Jumamosi, 23 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu” Sehemu ya Nne



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu” Sehemu ya Nne
Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”. Maudhui ya video hii: Kutubu kwa Kweli Ndani ya Mioyo ya Waninawi Kunawapa Rehema ya Mungu na Kwabadilisha Hatima Zao Wenyewe Huruma na Uvumilivu wa Mungu si Nadra—Kutubu kwa Kweli kwa Binadamu Ni Nadra Tabia ya Haki ya Muumba ni ya Kweli na Wazi Hisia za Dhati za Muumba kwa Wanadamu Muumba Aonyesha Hisia Zake za Kweli Kwa Binadamu
Mwenyezi Mungu anasema, "Licha ya vile ambavyo Mungu alikuwa na ghadhabu kwa Waninawi, mara tu walipotangaza kufunga na kuvalia nguo ya gunia pamoja na jivu, moyo Wake ulianza kutulia taratibu, na Akaanza kubadilisha moyo Wake. Wakati Alipowatangazia kwamba Angeangamiza mji wao—ule muda kabla ya kuungama na kutubu kwao kwa dhambi zao—Mungu alikuwa angali na ghadhabu na wao. Baada ya wao kupitia mfululizo wa vitendo vya kutubu, ghadhabu ya Mungu kwa watu wa Ninawi ikabadilika kwa utaratibu kuwa huruma na uvumilivu kwao. Hakuna kitu kinachohitilafiana kuhusu ufunuo wenye ulinganifu wa vipengele hivi viwili vya tabia ya Mungu katika tukio lilo hilo. Ni vipi ambavyo mtu anafaa kuelewa na kujua ukosefu huu wa kuhitilafiana? Mungu alionyesha na kufichua viini hivi viwili tofauti kabisa kwa mfululizo wakati watu wa Ninawi walipokuwa wakitubu na Akawaruhusu watu kuona uhalisi na kutokosewa kwa kiini cha Mungu. Mungu alitumia mtazamo Wake kuambia watu yafuatayo: Si kwamba Mungu havumilii watu, au hataki kuwaonyesha huruma; ni kwamba wao hutubu kwa kweli mara nadra kwa Mungu, na ni nadra kwa watu kugeuka kwa kweli kutoka kwa njia zao ovu na kuacha vurugu iliyo mikononi mwao. Kwa maneno mengine, wakati Mungu ameghadhabishwa na binadamu, Anatumaini kwamba binadamu ataweza kutubu kwa kweli na Anatumaini kumwona binadamu akitubu kwa kweli, ambapo Ataendelea kumpa binadamu huruma na uvumilivu Wake kwa ukarimu. Hivi ni kusema kwamba mwenendo mbovu wa mwanadamu ndio husababisha hasira ya Mungu, huku nazo rehema na uvumilivu wa Mungu zikipewa wale wanaomsikiliza Mungu na kutubu kwa kweli mbele Yake, kwa wale wanaoweza kugeuka kutoka kwa njia zao ovu na kuacha vurugu iliyo mikononi mwao. Mtazamo wa Mungu ulifichuliwa waziwazi sana katika jinsi Alivyowatendea Waninawi: Huruma na uvumilivu wa Mungu si vigumu kuvipokea hata kidogo; Anahitaji toba ya kweli ya mtu. Mradi tu watu wageuka kutoka kwa njia zao ovu na kuuacha vurugu iliyo mikononi mwao, Mungu atabadilisha moyo Wake na kubadilisha mtazamo Wake kwao."

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Sikiliza zaidi: Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu” Sehemu ya Pili








Hakuna maoni:

Chapisha Maoni