Jumatano, 7 Februari 2018

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III | 3. Mfano wa Kondoo Aliyepotea

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu,
Mfano wa Kondoo Aliyepotea

Umeme wa Mashariki | 3. Mfano wa Kondoo Aliyepotea

(Mat 18:12-14) Mnaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia moja, na mmoja wao apotee, je, hawaachi wale tisini na tisa, aende milimani, na kumtafuta yule aliyepotea? Na iwapo atapata kumwona, amini nawaambieni, anamfurahia huyo kondoo mmoja zaidi, kuliko wale tisini na tisa ambao hawakupotea. Vivyo hivyo sio mapenzi ya Baba yenu aliye mbinguni, kwamba mmoja wa wadogo hawa aangamie.
Mwenyezi Mungu alisema, Hii ni sitiari—unapata hisia gani kutoka katika dondoo hii? Namna ambavyo sitiari hii inaelezwa inatumia mbinu za lugha katika lugha ya binadamu; ni kitu kilicho ndani ya mawanda ya maarifa ya binadamu. Kama Mungu angekuwa amesema kitu kinachofanana katika Enzi ya Sheria, watu wangehisi kwamba hakikuambatana na Alichokuwa Mungu , lakini wakati Mwana wa Adamu alivyoonyesha ufahamu huu katika Enzi ya Neema, ilionekana ya kufariji, yenye uzuri, na iliyo karibu kwa watu. Wakati Mungu alipokuwa mwili, wakati Alipoonekana katika umbo la binadamu, Alitumia sitiari inayofaa sana kuonyeshakuonyesha sauti Yake katika binadamu. Sauti hii iliwakilisha sauti binafsi ya Mungu na kazi Aliyotaka kufanya katika enzi hiyo. Pia iliwakilisha mtazamo ambao Mungu alikuwa nao kwa watu katika Enzi ya Neema. Tukiangalia kutoka kwa mtazamo wa mwelekeo wa Mungu kwa watu, Alimfananisha kila mtu na kondoo. Kama kondoo amepotea, Atafanya kila awezalo ili kumpata. Hii inawakilisha kanuni ya kazi ya Mungu miongoni mwa wanadamu wakati huu katika mwili. Mungu aliutumia mfano huu kufafanua uamuzi na mwelekeo Wake katika kazi hiyo. Haya ndiyo yaliyokuwa manufaa ya Mungu kuwa mwili: Angeweza kutumia vizuri maarifa ya mwanadamu na kutumia lugha ya binadamu kuongea na watu, kuonyesha mapenzi Yake. Aliewalezea au “aliwatafsiria” binadamu lugha Yake ya maana sana, ya kiungu ambayo watu walipata ugumu kuelewa kupitia lugha ya binadamu, kwa njia ya kibinadamu. Hii iliwasaidia watu kuelewa mapenzi Yake na kujua kile Alichotaka kufanya. Angeweza pia kuwa na mazungumzo na watu kutoka katika mtazamo wa kibinadamu, kwa kutumia lugha ya kibinadamu, na kuwasiliana na watu kwa njia waliyoelewa. Aliweza pia kuongea na kufanya kazi kwa kutumia lugha na maarifa ya kibinadamu ili watu wangeweza kuhisi wema na ukaribu wa Mungu, ili wangeweza kuuona moyo Wake. Unaona nini katika haya? Kwamba hakuna kuzuiliwa katika maneno na vitendo vya Mungu? Namna watu wanavyoona, hakuna njia ambayo Mungu angetumia maarifa ya kibinadamu, lugha, au njia za kuongea ili kuzungumza kuhusu kile ambacho Mungu Mwenyewe alitaka kusema, kazi Aliyotaka kufanya, au kuonyesha mapenzi Yake mwenyewe; huku ni kufikiria ambako si sahihi. Mungu alitumia aina hii ya sitiari ili watu wangeweza kuhisi ule uhalisi na uaminifu wa Mungu, na kuona mwelekeo Wake kwa watu katika kipindi hicho cha muda. Mfano huu uliwazindua watu waliokuwa wakiishi chini ya sheria kwa muda mrefu kutoka katika ndoto, na vilevile uliweza kuhemsha kizazi baada ya kizazi cha watu walioishi katika Enzi ya Neema. Kwa kuisoma dondoo ya mfano huu, watu wanajua uaminifu wa Mungu katika kumwokoa mwanadamu na wanaelewa uzito wa mwanadamu katika moyo Wake.
Hebu tuangalie kwa mara nyingine sentensi ya mwisho katika dondoo hii: “Vivyo hivyo sio mapenzi ya Baba yenu aliye mbinguni kwamba mmoja wa wadogo hawa aangamie.” Haya yalikuwa maneno binafsi ya Bwana Yesu, au yalikuwa maneno ya Baba Yake aliye mbinguni? Kwa juujuu, yaonekana alikuwa Bwana Yesu akiongea, lakini mapenzi Yake yanawakilisha mapenzi ya Mungu Mwenyewe, na ndio maana Akasema: “Vivyo hivyo sio mapenzi ya Baba yenu aliye mbinguni kwamba mmoja wa wadogo hawa aangamie.” Watu wakati huo walimtambua tu Baba aliye mbinguni kama Mungu, na mtu huyu waliyeona mbele ya macho yao alikuwa ametumwa tu na Yeye, na hakuweza kuwakilisha Baba aliye mbinguni. Ndiyo maana Bwana Yesu alilazimika kusema hivyo vilevile, ili waweze kuhisi kwa kweli mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu, na kuhisi ule uhalali na usahihi wa kile Alichosema. Hata ingawa jambo hili lilikuwa jepesi kusema, lilikuwa lenye utunzaji mwingi na lilifichua unyenyekevu na ufiche wa Bwana Yesu. Bila kujali kama Mungu alikuwa mwili au Alifanya kazi katika himaya ya kiroho, Aliujua moyo wa binadamu kwa njia bora zaidi, na Alielewa kwa njia bora zaidi kile watu wAlichohitaji, Alijua ni nini watu walikuwa na wasiwasi kuhusu, na kile kilichowakanganya, hivyo Akaongeza mstari huu. Mstari huu uliangazia tatizo lililofichika ndani ya mwanadamu: Watu hawakuamini kile Mwana wa Adamu alisema, hivi ni kusema kwamba, wakati Bwana Yesu alipokuwa akiongea Alilazimika kuongeza: “Vivyo hivyo sio mapenzi ya Baba yenu aliye mbinguni kwamba mmoja wa wadogo hawa aangamie.” Ni katika kauli hii tu ndiyo maneno Yake yangezaa matunda, kuwafanya watu kuamini usahihi wao na kuboresha kiwango cha kuaminika kwa maneno hayo. Hii inaonyesha kwamba wakati Mungu alipokuwa Mwana wa Adamu wa kawaida, Mungu na mwanadamu walikuwa na uhusiano wa kufedhehesha sana, na kwamba hali ya Mwana wa Adamu ilikuwa ya kuaibisha mno. Inaonyesha pia namna ambavyo hadhi ya Bwana Yesu ilivyokuwa isiyo na maana miongoni mwa binadamu wakati huo. Aliposema haya, kwa hakika ilikuwa ni kuwaambia watu: Mnaweza kuwa na uhakika kwamba—haya hayawakilishi yale yaliyo moyoni Mwangu mwenyewe, lakini ni mapenzi ya Mungu aliye mioyoni mwenu. Kwa mwanadamu, jambo hili halikuwa la kejeli? Ingawa Mungu Akifanya kazi katika mwili Alikuwa na manufaa mengi ambayo Hakuwa nayo katika nafsi Yake, Alilazimika kustahimili shaka na kukataliwa na wao pamoja na kutojali na kutochangamka kwao. Yaweza kusemekana kwamba mchakato wa kazi ya Mwana wa Adamu ulikuwa mchakato wa kupitia kukataliwa na mwanadamu, na mchakato wa kupitia mwanadamu akishindana dhidi Yake. Zaidi ya hayo, ulikwa ni mchakato wa kufanya kazi ili kuendelea kushinda imani ya mwanadamu na kumshinda mwanadamu kupitia kile Alicho nacho na kile Alicho, kupitia kiini Chake binafsi halisi. Haikuwa sana kwamba Mungu mwenye mwili Alikuwa akipigana vita vikali dhidi ya Shetani; ilikuwa zaidi kwamba Mungu aligeuka na kuwa binadamu wa kawaida na kuanzisha mapambano pamoja na wale wanaomfuata Yeye, na katika mapambano haya Mwana wa Adamu alikamilisha kazi Yake kwa unyenyekevu Wake, pamoja na kile Alicho nacho na kile Alicho, na upendo na hekima Yake. Aliweza kupata watu Aliowataka, kushinda utambulisho na hadhi Aliyostahili, na kurudi kwa kiti Chake cha enzi.
Kifuatacho, hebu tuangalie dondoo mbili zifuatazo katika maandiko.
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
Kujua zaidi: Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni