Shahidi uzoefu wa Kanisa la Mwenyezi Mungu | Nilifurahia karamu kubwa(2)
Baada ya kupitia kuadibiwa huko na hukumu hali yangu ilibadilika. Tabia na mwenendo wangu zikawa bila makeke zaidi, na mimi nilielewa kazi ya Mungu kidogo, kazi ambayo hailingani na dhana za mwanadamu. Lakini punde, kwa sababu ya ufunuo mwingine wa Mungu, niliona tena kwamba ufahamu wangu ulikuwa wa juujuu mno. Mapema mwezi wa Agosti nilipandishwa cheo kufanya kazi katika eneo. Wakati huo nilikuwa na uchangamfu na nikala kiapo kwa siri: Mungu, asante kwa kuniinua na kwa kunipa agizo kubwa jinsi hiyo. Sitaki kukosea imani Yako kwangu, na ninataka kufanya kila liwezekanalo, na kutumaini kuwa Utaniongoza na kunielekeza.
Na hivyo nikajitupa kwenye ratiba ya kazi yenye shughuli nyingi. Kila siku nilikabiliwa na rundo la ujumbe niliouhitaji kujibu, nikitoa mwongozo kwa kila mmoja. Ningeandika mara nyingi hadi asubuhi, lakini nilifurahia kufanya hivyo. Wakati mwingine ningekabiliwa na hali ambayo sikuifahamu au ambayo haikuwa wazi, na ningemwomba Mungu na kuona uongozi Wake na mwongozo, na kazi iliendelea vizuri. Na bila kujua nikawa mwenye kiburi tena, nikifikiri: Mimi ni wa kufaa sana, mimi ni mfanyakazi mwenye uwezo. Siku moja nilikumbana na matatizo kadhaa. Sikujua jinsi ya kugawa vitabu vya eneo hilo, kazi ilikuwa imevurugika, barua zilikuwa zikipelekwa na kurudishwa polepole, na mambo yalikuwa yakicheleweshwa. Kwa hiyo niliomba na kutafakari jinsi ya kuondoa mawazo yangu, na kisha nikahisi yalikuwa wazi: Tafuta mbinu iliyotumika kabla ya tukio hilo kufanyika, jaza nafasi zote za kazi zilizo wazi, na uwateue wafanyakazi kadhaa wapya wa wilaya, halafu kazi inaweza kuendelea mbele kwa wepesi. Kwa hiyo nikaandika barua kwa kiongozi wangu kutoa maoni haya na kuuliza kama ingewezekana au la. Wakati nilipokuwa nikiandika barua hii nilidhani kiongozi huyo hakika angefikiri nimechukua mzigo na kuwa mimi ni mfanyakazi mwenye uwezo. Nilisubiri jibu, nikitumainia sifa zao. Siku chache baadaye nilifurahi kupokea jibu, lakini baada ya kulifungua na kulisoma nilihisi kujawa na huzuni. Huyu kiongozi hakukosa tu kunisifu, jibu lake lilijaa kunishughulikia na kunipogoa, likisema "Wewe una tabia mbaya kufanya hili, unataka umaarufu, na kama utaendelea kwa njia hii utakatiza kazi ya Mungu! Ikiwa wilaya zinaweza kushughulikia kazi zao zenyewe, ziruhusu, kama haziwezi iweke kando tu. Unapaswa kufanya ibada za kiroho kwa haraka na kuandika makala ….” Wakati huo nilikuwa nimeshikilia wema na ubaya na nilihisi kuwa nilikuwa nimetendewa vibaya: "Huyu ni kiongozi wa aina gani, ambaye hatatui matatizo ya wasaidizi? Kumekuwa na tukio katika eneo letu, kazi yetu yote imevurugika: Si tunaka mipangilio? Wilaya zikishughulikia kazi zao zenyewe, ni nini kitakachofanyikia barua hizi zote? Je, vifaa kuhusu kuondoshwa na kufukuzwa na video havitapelelezwa? Ndugu wa kiume na wa kike hawajui jinsi ya kusambaza vitabu vya eneo, na tunakabiliwa na mgogoro, na wanaandika jumbe ili kuharakisha mambo—hili litapuuzwa pia? Sitaki umaarufu, nilitaka tu kuufungua mchakato wetu wa kazi. …"Nilishindwa kabisa kujichunguza na nilikuwa na hasira sana kiasi kwamba nililalamika kwa dada mwenyeji wangu, na hata nikafikiri: Nitaacha kazi, nisipoiacha mimi ni madakizo, nimekuwa nikifanya kazi kwa bidii sana na bado mimi ni madakizo. Kuna haja gani?
Siku iliyofuata nilisimama mbele ya Mungu na kuchunguza kile nilichokuwa nimekifichua, nikifikiria jinsi ambavyo huyo aliye juu alivyokuwa amesema kuwa kukataa kupogolewa na kushughulikiwa kunaonyesha kushindwa kuupenda ukweli, na watu ambao hawapendi ukweli wana asili mbaya. Kwa hiyo niliangalia kwa utambuzi "Kanuni ya Kukubali Kupogolewa na Kushughulikiwa." Niliona kwamba maneno ya Mungu yanasema: “Watu wengine wanakuwa wa kutoonyesha hisia baada ya kupogolewa na kushughulikiwa; wanahisi wanyonge kiasi cha kutotekeleza wajibu wao na wanapoteza uaminifu wao na kujitolea kwao. Kwanini hivi? Hili kwa kiasi ni kwa ajili ya watu kukosa ufahamu kuhusu kiini cha matendo yao ambayo hupelekea kutokubali kupogolewa na kushughulikiwa. Pia kwa kiasi ni kwa ajili ya watu kutoelewa umuhimu wa kushughulikiwa na kupogolewa, wakiamini hilo kuwa ishara ya kuamuliwa kwa matokeo yao. Kwa sababu hiyo, kimakosa watu huamini kuwa wakiwa na uaminifu fulani na kujitolea kwa Mungu, basi hawawezi kushughulikiwa na kupogolewa; wakishughulikiwa, haiwezi kuwa haki ya Mungu. Kutoelewa kama huku kunawafanya wengi kutoaminika na kutojitolea kwa Mungu. Hakika, yote ni kwa sababu watu ni waongo sana; hawataki kupitia ugumu—wanataka kupata baraka kwa njia rahisi. Hawana ufahamu wa haki ya Mungu. Si kwamba Mungu hajafanya lolote la haki ama kwamba hatafanya lolote la haki, ni tu kwamba watu daima hawafikiri kwamba Anayofanya Mungu ni haki. Machoni pa wanadamu, kama kazi ya Mungu haipatani na mapenzi ya mwanadamu ama kama si matarajio yao, ina maana kuwa Yeye si mwenye haki. Watu kamwe hawatambui wakati kile wanachofanya si sahihi ama haiambatani na ukweli; katu hawatambui kwamba wanampinga Mungu” (“Maana ya Utendaji wa Watu Kuamua Matokeo Yao” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Maneno ya Mungu yalifichua ukweli wangu wa ndani. Sikukubali kupogolewa na kushughulikiwa kwa sababu sikuwa na ufahamu wa asili ya kile nilichokifanya. Nilidhani hakukuwa na kitu kibaya katika kile nilichokifanya, lakini kazi yangu na kutimiza wajibu wangu vilikuwa vimeondoka kwa mipango ya kazi kitambo, lakini nilidhani nilikuwa nikionyesha moyo wa ibada kamili. Nikikumbuka kuwa yule aliye juu alikuwa amesema kuwa "hukuna haja ya kuhangaika juu ya matatizo ya jumla…, hakuna haja ya mtu kulitatua. … Hakuna haja ya uangalifu maalumu, kiongozi wa umma anaweza kulishughulikia." Yule aliye juu hakututaka tushughulikie matatizo ya jumla, wakati mtazamo wangu ulikuwa kwamba maswali yote yaliyotumwa juu kutoka chini yalipaswa kupokea mwongozo na majibu, bila kujali suala lilikuwa kubwa kiasi gani. Ni kama tu matatizo yalishughulikiwa ambapo ningeweza kutulia na kufanya ibada za kiroho. Nilipokabiliwa na ukweli niliona kuwa sikuwa nimeitii kabisa na bila masharti mipango ya aliye juu, na hivyo nilijitahidi kuendelea na mwelekeo mpya wa kazi ya Roho Mtakatifu. Nilikuwa na wasiwasi mwingi mno ambao sikuweza kuuwacha na nilikuwa na kiburi kiasi cha kutokuwa na mantiki. Mungu alikuwa akitumia mratibu kuyashughulikia mambo ndani yangu ambayo hayakulingana na mapenzi ya Mungu, hivyo ningeelewa asili yangu ya kumpinga na kumsaliti Mungu na mwelekeo mpya wa kazi ya Roho Mtakatifu na mapenzi ya Mungu: Ibada za kiroho na kujichunguza zinapaswa kuwa za msingi, na sipaswi kuzingatia kazi tu. Lakini sikutambua kwamba asili ya matendo yangu ilikuwa kinyume na mahitaji ya aliye juu na ilienda dhidi ya, na kumpinga Mungu. Nilishikilia mema na mabaya. Nilishindwa kuielewa roho, nilishindwa kuielewa kazi ya Mungu. Halafu nikakumbuka tena mawasiliano ya mwanadamu: "Haijalishi ni mtu yupi, kiongozi yupi, mfanyakazi, ambaye hunipogoa na kunishughulikia, haijalishi kama linalingana kabisa na ukweli. Almradi linalingana kiasi nalikubali na kulitii, ninalikubali kabisa; sitoi maelezo au kusema kuwa ninakubali asilimia fulani yalo lakini siyo masalio, na kwa kufanya hivyo ninaonyesha kuwa ninaitii kazi ya Mungu. Kama hutayatii maneno ya Mungu na kazi ya Mungu kwa njia hii, itakuwa vigumu kwako kupata ukweli, itakuwa vigumu kwako kuingia katika ukweli wa maneno ya Mungu" ("Jinsi ya Kupata Matokeo Kutoka kwa Kula na Kunywa Maneno ya Mungu" katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha (I)). Ndiyo, hata kama maneno ya mratibu hayakukubaliani kabisa na hali yangu ni lazima niyatii na kuyakubali. Na kwa vyovyote kutimiza kwangu kwa wajibu wangu kulikuwa kumekwisha kwenda kinyume zamani na mipango ya aliye juu na kazi ya Roho Mtakatifu. Si hata ningefanya haraka zaidi kutii, kukubali na kubadilika? Baadaye kwa utambuzi nilifanya kila lililowezekana kutimiza matakwa ya aliye juu wakati nilikuwa nimejiendeleza kidogo na kutulia, kushiriki katika ibada za kiroho, kufanya mazoezi ya kuandika makala, niliona kwamba Mungu Mwenyewe alikuwa akiilinda kazi ya Mungu, na ilikuwa inaendelea kama kawaida, bila kuchelewa.
Matukio haya mawili ya kuadibu na hukumu, ya kupogolewa na kushughulikiwa yalikuwa matatizo, lakini yaliniacha na ufahamu zaidi juu yangu mwenyewe na kwa haraka yalibadilisha hali yangu. Baadaye niliona kwamba maneno ya Mungu yanasema: “Dutu Yake ni nzuri. Yeye ni udhihirisho wa uzuri wote na wema, vile vile upendo wote” (“Kiini Cha Kristo ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba Wa Mbinguni” katika Neno Laonekana katika Mwili). “Yeye hukulaani ili uweze kumpenda, na ili uweze kujua kiini cha mwili; Yeye hukuadibu ili uweze kuamshwa, kukuruhusu wewe ujue kasoro zilizo ndani yako, na kujua kutostahili kabisa kwa mwanadamu. Hivyo, laana za Mungu, hukumu Yake, na uadhama na ghadhabu Yake—yote ni kwa ajili ya kumfanya mwanadamu awe mkamilifu. Yote ambayo Mungu anafanya leo, na tabia yenye haki ambayo Yeye huifanya kuwa wazi ndani yenu—yote ni kwa ajili ya kumfanya mwanadamu awe mkamilifu, na huo ndio upendo wa Mungu” (“Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Sikuweza kujizuia kushusha pumzi: Ndiyo, Mungu ni maonyesho ya uzuri na wema wote, kiini Chake ni uzuri na wema, kiini Chake ni upendo, hivyo kila kitu kitokacho kwa Mungu ni chema na kizuri, iwe ni hukumu, kuwe ni kuadibu, au kama watu, matukio na vitu vilivyo karibu na sisi hutumiwa kutupogoa na kutushugulikia—hii inaweza kuhisi kama tatizo au mashambulizi ya mwili wa mwanadamu, lakini kile Mungu afanyacho ni cha manufaa kwa maisha yetu, yote ni wokovu na upendo. Lakini sikumwelewa Mungu au kazi Yake, wala sikuziona nia Zake njema. Nikiwa nimekabiliwa na hukumu na kuadibiwa, nikiwa napogolewa na kushughulikiwa, nilipinga kwa kutishia kuiacha kazi yangu, nikishindwa kukubali hili kutoka kwa Mungu, kana kwamba watu walikuwa wananisababishia shida. Kupitia ufunuo wa Mungu wa mara mbili, niliona kuwa licha ya kula na kunywa neno la Mungu kwa miaka mingi, kusikia mahubiri mengi sana, msukumo wangu wa kuasi wakati nimekabiliwa na hukumu na kuadibiwa, na kupogolewa na kushughulikiwa, ulikuwa wenye nguvu na niliukataa kabisa. Niliweza kuona kwamba licha ya kumwamini Mungu wakati huu wote tabia yangu ilikuwa haijabadilika, asili ya Shetani ilikuwa yenye mizizi imara, asili ya kumpinga na kumsaliti Mungu, na nilikuwa nimekwisha kuwa nguvu ya kumpinga Mungu. Ghafla nilitambua kwamba nilihitaji hukumu na kuadibiwa, kupogolewa na kushughulikiwa. Bila ya aina hii ya kazi na Mungu singeuona uso wangu wa kweli, singekuwa na ufahamu wa kweli juu yangu mwenyewe, sembuse kutambua jinsi asili ya Shetani ilikuwa na mizizi imara ndani yangu. Ni sasa tu ninapoelewa kwa nini Mungu anasema wanadamu waliopotoka ni adui Yake, na kwamba sisi ni dhuria wa Shetani …. Hili lilifichuliwa kupitia hukumu ya Mungu na kuadibu, kunipogoa na kunishughulikia, na hili ndilo nililojifunza kutoka kwa mchakato huo. Nikitafakari maneno ya Mungu, moyo wangu ukapata nuru. Ninaona jinsi Mungu anavyonipangia kwa uangalifu kupata uzoefu wa kazi Yake, kuingia katika uhalisi wa ukweli, na kuniongoza kwenye njia ya kweli ya uzima. Mungu huniinua na kunitendea kwa huruma. Nilikuja kutambua pia kwamba kila kitu ambacho Mungu hufanya kwa ajili ya mwanadamu ni upendo. Hukumu ya Mungu na kuadibu, kupogoa na kushughulikia ndizo haja kubwa mno za mwanadamu na wokovu bora zaidi. Utukufu wote Uwe kwa Mwenyezi Mungu!
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Soma zaidi: Chanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni