Ijumaa, 2 Februari 2018

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II | 5. Ayubu Baada ya Majaribio yake

 Umeme wa Mashariki | 5. Ayubu Baada ya Majaribio yake

(Ayubu 42:7-9) Basi ikawa, baada ya BWANA kumwambia Ayubu maneno hayo, BWANA akamwambia huyo Elifazi Mtemani, Hasira yangu inawaka juu yako, na juu ya hao rafiki zako wawili: kwa kuwa nyinyi hamjanena yaliyo sawa kunihusu, kama alivyofanya mtumishi wangu Ayubu. Basi sasa, jichukulieni ng’ombe waume saba, na kondoo waume saba, muende kwa mtumishi wangu Ayubu, na mjitolee sadaka ya kuteketezwa; na mtumishi wangu Ayubu atawaombea: kwa kuwa yeye Nitamkubali: nisije Nikawatendea kulingana na makosa yenu, hivi kwamba nyinyi hamkunena maneno yaliyo sawa kunihusu, kama alivyofanya mtumishi wangu Ayubu. Hivyo Elifazi, Mtemani, na Bildadi, Mshuhi, na Sofari, Mnaamathi, wakaenda, wakafanya vile BWANA alivyowaamuru: BWANA pia akamkubali Ayubu.

(Ayubu 42:10) Kisha BWANA akaugeuza uteka wa Ayubu, alipowaombea rafiki zake: BWANA pia akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kabla.
(Ayubu 42:12) Basi hivyo BWANA akaubariki mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake: kwani alikuwa na kondoo kumi na nne elfu, na ngamia elfu sita, na jozi za ng’ombe elfu moja, na punda wa kike elfu moja.
(Ayubu 42:17) Basi Ayubu akafa, akiwa mzee sana na mwenye kujawa na siku.

Wale Wanaomcha Mungu na Kujiepusha Na Maovu Wanatazamiwa kwa Utunzwaji na Mungu, Huku Wale Walio Wajinga Wanaonekana kuwa Wanyenyekevu

Mwenyezi Mungu alisema, Katika Ayubu 42:7-9, Mungu Anasema kwamba Ayubu ni mtumishi Wake. Matumizi Yake ya neno “mtumishi” kumrejelea Ayubu yanaonyesha umuhimu wa Ayubu katika moyo Wake; ingawaje Mungu hakumwita Ayubu kitu chenye heshima zaidi, jina hili halikuwa na uamuzi wowote katika umuhimu wa Mungu ndani ya moyo wa Ayubu. “Mtumishi” hapa ni jina la lakabu la Mungu kwa Ayubu. Marejeleo mbali mbali ya Mungu kwa “mtumishi wangu Ayubu” yanaonyeshwa ni vipi ambavyo Alipendezwa na Ayubu, ingawaje Mungu hakuongea kuhusu maana ya nyuma ya neno “Mtumishi,” ufafanuzi wa Mungu wa neno “mtumishi” unaweza kuonekana kupitia kwa maneno Yake katika kifungu hiki ya maandiko. Kwanza Mungu alimwambia Elifazi Mtemani: “Hasira yangu inawaka juu yako, na juu ya hao rafiki zako wawili: kwa kuwa nyinyi hamjanena yaliyo sawa kunihusu, kama alivyofanya mtumishi wangu Ayubu.” Maneno haya ndiyo ya mara ya kwanza kwa Mungu kuambia watu waziwazi kwamba alikuwa amekubali yale yote yaliyokuwa yamesemwa na kufanywa na Ayubu baada ya majaribio ya Mungu kwake yeye, na ndiyo mara ya kwanza Alikuwa amedhibitisha waziwazi ukweli na usahihi wa yale yote Ayubu alikuwa amefanya na kusema. Mungu alikuwa na ghadhabu kwake Elifazi na wengine kwa sababu ya mazungumzo yao yasiyokuwa sahihi na mabovu, kwa sababu, kama Ayubu wasingeweza kuona mwonekano wa Mungu au kusikia maneno aliyoongea katika maisha yao ilhali Ayubu alikuwa na maarifa sahihi Kumhusu Mungu, huku nao waliweza tu kukisia bila mpango kuhusu Mungu, kukiuka mapenzi ya Mungu na kujaribu uvumilivu wake kwa yote waliyoyafanya Kwa hivyo, wakati sawa na kukubali yote yalikuwa yamefanywa na kusemwa na Ayubu, Mungu alizidi kuongeza hasira zake kwa wale wengine, kwani ndani yao Hakuweza tu kuuona uhalisia wowote wa kumcha Mungu, lakini pia Hakusikia chochote cha kumcha Mungu kwa yale waliyoyasema. Na hivyo Mungu kwa kilichofuata Alisema madai yafuatayo kuwahusu. “Basi sasa, jichukulieni ng’ombe waume saba, na kondoo waume saba, muende kwa mtumishi wangu Ayubu, na mjitolee sadaka ya kuteketezwa; na mtumishi wangu Ayubu atawaombea: kwa kuwa yeye Nitamkubali: Nisije Nikawatendea kulingana na makosa yenu.” Katika kifungu hiki Mungu anamwambia Elifazi na wengine kufanya jambo ambalo litakomboa dhambi zao, kwani upumbavu wao ulikuwa ni dhambi dhidi ya Yehova Mungu, na hivyo wangelazimika kutoa sadaka zilizoteketezwa ili kusuluhisha makosa yao. Sadaka zilizoteketezwa mara nyingi zinatolewa kwa Mungu, lakini kile kisicho cha kawaida kuhusu sadaka hizi zilizoteketezwa ni kwamba zilitolewa kwa Ayubu. Ayubu alikubaliwa na Mungu kwa sababu alikuwa nao ushuhuda kwa Mungu wakati wa majaribio yake. Rafiki hawa wa Ayubu, nao walifichuliwa katika kipindi kile cha majaribio yake, kwa sababu ya upumbavu wao, walishutumiwa na Mungu na wakachochea hasira ya Mungu, na wanafaa kuadhibiwa na Mungu—kuadhibiwa kwa kutoa sadaka zilizoteketezwa mbele ya Ayubu—na baadaye Ayubu aliwaombea wao ili kuiondoa ile adhabu na hasira ya Mungu kwao. Nia ya Mungu ilikuwa ni kuwaaibisha wao, kwani hawakuwa watu waliomcha Mungu na wa kujiepusha na maovu, na walikuwa wameshutumu uadilifu wa Ayubu. Kwa upande mmoja, Mungu alikuwa akiwaambia kwamba Hakukubali vitendo vyao lakini Alikubali pakubwa na Alifurahishwa na Ayubu; kwa upande mwingine, Mungu alikuwa akiwaambia kwamba kukubaliwa na Mungu kunampandisha daraja binadamu mbele ya Mungu, kwamba binadamu anachukiwa na Mungu kwa sababu ya upumbavu wake, na anamkosea Mungu kwa sababu ya hali hii, na anakuwa mdogo na mbaya mbele ya macho ya Mungu. Huu ndio ufafanuzi uliotolewa na Mungu kuhusu watu wa aina mbili, ni mielekeo ya Mungu kwa watu hawa wa aina mbili na ni ufafanuzi wa Mungu kuhusu thamani na hadhi ya watu wa aina hizi mbili. Ingawaje Mungu alimwita Ayubu mtumishi Wake, ndani ya macho ya Mungu huyu “mtumishi” alikuwa mpendwa Wake, na alipewa mamlaka ya kuwaombea wengine na kuwasamehe makosa yao. “Mtumishi huyu” aliweza kuongea moja kwa moja na Mungu na kuwa na mgusano wa moja kwa moja na Mungu, hadhi yake ilikuwa ya juu zaidi na ya heshima zaidi kuliko ya wale wengine. Haya ndiyo maana halisi ya neno “mtumishi” kama Mungu alivyoongea. Ayubu alipewa heshima hii maalum kwa sababu ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, na sababu iliyofanya wengine kutoitwa watumishi na Mungu ni kwa sababu hawakumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Mielekeo hii miwili tofauti na maalum ya Mungu ndiyo mielekeo yake kwa watu wa aina mbili: Wale wanaomcha Mungu na kujiepusha na maovu wanakubaliwa na Mungu, na wanaonekana wenye thamani mbele ya macho Yake, huku wale walio wapumbavu hawajamcha Mungu na hawawezi kujiepusha na maovu, na hawawezi kupokea kibali cha Mungu, mara nyingi wanachukiwa na kushutumiwa na Mungu, na ni wadogo mbele ya macho ya Mungu.

Mungu Anamtawaza Mamlaka Ayubu

Ayubu aliwaombea rafiki zake, na baadaye, kwa sababu ya maombi ya Ayubu, Mungu hakushughulika nao kama walivyostahili juu ya upumbavu wao —Hakuwaadhibu au kuchukua adhabu yoyote dhidi yao. Na sababu ilikuwa nini? Kwa sababu kulingana na wao maombi yanayohusu mtumishi wa Mungu, Ayubu, yalikuwa yamefikia masikio Yake; Mungu naye aliwasamehe kwa sababu Aliyakubali maombi ya Ayubu. Na tunaona nini katika haya? Wakati Mungu anapombariki mtu, Anampa tuzo nyingi, na si tu zile za kidunia, pia: Mungu anawapa pia mamlaka, na Kuwaambia kuwa wanastahili kuwaombea wengine, naye Mungu husahau na kusamehe makosa ya hao watu kwa sababu Anayasikia maombi haya. Haya ndiyo mamlaka yenyewe ambayo Mungu alimpa Ayubu. Kupitia kwa maombi ya Ayubu kusitisha kushutumiwa kwao, Yehova Mungu aliwaletea aibu wale watu wapumbavu— ambayo, bila shaka, ndiyo iliyokuwa adhabu Yake maalum kwa Elifazi na wale wengine.

Ayubu Anabarikiwa kwa Mara Nyingine Tena na Mungu, na Hashtakiwi Tena na Shetani

Miongoni mwa matamko ya Yehova Mungu ni maneno kwamba “hivi kwamba nyinyi hamkunena maneno yaliyo sawa kunihusu, kama alivyofanya mtumishi wangu Ayubu.” Ni nini kile ambacho Ayubu alikuwa amesema? Ni kile tulichozungumzia awali, pamoja na kile ambacho kurasa nyingi za maneno kwenye kitabu cha Ayubu ambacho Ayubu amerekodiwa kuwa alisema. Katika kurasa hizi nyingi za maneno, Ayubu hajawahi hata mara moja kuwa na malalamiko au mashaka yoyote kumhusu Mungu. Yeye anasubiria tu matokeo. Ni kusubiri huku ambako ndiko mwelekeo wake wa uaminifu, matokeo yake yakiwa, na kutokana na maneno aliyomwambia Mungu, Ayubu alikubaliwa na Mungu. Alipovumilia majaribio na kupata mateso ya Ugumu, Mungu alikuwa upande wake na ingawaje ugumu wake hukupunguzwa na uwepo wa Mungu, Mungu aliona kile Alichotaka kuona na kusikia kile Alichotaka kusikia. Kila mojawapo ya vitendo na maneno ya Ayubu kiliweza kufikia macho na masikio ya Mungu; Mungu alisikia na Akaona—na hii ni ukweli. Maarifa ya Ayubu kumhusu Mungu na fikira zake kumhusu Mungu katika moyo wake wakati huo, katika kipindi hicho, hazikuwa kwa hakika kama zile za watu wa leo, lakini katika muktadha wa wakati huo, Mungu aliweza kutambua bado kila kitu alichokuwa amesema, kwa sababu tabia yake na fikira zake ndani ya moyo wake, na kile alichokuwa ameelezea na kufichua, kilikuwa tosha kwa mahitaji Yake. Katika kipindi hiki cha wakati ambao Ayubu alipitia majaribio, yale ambayo alifikiria katika moyo wake na kuamua kufanya yaliweza kumwonyesha Mungu matokeo, yale ambayo yalimtosheleza Mungu, na baadaye Mungu akayaondoa majaribio ya Ayubu, Ayubu akaibuka kutoka kwenye matatizo yake, na majaribio yake yakawa yameondoka yasiwahi kumpata tena yeye. Kwa sababu Ayubu alikuwa tayari amepitia majaribio, na akawa amesimama imara katika majaribio haya, na akamshinda kabisa Shetani, Mungu alimpatia baraka ambazo kwa kweli alistahili. Kama ilivyorekodiwa katika Ayubu 42:10, 12, Ayubu alibarikiwa kwa mara nyingine tena, na akabarikiwa zaidi ya hata mara ya kwanza. Wakati huu Shetani alikuwa amejiondoa, na hakusema tena au kufanya chochote, na kutoka hapo kuenda mbele Ayubu hakuhitilafiana tena na Shetani au kushambulia Shetani, na Shetani hakutoa mashtaka tena dhidi ya baraka za Mungu kwa Ayubu.

Ayubu Atumia Nusu ya Mwisho ya Maisha Yake Katikati ya Baraka za Mungu

Ingawaje baraka Zake wakati huo zilikuwa tu zinajumuisha kondoo, ng'ombe, ngamia, na rasilimali za dunia, na kadhalika, baraka ambazo Mungu alitaka kumpa Ayubu katika moyo Wake zilikuwa mbali zaidi na hizi. Kwa wakati huo ziliporekodiwa, ni aina gani za ahadi za milele ambazo Mungu alipenda kumpa Ayubu? Katika baraka Zake kwa Ayubu, Mungu hakugusia au kutaja kuhusu mwisho wake, na haijalishi umuhimu au cheo ambacho Ayubu alishikilia ndani ya moyo wa Mungu, kwa ujumla Mungu alikuwa akitambua katika baraka Zake. Mungu hakutangaza mwisho wa Ayubu. Hii inamaanisha nini? Wakati huo, wakati mpango wa Mungu ulikuwa bado haujafikia sehemu ya kutangaza mwisho wa binadamu, mpango huo ulikuwa bado uingie kwenye awamu ya mwisho ya kazi yake, Mungu hakutaja chochote kuhusu mwisho, huku akimpa binadamu baraka za rasilimali za dunia tu. Maana ya hii ni kwamba nusu ya mwisho ya maisha ya Ayubu ilipita katikati ya baraka za Mungu na hii ndiyo iliyomfanya kuwa tofauti na wale watu wengine—lakini kama wao alizeeka, na kama mtu yeyote yule wa kawaida siku ilifika ambapo aliuambia ulimwengu kwaheri. Na hivyo imerekodiwa kwamba “Basi Ayubu akafa, akiwa mzee sana na mwenye kujawa na siku” (Ayubu 42:17). Nini maana ya “akafa… mwenye kujawa na siku” hapa? Katika enzi ya kabla Mungu kutangaza mwisho, Mungu alimwekea Ayubu matarajio ya maisha ambayo angeishi, na wakati umri huo ulipofikiwa Alimruhusu Ayubu kuondoka kiasili kutoka ulimwengu huu. Kutoka baraka ya pili ya Ayubu hadi kifo chake, Mungu hakuongezea ugumu wowote. Kwake Mungu, kifo cha Ayubu kilikuwa cha kiasili, na pia kilihitajika, kilikuwa kitu cha kawaida sana na wala si hukumu au shutuma. Alipokuwa hai, Ayubu alimwabudu na kumcha Mungu; kuhusiana na ni aina gani ya mwisho aliyokuwa nayo kufuatia kifo chake, Mungu hakusema chochote, wala kutoa maoni yoyote kuhusu hilo. Mungu ni mwenye busara katika kile Anachosema na kufanya, na maudhui na kanuni za maneno na vitendo vyake yanalingana na awamu ya kazi Yake na kipindi Anachofanyia kazi. Ni aina gani ya mwisho ambayo mtu kama Ayubu alikuwa nayo katika moyo wa Mungu? Je, Mungu alikuwa amefikia aina yoyote ya uamuzi katika moyo Wake? Bila shaka Alikuwa! Ni vile tu hili lilikuwa halijulikani kwa binadamu; Mungu hakutaka kumwambia binadamu wala Hakuwa na nia yoyote ya kumwambia binadamu. Na hivyo, kwa kuongea juujuu tu, Ayubu alikufa akiwa amejawa na siku, na hivyo ndivyo maisha ya Ayubu yalivyokuwa.
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, uaminifu,
Umri wa kazi alikuwa ameridhika kufa

Gharama Iliyoishi kwa kudhihirishwa na Ayubu Wakati wa Maisha Yake

Je Ayubu aliishi maisha ya thamani? Thamani yake ilikuwa wapi? Ni kwa nini inasemwa kwamba aliishi maisha yenye thamani? Kwa binadamu, thamani yake ilikuwa gani? Kutoka katika mtazamo wa binadamu, aliwawakilisha wanadamu ambao Mungu alitaka kuokoa, kwa kuwa na ushuhuda wa kipekee kwa Mungu mbele ya Shetani na watu wa ulimwengu. Alitimiza wajibu ambao ulistahili kutimizwa na kiumbe wa Mungu, na kuweka mfano halisi wa kuigiwa, na kutenda kama kielelezo, kwa wale wote ambao Mungu angependa kuwaokoa, akiruhusu watu kuona kwamba inawezekana kabisa kushinda Shetani kwa kumtegemea Mungu. Nayo thamani yake kwa Mungu ilikuwa gani? Kwa Mungu, thamani ya maisha ya Ayubu ilikuwa ndani ya uwezo wake wa kumcha Mungu, kumwabudu Mungu, kutolea ushuhuda vitendo vya Mungu, na kusifu vitendo vya Mungu, kumpa Mungu tulizo na kitu cha kufurahia; kwa Mungu, thamani ya maisha ya Ayubu ilikuwa pia kwa namna ambavyo, kabla ya kifo chake, Ayubu alipitia majaribio na kushinda Shetani, na akawa na ushuhuda wa kipekee kwa Mungu mbele ya Shetani na watu wa ulimwengu, akimtukuza Mungu miongoni mwa wanadamu, akiutuliza moyo wa Mungu na kuruhusu moyo wa Mungu wenye hamu kuyaona matokeo, na kuliona tumaini. Ushuhuda wake uliweka mfano wa kufuatwa kutokana na uwezo wake wa kusimama imara katika ushuhuda wa Mungu, na kuweza kumwaibisha Shetani kwa niaba ya Mungu, katika kazi ya Mungu ya kuwasimamia wanadamu. Je, hii si thamani ya maisha ya Ayubu? Ayubu alileta tulizo kwa moyo wa Mungu, alimpa Mungu kionjo cha furaha ya kutukuzwa, na akaanzisha mwanzo mzuri kwa mpango wa usimamizi wa Mungu. Na kuanzia hapo kuenda mbele jina la Ayubu likawa ishara ya utukuzaji wa Mungu na ishara ya kushinda kwa wanadamu dhidi ya Shetani. Kile Ayubu aliishi kwa kudhihirisha wakati wa maisha yake na ushindi wake wa kipekee dhidi ya Shetani milele utabakia ukifurahiwa mno na Mungu na utimilifu wake, unyofu, na hali yake ya kumcha Mungu itaheshimiwa na kuigwa na vizazi vitakavyokuja. Milele atafurahiwa mno na Mungu kama johari lisilo na makosa, wala dosari, na pia ndivyo alivyo na thamani ya kuthaminiwa sana na binadamu!
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni