Umeme wa Mashariki | Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)
Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII |
Mwenyezi Mungu alisema, Tuendelee na mada ya mawasiliano ya wakati uliopita. Je, mnaweza kukumbuka ni mada gani tuliwasiliana wakati uliopita? (Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote.) Je, “Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote” ni mada mnayohisi ikiwa mbali sana nanyi? Mtu fulani anaweza kuniambia wazo kuu la mada hii tuliyowasiliana wakati uliopita? (Kupitia kwa uumbaji wa Mungu wa vitu vyote, ninaona kwamba Mungu hulea vitu vyote na hulea wanadamu. Katika siku zilizopita, kila mara nilifikiria kwamba Mungu anapompa mwanadamu, Anawapa tu watu Wake waliochaguliwa neno Lake, lakini kamwe sikuona, kupitia kwa sheria za vitu vyote, kwamba Mungu anawalea wanadamu.
Ni kupitia tu kwa mawasiliano ya Mungu ya kipengele hiki cha ukweli ndipo ninaona sasa kwamba uhai wa vitu vyote unapewa na Mungu, kwamba Mungu anatengeneza sheria hizi, na kwamba Anavilea vitu vyote. Kutokana na uumbaji Wake wa vitu vote ninaona upendo wa Mungu na kuhisi kwamba Mungu ni chanzo cha vitu vyote.) Mm, wakati uliopita, kimsingi tuliwasiliana kuhusu uumbaji wa Mungu wa vitu vyote na jinsi Aliunda sheria na kanuni kwa ajili ya vitu hivyo. Chini ya sheria hizi na chini ya kanuni hizi, vitu vyote huishi na kufa na wanadamu na kuishi pamoja kwa amani na wanadamu chini ya utawala wa Mungu na machoni pa Mungu. Tulizungumzia nini kwanza? Mungu aliumba vitu vyote na akatumia mbinu Zake kutunga sheria za ukuaji wa vitu vyote, na vilevile njia na mpangilio wa ukuaji wa vitu hivyo, na pia alitunga njia za kuwepo kwa vitu vyote duniani, ili viweze kuishi kwa kuendelea na kutegemeana. Kwa mbinu na sheria hizi, vitu vyote vinaweza kuwepo na kukua katika nchi hii kwa ufanisi na kwa amani. Ni kwa kuwa tu na mazingira kama haya ndipo wanadamu wanaweza kuwa na makao na mazingira ya kuishi yaliyo thabiti, na chini ya uongozi wa Mungu, waendelee kukua na kusonga mbele, kukua na kusonga mbele.
Wakati uliopita tulijadili kuhusu wazo la msingi la Mungu kupeana vitu vyote. Mungu kwanza huvipa vitu vyote kwa njia hii ili vitu vyote viwepo na kuishi kwa ajili ya wanadamu. Mazingira kama haya yapo kwa ajili ya sheria zilizotungwa na Mungu. Ni tu kwa Mungu kudumisha na kusimamia sheria kama hizi ndio wanadamu wana mazingira ya kuishi waliyonayo sasa. Tulichozungumzia wakati uliopita ni hatua kubwa kutoka kwa ufahamu wa Mungu tuliozungumzia awali. Kwa nini hatua kama hiyo ipo? Kwa sababu tulipozungumzia hapo awali kuhusu kuanza kumjua Mungu, tulikuwa tunajadili katika eneo la Mungu kuwaokoa na kuwasimamia wanadamu—yaani, uokoaji na usimamizi wa watu waliochaguliwa na Mungu—kuhusu kumjua Mungu, matendo ya Mungu, tabia Yake, kile Anacho na Alicho, makusudi Yake, na vile Anampa mwanadamu ukweli na uhai. Lakini mada tuliyozungumza kuihusu wakati uliopita haikujikita tu katika mipaka ya Biblia na katika eneo la Mungu kuwaokoa watu Wake waliochaguliwa. Badala yake, ilitoka nje ya eneo hili, nje ya Biblia, na nje ya mipaka ya hatua tatu za kazi ambayo Mungu anafanya kwa watu Wake waliochaguliwa na kujadili Mungu Mwenyewe. Hivyo basi ukisikia sehemu hii ya mawasiliano Yangu, lazima usiwekee mipaka ufahamu wako wa Mungu kwa Biblia na hatua tatu za kazi ya Mungu. Badala yake, unahitaji kuuweke wazi mtazamo wako na uone matendo ya Mungu na kile Anacho na alicho miongoni mwa vitu vyote, na vile Mungu anatawala na kusimamia vitu vyote. Kupitia kwa mbinu hii na juu ya msingi huu, unaweza kuona vile Mungu anapeana vitu vyote. Hii inawawezesha wanadamu kuelewa kwamba Mungu ni chanzo halisi cha uhai kwa vitu vyote na kwamba huu ni utambulisho halisi wa Mungu Mwenyewe. Hiyo ni kusema, utambulisho wa Mungu, hadhi na mamlaka na kila kitu Chake havilengwi tu kwa wale wanaomfuata Yeye wakati huu—kumaanisha havilengwi tu kwa ninyi watu—bali kwa vitu vyote. Basi ni nini eneo la vitu vyote? Eneo la vitu vyote ni pana sana. Ninatumia “vitu vyote” kueleza eneo la utawala wa Mungu juu ya vitu vyote kwa sababu Ninataka kuwaambia kwamba vitu vinavyotawaliwa na Mungu si vile mnavyoweza tu kuona kwa macho yenu, bali vinahusisha ulimwengu yakinifu ambao watu wote wanaweza kuuona, na vilevile ulimwengu mwingine usioweza kuonekana kwa macho ya binadamu nje ya ulimwengu yakinifu, na zaidi unahusisha anga na sayari nje ya mahali ambapo wanadamu wapo sasa. Hilo ni eneo la utawala wa Mungu juu ya vitu vyote, na wazo hili kwamba Mungu anatawala kila kitu. Eneo la utawala wa Mungu juu ya vitu vyote ni pana zaidi. Kwenu ninyi, mnachopaswa kuelewa, mnachopaswa kuona, na kutoka kwa vitu mnavyopaswa kupata maarifa—hivi ndivyo kila mmoja wenu anayeketi hapa anahitaji na ni lazima aelewe, aone, na awe na hakika navyo. Ingawa eneo la hivi “vitu vyote” ni pana, Sitawaambia kuhusu eneo msiloweza kuona kabisa au msiloweza kukutana nalo. Nitawaambia tu kuhusu eneo ambalo binadamu wanaweza kukutano nalo, wanaweza kuelewa, na wanaweza kufahamu, ili kila mmoja aweze kuhisi maana halisi ya kirai hiki “Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote.” Hivyo, chochote Ninachowasilisha kwenu hakitakuwa maneno matupu. Wakati uliopita, Nilitumia mbinu ya kuhadithia ili kutoa maelezo rahisi ya jumla ya mada hii “Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote,” ili muwe na ufahamu wa msingi wa jinsi Mungu huvipa vitu vyote. Ni nini kusudi la kuwafundisha kidogokidogo wazo hili la msingi? Ni kuwafanya mjue kwamba, nje ya Biblia na hatua tatu za kazi Yake, Mungu pia anafanya hata kazi nyingi zaidi ambayo wanadamu hawawezi kuiona au kukutana nayo. Kazi kama hiyo inatendwa binafsi na Mungu. Kama Mungu angekuwa anaongoza tu watu Wake waliochaguliwa kwenda mbele, bila hii kazi iliyo nje ya kazi Yake ya usimamizi, basi ingekuwa vigumu sana kwa ubinadamu huu, pamoja na ninyi nyote, kuendelea kusonga mbele, na ubinadamu huu na ulimwengu huu haungeweza kuendelea kukua. Huo ndio umuhimu wa kirai hiki “Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote” Ninachowasilisha kwenu siku hii.
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
Kujua zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni