Alhamisi, 7 Juni 2018

Umeme wa Mashariki | Trela ya Filamu "Yule Anayeshikilia Ukuu juu ya Kila Kitu" | Ushuhuda wa Nguvu ya Mungu


Umeme wa Mashariki | Trela ya Filamu "Yule Anayeshikilia Ukuu juu ya Kila Kitu" | Ushuhuda wa Nguvu ya Mungu


Utambulisho


Throughout the vast universe, all celestial bodies move precisely within their own orbits. Under the heavens, mountains, rivers, and lakes all have their boundaries, and all creatures live and reproduce throughout the four seasons in accordance with the laws of life…. This is all so exquisitely designed—is there a Mighty One ruling and arranging all this? Since coming into this world crying we have begun playing different roles in life. We move from birth to old age to illness to death, we go between joy and sorrow…. Where does mankind really come from, and where will we really go? Who is ruling our fates? From ancient times to modern days, great nations have risen up, dynasties have come and gone, and countries and peoples have flourished and perished in the tides of history…. Just like the laws of nature, the laws of humanity's development contain infinite mysteries. Would you like to know the answers to them? The documentary The One Who Holds Sovereignty Over Everything will guide you to get to the root of this, to unveil all of these mysteries!

Ingawaje Binadamu Amepotoka, Angali Anaishi Chini ya Ukuu wa Mamlaka ya Muumba


Mwenyezi Mungu alisema, Shetani amekuwa akipotosha mwanadamu kwa maelfu ya miaka. Ameleta kiwango kisichosemezeka cha maovu, amedanganya vizazi baada ya vizazi, na ametenda uhalifu wa kuchukiza ulimwenguni. Amedhulumu binadamu, amedanganya binadamu, ameshawishi binadamu ili ampinge Mungu, na ametenda vitendo vya maovu ambavyo vimetatiza na kuharibu mpango wa Mungu mara kwa mara. Ilhali, chini ya mamlaka ya Mungu, viumbe vyote na viumbe vyenye uhai vinaendelea kutii kanuni na sheria zilizowekwa wazi na Mungu. Yakilinganishwa na mamlaka ya Mungu, asili ovu ya Shetani na kuenea kwake ni vitu vibaya mno, vinakera mno na ni vya kuleta aibu na ni vidogo mno na vinyonge. Hata ingawaje Shetani anatembea miongoni mwa viumbe vyote vilivyoumbwa na Mungu, hawezi kutekeleza mabadiliko madogo zaidi kwa watu, vitu, na vifaa vilivyoamriwa na Mungu. Miaka elfu kadhaa imepita, na mwanadamu angali anafurahia nuru na hewa aliyopewa na Mungu, angali anapumua pumzi iliyotolewa na Mungu Mwenyewe, angali anafurahia maua, ndege, samaki na wadudu walioumbwa na Mungu, na kufurahia viumbe vyote vilivyotolewa na Mungu; mchana na usiku zingali zinabadilishana nafasi zao bila kusita; hiyo misimu minne inabadilishana kama kawaida; nayo batabukini wanaopaa wanaondoka msimu huu wa kipupwe, lakini bado watarudi kwenye msimu ujao wa machipuko; samaki ndani ya maji hawajawahi kuondoka kwenye mito, maziwa—maskani yao; wadudu aina ya nyenje (cicadas) kwenye mchanga wanaimba kwelikweli kwenye siku za kiangazi; nyenje kwenye nyasi wanaimba kwa sauti ya polepole huku wakikaribisha msimu wa mapukutiko, wale batabukini wanaanza kutembea kwa makundi, huku nao tai wanabakia pweke; fahari za simba wakijitosheleza wenyewe kwa kuwinda; nao kunguni wa kaskazini wa ulaya hawatoki kwenye nyasi na maua…. Kila aina ya kiumbe kilicho hai miongoni mwa viumbe vyote kinaondoka na kurudi, kisha kinaondoka tena, mabadiliko milioni yanafanyika kwa muda wa kufumba na kufumbua—lakini kile kisichobadilika ni silika zao na sheria za kusalia. Wanaishi katika ruzuku na kustawishwa na Mungu, na hakuna mtu anayeweza kubadilisha silika zao, na vilevile hakuna mtu yeyote anayeweza kukiuka sheria hizi za kuishi. Ingawaje mwanadamu, anayeishi miongoni mwa viumbe vyote amepotoka na kudanganywa na shetani, angali hawezi kupuuza maji yaliyoumbwa na Mungu, hewa iliyoumbwa na Mungu, na vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu, na binadamu angali bado anaishi na kuzaana kwenye anga hii iliyoumbwa na Mungu. Silika za mwanadamu zingali hazijabadilika. Binadamu angali anategemea macho yake kuona, masikio yake kusikia, ubongo wake kufikiria, moyo wake kuelewa, miguu na viganja vyake kutembea, mikono yake kufanya kazi, na kadhalika; silika zote ambazo Mungu alimpa binadamu ili aweze kukubali toleo la Mungu limebakia hivyo bila kubadilishwa, welekevu ambao binadamu alitumia kushirikiana na Mungu bado haujabadilika, welekevu wa mwanadamu wa kutenda wajibu wa kiumbe kilichoumbwa haujabadilishwa, mahitaji ya kiroho ya mwanadamu hayajabadilika, tamanio la mwanadamu kuweza kujua asili zake halijabadilika, hamu ya mwanadamu kuweza kuokolewa na Muumba haijabadilika. Hizi ndizo hali za sasa za mwanadamu, anayeishi katika mamlaka ya Mungu, na ambaye amevumilia maangamizo mabaya yaliyoletwa na Shetani. Ingawaje mwanadamu amepitia unyanyasaji wa Shetani, na yeye si Adamu na Hawa tena kutoka mwanzo wa uumbaji, badala yake amejaa mambo ambayo yana uadui na Mungu kama vile maarifa, fikira na kadhalika, na amejaa tabia ya kishetani iliyopotoka, kwenye macho ya Mungu, mwanadamu yungali bado mwanadamu yule yule Aliyemuumba. Mwanadamu angali anatawaliwa na kupangiwa na Mungu, na angali anaishi ndani ya mkondo uliowekwa wazi na Mungu, na kwa hivyo kwenye macho ya Mungu, mwanadamu ambaye amepotoshwa na Shetani amefunikwa tu na uchafu na tumbo linalonguruma, na miitikio ambayo ni ya kujikokota kidogo, kumbukumbu ambayo si nzuri kama ilivyokuwa, na mwenye umri ulioongezeka kidogo—lakini kazi na silika zote za binadamu bado hazijapata madhara kamwe. Huyu ndiye mwanadamu ambaye Mungu ananuia kuokoa. Mwanadamu huyu anahitaji tu kusikia mwito wa Muumba na kusikia sauti ya Muumba, naye atasimama wima na kukimbia kutafuta ni wapi sauti imetokea. Mwanadamu huyu lazima tu aweze kuona umbo la Muumba naye hatakuwa msikivu wa kila kitu kingine, ataacha kila kitu, ili kuweza kujitolea mwenyewe kwa Mungu, na hata atayatenga maisha yake kwa ajili Yake. Wakati moyo wa mwanadamu unapoelewa maneno hayo ya moyoni kutoka kwa Muumba, mwanadamu atakataa Shetani na atakuja upande wake Muumba; wakati mwanadamu atakuwa ametakasa kabisa uchafu kutoka kwenye mwili wake, na amepokea kwa mara nyingine toleo na ukuzaji kutoka kwa Muumba, basi kumbukumbu la mwanadamu litarejeshwa, na kwa wakati huu mwanadamu atakuwa amerejea kwa kweli katika utawala wa Muumba.
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili

Kujua zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni