Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 105
Kwa sababu ya kanuni za maneno Yangu, kwa sababu ya utaratibu wa kazi Yangu, watu hunikana; hili ndilo kusudi Langu la kuzungumza kwa muda mrefu (imezungumzwa kuhusu wazao wote wa joka kubwa jekundu). Ni njia ya hekima ya kazi Yangu; ni hukumu Yangu ya joka kubwa jekundu; huu ni mkakati Wangu, hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuuelewa kikamilifu. Katika kila kipindi muhimu, yaani, katika kila awamu ya mpito ya mpango Wangu wa usimamizi, baadhi ya watu lazima waondolewe; wanaondolewa kulingana na utaratibu wa kazi Yangu.
Hii pekee ndiyo njia ya kazi ya mpango Wangu wote wa usimamizi. Baada ya kuwatupa nje, mmoja baada ya mwingine, watu Ninaotaka kuwaoondoa, kisha Ninaanza hatua inayofuata ya kazi Yangu. Hata hivyo, wakati huu wa kuondosha ni wakati wa mwisho (ndani ya makanisa ya China), na pia ni wakati ambapo idadi kubwa ya watu itaondolewa katika awamu ya mpito tangu uumbaji wa ulimwengu. Katika historia yote, kila wakati ambapo watu wameondolewa kumekuwa na sehemu iliyoachwa ili kutoa huduma kwa kazi ya baadaye, lakini wakati huu sio sawa na hapo awali; ni nyumbufu na safi, ni muhimu zaidi na kamilifu zaidi kuliko nyakati zote. Hata ingawa baada ya kusoma maneno Yangu, watu wengi hujaribu kuyalazimishia shaka kutoka akilini mwao, lakini mwishoni wao hawawezi kuyashinda, na hatimaye wanaanguka katika mapambano yao. Hili sio juu ya mwanadamu kuamua, kwa sababu wale ambao Nimewajaalia hawawezi kutoroka, na wale ambao Sijawajaalia Ninaweza kuwadharau tu. Ni wale ambao Ninawaangalia kwa fadhila pekee ndio ambao Ninawapenda, vinginevyo, hakuna hata mtu mmoja anayeweza kuondoka na kuingia kwa hiari katika ufalme Wangu; huu ndio utawala Wangu mkali, na huu pekee ndio ushahidi wenye nguvu na udhihirisho kamili wa kutekeleza amri Zangu za utawala. Hakika hili si suala la kuwa na moyo wenye ari tu. Kwa nini Nimesema Shetani ni dhaifu na aliyeanguka? Mara ya kwanza alikuwa na nguvu, lakini yuko katika mikono Yangu; Nikimwambia alale chini, ni lazima alale; Nikimwambia ainuke ili kunitolea huduma, ni lazima ainuke na kutoa huduma Kwangu vizuri. Siyo kwamba Shetani ako radhi kufanya haya, ni kwamba fimbo Yangu ya chuma humtawala Shetani, na ni wakati huo pekee ndipo anaridhika moyoni na kwa neno. Amri Zangu za utawala humwongoza, Nina uwezo Wangu, na hivyo hana budi ila kuridhika kabisa, lazima apondwe chini ya kiti Changu cha miguu, bila dalili ya upinzani. Hapo zamani wakati ambapo alikuwa akiwahudumia wana Wangu, alikuwa fidhuli kupita kiasi na aliwadhulumu wana Wangu kwa hiari, akitumai kwa njia hiyo kuniaibisha Mimi, akisema kuwa Sina uwezo. Kipofu alioje! Nitakukanyaga hadi ufe! Wewe thubutu tu kuwa nduli tena! Wewe thubutu tu kuwatendea wana Wangu kwa kutojali kwa baridi tena! Kadiri watu wanavyokuwa waaminifu zaidi, na kadiri wanavyozidi kusikiliza maneno Yangu na kufanya matendo Yangu yawe sheria, ndivyo unavyozidi kuwadhalimu, na ndivyo unavyozidi kuwatenga (hii ina maana kuwasajili watu, kuwaunganisha pamoja). Sasa siku zako za ukatili ziko mwishoni, kidogo kidogo Ninalipiza kisasi kwako, na Sitakuachilia kwa urahisi hata kidogo. Sasa sio wewe—Shetani—ambaye umechukua mamlaka; badala yake Nimechukua mamlaka hayo tena, na wakati wa kuwaita wana Wangu kukushughulikia umewadia. Ni lazima utii, na usiwe na upinzani hata kidogo. Bila kujali jinsi ulivyokuwa na mwenendo mzuri mbele Yangu hapo zamani, hilo halitakusaidia leo. Kama wewe si mmoja wa wale Ninaowapenda, basi Sikutaki. Mmoja zaidi ya idadi hiyo haikubaliki, lazima iwe nambari Niliyoamua kabla; mmoja chini ya hiyo ni mbaya zaidi. Shetani, usiwe mdakizi! Je, inaweza kuwa kwamba Sina hakika katika moyo Wangu kuhusu yule ambaye Ninampenda na ambaye Ninamchukia? Je, Ninahitaji kukumbushwa nawe? Shetani anaweza kuzaa wana Wangu? Wote ni wa upuuzi! Wote ni duni! Nitawatupa kabisa na kikamilifu, hakuna hata mmoja anayetakikana, wote lazima waondoke! Mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita umefika mwisho, Kazi Yangu imekamilika, ni lazima Niwaondoe wenye tabia mbaya na wakatili!
Wale wanaoamini maneno Yangu na kutekeleza matendo Yangu lazima wawe wale Ninaowapenda, Sitamwacha hata mmoja, hakuna hata mmoja atakayeachwa huru, hivyo wale ambao ni wana wazaliwa wa kwanza hawana haja ya kuwa na wasiwasi. Kwa kuwa imetolewa na Mimi, hakuna mtu anayeweza kuichukua, na Sina budi kuwakirimu wale Ninaowabariki. Wale ambao Ninawakubali (kabla ya uumbaji wa ulimwengu), Ninawabariki (leo). Hivi ndivyo Ninavyofanya kazi, pia ndiyo kanuni kuu ya kila kifungu cha amri Zangu za utawala, na hakuna mtu anayeweza kubadilisha hili; neno moja zaidi haliwezi kuongezwa, wala sentensi moja zaidi, na hata zaidi neno moja haliwezi kuachwa, wala sentensi moja. Hapo zamani mara nyingi Nilisema kuwa nafsi Yangu inaonekana kwenu; hivyo basi nafsi Yangu ni nini, na huonekana vipi? Je, ina maana Mimi Mwenyewe tu? Je, ina maanaya kila sentensi ambayo Ninasema tu? Vipengele hivi viwili, huku vikiwa vya msingi, vinachukua tu sehemu ndogo, yaani, hivyo sio maelezo kamili ya nafsi Yangu. Nafsi Yangu inajumuisha Mimi Mwenyewe, maneno Yangu, na pia matendo Yangu, lakini ufafanuzi halisi ni kwamba Mimi na wana Wangu wazaliwa wa kwanza tu nafsi Yangu. Yaani, kikundi cha Wakristo wenye utaratibu, ambao hutawala na wana mamlaka, ni nafsi Yangu. Kwa hivyo, kila mmoja wa wana wa kwanza ni muhimu, ni sehemu ya nafsi Yangu, na tangu sasa Nasisitiza kwamba idadi ya watu haiwezi kuwa zaidi kwa mmoja (ikidhalilisha jina Langu), wala, hata muhimu zaidi, haiwezi kuwa ndogo kwa mmoja (haliwezi kuwa dhihirisho Langu kamili), na Nasisitiza tena na tena kwamba wana wa kwanza ni wapendwa Wangu, tunu Yangu, udhihirisho wa mpango Wangu wa usimamizi wa miaka elfu sita; ni wazaliwa wa kwanza pekee wanaoweza kuwa dhihirisho Langu timilifu na kamili, Mimi Mwenyewe pekee ndiye ninayeweza kuwa onyesho kamili la nafsi Yangu, ni wana wa kwanza pekee wanaoweza kusemekana kuwa ni onyesho timilifu na kamili. Kwa hivyo nina madai makali kwa wana Wangu wa kwanza, bila kusamehe chochote, na kukata na kuua wale wote walio tofauti na wana Wangu wa kwanza tena na tena; hiki ndicho kiini cha yote ambayo Nimeyasema, ndilo lengo kuu la yote ambayo Nimeyasema. Zaidi ya hayo, mara nyingi Mimi husisitiza kuwa lazima wawe wale walioidhinishwa na Mimi, wale ambao Nimewachagua binfasi tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Hivyo, sasa ni ipi namna ya kueleza "kuonekana"? Je, ni wakati wa kuingia katika ulimwengu wa kiroho? Watu wengi wanaamini kwamba ni wakati ambapo Mimi Mwenyewe Nilitiwa mafuta, au wakati ambapo waliniona Mimi Mwenyewe; yote haya ni uongo, hata hayakaribii ukweli. "Kuonekana" kwa mujibu wa maana yake ya asili si vigumu kuelewa kabisa, lakini kuelewa kulingana na nia Yangu ni vigumu sana. Inaweza kusemwa hivi: Wakati ambapo niliwaumba binadamu, Nilikuwa nikiweka ubora Wangu katika kundi hili la watu Niliowapenda, na kundi hili la watu lilikuwa nafsi Yangu. Ili kuieleza kwa njia nyingine, nafsi Yangu ilikuwa tayari imeonekana wakati huo. Siyo kwamba nafsi Yangu ilionekana baada ya jina hili kupokewa, bali badala yake ilionekana baada ya kuliamua kabla kundi hili la watu, kwa sababu lina ubora Wangu (asili yao haibadiliki, wao bado ni sehemu ya nafsi Yangu). Kwa hivyo, nafsi Yangu, tangu uumbaji wa ulimwengu mpaka siku ya sasa, imeonekana daima. Katika dhana za watu, wengi wanaamini kwamba Mimi Mwenyewe ndimi nafsi Yangu, ambayo sivyo kabisa; hayo yote ni mawazo ya watu, fikra za watu. Kama Mimi Mwenyewe pekee Ningekuwa nafsi Yangu, hiyo haingeweza kumwaibisha Shetani, isingeweza kulitukuza jina Langu, na kwa kweli ingekuwa na athari za kinyume, na hivyo kuliaibisha jina Langu, na kuwa alama ya Shetani kuliabisha jina Langu katika enzi zote. Mimi ni Mungu mwenye hekima Mwenyewe, na siwezi kamwe kufanya jambo la upumbavu kama hilo.
Kazi Yangu lazima iwe na matokeo, hata zaidi ni lazima Niseme maneno kwa utaratibu; Maneno Yangu yote na matamshi Yangu yanasemwa kwa kufuata Roho Wangu, na mimi husema kulingana na yote ambayo Roho Wangu hufanya. Kwa hivyo wote wanapaswa, kwa njia ya maneno Yangu, kuhisi Roho Wangu, kuona ni nini hasa ambacho Roho Wangu anafanya, kuona ni nini hasa Ninachotaka kufanya, kuona njia Yangu ya kufanya kazi kulingana na maneno Yangu, na kuona kanuni za mpango Wangu mzima wa usimamizi ni zipi. Mimi hutazama taswira nzima ya ulimwengu: Kila mtu, kila tukio, na kila mahali, vyote viko chini ya utawala Wangu. Hakuna mtu anayeweza kukiuka mpango Wangu; wote husonga mbele hatua kwa hatua kwa utaratibu ambao Nimeagiza. Huu ni uwezo Wangu, ni pale ambapo hekima ya kusimamia mpango Wangu wote upo. Hakuna anayeweza kuelewa kikamilifu, hakuna anayeweza kusema waziwazi. Yote hufanywa na Mimi binafsi, na kudhibitiwa na Mimi pekee. Yote hufanywa na Mimi binafsi, na kudhibitiwa na Mimi pekee.
kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Neno la Mwenyezi Mungu | Sura ya 104
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni