Jumapili, 18 Februari 2018

1. Mazingira ya Kuishi ya Msingi Ambayo Mungu Anawaumbia Wanadamu | (2) Halijoto

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, neema,
Joto - unyoosha kwenye jua

Umeme wa Mashariki | (2) Halijoto

Mwenyezi Mungu alisema, Kitu cha pili ni halijoto. Kila mtu anajua halijoto ni nini. Halijoto ni kitu ambacho mazingira yanayofaa kuishi kwa wanadamu ni lazima yawe nacho. Ikiwa halijoto iko juu sana, tuseme ikiwa halijoto iko juu zaidi ya nyuzi 40 Selisiasi, basi itakuwa yenye taabu kwa wanadamu kuishi. Je, haitakuwa ya kumaliza sana? Je, na halijoto ikiwa chini sana, na kufikia nyuzi hasi 40 Selisiasi? Wanadamu hawataweza pia kuistahimili. Kwa hiyo, Mungu alikuwa mwangalifu sana katika kuviweka vipimo hivi vya halijoto. Vipimo vya halijoto ambavyo mwili wa mwanadamu unaweza kufanya mabadiliko kimsingi ni nyuzi hasi 30 Selisiasi hadi nyuzi 40 Selisiasi. Hiki ndicho kipimo cha halijoto cha msingi kutoka kaskazini mpaka kusini. Katika maeneo ya baridi, halijoto inaweza kufika nyuzi hasi 50 Selisiasi. Eneo kama hilo si mahali ambapo Mungu anamruhusu mwanadamu kuishi. Mbona kuna maeneo ya baridi hivyo? Katika hayo kuna hekima na makusudi ya Mungu. Hakuruhusu kusonga karibu na sehemu hizo. Mungu hulinda sehemu zilizo na joto sana na baridi sana, kumaanisha Hayuko tayari kumruhusu mwanadamu kuishi huko. Si kwa wanadamu. Kwa nini akaruhusu sehemu kama hizo kuwepo duniani? Ikiwa Mungu hangemruhusu mwanadamu kuishi au kuwepo huko, basi kwa nini akaziumba? Hekima ya Mungu imo humo. Yaani, halijoto ya msingi ya mazingira ya kuendelea kuishi kwa mwanadamu pia imerekebishwa na Mungu vya kutosha. Kuna sheria hapa pia. Mungu aliumba vitu vingine kusaidia kudumisha halijoto kama hiyo, kudhibiti halijoto hiyo. Ni vitu gani vinatumiwa kudumisha halijoto hii? Kwanza kabisa, jua linaweza kuwaletea watu uvuguvugu, lakini watu hawataweza kustahimili iwapo ni vuguvugu sana. Je, kuna kifaa chochote duniani kinachoweza kusonga karibu na jua? (La.) Mbona? Ni joto sana. Kitayeyuka. Kwa hiyo, Mungu pia ametengeneza kipimo maalum cha umbali wa jua kutoka kwa wanadamu. Mungu ana kiwango cha umbali huu. Vilevile kuna Ncha ya kusini na Ncha ya Kaskazini za dunia. Kuna nini katika Ncha ya Kusini na Ncha ya Kaskazini? Kote kuna mito ya barafu. Wanadamu wanaweza kuishi juu ya mito ya barafu? Inafaa kuishi kwa wanadamu? (La.) La, hivyo hutaenda huko. Kwa vile huendi katika Ncha za Kusini na Kaskazini, mito ya barafu itahifadhiwa, na itaweza kufanya wajibu wake, ambao ni kudhibiti halijoto. Unaelewa? Ikiwa hakuna Ncha za Kusini na Kaskazini na jua linawaka juu ya dunia kila wakati, basi watu wote juu ya dunia watakufa kutokana na joto. Je, Mungu hutumia tu vitu hivi viwili kudhibiti halijoto? La, Hatumii tu vitu hivi viwili kudhibiti halijoto inayofaa kuishi kwa wanadamu. Pia kuna kila aina za viumbe vyenye uhai, kama vile nyasi juu ya mbuga za malisho, aina mbalimbali za miti na kila aina ya mimea iliyo ndani ya misitu. Vinafyonza joto la jua na kusanisi nishati ya joto ya jua kurekebisha halijoto ambayo wanadamu wanaishi ndani. Pia kuna vyanzo vya maji, kama vile mito na maziwa. Sehemu ya juu ya mito na maziwa si kitu kinachoweza kuamuliwa na yeyote. Je, kuna yeyote anayeweza kudhibiti kiasi cha maji yaliyo juu ya dunia, wapi maji hayo yanatiririka, mwelekeo wa kutiririka huko, wingi wa maji hayo, au spidi ya mtiririko huo? Hakuna anayeweza kuidhibiti. Mungu pekee ndiye ajuaye. Vyanzo hivi mbalimbali vya maji, yakiwemo maji ya chini ya ardhi na mito na maziwa yaliyo juu ya ardhi ambayo watu wanaweza kuona, yanaweza pia kurekebisha halijoto ambayo wanadamu wanaishi ndani. Mbali na hayo, kuna kila aina ya uumbaji wa kijiografia, kama vile milima, tambarare, korongo kuu na ardhi ya majimaji. Sehemu ya juu na ukubwa wa uumbaji huu mbalimbali wa kijiografia vinaweza vyote kudhibiti halijoto. Kwa mfano, ikiwa mlima huu una nusu kipenyo cha kilomita 100, kilomita hizi 100 zitakuwa na athari ya kilomita 100. Lakini kuhusu safu za milima na korongo kuu ngapi kama hizo ambazo Mungu ameumba juu ya dunia, hili ni jambo ambalo Mungu amelifikiria kabisa. Kwa maneno mengine, nyuma ya kuwepo kwa kila kitu kilichoumbwa na Mungu kuna hadithi, na pia ina hekima na mipango ya Mungu. Tuseme, kwa mfano, misitu na kila aina ya mimea—sehemu ya juu na ukubwa wa sehemu ambamo vinakua haviwezi kudhibitiwa na mwanadamu yeyote, wala mwanadamu yeyote hana usemi wa mwisho kuhusu vitu hivi. Kiasi cha maji ambayo vinafyonza, kiasi cha nishati ya joto ambayo vinafyonza kutoka kwa jua pia haviwezi kudhibitiwa na mwanadamu yeyote. Vitu hivi vyote viko katika eneo la kile kilichopangwa na Mungu alipoumba vitu vyote.
Ni kwa sababu tu ya upangaji wa makini, fikira, na utaratibu wa Mungu katika vipengele vyote ndio mwanadamu anaweza kuishi katika mazingira yaliyo na halijoto ya kufaa hivyo. Kwa hiyo, kila kitu ambacho mwanadamu anakiona kwa macho yake, kama vile jua, au Ncha za Kusini na Kaskazini ambazo watu mara nyingi husikia kuzihusu, vilevile viumbe mbalimbali vilivyo hai juu na chini ya ardhi na ndani ya maji, na sehemu za juu zenye misitu na aina zengine za mimea, na vyanzo vya maji, mikusanyiko mbalimbali ya maji, kuna kiasi gani cha maji chumvi na maji baridi, kuongezea mazingira mbalimbali ya kijiografia—Mungu hutumia vitu hivi kudumisha halijoto ya kawaida kwa kuishi kwa mwanadamu. Hii ni thabiti. Ni kwa sababu tu Mungu ana fikira kama hizi ndio mwanadamu anaweza kuishi katika mazingira yaliyo na halijoto ya kufaa hivyo. Haiwezi kuwa baridi zaidi wala joto zaidi: sehemu zenye joto zaidi na ambapo halijoto inazidi kile ambacho mwili wa mwanadamu unaweza kubadilikia bila shaka hazijatayarishwa na Mungu kwa ajili yako. Sehemu zenye baridi zaidi na ambapo halijoto ni ya chini zaidi; sehemu ambazo, punde tu wanadamu wanapowasili, zitawafanya wagande sana baada ya dakika chache mpaka wasiweze kuzungumza, ubongo wao utaganda, wasiweze kufikiri, na hatimaye watakosa hewa—sehemu kama hizo pia hazijatayarishwa na Mungu kwa ajili ya wanadamu. Haijalishi ni aina gani ya uchunguzi wanadamu wanataka kufanya, au kama wanataka kuvumbua au wanataka kutengua mipaka hiyo—haijalishi watu wanafikiria nini, hawataweza kamwe kuzidi mipaka ya kile ambacho mwili wa mwanadamu unaweza kubadilikia. Hawataweza kuondoa mipaka hiyo ambayo Mungu alimuumbia mwanadamu. Kwa vile Mungu aliwaumba wanadamu, Mungu anajua bora zaidi ni halijoto gani mwili wa mwanadamu unaweza kubadilikia. Je, wanadamu wenyewe wanajua? (La.) Mbona unasema wanadamu hawajui? Ni mambo gani ya upumbavi ambayo wanadamu wamefanya? Je, hakujakuwa na watu wachache ambao kila mara wanataka kushindana na Ncha za Kaskazini na Kusini? Kila mara wanataka kwenda huko kumiliki ardhi hiyo, ili waweze kukita mizizi na kuiendeleza. Je, hiki si kitendo cha kujiangamiza? (Ndiyo.) Tuseme umechunguza kikamilifu Ncha za Kusini na Kaskazini. Lakini hata kama unaweza kubadilikia halijoto hiyo, je, kubadilisha mazingira ya kuishi na mazingira ya kuendelea kuishi ya Ncha za Kusini na Kaskazini kungemfaidi mwanadamu kwa njia yoyote? Je, utafurahi ikiwa barafu ya Ncha za Kusini na Kaskazini itayeyuka? Hili ni la kushangaza. Ni kitendo cha upuuzi. Wanadamu wana mazingira wanayoweza kuendelea kuishi ndani, lakini hawawezi tu kukaa hapa kimya na kwa uangalifu, na wanapaswa kwenda wasikoweza kuendelea. Kwa nini ni hivyo? Wamechoshwa na kuishi katika halijoto hii ya kufaa. Wamefurahia baraka nyingi sana. Mbali na hayo, haya mazingira ya kuishi ya kawaida yameharibiwa kiasi sana na wanadamu, hivyo wanaweza basi kwenda kwa Ncha ya Kusini na Ncha ya Kaskazini ili wafanye madhara mengi zaidi au kujihusisha katika “kusudi,” fulani ili waweze kuwa “watangulizi” wa aina fulani. Si huu ni upumbavu? Chini ya uongozi wa babu yao Shetani, wanadamu hawa wanaendelea kufanya kitu kimoja cha upuuzi baada ya kingine, wakiharibu bila hadhari na kwa utukutu makao mazuri ambayo Mungu aliwaumbia wanadamu. Hili ndilo Shetani alifanya. Zaidi ya hayo, kwa kuona kwamba kuendelea kuishi kwa wanadamu duniani kuko katika hatari kidogo, watu wengi sana wanataka kutafuta njia za kwenda kuishi juu ya mwezi, kutafuta njia ya kuondoka kwa kuona ikiwa wanaweza kuishi huko. Hatimaye, ni nini kinakosekana huko? (Oksijeni.) Je, wanadamu wanaweza kuendelea kuishi bila oksijeni? (La.) Kwa vile mwezi hauna oksijeni, si mahali ambapo mwanadamu anaweza kuishi huko, ilhali mwanadamu anaendelea kutaka kwenda huko. Hii ni nini? (Ni kujiangamiza na kutafuta taabu.) Ni kujiangamiza, sivyo? Ni mahali pasipo na hewa, na halijoto haifai kwa kuendelea kuishi kwa mwanadamu, hivyo hapajatayarishwa na Mungu kwa ajili ya mwanadamu.
Halijoto ambayo tumezungumzia ni kitu ambacho watu wanaweza kukutana nacho katika maisha yao ya kila siku. “Hali ya hewa ni nzuri sana leo, nyuzi 23 Selisiasi. Hali ya hewa ni angavu, anga haina mawingu, na hewa inaburudisha. Vuta pumzi ya hewa safi. Jua linawaka. Jinyoshe chini ya mwanga wa jua. Ninajisikia vizuri!” Au “Leo hali ya hewa ni baridi sana. Ukinyosha nje mikono yako itaganda mara moja. Kuna baridi kali, hivyo usikae nje muda mrefu. Harakisha na urudi, usije ukaganda!” Halijoto ni kitu ambacho miili yote ya wanadamu inaweza kuhisi, lakini hakuna anayefikiria vile halijoto hii iliumbwa, au ni nani anasimamia na kudhibiti halijoto ya kufaa kuishi kwa wanadamu. Hiki ndicho tunaanza kujua sasa. Je, kuna hekima ya Mungu katika hili? Je, kuna kitendo cha Mungu katika hili? (Ndiyo.) Ukifikiria kwamba Mungu aliumba mazingira yenye halijoto ya kufaa kuishi kwa wanadamu, je, hii ni njia moja ambayo Mungu huvipa vitu vote? Ndiyo kweli. Hii inaonyesha kwamba upaji na usimamiaji wa vitu vyote na Mungu kweli ni wa utendaji!
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni