Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Imepangwa-kwa-makini. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Imepangwa-kwa-makini. Onyesha machapisho yote

Jumapili, 18 Februari 2018

1. Mazingira ya Kuishi ya Msingi Ambayo Mungu Anawaumbia Wanadamu | (2) Halijoto

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, neema,
Joto - unyoosha kwenye jua

Umeme wa Mashariki | (2) Halijoto

Mwenyezi Mungu alisema, Kitu cha pili ni halijoto. Kila mtu anajua halijoto ni nini. Halijoto ni kitu ambacho mazingira yanayofaa kuishi kwa wanadamu ni lazima yawe nacho. Ikiwa halijoto iko juu sana, tuseme ikiwa halijoto iko juu zaidi ya nyuzi 40 Selisiasi, basi itakuwa yenye taabu kwa wanadamu kuishi. Je, haitakuwa ya kumaliza sana? Je, na halijoto ikiwa chini sana, na kufikia nyuzi hasi 40 Selisiasi? Wanadamu hawataweza pia kuistahimili. Kwa hiyo, Mungu alikuwa mwangalifu sana katika kuviweka vipimo hivi vya halijoto. Vipimo vya halijoto ambavyo mwili wa mwanadamu unaweza kufanya mabadiliko kimsingi ni nyuzi hasi 30 Selisiasi hadi nyuzi 40 Selisiasi. Hiki ndicho kipimo cha halijoto cha msingi kutoka kaskazini mpaka kusini.