda au mahali gani ulikaribisha chochote kile kilichomsibu. Ayubu hakutoa mahitaji yoyote kwa Mungu. Kile alichohitaji kutoka kwake kilikuwa kusubiria, kukubali, kukabiliana na kutii mipangilio yote iliyotoka kwa Mungu; Ayubu alisadiki hili kuwa wajibu wake, na ndio hasa kile ambacho Mungu Alitaka. Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu wala kumsikiliza Akiongea mambo yoyote, akitoa amri zozote, akiyatoa mafundisho yoyote, au kuelekeza yeye kuhusu chochote. Kwa maneno ya leo, kwake yeye kuweza kumiliki mwelekeo kama huo kwa Mungu, wakati Mungu alikuwa hajampa nuru, mwongozo, au toleo kuhusiana na ukweli—hili lilikuwa lenye thamani sana, na kwake yeye kuonyesha mambo kama hayo kulitosha kwa Mungu, na ushuhuda wake ulipongezwa na Mungu, na kutunzwa na Mungu. Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu au kumsikia Mungu binafsi akitamka mafundisho yoyote kwake yeye, lakini kwa Mungu moyo wake na yeye mwenyewe vyote vilikuwa vyenye thamani zaidi kuliko wale watu ambao, mbele ya Mungu waliweza tu kuongea kuhusu nadharia kuu, ambao waliweza tu kujigamba na kuongea kuhusu kutoa sadaka lakini walikuwa hawajawahi kuwa na maarifa ya kweli ya Mungu na walikuwa hawajawahi kumcha Mungu kwa kweli. Kwani moyo wa Ayubu ulikuwa safi, na haukufichwa kuonekana na Mungu, na ubinadamu wake ulikuwa wenye uaminifu na ukarimu, na alipenda haki na kile kilichokuwa kizuri. Binadamu kama huyu pekee aliyemiliki moyo kama huo na ubinadamu ndiye aliyeweza kufuata njia ya Mungu, na kuwa na uwezo wa kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Binadamu kama huyo angeona ukuu wa Mungu, angeona mamlaka na nguvu Yake, na angeweza kutimiza utiifu kwa ukuu Wake na mipangilio. Binadamu tu kama huyo ndiye angeweza kusifu jina la Mungu kwa kweli. Hii ni kwa sababu hakuangalia kama Mungu angembariki yeye au Angemletea janga, kwa sababu alijua kwamba kila kitu kinadhibitiwa na mkono wa Mungu, na kwamba binadamu kuwa na wasiwasi ni ishara ya ujinga, kutojua, na kutoweza kufikiria vyema, kuwa na shaka katika ukweli wa ukuu wa Mungu juu ya mambo yote, na ya kutomcha Mungu. Maarifa ya Ayubu hasa ndiyo ambayo Mungu alitaka. Hivyo basi, Ayubu alikuwa na maarifa makubwa ya kinadharia kumhusu Mungu kuliko wewe? Kwa sababu kazi na matamko ya Mungu wakati huo yalikuwa machache, halikuwa jambo rahisi kutimiza maarifa ya Mungu. Mafanikio kama hayo ya Ayubu hayakukuwa jambo dogo. Alikuwa hajapitia kazi ya Mungu wala hakuwahi kusikia Mungu akiongea, au kuuona uso wa Mungu. Kwamba aliweza kuwa na mwelekeo kama huo kwa Mungu yalikuwa ni hasa matokeo yaliyoonyesha ubinadamu wake na ufuatiliaji wake wa kibinafsi, ubinadamu na ufuatiliaji ambao haujamilikiwa na watu leo. Hivyo, katika enzi hiyo, Mungu alisema, “hakuna kama yeye duniani, mtu mkamilifu na aliye mnyoofu mwenye kumcha Mungu, na kuuepuka uovu.” Katika enzi hiyo, Mungu alikuwa tayari amefanya ukadiriaji wake Ayubu, na alikuwa amefikia hitimisho fulani. Ungekuwa ukweli zaidi kwa kiasi kipi hii leo?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Biblia,
                                           Ayubu anaelewa kazi za Mungu katika vitu vyote - usiku

Ingawaje Mungu Amefichwa Kutoka kwa Binadamu, Matendo Yake Miongoni mwa Mambo Yote Yanatosha Binadamu Kumjua Yeye

Ayubu alikuwa hajauona uso wa Mungu, wala kusikia matamshi yaliyoongelewa na Mungu, isitoshe yeye mwenyewe binafsi alikuwa hajapitia kazi ya Mungu, lakini kumcha kwake Mungu na ushuhuda aliyokuwa nao wakati wa majaribio kunashuhudiwa na kila mmoja, na kunapendwa, kunafurahiwa, na kupongezwa na Mungu na watu wakayaonea wivu na kuvutiwa nayo, na vilevile, wakaimba nyimbo zao za sifa. Hakukuwepo chochote kikubwa au kisicho cha kawaida kuhusu maisha yake: Kama vile tu mtu yeyote wa kawaida, aliishi maisha yasiyo ya kina, akienda kufanya kazi wakati wa macheo na akirudi nyumbani kupumzika wakati wa magharibi. Tofauti ni kwamba wakati wa miongo hii mbalimbali isiyo ya kina, alipata maono kuhusu njia ya Mungu, na akatambua na kuelewa nguvu kubwa na ukuu wa Mungu, kuliko mtu yeyote mwingine.. Hakuwa mwerevu zaidi kuliko mtu yeyote wa kawaida, maisha yake hayakukuwa sanasana yenye ushupavu, wala, zaidi, yeye hakuwa na mbinu maalum zisizoonekana. Kile alichomiliki, hata hivyo, kilikuwa ni hulka iliyokuwa na uaminifu, upole, unyofu, na hulka iliyopenda kutopendelea na haki, na iliyopenda mambo mazuri—hakuna kati ya haya aliyomiliki yalimilikiwa na watu wa kawaida wengi. Alitofautisha kati ya upendo na chuki, alikuwa na hisia ya haki, hakukubali kushindwa na alikuwa hakati tamaa, na alikuwa mwenye bidii katika fikira zake, na hivyo basi wakati wake usio wa kina duniani aliyaona mambo yote yasiyo ya kawaida ambayo Mungu alikuwa amefanya, na akauona ukubwa, utakatifu, na uhaki wa Mungu, aliona kujali kwa Mungu, neema yake, na ulinzi wake wa binadamu, na kuona utukufu na mamlaka ya Mungu mwenye mamlaka zaidi. Sababu ya kwanza iliyomfanya Ayubu kuweza kupata mambo haya yaliyokuwa zaidi ya mtu yeyote wa kawaida ilikuwa ni kwa sababu alikuwa na moyo safi, na moyo wake ulimilikiwa na Mungu na kuongozwa na Muumba. Sababu ya pili ilikuwa ni ufuatiliaji wake: ufuatiliaji wake wa kuwa maasumu, na mtimilifu, na mtu aliyekubaliana na mapenzi ya Mbinguni, aliyependwa na Mungu, na kujiepusha na uovu. Ayubu alimiliki na kufuata mambo haya huku akiwa hawezi kumwona Mungu au kusikia maneno ya Mungu; ingawaje alikuwa hajawahi kumwona Mungu, alikuwa amejua mbinu ambazo Mungu alitawala mambo yote, na kuelewa hekima ambayo Mungu anatumia ili kufanya hivyo. Ingawaje alikuwa hajawahi kusikia maneno ambayo yalikuwa yametamkwa na Mungu, Ayubu alijua kwamba matendo ya kutuna binadamu na kuchukua kutoka kwa binadamu yote yalitoka kwa Mungu. Ingawaje miaka ya maisha yake haikuwa tofauti na ile ya mtu wa kawaida, hakuruhusu ukosefu wa kina hiki cha maisha yake kuathiri maarifa yake ya ukuu wa Mungu juu ya mambo yote, au kuathiri kufuata kwake kwa njia za kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Katika macho yake, sheria za mambo yote zilijaa matendo ya Mungu na ukuu wa Mungu ungeweza kuonekana katika sehemu yoyote ya maisha ya mtu. Alikuwa hajamwona Mungu lakini aliweza kutambua kwamba Matendo ya Mungu yako kila pahali, na katika wakati wake usiokuwa wa kina duniani, katika kila kona ya maisha yake aliweza kuona na kutambua matendo ya kipekee na ya maajabu ya Mungu, na aliweza kuona mipangilio ya ajabu ya Mungu. Ufiche na kimya cha Mungu hakikuzuia utambuzi wa Ayubu wa matendo ya Mungu, wala hakikuathiri maarifa yake kuhusu ukuu wa Mungu juu ya mambo yote. Maisha yake yalikuwa utambuzi wa ukuu na mipangilio ya mungu, ambaye amefichwa miongoni mwa mambo yote, katika maisha yake ya kila siku. Katika maisha yake ya kila siku alisikia pia na kuelewa sauti na maneno ya moyoni, ambayo Mungu, akiwa kimya miongoni mwa mambo yote, alionyesha kupitia kwa kutawala Kwake kwa sheria ya mambo yote. Unaona, basi, kwamba kama watu wanao ubinadamu sawa na ufuatiliaji kama Ayubu, basi wanaweza kupata utambuzi na maarifa sawa kama Ayubu, na kupata ule uelewa na maarifa sawa ya ukuu wa Mungu juu ya mambo yote kama Ayubu. Mungu alikuwa hajajionyesha kwa Ayubu au kuongea na yeye, lakini Ayubu aliweza kuwa mtimilifu na mnyofu, na pia aliweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kwa maneno mengine, bila ya Mungu kuweza kujitokeza kwa au kuongea na binadamu, matendo ya Mungu miongoni mwa mambo yote na ukuu Wake juu ya mambo yote ni tosha kwa binadamu ili kuweza kuwa na ufahamu wa uwepo wa Mungu, nguvu na mamlaka ya Mungu ni tosha kumfanya binadamu huyu kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kwa sababu binadamu wa kawaida kama vile Ayubu aliweza kutimiza hali ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, basi kila mtu wa kawaida anayemfuata Mungu anafaa pia kuweza kufanya hivyo. Ingawaje maneno haya yanaweza kusikika ni kana kwamba ni hitimisho ya kimantiki. Hii haikiuki sheria ya mambo. Bado ukweli haujalingana na matarajio: Kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, kunaweza kuonekana, ni hifadhi ya Ayubu na Ayubu pekee. Kwa kutaja “kumcha Mungu na kujiepusha na maovu,” watu hufikiria kwamba hii inafaa tu kufanywa na Ayubu, ni kana kwamba njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu ilikuwa imebandikwa jina la Ayubu na haikuhusika na watu wengine. Sababu ya hii ni wazi: Kwa sababu Ayubu tu ndiye aliyemiliki hulka iliyokuwa na uaminifu, ukarimu, na nyofu, na iliyopenda kutopendelea na haki na mambo yaliyokuwa mazuri, hivyo ni Ayubu tu ambaye angeweza kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Lazima nyinyi wote mkuwe mmeelewa matokeo hapa—ambayo ni kwamba kwa sababu hakuna yule anayemiliki ubinadamu ulio na uaminifu, ukarimu, na unyofu, na ule ambao unapenda kutopendelea na haki na ule ambao ni mzuri, hakuna mtu anayeweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, na hivyo hawezi kupata furaha ya Mungu au kusimama imara katikati ya majaribio. Ambayo pia inamaanisha kwamba, bila kujumuisha Ayubu, watu wote wangali wamefungwa na kunaswa na Shetani, wote wanashtakiwa, wanashambuliwa, na kudhulumiwa na Shetani, na wale ambao Shetani anajaribu kumeza, na wote hawana uhuru, ni wafungwa ambao wametekwa nyara na Shetani.

Kama Moyo wa Binadamu Unao Uadui na Mungu, Anawezaje Kumcha Mungu na Kujiepusha na Maovu

Kwa sababu watu wa leo hawamiliki ubinadamu sawa na Ayubu, na je kiini cha asili yao, na mwelekeo wao kwa Mungu? Wanamcha Mungu? Wanajiepusha na maovu? Wale wasiomcha Mungu na kujiepusha na maovu wanaweza kujumuishwa tu kwa maneno manne: Ni adui za Mungu. Mara nyingi mnasema maneno haya, lakini hamjawahi kujua maana yake halisi. Maneno “ni adui za Mungu” yanayo kiini ndani yake: Hayasemi kwamba Mungu anamuona binadamu kama adui, lakini kwamba binadamu anamuona Mungu kama adui. Kwanza, wakati watu wanapoanza kusadiki Mungu, ni nani asiyekuwa na nia, motisha na maono yake binafsi? Ingawaje sehemu moja yao inasadiki uwepo wa Mungu, na imeona uwepo wa Mungu, imani yao katika Mungu bado inayo hiyo motisha, na nia yao kuu ya kusadiki Mungu ni kupokea baraka Zake na mambo wanayotaka. Katika uzoefu wa watu katika maisha yao, mara nyingi wanafikiria ndani yao, nimetoa familia yangu na ajira yangu kwa Mungu, na Amenipatia nini? Lazima niongezee na kuthibitisha haya—je, nimepokea baraka zozote hivi majuzi? Nimetoa mengi sana wakati huu, nimekimbia na kukimbia na kuteswa sana—je Mungu amenipa ahadi zozote baada ya haya? Je Amekumbuka matendo yangu mazuri? Mwisho wangu utakuwa vipi? Ninaweza kuzipokea baraka za Mungu? … Kila mtu kila wakati, na mara nyingi hufanya hesabu kama hizi ndani ya mioyo yao, na wao wanatoa madai yao kwa Mungu yanayoonyesha motisha yao na malengo na mipango. Hivi ni kusema, ndani ya moyo wake binadamu siku zote anamweka Mungu majaribuni, siku zote anaunda njama kumhusu Mungu, na kila wakati anabishana na Mungu kuhusu kesi yake na kujaribu kumfanya Mungu kutoa kauli, ili aweze kuona kama Mungu anaweza kumpa kile anachotaka au hawezi. Wakati huohuo akimfuata Mungu, binadamu hamchukulii mungu kama Mungu. Siku zote amejaribu kufanya mipango na Mungu, akitoa madai bila kusita kwake Yeye na hata akimsukuma Yeye kwa kila hatua, akijaribu kupiga hatua ya maili licha ya kupewa inchi moja. Wakati huohuo akijaribu kuunda mipango na Mungu, binadamu pia anabishana na Yeye, na wapo hata watu ambao, wakati majaribio yanapowapata au wanapojipata katika hali ya kuteketea, mara nyingi wanakuwa wanyonge, wananyamaza na kuzembea katika kazi yao, na wanajaa malalamiko kuhusu Mungu. Tangu wakati ule alipoanza kusadiki Mungu, binadamu amemchukulia Mungu kama alama ya pembe inayoonyesha wingi wa neema, kisu cha Kijeshi cha Uswisi, na amejichukulia yeye mwenyewe kuwa mdaiwa mkubwa zaidi wa Mungu, ni kana kwamba kujaribu kupata baraka na ahadi kutoka kwa Mungu ni haki yake ya asili na jukumu, huku jukumu la Mungu likiwa ni kulinda na kutunza binadamu na kumtoshelezea. Huu ndio uelewa wa kimsingi wa “imani katika Mungu” wa wale wote wanaosadiki Mungu, na uelewa wao wa kina zaidi wa dhana ya imani katika Mungu. Kutoka kwenye kiini cha asili ya binadamu hadi katika ufuatiliaji wake wa kibinafsi, hakuna kitu chochote kinachohusiana na kumcha Mungu. Nia ya binadamu kwa kusadiki Mungu huenda isiwe na uhusiano na kuabudu Mungu. Hivi ni kusema kwamba, binadamu hajawahi kufikiria wala kuelewa kwamba imani katika Mungu inahitaji kumcha Mungu, na kumwabudu Mungu. Kwa mujibu wa haya yote, kiini cha binadamu ni wazi. Na kiini hicho ni nini? Ni kwamba moyo wa binadamu una kijicho, unabeba udanganyifu na ujanja, haupendi mambo ya kutopendelea na haki, au kile kilicho kizuri, nao ni wenye kuleta dharau na ulafi. Moyo wa binadamu usingeweza kumzuia Mungu zaidi, hajaupatia Mungu kamwe. Mungu hajawahi kuona moyo wa kweli wa binadamu, wala hajawahi kuabudiwa na binadamu. Haijalishi ni gharama gani ambayo Mungu amelipia, au ni kiasi kipi cha kazi Anachofanya, au ni kiwango kipi Anachompa binadamu, binadamu anabakia yule asiyeona hayo yote, na hajali. Binadamu hajawahi kumpa Mungu moyo wake, anataka tu kujali moyo wake wenyewe, kufanya uamuzi wake mwenyewe—mada madogo ambayo ni kwamba binadamu hataki kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, au kutii ukuu na mipangilio ya Mungu, wala hataki kumwabudu Mungu kama Mungu. Hivyo ndivyo mwanadamu anavyozungukwa na hali mbalimbali leo. Sasa hebu tumwangalie tena Ayubu. Kwanza kabisa, aliweza kufanya mpango na Mungu? Alikuwa na nia zozote fiche katika kushikilia njia ile ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu? Wakati huo, je, Mungu alikuwa ameongea na yeyote kuhusu mwisho ujao? Wakati huo, Mungu alikuwa hajatoa ahadi zozote kwa yeyote kuhusu mwisho, na ilikuwa katika hali hii ndipo Ayubu aliweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Je, watu wa leo wanaweza kulinganishwa na Ayubu? Kunazo tofauti nyingi, wanapatikana katika nyanja tofauti. Ingawaje Ayubu hakuwa na maarifa mengi ya Mungu, alikuwa ameutoa moyo wake kwa Mungu na ulimilikiwa na Mungu. Hakuwahi kupanga chochote na Mungu, na hakuwa na matamanio yoyote ya zaidi au madai kwa Mungu; badala yake, alisadiki kwamba “Bwana alitoa na Bwana atatwaa.” Hii ndiyo alikuwa ameona na kupata kutokana na kushikilia ukweli njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu wakati wa miaka yake mingi ya maisha. Vilevile, alikuwa amepata matokeo ya “Vipi? Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya?” Sentensi hizi mbili ndizo ambazo alikuwa ameona na akaja kujua kutokana na mwelekeo wake wa utiifu kwa Mungu katika uzoefu wa maisha yake, na ndizo pia zilikuwa silaha zake zenye nguvu zaidi ambazo alitumia akashinda majaribio ya Shetani, na msingi wa yeye kusimama imara katika ushuhuda kwa Mungu. Wakati huu, bado unamwona Ayubu kama mtu mzuri? Je unatumaini kuwa mtu kama huyo? Unaogopa kupitia majaribio ya Shetani? Unaamua kumwomba Mungu ili aweze kukupitisha kwenye majaribio kama haya ya Ayubu? Bila shaka watu wengi wasingethubutu kuombea mambo kama hayo. Ni wazi, basi, kwamba imani yako ni ndogo ya kusikitiwa; ikilinganishwa na ile ya Ayubu, imani yako haistahili kutajwa. Nyinyi ndio adui za Mungu, hamchi Mungu, hamwezi kusimama imara katika ushuhuda kwa Mungu, na hamwezi kushangilia dhidi ya mashambulio, mashtaka, na majaribio ya Shetani. Ni nini kinachowafanya kufuzu ili kupokea ahadi za Mungu? Baada ya kusikia hadithi ya Ayubu na kuelewa nia ya Mungu katika kuokoa binadamu, na maana ya wokovu wa binadamu, je mnayo sasa imani ya kukubali majaribio sawa na ya Ayubu? Hamfai kuwa na kusudio kidogo, ili mjiruhusu kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu?

Msiwe na Wasiwasi Wowote Kuhusu Majaribio ya Mungu

Baada ya kuupokea ushuhuda kutoka kwa Ayubu kufuatia mwisho wa majaribio yake, Mungu aliamua kwamba angepata kundi au zaidi ya kundi—la watu kama Ayubu, ilhali aliamua kutowahi tena kumruhusu Shetani kushambulia au kunyanyasa mtu yeyote mwingine kwa kutumia mbinu ambazo alikuwa amemjaribu, akamshambulia na kumnyanyasa Ayubu, kwa kucheza karata na Mungu; Mungu hakumruhusu Shetani tena kufanya mambo kama hayo kwa binadamu ambaye ni mnyonge, mjinga, na asiyejua—ilikuwa tosha kwamba Shetani alikuwa amemjaribu Ayubu! Kutomruhusu Shetani kuwanyanyasa watu vyovyote anavyotaka ndiyo rehema ya Mungu. Kwa Mungu, ilitosha kwamba Ayubu alikuwa ameteseka majaribio na minyanyaso ya Shetani. Mungu hakumruhusu Shetani tena kufanya mambo kama hayo, kwani maisha na kila kitu cha watu wanaomfuata Mungu yanatawaliwa na kupangiliwa na Mungu, na Shetani hastahili kutawala waliochaguliwa na Mungu apendavyo—unafaa kuwa wazi kuhusu hoja hii! Mungu anajali kuhusu unyonge wa binadamu, na kuelewa ujinga na kutojua kwake. Ingawaje, ili binadamu aweze kuokolewa kabisa, lazima Mungu amkabidhi kwa Shetani, Mungu hayuko radhi kumwona tena binadamu akichezewa tena kama kikaragosi na Shetani na kunyanyaswa na Shetani na hataki kumwona binadamu siku zote akiteseka. Binadamu aliumbwa na Mungu, na inaeleweka kikamilifu kwamba Mungu anatawala na anapangilia kila kitu cha binadamu; hili ni jukumu la Mungu na mamlaka ambayo Mungu anatawala mambo yote! Mungu hamruhusu Shetani kunyanyasa na kutumia vibaya binadamu apendavyo, Hamruhusu Shetani kutumia mbinu mbalimbali za kumpotosha binadamu, na vilevile, Hamruhusu Shetani kuingilia kati ukuu wa Mungu wa binadamu, wala Hamruhusu Shetani kukanyaga na kuangamiza Sheria ambazo Mungu anatawalia mambo yote, kutosema chochote kuhusu kazi kuu ya Mungu ya kusimamia na kuwaokoa wanadamu! Wale ambao Mungu anataka kuokoa na wale ambao wanaweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu, ndio msingi na hali halisi ya kazi ya Mungu ya mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita, pamoja na bei ya jitihada zake katika kazi yake ya miaka elfu sita. Mungu anawezaje kuwakabidhi watu hawa kwa Shetani hivihivi.
Watu mara nyingi wanakuwa na wasiwasi kuhusu na wana uoga ya majaribio ya Mungu, ilhali siku zote wanaishi katika mtego wa Shetani na kuishi katika maeneo hatari ambapo wanashambuliwa na kunyanyaswa na Shetani—lakini hawaogopi na hawashangazwi. Nini kinaendelea? Imani ya binadamu katika Mungu ni finyu mno kwa mambo anayoweza kuona. Hana shukrani hata chembe kuhusu upendo na kujali kwa Mungu kwa binadamu, au wema Wake na utiliaji maanani kwa binadamu. Lakini kwa hofu na wasiwasi kidogo kuhusu majaribio, hukumu na kuadibu kwa Mungu na adhama na hasira Yake, binadamu hana hata chembe cha uelewa wa nia nzuri za Mungu. Kwa kutajwa kwa majaribio, watu wanahisi ni kana kwamba Mungu anazo nia nyingine zisizo wazi na hata baadhi wanasadiki kwamba Mungu ana mipango ya maovu, wasijue hata kile ambacho Mungu atawafanyia; hivyo, wakati huohuo kutaka kuwa watiifu kabisa kwa ukuu na mipangilio ya Mungu, wanafanya kila wawezalo kuzuia na kupinga ukuu wa Mungu juu ya binadamu na mipangilio kwa binadamu, kwani wanasadiki kwamba kama hawatakuwa makini watapotoshwa na Mungu, na kama hawatakuwa na mshikilio thabiti ya hatima yao binafsi, basi kila kitu walichonacho kinaweza kuchukuliwa na Mungu, na maisha yao huenda hata yakaisha. Binadamu yumo kwenye kambi la Shetani, lakini hawi na wasiwasi kamwe kuhusu kunyanyaswa na Shetani, na ananyanyaswa na Shetani lakini haogopi kamwe kutekwa nyara na Shetani. Siku zote anasema kwamba anaukubali wokovu wa Mungu, ilhali hajawahi kumwamini Mungu au kusadiki kwamba Mungu atamwokoa kwa kweli binadamu kutoka kwenye makucha ya Shetani. Kama, sawa na Ayubu, binadamu anaweza kunyenyekea kwa mipango na mipangilio ya Mungu na anaweza kuitoa nafsi nzima kwa mikono ya Mungu, basi hatima ya binadamu haitakuwa sawa na ile ya Ayubu—kupokea baraka za Mungu? Kama binadamu anaweza kukubali na kunyenyekea Sheria ya Mungu, nini kipo cha kupoteza? Na hivyo Napendekeza kwamba uwe makinifu kwa vitendo vyako, utahadhari na kila kitu ambacho kiko karibu kukufanyikia wewe. Usiwe wa pupa au msukumo na umshughulikie Mungu na watu, masuala, vitu alivyokupangilia kwa namna mshawasha unavyokupeleka, au kulingana na nafsi yako ya kiasili au kufikiria na dhana zako; lazima uwe mmakinifu katika vitendo vyako na lazima uombe na utafute zaidi, kuepuka kuchochea hasira ya Mungu. Kumbuka hili!
Kisha, tutaangalia vile Ayubu alikuwa baada ya majaribio yake.
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili 
Yaliyopendekezwa: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni