Shahidi uzoefu wa Kanisa la Mwenyezi Mungu | Nilifurahia karamu kubwa(1)
Xinwei Mkoa wa Zhejiang
Juni 25 na 26 zilikuwa siku zisizohaulika. Eneo letu la Zhejiang lilipata tukio kubwa, viongozi wengi na wafanyakazi wa eneo wakiwa wamekamatwa na joka kubwa jekundu. Ni wachache wetu tu tuliokimbia bila kuumia na, mioyo yetu ikiwa imejaa shukrani, tulikula kiapo cha siri kwa Mungu: kushirikiana vizuri na kazi iliyokuwa ifuate. Kufuatia hilo tulianza kazi yenye msisimko na shughuli nyingi ya kushughulika na matokeo. Na baada ya karibu mwezi mmoja, mipango ilikuwa inakaribia kukamilika. Mwezi huo ulikuwa wa joto, na wakati tulikuwa tumeteseka kimwili mioyo yetu ilikuwa imeridhika yenye furaha, kazi yetu ikiwa imeendelea vizuri mbele ya joka kubwa jekundu.
Wakati kazi ilipokuwa imekamilika mimi bila kujua nilijikuta katika hali ya kujiridhisha, nifikiria jinsi nilivyokuwa mwerevu kupanga hiyo kazi vizuri sana. Jinsi nilivyokuwa mfanyakazi mwenye uwezo! Na ilikuwa ni wakati huu ambapo Mungu alipatiliza hukumu Yake kwangu na kuniadibu …
Jioni moja mimi na dada kadhaa tulikuwa tukiongea. Dada mmoja alipendekeza niwaandikie barua fulani na fulani, alinipa kazi fulani, na akaongeza sentensi moja ya mwisho: "Usikurupuke huku na kule tu, sasa ndio wakati wa kujificha na kufanya ibada za kiroho. Zingatia ibada za kiroho na kuingia katika maisha." Mara tu niliposikia maneno haya moyo wangu uliyakataa: Ni lazima niandike barua, ni lazima nifanye kazi. Wakati uko wapi wa ibada za kiroho? Wewe ni mgeni, mimi ni mwenyeji, mimi ninakukinga kwa kutokuruhusu kwenda nje na kufanya kazi, na unanihakiki? Nikiketi nyumbani nikifanya ibada za kiroho siku nzima kama ufanyavyo, ni nani angeenda na kufanya kazi? Kazi inayostahili kufanywa inahitaji kuzingatiwa wakati wa kugawa kazi; na hali inahitaji kuzingatiwa kabla ya kunipogoa. … Asubuhi iliyofuata kila mtu alikuwa akila na kunywa na kuwasiliana maneno ya Mungu, lakini nilikuwa nimevurugika, nikikosa kufurahia kula na kunywa huko. Dada wote walikuwa wakiongea juu ya ufahamu wao wa maneno ya Mungu, huku nikiwa nimekaa kimya. Kisha huyo dada akaniuliza: "Kwa nini huzungumzi?" Nikajibu kwa hasira: "Sina ufahamu wowote." Huyo dada akandelea: "Naona huko katika hali nzuri." Nilijibu bila kufikiri: "Sijahakiki shida yoyote." Lakini kwa kweli mawazo yangu yalikuwa yamepangwa kupasuka na kutoka nje yangu. Hatimaye sikuweza kuyadhibiti tena na nikamwambia kilichokuwa kikinisumbua. Dada huyo alisikiliza na kukiri mara moja kwamba alikuwa mwenye kujiamini mno na hakupaswa kunipa kazi jinsi alivyotaka. Lakini hili halikunitosha kuupuuza upinzani wangu—kwa kinyume, nilihisi kazi yangu wakati huu yote ilikuwa kuweka ukweli katika vitendo, na hakupaswa kusema kuwa sikuwa katika hali njema. Viongozi wa wilaya kando yetu wangefikirije? Kisha dada huyo aliendelea: "Nina wasiwasi kuwa ukifanya kazi tu bila wakati wowote wa kuingia kwako mwenyewe utakuwa mpotovu….” Alivyozidi kuzungumza ndivyo nilivyozidi kumpinga, nifikiri: Unaniita mpotovu? Nafikiri niko katika hali nzuri sana, sitakuwa mpotovu! Sikukubaliana kabisa na mawasiliano yake. Baada ya kifungua kinywa nilikwenda kazini, nikihisi nimekasirika na kufikiri: Nitaacha kazi kama kiongozi, nifanye kazi za kawaida na kumalizana nalo. Kama anasema mimi ni mpotovu na sina ingizo katika maisha, ninawezaje kuwaongoza wengine hata hivyo? Jinsi nilivyozidi kufikiri ndivyo roho yangu ilivyozidi kuhuzunika, nikifikiria: Wakati kazi hizi zitakapokamilika nitajiuzulu. Kisha nikajihisi tu mdhaifu mwili wangu mzima, kana kwamba nilikuwa mgonjwa. Nilitambua kuwa hali yangu ilikuwa mbaya. Niliporudi nyumbani nilikuja mbele ya Mungu na kuomba: "Mwenyezi Mungu, nimekuwa mwenye kiburi sana na mwenye kushikilia maoni yangu, sijauupenda ukweli, sijaweza kukubali kuadibu Kwako na hukumu Yako, kunishughulikia Kwako na kunipogoa. Natumaini kwamba Unaweza kunisaidia na kuulinda moyo wangu, roho yangu, kunifanya niweze kuitii kazi Yako, kujichunguza kwa unyofu, na kujifahamu kwa kweli." Baadaye niliona maneno yafuatayo: "Wewe kujijua ni: Jinsi unavyozidi kuhisi kuwa umefanya vyema katika eneo fulani, ndivyo unavyozidi kufikiria kuwa umefanya jambo sahihi katika eneo fulani, ndivyo unavyozidi kufikiri unaweza kuyaridhisha malengo ya Mungu katika eneo fulani, na ndivyo unavyozidi kufikiri wewe ni wa kustahili kujisifu katika eneo fulani—ndivyo ilivyo vyema zaidi kwako kujijua katika maeneo haya na ndivyo ilivyo vyema zaidi kwako kutafiti kwa kina maeneo hayo ili kuona ni uchafu gani uliomo na nini mambo gani ambayo hayawezi kuyaridhisha malengo ya Mungu. … Jambo hili juu ya Paulo hutupa kila mmoja wetu sisi waumini onyo leo, ambalo ni kwamba wakati tunapohisi kuwa tumefanya vyema hasa, au tunaamini kuwa sisi hasa tumetunukiwa kipaji katika kipengele fulani, au tunahisi hatuhitaji kubadilisha au kukubali kushughulikiwa katika kipengele fulani, tunapaswa kujaribu kujijua zaidi katika suala hilo hasa. Hili ni kwa sababu hungeweza kwa waziwazi kutafiti katika maeneo ambayo tayari unafikiri wewe ni mzuri, na hungeyatafakaria au kuyachangua ili kuona kama yana vitu vinavyompinga Mungu" ("Wewe Kujijua Kunahitaji Kujua Mawazo Yako Yenye Mizizi Imara na Maoni" katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Maneno ya Mungu yaliuakisi moyo wangu kama kwamba katika kioo chenye kung'aa. Mungu hututaka tujifahamu wenyewe kwa kuelewa mahali ambapo tunadhani tunanawiri, ambapo tunadhani tunafanya mema, na kujielewa wenyewe zaidi katika vipengele ambapo tunadhani hatuhitaji kushughulikiwa. Nikifikiria wakati huo, naona kwamba nilikuwa nikiubeba mzigo. Kazi yangu ilikuwa inaonyesha matokeo mema na nilikuwa nikishughulikia kazi nyingi kubwa vyema, nikidhani kuwa nilikuwa nikiweka ukweli katika vitendo, kwamba haya yote yalikuwa ni maingio halisi na hali yangu ilikuwa nzuri sana—hivyo sikuja mbele ya Mungu na kujichunguza. Leo, kwa sababu ya kupata nuru kutoka kwa maneno ya Mungu natambua kwamba wakati huo nilikuwa nikifanya kazi yangu vyema, lakini asili yangu ya kiburi ilikuwa ya kuenea pote. Nilidhani kuwa matokeo ya kazi yangu yalikuwa kwa sababu ya jitihada zangu, kwamba nilikuwa mfanyakazi mwenye uwezo. Nilikuwa mwenye kujikinai kabisa. Kwa kweli, nikifikiria nyuma kwa wakati huo sasa ninatambua kuwa nilikuwa tu nikifanya kazi, kufanya kile nilichoweza kufanya chini ya uongozi na ulinzi wa Roho Mtakatifu, lakini wakati nikifanya kazi sikuutafuta ukweli. Sikuwa na ingizo katika maisha, na kwa muda sikujifahamu mwenyewe, sikuwa na ufahamu wa Mungu, wala uzoefu wangu wa kazi ya Mungu haukuniletea ufahamu wa wazi zaidi wa kipengele chochote cha ukweli. Kwa kinyume nilikuwa mwenye kiburi kiasi cha kutomsikiliza yeyote, na kuiba utukufu wa Mungu kwa ajili ya sehemu yangu ndogo katika kazi Yake kuu. Hivyo tabia ya Shetani niliyoifichua ilikuwa imemkosea Mungu na ilitosha kwa Yeye kunitaja kuwa mwenye dhambi! Lakini kupitia kwa huyo dada, Mungu leo alinikumbusha kuzingatia ibada za kiroho, kuepuka upotovu. Hata hivyo bado sikulikubali. Kwa hakika sikujua vizuri tofauti ya wema na ubaya na nilikuwa mjinga mno kujihusu. Wakati huo huo nilihisi kuwa nilikuwa katika hali ya kutisha. Kama Mungu hakuwa amemsisimua huyo dada kuonyesha hali yangu na kunitaka nirudi kwa Mungu kwa haraka, ningeendelea kuishi katika upotovu, bila kujua kwamba nilikuwa nimepoteza kazi ya Roho Mtakatifu, na hatimaye ningekuwa nimefanya kosa kubwa dhidi ya Mungu. Ninaogopa ningekuwa nimekwisha, nimepotea. Wakati huu niliona jinsi nilivyokuwa na haja ya hukumu ya Mungu na kushughulikiwa ili kunilinda kwa njia iliyo mbele. Ingawa katika njia ya hukumu na kuadibiwa, ya kupogolewa na kushughulikiwa, nilihisi nilikuwa nimeaibika na kwamba hii ilikuwa dhiki, huu ulikuwa wokovu wa Mungu. Nilikuwa tayari kuikubali aina hii ya kazi zaidi kutoka kwa Mungu.
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Soma zaidi: Chanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni