Alhamisi, 25 Januari 2018

Swahili Christian Movie "Maskani Yangu Yako Wapi" | Mungu ni Kimbilio la Nafsi Yangu


Swahili Christian Movie "Maskani Yangu Yako Wapi" | Mungu ni Kimbilio la Nafsi Yangu


Utambulisho

    Wazazi wa Wenya walitengana alipokuwa na umri wa miaka miwili, na baada ya hapo aliishi na baba yake na mama wa kambo. Mamake wa kambo hakuweza kumvumilia na daima alikuwa akibishana na baba yake. Alikuwa na chaguo dogo — alilazimika kumpeleka Wenya nyumbani kwa mama yake, lakini mama yake alilenga kikamilifu kuendesha biashara yake na hakuwa na muda wa kumtunza Wenya, hivyo mara nyingi alipelekwa nyumbani kwa jamaa na marafiki zake kupata ulezi. Baada ya miaka mingi sana ya maisha ya kutunzwa na walezi, Wenya alihisi upweke na asiyejiweza, na alitamani ukunjufu wa nyumbani. Ni wakati tu ambapo baba yake na mama wa kambo walitangua ndoa ndipo alirudi upande wa baba yake, na kuanzia hapo na kuendelea alikuwa na nyumbani, wakati mzuri au mbaya. Mara Wenya alipokua, alikuwa mwangalifu na mtiifu sana, na alisoma kwa bidii. Lakini wakati ule ule alipokuwa akitia bidii ili kujiandaa kwa ajili ya mitihani yake ya kuingilia chuo, msiba ulimfika: mama yake alikuwa na hemoraji ya ubongo na akapooza na kuwa mgonjwa kitandani. Babake wa kambo alimtelekeza mama yake na hata kuchukua udhibiti juu ya mali yake yote, na kisha babake akapelekwa hospitalini kwa ajili ya saratani ya ini... Wenya hangeweza kabisa kujitwisha mzigo wa kaya, hivyo yote ambayo angeweza kufanya ni kuwasihi jamaa na marafiki, lakini alikataliwa. …
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ukweli,
Maskani Yangu Yako Wapi

    Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni