Ijumaa, 9 Februari 2018

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III | 10. Hukumu ya Wafarisayo kwa Yesu | 11. Wafarisayo Kukemewa na Yesu

Umeme wa Mashariki | 10. Hukumu ya Wafarisayo kwa Yesu | 11. Wafarisayo Kukemewa na Yesu

10. Hukumu ya Wafarisayo kwa Yesu.
(Marko 3:21-22) Na rafiki zake waliposikia kulihusu, wakatoka kwenda kumkamata: kwa maana walisema, Amerukwa na akili. Na waandishi walioshuka kutoka Yerusalemu wakasema, Ana Beelzebuli, na kwa mwana wa kifalme wa pepo huwatoa pepo.
11. Wafarisayo Kukemewa na Yesu.
(Mat 12:31-32) Ndiyo maana nawaambia, Kila aina ya dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu: lakini kumkufuru Roho Mtakatifu hawatasamehewa wanadamu. Na mtu yeyote atakayenena neno dhidi ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yule atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa, katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.
(Mat 23:13-15) Lakini ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni: Kwani nyinyi wenyewe hamwingii, wala wanaoingia manaowatesa hamwaachi waingie. Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnakula nyumba za wajane, na kwa unafiki mnasali sala ndefu; kwa hiyo mtapata hukumu iliyo kubwa zaidi. Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnazunguka katika bahari na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja kuwa mwongofu, na akiisha kufanyika, mnamfanya kuwa mwana wa jehanamu mara mbili zaidi kuwaliko nyinyi wenyewe.
    Kunazo dondoo mbili tofauti hapo juu—hebu kwanza tuangalie dondoo ya kwanza: Hukumu ya Wafarisayo kwa Yesu.
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Yesu,
Bwana aliwakemea Mafarisayo



    Mwenyezi Mungu alisema, Katika Biblia, tathmini ya Wafarisayo kwa Yesu Mwenyewe na mambo alioyafanya ilikuwa: “kwa maana walisema, Amerukwa na akili. … Ana Beelzebuli, na kwa mwana wa kifalme wa pepo huwatoa pepo.” (Marko 3:21-22). Hukumu ya waandishi na Wafarisayo kwa Bwana Yesu haikuwa ikikasuku mambo au ikifikiria tu kutoka popote—ilikuwa hitimisho yao kuhusu Bwana Yesu kutokana na yale walioyaona na kuyasikia kuhusu vitendo Vyake. Ingawa hitimisho yao ilitolewa kwa njia isiyo ya kweli au ya uongo kwa jina la haki, na kuonekana mbele ya watu ni kana kwamba ilikuwa imeshughulikiwa-vyema, kiburi ambacho walitumia kumhukumu Bwana Yesu kilikuwa kigumu hata kwa wao wenyewe kuvumilia. Nguvu zao mchafukoge za chuki yao kwa Bwana Yesu ziliweza kufichua maono yao binafsi yasiyo na mipaka na sura zao za kishetani na uovu, pamoja na maumbile yao yenye nia mbaya ya kumpinga Mungu. Mambo haya waliyoyasema katika hukumu yao kwa Bwana Yesu yaliendeshwa na maono yao yasiyo na misingi, ya wivu, na hali ya ubovu na ubaya na ukatili wao dhidiya Mungu na ukweli. Hawakuchunguza chanzo cha hatua za Bwana Yesu wala kuchunguza kiini cha kile Alichosema au kufanya. Badala yake, walimshambulia bila mpango, bila subira, kwa njia za kishenzi, na kwa makusudi ya kijicho pamoja na kutupilia mbali kile Alichokuwa Amefanya. Hii ilikuwa hadi kufikia kiwango cha kutupilia mbali Roho Wake bila kubagua, Yaani, Roho Mtakatifu, Roho wa Mungu. Hivi ndivyo waliyomaanisha waliposema “Amerukwa na akili,” “Beelzebuli na mkuu wa pepo.” Hii ni kusema kwamba walisema Roho wa Mungu alikuwa Beelzebuli na pia mkuu wa pepo. Waliweza kupatia sifa ya kazi ambayo Roho wa Mungu kuwa mwili uliokuwa umevalia na kurukwa akili. Hawakukufuru tu Roho wa Mungu kama Beelzebuli na mkuu wa pepo, lakini waliishutumu kazi ya Mungu. Walimshutumu na kumkufuru Bwana Yesu Kristo. Kiini cha upingaji wao na kukufuru Mungu kilikuwa sawa kabisa na kiini cha Shetani na upingaji wa Shetani na kumkufuru Mungu. Wao hawakuwakilisha wanadamu waliopotoka tu, lakini hata zaidi walikuwa mfano halisi wa Shetani. Walikuwa ni njia ya Shetani kutumia miongoni mwa wanadamu, na walikuwa washiriki na wajumbe wa Shetani. Kiini cha kukufuru kwao na utovu wao wa nidhamu kwa Bwana Yesu Kristo ndicho kilichokuwa mapambano yao na Mungu kwa ajili ya hadhi, mashindano yao na Mungu, na mapambano yao na Mungu yasiyoisha. Kiini cha upingaji wao kwa Mungu na mwelekeo wao wa ukatili kwake Yeye, pamoja na maneno yao na fikira zao moja kwa moja vilimkufuru na kumghadhabisha Roho wa Mungu. Hivyo basi, Mungu aliamua hukumu inayofaa ya na yale waliyoyasema na kufanya, na akaamua matendo yao kuwa dhambi ya kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu. Dhambi hii haiwezi kusameheka ulimenguni humu na hata baadaye, kama vile tu maandiko yafuatayo yanasema: “Kila neno la kumkufuru Roho Mtakatifu hawatasamehewa wanadamu” na “atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa, katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.” Leo, hebu tuzungumzie maana halisi ya maneno haya kutoka kwa Mungu “hatasamehewa, katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.” Hii ni kuweka wazi namna ambavyo Mungu hukamilisha matamshi yake “hatasamehewa, katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.”
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Bwana Yesu,
Waandishi walitawala na kumtukana kiburi cha Bwana Yesu




Kila kitu ambacho tumezungumzia kuhusu yote haya kinahusiana na tabia ya Mungu, na mweleko Wake kwa watu, masuala na mambo, na mambo. Kikawaida, dondoo hizo mbili hapo juu haziwezi kuachwa. Je, ulitambua chochote katika dondoo hizi mbili za maandiko? Baadhi ya watu husema wanaiona ghadhabu ya Mungu. Baadhi ya watu husema wanauoa upande wa tabia ya Mungu ambayo haivumilii kosa la wanadamu, na kwamba watu wakifanya kitu ambacho kinamkufuru Mungu, hawatapatamsamaha Wake. Licha ya hoja kwamba watu wanaona na kutambua ghadhabu na kutovumilia makosa ya wanadamu kwa Mungu katika dondoo hizi mbili, bado hawaelewi kwa kweli mtazamo Wake. Dondoo hizi mbili zinao ufafanuzi wa mwelekeo na mtazamo wa kweli wa Mungu kwa wale wanaomkufuru na kumghadhabisha Yeye. Dondoo hii katika maandiko inashikilia maana halisi ya mwelekeo na mtazamo Wake: “yule atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa, katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.” Watu wanapomkufuru Mungu, wakati wanapomghadhabisha Yeye, Yeye hutoa hukumu, na hukumu hii ndiyo matokeo Yake ya mwisho. Hali hii inafafanuliwa hivi katika Biblia: “Ndiyo maana nawaambia, Kila aina ya dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu: lakini kumkufuru Roho Mtakatifu hawatasamehewa wanadamu” (Mat 12:31), na “Ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, wanafiki!” (Mat 23:13). Hata hivyo, imerekodiwa katika Biblia matokeo yapi yalikuwepo kwa wale waandishi na Mafarisayo, pamoja na wale watu waliosema Alikuwa amerukwa na akili baada ya Bwana Yesu kuyasema mambo hayo? Je, imerekodiwa kama walipata adhabu yoyote? Kuna uhakika kwamba hakukuwa na adhabu: Kusema hapa kwamba “hakukuwa” si kwamba haikurekodiwa, lakini kwa hakika hakukuwa na matokeo yoyote ambayo yangeonekana kwa macho ya binadamu. Neno hili “hakukuwa” linaelezea suala, yaani, mwelekeo na kanuni za Mungu katika kushughulikia mambo fulani. Namna ambavyo Mungu anawatendea watu wanaomkufuru au hata wanaompinga Yeye, au hata wale wanaomkashifu Yeye—watu wanaomshambulia kimakusudi, kumkashifu, na kumlaani Yeye—hajifanyi kwamba kila kitu kiko sawa. Anao mwelekeo wazi kwa hawa. Anawadharau watu hawa, na moyoni Mwake anawashutumu. Anatangaza waziwazi hata matokeo kwa ajili yao, ili watu waweze kujua kwamba Anao mwelekeo wazi kwao wanaomkufuru Yeye, na ili wajue namna atakavyoamua matokeo yao. Hata hivyo, baada ya Mungu kusema mambo haya, watu bado wangeona kwa nadra ukweli wa namna ambavyo Mungu angeshughulikia watu hao, na wasingeelewa kanuni zinazotawala matokeo ya Mungu, hukumu Yake kwao. Hiyo ni kusema, wanadamu hawawezi kuuona mwelekeo na mbinu fulani za Mungu katika kuwashughulikia. Hali hii inahusu kanuni za Mungu za kufanya mambo. Mungu hutumia ujio wa hoja katika kushughulikia tabia yenye uovu ya baadhi ya watu. Yaani, hatangazi dhambi yao na haamui matokeo yao, lakini Anatumia moja kwa moja ujio wa hoja ili kuwaruhusu kuadhibiwa, wao kupata adhabu wanayostahili. Wakati hoja hizi zinapofanyika, ni miili ya watu inayoteseka kwa adhabu; hili ni jambo ambalo linaweza kuonekana kwa macho ya binadamu. Wakati wa kushughulikia tabia ya uovu kwa baadhi ya watu, Mungu huwalaani tu kwa matamshi, lakini wakati uo huo, ghadhabu ya Mungu huwapata, na adhabu wanayopokea inaweza kuwa jambo ambalo watu hawalioni, lakini aina hii ya matokeo inaweza kuwa hata mbaya zaidi kuliko matokeo ambayo watu wanaweza kuona ya kuadhibiwa au kuuawa. Hii ni kwa sababu katika hali zile ambazo Mungu ameamua kutomwokoa mtu wa aina hii, kutoonyesha tena rehema au uvumilivu kwao, kutowapa fursa zaidi, mwelekeo Anaouchukua kwao ni kuwaweka pembeni. Ni nini maana ya “kuweka pembeni”? Maana ya kauli hii kibinafsi ni kuweza kitu kwa upande mmoja, kutokimakinikia tena. Hapa, wakati Mungu “anapoweka pembeni” kuna fafanuzi mbili tofauti kuhusu kile Alicho: Ufafanuzi wa kwanza ni kwamba Amempa Shetani kuyashugulikia maisha ya mtu huyo, na kila kitu cha mtu huyo. Mungu hatamwajibikia tena na hataweza kumsimamia tena. Kama mtu huyo amerukwa na akili, au ni mpumbavu, na kama katika maisha au kifo, au kama angeshushwa jahanamu ili kupata adhabu yake, hayo yote yasingemhusu Mungu. Hiyo ingemaanisha kwamba kiumbe hicho hakitakuwa na uhusiano wowote na Muumba. Ufafanuzi wa pili ni kwamba Mungu ameamua kwamba Yeye Mwenyewe anataka kufanya kitu na mtu huyu, kwa mikono Yake mweyewe. Inawezekena kwamba Ataweza kutumia jitihada za mtu wa aina hii, au kwamba atatumia mtu wa aina hii kama foili[b] . Inawezekana kwamba Atakuwa na njia maalum ya kushughulikia mtu wa aina hii, njia maalum ya kumshughulikia—kama tu Paulo. Hii ndio kanuni na mwelekeo katika moyo wa Mungu kuhusu namna Alivyoamua kumshughulikia mtu wa aina hii. Hivyo basi wakati watu wanapompinga Mungu, na kumkashifu na kumkufuru Yeye, kama wataendelea kusema ubaya kuhusu tabia Yake, au kama watafikia ile hali ya kimsingi ya Mungu, athari zake hazifikiriki. Athari zile mbaya zaidi ni kwamba Mungu anayakabidhi maisha yao na kila kitu chao kwa Shetani, mara moja na kabisa. Hawatasamehewa daima dawamu. Hii inamaanisha kwamba mtu huyu amekuwa chakula katika kinywa cha Shetani, mwanasesere katika mikono yake, na kuanzia hapo, Mungu hahusiki naye. Unaweza kufikiria ni aina gani ya masikitiko iliyokuweko wakati Shetani alipomjaribu Ayubu? Katika hali kwamba Shetani hakuruhusiwa kuyadhuru maisha ya Ayubu, hata hivyo, Ayubu aliteseka pakubwa. Na huoni kwamba ni ngumu hata zaidi kufikiria kupitia kwa mateso ya Shetani namna ambavyo mtu atakavyopitia ambaye amekabidhiwa Shetani kabisa, ambaye yumo katika mashiko ya Shetani kabisa, ambaye amepoteza kabisa utunzaji na rehema ya Mungu, ambaye hayuko tena katika utawala wa Muumba, ambaye amenyang’anywa haki ya kumwabudu Yeye, na haki ya kuwa kiumbe katika utawala wa Mungu, ambaye uhusiano wake na Bwana wa uumbaji umekatizwa kabisa? Kuteswa kwa Ayubu na Shetani kulikwa jambo ambalo lingeonekana kwa macho ya binadamu, lakini Mungu anapomkabidhi Shetani maisha ya mtu, athari zake zitakuwa jambo ambalo mtu hawezi kufikiria. Ni sawa tu na baadhi ya watu kuweza kuzaliwa tena wakiwa ng’ombe, au punda, au baadhi ya watu wakichukuliwa kabisa, na kumilikiwa na roho chafu, za uovu, na kadhalika. Haya ndiyo matokeo, mwisho wa baadhi ya watu ambao Mungu anawakabidhi kwa Shetani. Kwa nje, yaonekana kwamba watu hao waliomdhihaki, waliomkashifu, kumshutumu, na kumkufuru Bwana Yesu hawakupata athari zozote. Hata hivyo, ukweli ni kwamba Mungu Anao mwelekeo wa kushughulikia kila kitu. Huenda Asitumie lugha wazi kuwaambia watu matokeo ya namna Anavyowashughulikia kila aina ya watu. Wakati mwingine Haongei kwa njia ya moja kwa moja, lakini Anafanya mambo kwa njia ya moja kwa moja. Kwamba haongelei jambo haimaaishi kwamba hakuna matokeo—yawezekana kwamba matokeo ni mabaya zaidi. Inavyoonekana, yaelekea Mungu haongei na watu fulani ili kufichua mwelekeo Wake; kwa uhakika, Mungu hajataka kuwaza juu yao kwa muda mrefu. Hataki kuwaona tena. Kwa sababu ya mambo ambayo wamefanya, tabia yao, kwa sababu ya asili yao na kiini chao, Mungu anawataka tu watoweke machoni Mwake, Anataka kuwakabidhi moja kwa moja kwa Shetani, kumpa Shetani roho yao, nafsi yao na mwili wao, kumruhusu Shetani kufanya atakacho. Ni wazi ni hadi kiwango gani Mungu anawachukia, ni hadi kiwango gani Ameudhika nao. Kama mtu atamgabadhisha Mungu kufikia kiwango ambacho Mungu hataki kumwona tena, kwamba Atakata tamaa kabisa naye, hadi katika kiwango ambacho Mungu hataki tena kushugulika naye Yeye mwenyewe—kama itafikia kiwango hiki ambapo Atawakabidhi kwa Shetani ili aweze kufanya apendavyo, kumruhusu Shetani kumdhibiti, kumtumia, na kumtendea kwa njia yoyote-mtu huyu kwa kweli amemalizika. Haki yake ya kuwa binadamu imebatilishwa kabisa, na haki yake ya kuwa kiumbe imefikia mwisho. Je, huoni kwamba hii ndio adhabu mbaya zaidi?
Yote haya yaliyo hapo juu ni maelezo kamilifu ya maneno: “hatasamehewa, katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao,” na pia ni utoaji maoni mwepesi kuhusu dondoo za maandiko haya. Nafikiri ya kwamba unao ufahamu wake sasa!
Sasa hebu tusome dondoo za maandiko zilizo hapa chini.
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
Jifunze zaidi: Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni