Jumatano, 7 Februari 2018

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III | 4. Samehe Sabini Mara Saba | 5. Upendo wa Bwana

Umeme wa Mashariki | 4. Samehe Sabini Mara Saba | 5. Upendo wa Bwana

4. Samehe Sabini Mara Saba
(Mat 18:21-22) Kisha Petro akamwendea, na akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikosee mara ngapi na mimi nimsamehe? Mpaka mara saba? Yesu akamwambia, Sikuambii mpaka mara saba: bali, mpaka sabini mara saba.
5. Upendo wa Bwana
(Mat 22:37-39) Yesu akamwambia, Umpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri ya kwanza na iliyo kuu. Na ya pili inafanana nayo, Umpende jirani yako kama nafsi yako.
Mwenyezi Mungu alisema, Kati ya dondoo hizi mbili, moja yazungumzia msamaha na nyingine inazungumzia upendo. Mada hizi mbili zinaangazia kwa kweli kazi ambayo Bwana Yesu alitaka kutekeleza katika Enzi ya Neema.

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Biblia,
Samehe Sabini Mara Saba
Wakati Mungu alipokuwa mwili, Alileta pamoja naye hatua ya kazi Yake—Alileta pamoja naye kazi mahususi ya enzi hii na tabia Aliyotaka kuonyesha. Katika kipindi hicho, kila kitu ambacho Mwana wa Adamu alifanya kilizungukia kazi ambayo Mungu alitaka kutekeleza katika enzi hii. Asingeweza kufanya zaidi au kufanya kidogo zaidi. Kila kitu Alichosema na kila aina ya kazi Aliyotekeleza ilihusiana yote na enzi hii. Haijalishi kama Alionyesha kwa njia ya kibinadamu Akitumia lugha ya kibinadamu au kupitia kwa lugha ya kiungu—haijalishi ni njia gani, au kutoka kwa mtazamo gani—shabaha Yake ilikuwa ni kuwasaidia watu kuelewa kile Alichotaka kufanya, mapenzi Yake yalikuwa nini, na mahitaji Yake yalikuwa yapi kutoka kwa watu. Anaweza kutumia mbinu mbalimbali kutoka mitazamo mbalimbali ili kuwasaidia watu kuelewa na kujua mapenzi Yake, kuelewa kazi Yake ya kuokoa mwanadamu. Hivyo basi katika Enzi ya Neema tunamwona Bwana Yesu akitumia lugha ya kibinadamu mara kwa mara kuonyesha kile Alichotaka kuwasilisha kwa mwanadamu. Hata zaidi, tunamwona Yeye kutoka katika mtazamo wa mwelekezi wa kawaida Akiongea na watu, Akiwaruzuku mahitaji yao, Akiwasaidia na kile walichoomba. Njia hii ya kufanya kazi haikuonekana katika Enzi ya Sheria iliyokuja kabla ya Enzi ya Neema. Aligeuka na kuwa karibu zaidi na mwenye huruma zaidi kwa binadamu, pamoja na kuweza kutimiza zaidi matokeo ya kimatendo katika umbo Lake na tabia Yake. Usemi kusamehe watu “sabini mara saba” unafafanua zaidi hoja hii. Kusudio lililotimizwa kupitia kwa nambari katika usemi huu ni kuwaruhusu watu kuelewa nia ya Bwana Yesu wakati huo aliposema hayo. Nia yake ilikuwa kwamba watu wanafaa kuwasamehe wengine—si mara moja wala mara mbili na wala si hata mara saba, lakini sabini mara saba. Hili wazo la “sabini mara saba” ni la aina gani? Ni la kuwafanya watu kufanya msamaha kuwa wajibu wao wa kibinafsi, kitu ambacho lazima wajifunze, na njia ambayo lazima waendeleze. Hata ingawa huu ulikuwa usemi tu, ulikuwa hoja muhimu. Uliwasaidia watu kufahamu kwa kina kile Alichomaanisha na kugundua njia bora za kufanyia mazoezi na kanuni na viwango katika utendaji. Usemi huu uliwasaidia watu kuelewa waziwazi na ukawapa dhana sahihi kwamba wanafaa kujifunza kusamehe—kusamehe bila ya masharti na bila ya upungufu wowote, lakini kwa mtazamo wa uvumilivu na ufahamu kwa wengine. Wakati Bwana Yesu aliposema haya, ni nini kilichokuwa moyoni Mwake? Alikuwa akifikiria kwa kweli kuhusu sabini mara saba? Hakuwa akifiki kuhusu hilo. Ipo idadi fulani ambayo Mungu atasamehe binadamu? Kunao watu wengi walio na shauku katika “idadi” iliyotajwa, wanaotaka kwa kweli kuelewa asili na maana ya nambari hii. Wanataka kuelewa kwa nini nambari hii ilitoka kinywani mwa Bwana Yesu; wanaamini kwamba kunauhusisho wa kina zaidi katika nambari hii. Kwa hakika, huu ulikuwa ni usemi tu wa Mungu katika ubinadamu. Uhusisho au maana yoyote lazima ichukuliwe pamoja na mahitaji ya Bwana Yesu kwa mwanadamu. Wakati Mungu alikuwa bado hajawa mwili, watu hawakuelewa mengi ya Alichosema kwa sababu kilitoka katika uungu kamilifu. Mtazamo na muktadha wa kile Alichosema ulikuwa hauonekani na haufikiwi na mwanadamu; ulielezewa kutoka katika himaya ya kiroho ambayo watu wasingeweza kuiona. Kwa watu walioishi katika mwili, wasingeweza kupita katika himaya ya kiroho. Lakini baada ya Mungu kuwa mwili, Aliongea na mwanadamu kutoka katika mtazamo wa ubinadamu, na mazungumzo haya yalitokana na, na yakazidi ule upana wa himaya ya kiroho. Angeweza kuonyesha tabia Yake ya uungu, mapenzi, na mtazamo, kupitia mambo yale ambayo binadamu wangeweza kufikiria na mambo yale wangeweza kuona na kukumbana nayo katika maisha yao, kwa kutumia mbinu ambazo binadamu wangeweza kukubali, kwa lugha ambayo wangeweza kuelewa, na maarifa ambayo wangeweza kuelewa, ili kuruhusu mwanadamu kumwelewa na kumjua Mungu, kufahamu kile Alicho na viwango Vyake hitajika ndani ya mawanda ya uwezo wao; hadi kufikia kiwango ambacho wangeweza. Hii ndiyo iliyokuwa mbinu na kanuni ya kazi ya Mungu kwa ubinadamu. Ingawa njia za Mungu na kanuni Zake za kufanya kazi katika mwili ziliweza kutimizwa sana kwa, au kupitia kwa ubinadamu, ziliweza kwa kweli kutimiza matokeo ambayo yasingeweza kutimizwa kwa kufanya kazi moja kwa moja katika uungu. Kazi ya Mungu katika ubinadamu ilikuwa thabiti zaidi, halisi, na yenye malengo, mbinu zilikuwa zaweza kubadilika kwa urahisia zaidi, na kwa umbo iliweza kupita Enzi ya Sheria.
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Yesu,
Samehe Sabini Mara Saba


Hapa chini, hebu tuzungumzie kumpenda Bwana na kumpenda jirani yako kama unavyojipenda. Je, hili ni jambo linaloelezewa moja kwa moja kupitia uungu? Bila shaka silo! Haya yalikuwa mambo yote ambayo Mwana wa Adamu alisema katika ubinadamu; watu tu ndio wangeweza kusema kauli kama “Mpende jirani yako kama unavyojipenda. Kuwapenda wengine ni sawa na kuyatunza maisha yako binafsi,” na watu tu ndio wangeweza kuongea kwa njia hii. Mungu hajawahi kuongea kwa njia hiyo. Kwa kiwango cha chini zaidi, Mungu hana aina hii ya lugha katika uungu Wake kwa sababu Hahitaji aina hii ya imani, “Mpende jirani yako kama unavyojipenda” ili kudhibiti upendo Wake kwa mwanadamu, kwa sababu upendo wa Mungu kwa mwanadamu ni ufichuzi wa kiasili wa kile Alicho nacho na kile Alicho. Ni lini umewahi kumsikia Mungu akisema kitu kama “Nampenda mwanadamu kama Ninavyojipenda”? Kwa sababu upendo umo katika kiini cha Mungu, na ndani ya kile Alicho nacho na kile Alicho. Upendo wa Mungu kwa mwanadamu na jinsi Anavyowashughulikia watu na mtazamo Wake ni maonyesho ya kiasili na ufichuzi wa tabia Yake. Hahitaji kufanya hili kwa njia fulani kimakusudi, au kufuata mbinu fulani au mfumo wa maadili kimakusudi ili kutimiza kumpenda jirani Yake kama Anavyojipenda—tayari Anamiliki aina hii ya kiini. Unaona nini katika haya? Wakati Mungu alipofanya kazi katika ubinadamu, mbinu, maneno, na ukweli Wake mwingi vyote vilionyeshwa kwa njia ya kibinadamu. Lakini wakati uo huo tabia ya Mungu, kile Alicho nacho na kile Alicho, na mapenzi Yake vyote vilielezwa kwa watu kuweza kujua na kuvielewa. Kile wAlichojua na kuelewa kilikuwa hasa kiini Chake na Alicho nacho na kile Alicho, vyote ambavyo vinawakilisha utambulisho na hadhi ya asili ya Mungu Mwenyewe. Hivyo ni kusema kwamba, Mwana wa Adamu kwa mwili Alionyesha tabia ya asili na kiini cha Mungu Mwenyewe kwa kiwango kikubwa zaidi kinachowezekana na kwa usahihi zaidi unaowezekana. Ubinadamu wa Mwana wa Adamu haukuwa pingamizi au kizuizi cha mawasiliano na kuingiliana kwa binadamu na Mungu mbinguni tu, bali kwa hakika ilikuwa ndio njia ya pekee na daraja la pekee la mwanadamu kuungana na Bwana wa uumbaji. Wakati huu, huhisi kwamba kunayo mifanano mingi kati ya asili na mbinu za kazi iliyofanywa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema na awamu ya sasa ya kazi? Awamu ya sasa ya kazi inatumia pia lugha nyingi za kibinadamu kueleza tabia ya Mungu, na inatumia lugha na mbinu nyingi kutoka katika maisha ya kila siku ya mwanadamu na maarifa ya kibinadamu ili kuonyesha mapenzi binafsi ya Mungu. Punde Mungu anapokuwa mwili, haijalishi kama Anaongea kutoka kwa mtazamo wa kibinadamu au mtazamo wa kiungu, wingi wa lugha na mbinu Zake za maonyesho yote ni kupitia katika njia ya lugha na mbinu za kibinadamu. Yaani, wakati Mungu anapokuwa mwili, ndiyo fursa bora zaidi ya wewe kuweza kuona kudura ya ya Mungu na hekima Yake, na kujua kila kipengele halisi cha Mungu. Wakati Mungu alipogeuka na kuwa mwili, wakati Alipokuwa Akikua, Alipata kuelewa, kujifunza, na kuelewa baadhi ya maarifa ya mwanadamu, maarifa ya kawaida, lugha, na mbinu za maonyesho katika ubinadamu. Mungu mwenye mwili alimiliki mambo haya yaliyotokana na binadamu Aliyekuwa ameumba. Waligeuka na kuwa zana za Mungu katika mwili za kueleza tabia Yake na uungu Wake, na wakamruhusu kuifanya kazi Yake ya kufaa zaidi, halisi zaidi, na sahihi zaidi Alipokuwa akifanya kazi katikati ya mwanadamu, kutoka katika mtazamo wa kibinadamu na kwa kutumia lugha ya kibinadamu. Iliiwezesha kufikiwa zaidi na kueleweka kwa urahisi zaidi na watu, hivyo basi kutimiza matokeo ya kile Mungu Alichotaka. Je, si jambo la busara zaidi kwa Mungu kufanya kazi kupitia kwa mwili kwa njia hii? Je, hili si hekima ya Mungu? Wakati Mungu alipogeuka na kuwa mwili, wakati mwili wa Mungu uliweza kuchukua kazi Aliyotaka kutekeleza, ndipo Angeonyesha tabia Yake na kazi Yake akiwa mashinani, na huu ndio wakati pia ambao Angeanza rasmi huduma Yake kama Mwana wa Adamu. Hii ilimaanisha kwamba hakukuwepo tena na ghuba kati ya Mungu na binadamu, kwamba Mungu angesitisha karibuni kazi Yake ya kuwasiliana kupitia kwa wajumbe, na kwamba Mungu Mwenyewe binafsi angeweza kuonyesha maneno na kazi zote Alizotaka kufanya katika mwili. Hii ilimaanisha pia kwamba watu ambao Mungu huokoa walikuwa karibu na Yeye, na kwamba kazi Yake ya usimamizi ilikuwa imeingia eneo jipya, na kwamba ubinadamu mzima ulikuwa karibu kukumbwa na enzi mpya.
Kila mtu ambaye amesoma Biblia anajua kwamba mambo mengi yalifanyika wakati Bwana Yesu alipozaliwa. Kubwa zaidi miongoni mwa hayo lilikuwa kutafutwa na Shetani, hadi kufikia kiwango cha watoto wote wenye umri wa miaka miwili na chini katika eneo hilo kuchinjwa. Ni dhahiri kwamba Mungu alichukua hatari kubwa kwa kuwa mwili miongoni mwa binadamu; gharama kubwa Aliyolipia kwa ajili ya kukamilisha usimamizi Wake wa kumwokoa mwanadamu pia ni wazi. Matumaini makubwa ambayo Mungu alishikilia kwa ajili ya kazi Yake miongoni mwa wanadamu katika mwili pia ni wazi. Wakati mwili wa Mungu uliweza kuchukua kazi miongoni mwa wanadamu, Alikuwa anahisi vipi? Watu wanafaa kuweza kuelewa hilokiasi, sivyo? Kwa kiwango cha chini zaidi, Mungu alifurahia kwa sababu Angeanza kuendeleza kazi Yake mpya miongoni mwa wanadamu. Wakati Bwana Yesu alipobatizwa na kuanza rasmi kazi Yake kukamilisha huduma Yake, moyo wa Mungu ulijawa na furaha kwa sababu baada ya miaka mingi sana ya kusubiri na matayarisho, hatimaye Angeweza kuuvaa mwili wa binadamu wa kawaida na kuanza kazi Yake mpya katika umbo la binadamu aliye na mwili na damu ambao watu wangeweza kuona na kugusa. Angeweza kuzungumza ana kwa ana na moyo kwa moyo na watu kupitia utambulisho wa binadamu. Mungu hatimaye angeweza kuwa ana kwa ana na mwanadamu katika lugha ya kibinadamu, kwa njia ya kibinadamu; Angeweza kumruzuku mwanadamu, kumwelimisha binadamu, na kumsaidia binadamu kwa kutumia lugha ya kibinadamu; angeweza kulia meza moja na kuishi katika nafasi sawa na binadamu. Angeweza pia kuwaona binadamu, kuona vitu, na kuona kila kitu kwa njia ambayo binadamu walifanya hivyo na hata kupitia kwa macho yao. Kwake Mungu, huu ulikuwa tayari ushindi Wake wa kwanza wa kazi Yake katika mwili. Yaweza pia kusemekana kwamba yalikuwa ni ufanikishaji wa kazi kubwa—hii bila shaka ndiyo ambayo Mungu alifurahi zaidi kuihusu. Kuanzia hapo ndiyo mara ya kwanza ambayo Mungu alihisi tulizo fulani katika kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Matukio haya yote yalikuwa ya kimatendo sana na ya asili sana, na tulizo ambalo Mungu alihisi lilikuwa halisi. Kwa mwanadamu, kila mara hatua mpya ya kazi ya Mungu inapokamilishwa, na kila mara Mungu anapohisi kuridhika, ndipo mwanadamu anapoweza kusogea karibu zaidi na Mungu, na ndipo watu wanapoweza kusonga karibu zaidi na wokovu. Kwa Mungu, huu pia ni uzinduzi wa kazi Yake mpya, wakati mpango Wake wa usimamizi unapoendelea hatua moja zaidi, na, aidha, wakati mapenzi Yake yanapokaribia mafanikio kamili. Kwa mwanadamu, kuwasili kwa fursa kama hiyo ni bahati, na mzuri sana; kwa wale wote wanaosubiria wokovu wa Mungu, ni habari za maana sana. Wakati Mungu anapotekeleza hatua mpya ya kazi, basi Anao mwanzo mpya na wakati ambapo kazi hii mpya na mwanzo mpya vinazinduliwa na kufahamishwa miongoni mwa wanadamu, ni wakati ambao matokeo ya awamu hii ya kazi tayari yameamuliwa, na kufanikishwa, naye Mungu tayari ameona athari yake ya mwisho na tunda. Huu pia ndio wakati ambapo athari hizi zinamfanya Mungu kuridhika, na moyo Wake, bila shaka una furaha. Kwa sababu katika macho ya Mungu, tayari meona na kuamua watu anaowatafuta, na tayari Amepata kundi hili, kundi ambalo linaweza kufanya kazi Yake kufanikiwa na kumpa utoshelevu, Mungu anahisi Akiwa ameondolewa shaka, Anaweka pembeni wasiwasi Wake, na Anahisi mwenye furaha. Kwa maneno mengine, wakati mwili wa Mungu unaweza kuanza kazi mpya miongoni mwa binadamu, na Anaanza kufanya kazi ambayo lazima Afanye bila ya kizuizi, na wakati Anapohisi kwamba yote yamefanikishwa, tayari Ameuona mwisho. Na kwa sababu ya mwisho huu Yeye ametosheka, na mwenye moyo wa furaha. Furaha ya Mungu inaonyeshwa vipi? Unaweza kufikiria hayo? Je, Mungu Angeweza kulia? Mungu Anaweza kulia? Mungu Anaweza kupiga makofi? Mungu Anaweza kucheza? Mungu Anaweza kuimba? Na wimbo huo ungekuwa upi? Bila shaka Mungu Angeweza kuimba wimbo mzuri, wa kusisimua, wimbo ambao ungeweza kuonyesha shangwe na furaha katika moyo Wake. Angeweza kuuimbia wanadamu, Kujiimbia mwenyewe, na kuuimba kwa viumbe vyote. Furaha ya Mungu inaweza kuonyeshwa kwa njia yoyote—yote haya ni kawaida kwa sababu Mungu anayo shangwe na huzuni, na hisia Zake mbalimbali zinaweza kuelezewa kwa njia mbalimbali. Hii ndiyo haki Yake na ndilo jambo la kawaida zaidi. Hufai kufikiria chochote kingine kuhusu hili, na hufai kusingizia vizuizi vyako binafsi kwa Mungu, huku ukimwambia kwamba Yeye hafai kufanya hiki wala kile, Hafai kutenda kwa njia hii au ile, kuwekea mipaka shangwe Yake au hisia yoyote ile Aliyo nayo. Katika mioyo ya watu Mungu hawezi kuwa na furaha, Hawezi kutokwa na machozi, Hawezi kulia—Hawezi kuonyesha hisia zozote. Kupitia yale tuliyowasiliana nanyi katika nyakati hizi mbili, Ninasadiki hamtamwona tena Mungu kwa njia hii, lakini mtaruhusu Mungu kuwa na uhuru na uwachiliaji fulani. Hiki ni kitu kizuri. Katika siku za usoni kama mtaweza kuhisi kwa kweli huzuni ya Mungu wakati mnaposikia kwamba Yeye anayo huzuni, na mnaweza kuhisi kwa kweli shangwe Yake mnaposikia kuhusu Yeye kuwa na furaha—angalau, mnaweza kujua na kuelewa waziwazi kile kinachomfanya Mungu kuwa na furaha na kile kinachomfanya Yeye kuwa na huzuni—unapoweza kuhisi huzuni kwa sababu Mungu anayo huzuni na kuhisi furaha kwa sababu Mungu anayo furaha, Atakuwa ameupata moyo wako na hakutakuwa tena na kizuizi chochote na Yeye. Hamtajaribu tena kumzuilia Mungu na fikira dhana na maarifa ya binadamu. Wakati huo, Mungu atakuwa hai na dhahiri moyoni mwako. Atakuwa Mungu wa maisha yako na Bwana wa kila kitu chako. Je, mnalo imani kama hii? Je, mnayo imani kuwa mnaweza kutimiza haya?
Halafu hebu tusome fahamu zifuatazo.
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
Yaliyopendekezwa: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni