Kanisa la Mwenyezi Mungu Lilikujaje Kuwepo? |
Kanisa la Mwenyezi Mungu Lilikujaje Kuwepo?
Kama makanisa ya Ukristo, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilikuja kuwepo kwa sababu ya kazi ya Mungu kupata mwili. Makanisa ya Ukristo yalipata kuwepo kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Bwana Yesu aliyepata mwili, na Kanisa la Mwenyezi Mungu lilipata kuwepo kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu mwenye mwili wa siku za mwisho. Hivyo, makanisa kotekote katika enzi yamefanyizwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mungu Aliyepata mwili. Kazi ya kila hatua ya kupata mwili kwa Mungu huonyesha ukweli mwingi, na watu wengi hupata kukubali na kufuata Mungu kwa sababu ya ukweli huu unaoonyeshwa na Mungu, hivyo ukisababisha makanisa. Kutokana na hili inaweza kuonekana kwamba makanisa huanzishwa kutoka kwa wale wanaoikubali kazi ya Mungu na kumfuata Mungu. Mikusanyiko hii ya wateule wa Mungu inaitwa makanisa.
Makanisa ya Ukristo yaliletwa na kuonekana na kazi ya Bwana Yesu mwenye mwili miaka elfu mbili iliyopita. Bwana Yesu alihubiri, “Tubuni nyinyi: kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia” (Mat 4:17), na Alifanya kazi ya ukombozi, na kuonyesha ukweli ambao watu wa Enzi ya Neema iliwalazimu kuweka katika vitendo na kuingia ndani, kisha watu wengi wakaanza kumwamini na kumfuata Bwana, na hivyo makanisa ya wakati huo yakaja kuwepo. Baadaye, injili ya Bwana Yesu ikaenea kwa kila nchi na eneo, mpaka siku za mwisho ilipokuwa imeenea kwa miisho ya dunia, na makanisa ya kikristo yakaibuka katika kila nchi. Haya yalikuwa ndiyo makanisa ya Enzi ya Neema. Katika hatua za mwisho za siku za mwisho, Mwenyezi Mungu mwenye mwili hutokea na kufanya kazi hina Bara. Juu ya msingi wa kazi ya ukombozi wa Bwana Yesu wakati wa Enzi ya Neema, Mwenyezi Mungu hutekeleza kazi ya “lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu” (1 Petro 4:17) ilivyotabiriwa katika Biblia. Kwa wanadamu wote, Mwenyezi Mungu huonyesha mafumbo yote ya mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita, na huonyesha ukweli wote kwa ajili ya utakaso na wokovu wa wanadamu. Kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho, watu wengi kutoka kwa kila kikundi na madhehebu ya ulimwengu wa kidini, watu ambao wameamini katika Bwana kwa miaka mingi, mwishowe wameisikia sauti ya Mungu na kuona kwamba Bwana Yesu amekuja na ametekeleza kazi ya hukumu ya siku za mwisho. Wamethibitisha kwamba Mwenyezi Mungu ni kurudi kwa Bwana Yesu, na kwa sababu ya hili wamekubali kazi Mwenyezi Mungu ya siku ya mwisho. Katika China Bara, angalau watu milioni kadhaa (makumi ya mamilioni kulingana na takwimu kutoka kwa Serikali ya Kikomunisti ya China) wamekubali na sasa wanamfuata Mwenyezi Mungu. Hivyo, Kanisa la Mwenyezi Mungu lote ni matokeo ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu. Lilianzishwa na Mwenyezi Mungu , na siyo na mtu yeyote. Kila Mkristo katika Kanisa la Mwenyezi Mungu anafahamu kikamilifu kwamba Mwenyezi Mungu ndiye kurudi kwa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho, na kuonekana kwa Mungu. Wakristo wa Kanisa la Mwenyezi Mungu huomba kwa jina la Mwenyezi Mungu. Wanayoyasoma, kusikiliza, na kufanyia ushirika ni maneno ya Mwenyezi Mungu, na yale wanayoshikilia ni ukweli wote ulioonyeshwa na Mwenyezi Mungu. Ukweli huu ni njia ya uzima wa milele ulioletwa na Mungu wakati wa siku za mwisho. Katika kazi Yake, Mungu mwenye mwili wa siku za mwisho pia Aliteua na kushuhudia binafsi kwa mtu aliyetumiwa na Mungu, ili aweze kushirikiana katika kazi ya Mungu–kama tu wakati Bwana Yesu alifanya kazi, Yeye binafsi aliwachagua na kuwateua mitume kumi na wawili. Watu hawa ambao hutumiwa na Mungu, hata hivyo, hushirikiana tu katika kazi ya Mungu, na wao hawana uwezo wa kufanya kazi badala ya Mungu. Makanisa hayakuanzishwa na wao, na yule ambaye wateule wa Mungu humwamini na kumfuata si wale ambao hutumiwa na Mungu. Makanisa ya Enzi ya Neema hayakuasisiwa na Paulo na wale mitume wengine, bali yalisababishwa na kazi ya Bwana Yesu; yalianzishwa na Bwana Yesu binafsi. Kadhalika, Kanisa la Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho pia halikuasisiwa na mtu aliyetumiwa na Mungu, lakini lilizaliwa kutoka kwa na kazi ya Mwenyezi Mungu. Lilianzishwa na Mwenyezi Mungu, na linaongozwa na Yeye Mwenyewe; mtu anayetumiwa na Mungu hunyunyizia tu, huruzuku, na kuongoza makanisa, akifanya kazi yake. Ingawa wateule wa Mungu huongozwa, kunyunyiziwa, na kukimiwa na mtu atumiwaye na Mungu, Yule ambaye wateule wa Mungu huamini na kufuata ni Mwenyezi Mungu–ambao ni ukweli usioweza kukanushwa na yeyote. Wengi katika Kanisa la Mwenyezi Mungu ni watu kutoka makundi na madhehebu tofauti ya kidini ambao wameamini katika Bwana kwa miaka mingi. Wote wanaelewa Biblia, na katika makundi na madhehebu hayo mbalimbali ya kidini wao hushuhudia kwamba Bwana Yesu amekuja, kwamba Yeye ni Mwenyezi Mungu, na amefanya kazi ya hukumu ya siku za mwisho. Kama matokeo ya kuona kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu ni ukweli, na sauti ya Mungu, watu wengi hupata kumkubali Mwenyezi Mungu. Wao ni kundi la kwanza la watu ambao hujikuta mbele ya Mungu. Kanisa la Mwenyezi Mungu lilizaliwa na watu wa Ukristo, Ukatoliki, na makundi mengine na madhehebu ya kidini ambao walikubali jina la Mwenyezi Mungu. Leo, watu wengi sana kutoka makundi na madhehebu mbalimbali na madhehebu ya kidini wameanza kuichunguza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, hivyo wakitimiza unabii katika Biblia kuwa “mataifa yote watauendea kwa wingi” (Isaya 2: 2). Hatimaye, wote ambao kwa hakika huamini katika Mungu lazima watarudi kwa Mwenyezi Mungu; hili haliepukiki, kwa sababu lilipangwa kitambo na Mungu, ni amri ya Mungu, na hakuna anayeweza kulibadilisha!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni