Ijumaa, 22 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | "Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Ishirini na Saba”



Matamshi ya Mungu | "Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Ishirini na Saba”

Mwenyezi Mungu anasema, “Katika furaha na huzuni ya kutengana na kisha kuunganika Kwangu na mwanadamu, hatuwezi kubadilishana mawazo. Kwa sababu tumetengana mbinguni na wanadamu ardhini, hatukutani mara kwa mara. Ni nani anayeweza kujitoa katika kuwaza mambo mazuri ya kale? Ni nani anayeweza kuzuia picha hizi za ukumbusho kumwonekania? Ni nani asingetumaini kuendelea kwa hisia hizi nzuri? Ni nani hawezi kutarajia kurudi Kwangu? Ni nani asingetamani sana kuunganishwa Kwangu na mwanadamu tena? Moyo Wangu una hofu nyingi, na nafsi ya binadamu imejawa na wasiwasi mwingi. Licha ya sisi kuwa katika nafsi moja, hatuwezi kuwa pamoja mara kwa mara, na hatuwezi kuonana mara kwa mara. … Wanaponisihi kwa sauti, Ninageuza uso Wangu kutoka kwao, kwa maana Sitaki kushuhudia zaidi ya hayo; Lakini, itawezekanaje Nisisikie vilio vya watu hawa? Nitarekebisha udhalimu katika dunia ya mwanadamu. Nitafanya kazi Yangu kwa mikono Yangu mwenyewe ulimwenguni kote, Nikimkomesha Shetani asiwadhuru watu Wangu tena, Nikiwakataza maadui wasifanye kile wapendacho tena. Nitakuwa Mfalme duniani na kukipeleka kiti Changu cha enzi huko, na kuwafanya maadui Wangu wote waanguke chini na kukiri makosa yao mbele Yangu. Katika hali Yangu ya huzuni, hasira imechanganywa, Nitaukanyaga ulimwengu wote sawasawa, bila kumwacha yeyote, na kuwatia maadui Wangu hofu kubwa. Naiangamiza dunia yote, na kuwafanya maadui Wangu waanguke katika maangamizi hayo, ili toka sasa na kuendelea wasiwapotoshe wanadamu tena.”

Tazama zaidi: Maonyesho ya Mungu | “Wewe U Mwaminifu kwa Nani?”

Yaliyopendekezwa: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni