Jumatatu, 1 Januari 2018

Umeme wa Mashariki | Matunda Machungu ya Kiburi | kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa,
Umeme wa Mashariki | Matunda Machungu ya Kiburi

17. Umeme wa MasharikiMatunda Machungu ya Kiburi

Hu Qing Jijini Suzhou, Mkoani Anhui
Nilipoona maneno ya Mungu yakisema: “Wale miongoni mwenu ambao huhudumu kama viongozi daima hutaka kuwa na ubunifu mkubwa, kuwa wazuri kuliko wengine, kupata hila mpya ili Mungu aweze kuona jinsi kweli mlivyo viongozi wakuu. … Nyinyi daima hutaka kuringa; si huu ni ufunuo kwa usahihi wa asili ya kiburi?” (“Bila Ukweli Ni Rahisi Kumkosea Mungu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo), Nilifikiri mwenyewe: Nani ana ujasiri kama huo kujaribu kupata ujanja mpya ya ubunifu? Nani hajui kuwa tabia ya Mungu haistahimili kosa la mwanadamu? Bila shaka siwezi kuthubutu! Mimi binafsi niliamini kuwa nilikuwa na moyo wa kumcha Mungu, na katika kazi yangu sikuthubutu kujaribu kutafuta mbinu. Hata hivyo, ilikuwa tu katika ufunuo wa Mungu wa ukweli ndio nilitambua kuwa kujaribu kutafuta mbinu mpya sio kile mtu huthubutu au hathubutu kufanya—kunaamuliwa kabisa na asili ya kiburi.
Si muda mrefu uliopita, niligundua kuwa kulikuwa na kanisa lilikuwa na kiongozi ambaye hakuwa na uwezo wa kutosha. Alilala wakati wa mikusanyiko na hakuwa na asili ya ukarimu, wakati mbia wake alikuwa na majukumu mengi. Kwa hiyo, nilitaka kubadilisha kiongozi huyu wa kanisa na kuruhusu mbia wake kufanya kazi ya kiongozi wa kanisa. Hata hivyo, nilikuwa na wasiwasi kuwa hili lingesababisha kiongozi wa kanisa kuwa hasi, dhaifu, na kuacha imani yake, au kuwa angevuruga mambo katika kanisa. Baada ya kutafakari sana, nilifikiria juu ya "mpango wa kijanja." Ningemfanya mbia wake kuchukua mawanda nzima ya kazi kwa siri; kila kitu kilichopangwa na kanisa kingeshughulikiwa na mbia wake, na kiongozi wa kanisa hangekuwa chochote bali mkubwa wa jina tu. Hivyo sikuwa nimemtafuta Mungu wala kutazama mipangilio ya kazi na kanuni za kazi. Nilikuwa nimefanya jambo hili tu baada ya kumwambia mbia wa kiongozi wa wilaya na mhubiri wa wilaya. Baada ya hiyo, nilijipongeza sana, nikiamini kuwa nilikuwa mwerevu sana na nilikuwa na busara kabisa katika kazi yangu. Nilifikiria: Ikiwa kiongozi angejua kuhusu hili, bila shaka angesema kuwa nina uwezo katika kazi yangu, na labda hata mwishowe angenipandisha cheo. Lakini sikuwa nimefikiria kuwa nilipomwambia kiongozi kuhusu hili, angesema: "Huyu ni wewe ukijaribu kutafuta ujanja mpya. Ni wapi katika mipangilio ya kazi ilisemwa kuwa ungeweza kufanya hivi? Kiongozi asiye na uwezo wa kutosha anaweza kubadilishwa, lakini hatuwezi kufanya kazi kulingana na mapenzi yetu wenyewe na kuweka kando kanuni za kanisa. Huu ni upinzani mkali dhidi ya Mungu. …” Baada ya kusikia mawasiliano haya kutoka kwa kiongozi, nilishtuka. Kamwe kabisa sikuwahi kufikiri kuwa ningejaribu kutafuta ujanja mpya bila kujua. Nilichoamini kuwa "mpango wa kijanja" kwa kweli ulikuwa ni upinzani mkali dhidi ya Mungu, na kweli nilikuwa na aibu sana wakati nilikabiliwa ukweli. Wakati huo, sikuwa na budi ila kufikiria matamko ya Mungu: “Kwa mfano, kama una kiburi na majivuno ndani mwako, haitawezekana kutomkataa Mungu, lakini badala yake utafanywa kumkataa. Hutalifanya kimakusudi; utalifanya chini ya utawala wa asili yako ya kiburi na majivuno. Kiburi na majivuno yako vitakufanya umdharau Mungu, vitakufanya umwone Mungu kuwa asiyefaa …” (“Kwa Kutafuta Ukweli Tu Ndio Unaweza Kupata Mabadiliko Katika Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Ilikuwa kweli. Nilipokabiliwa na suala hili sikuwa nimemtafuta Mungu, wala sikulifikiri kupitia kanuni za kanisa. Nilikuwa nimetenda tu kulingana na mapenzi yangu. Niliona asili yangu ya kiburi na majivuno, kwamba sikuwa na moyo wa kumcha Mungu, na kuwa Mungu hakuwa na nafasi katika moyo wangu. Ni wakati huo tu ndipo nilipogundua kuwa kutafuta ujanja mpya hakukuwa kitu ambacho nilithubutu au sikuthubutu kufanya, lakini kilikuwa kitu kilichoamuliwa na asili yangu ya kiburi. Ikiwa singetambua asili yangu ya kiburi, singeweza kamwe kujielewa. Siku moja pengine nitaweza hata kufanya kitu kumpinga Mungu ambacho kitamfanya Ahisi maudhi na chuki. Ni wakati huo tu ndio niliona kuwa kumtumikia Mungu sio jambo rahisi. Ikiwa sina ukweli, ikiwa hakuna mabadiliko katika tabia, ikiwa sitambui asili yangu ya kiburi, ningeweza kuikosea tabia ya Mungu bila kujua. Hiyo kwa hakika ni hatari sana! Kwa sababu ya nuru ya Mungu, nilielewa kutokana na tukio hili ni kwa nini nyumba ya Mungu mara kwa mara imetutaka kufanya kazi kulingana na mipangilio ya kazi na kanuni. Ni kwa sababu asili ya mwanadamu daima ni yenye kiburi na sisi sote tunatafuta kujigamba, "kufunua" uwezo wetu ili Mungu aone, kwa hivyo mara nyingi tunampinga Mungu na kuikosea tabia Yake. Ni kwa kufanya kazi kwa uaminifu tu kulingana na mipangilio ya kazi ndio tunaweza kujilinda.
Ee Mungu! Asante kwa kufunua asili yangu ya kiburi na majivuno. Kuanzia siku hii na kuendelea, hakika nitachukulia hili kama onyo na kuweka juhudi zaidi katika kujua asili yangu. Nitafanya kazi hasa kulingana na mipangilio ya kazi. Kwa kweli nitakuwa mtu mwenye mantiki, anayezingatia kanuni, na aliye na moyo wa uchaji Kwako.
                         kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni