Jumapili, 28 Aprili 2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II Sehemu ya Saba

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Msiwe na Wasiwasi Wowote Kuhusu Majaribio ya Mungu
Baada ya kuupokea ushuhuda kutoka kwa Ayubu kufuatia mwisho wa majaribio yake, Mungu aliamua kwamba angepata kundi au zaidi ya kundi—la watu kama Ayubu, ilhali aliamua kutowahi tena kumruhusu Shetani kushambulia au kunyanyasa mtu yeyote mwingine kwa kutumia mbinu ambazo kwazo alimjaribu, kumshambulia na kumnyanyasa Ayubu, kwa kufanya mzaha na Mungu; Mungu hakumruhusu Shetani tena kufanya mambo kama hayo kwa binadamu ambaye ni mnyonge, mjinga, na asiyejua—ilikuwa tosha kwamba Shetani alikuwa amemjaribu Ayubu! Kutomruhusu Shetani kuwanyanyasa watu vyovyote anavyotaka ndiyo rehema ya Mungu. Kwa Mungu, ilitosha kwamba Ayubu alikuwa ameteseka majaribio na minyanyaso ya Shetani. Mungu hakumruhusu Shetani tena kufanya mambo kama hayo, kwani maisha na kila kitu cha watu wanaomfuata Mungu yanatawaliwa na kupangiliwa na Mungu, na Shetani hastahili kutawala waliochaguliwa na Mungu apendavyo—mnafaa kuwa wazi kuhusu hoja hii! Mungu anajali kuhusu unyonge wa binadamu, na kuelewa ujinga na kutojua kwake. Ingawaje, ili binadamu aweze kuokolewa kabisa, lazima Mungu amkabidhi kwa Shetani, Mungu hayuko radhi kumwona tena binadamu akichezewa kama kikaragosi na Shetani na kunyanyaswa na Shetani na hataki kumwona binadamu siku zote akiteseka. Binadamu aliumbwa na Mungu, na inaeleweka kikamilifu kwamba Mungu anatawala na anapangilia kila kitu cha binadamu; hili ni jukumu la Mungu na mamlaka ambayo Mungu anatawala mambo yote! Mungu hamruhusu Shetani kunyanyasa na kutumia vibaya binadamu apendavyo, Hamruhusu Shetani kutumia mbinu mbalimbali za kumpotosha binadamu, na vilevile, Hamruhusu Shetani kuingilia kati ukuu wa Mungu kwa binadamu, wala Hamruhusu Shetani kukanyaga na kuangamiza Sheria ambazo Mungu anatawalia mambo yote, kutosema chochote kuhusu kazi kuu ya Mungu ya kusimamia na kuwaokoa wanadamu! Wale ambao Mungu anataka kuokoa na wale ambao wanaweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu, ndio msingi na hali halisi ya kazi ya Mungu ya mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita, pamoja na bei ya jitihada zake katika kazi yake ya miaka elfu sita. Mungu anawezaje kuwakabidhi watu hawa kwa Shetani hivihivi.
Watu mara nyingi wanakuwa na wasiwasi kuhusu na wana uoga wa majaribio ya Mungu, ilhali siku zote wanaishi katika mtego wa Shetani na kuishi katika maeneo hatari ambapo wanashambuliwa na kunyanyaswa na Shetani—lakini hawaogopi na hawashangazwi. Nini kinaendelea? Imani ya binadamu katika Mungu ni finyu mno kwa mambo anayoweza kuona. Hana shukrani hata chembe kuhusu upendo na kujali kwa Mungu kwa binadamu, au wema Wake na utiliaji maanani kwa binadamu. Lakini kwa hofu na wasiwasi kidogo kuhusu majaribio, hukumu na kuadibu kwa Mungu na adhama na hasira Yake, binadamu hana hata chembe cha uelewa wa nia nzuri za Mungu. Kwa kutajwa kwa majaribio, watu wanahisi ni kana kwamba Mungu anazo nia nyingine zisizo wazi na hata baadhi wanasadiki kwamba Mungu ana mipango ya maovu, wasijue hata kile ambacho Mungu atawafanyia; hivyo, wakati huohuo kutaka kuwa watiifu kabisa kwa ukuu na mipangilio ya Mungu, wanafanya kila wawezalo kuzuia na kupinga ukuu wa Mungu juu ya binadamu na mipangilio kwa binadamu, kwani wanasadiki kwamba kama hawatakuwa makini watapotoshwa na Mungu, na kama hawatakuwa na mshikilio thabiti wa hatima yao binafsi, basi kila kitu walicho nacho kinaweza kuchukuliwa na Mungu, na maisha yao huenda hata yakaisha. Binadamu yumo kwenye kambi la Shetani, lakini hawi na wasiwasi kamwe kuhusu kunyanyaswa na Shetani, na ananyanyaswa na Shetani lakini haogopi kamwe kutekwa nyara na Shetani. Siku zote anasema kwamba anaukubali wokovu wa Mungu, ilhali hajawahi kumwamini Mungu au kusadiki kwamba Mungu atamwokoa kwa kweli kutoka kwenye makucha ya Shetani. Kama, sawa na Ayubu, binadamu anaweza kunyenyekea kwa mipango na mipangilio ya Mungu na anaweza kuitoa nafsi nzima kwa mikono ya Mungu, basi hatima ya binadamu haitakuwa sawa na ile ya Ayubu—kupokea baraka za Mungu? Kama binadamu anaweza kukubali na kunyenyekea Sheria ya Mungu, nini kipo cha kupoteza? Na hivyo Napendekeza kwamba muwe makinifu kwa vitendo vyenu, mtahadhari na kila kitu ambacho kiko karibu kuwafanyikia ninyi. Usiwe wa pupa au msukumo na umshughulikie Mungu na watu, masuala, vitu alivyokupangilia kwa namna mshawasha unavyokupeleka, au kulingana na nafsi yako ya kiasili au kufikiria na dhana zako; lazima uwe mmakinifu katika vitendo vyako na lazima uombe na utafute zaidi, kuepuka kuchochea hasira ya Mungu. Kumbuka hili!
Kisha, tutaangalia vile Ayubu alikuwa baada ya majaribio yake.
5. Ayubu Baada ya Majaribio Yake
Ayubu 42:7-9 Na basi ikawa, kwamba baada ya Yehova kusema maneno haya kwa Ayubu, Yehova akasema kwa Elifazi Mtemani, Ghadhabu yangu inawaka dhidi yako, na dhidi ya hao marafiki zako wawili: kwa sababu nyinyi hamjasema kunihusu kile kilicho sawa, jinsi alivyofanya mtumishi wangu Ayubu. Kwa hivyo sasa, jichukulieni ng’ombe wa kiume saba, na kondoo wa kiume saba, na muende kwake mtumishi wangu Ayubu, na mjitolee sadaka ya kuteketezwa; na mtumishi wangu Ayubu atawaombea: kwa kuwa yeye nitamkubali: nisije nikawatendea kulingana na makosa yenu, hivi kwamba nyinyi hamkusema kunihusu kile kilicho sawa, kama alivyofanya mtumishi wangu Ayubu. Hivyo Elifazi Mtemani, na Bildadi Mshuhi, na Sofari Mnaamathi, wakaenda, na kufanya vile Yehova alivyowaamrisha: Yehova pia akamkubali Ayubu.
Ayubu 42:10 Naye Yehova akaubadilisha uteka wa Ayubu, wakati alipowaombea marafiki zake: Yehova pia akampa Ayubu kiasi kilichozidishwa mara mbili kuliko yale aliyokuwa nayo awali.
Ayubu 42:12 Kwa hivyo Yehova akabariki Ayubu zaidi baadaye maishani kuliko mwanzo wake: kwa sababu alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, na ngamia elfu sita, na elfu moja ya jozi za ng’ombe, na elfu moja ya punda wa kike.
Ayubu 42:17 Kwa hivyo Ayubu akafariki, akiwa mzee na aliyejawa na siku.
Wale Wanaomcha Mungu na Kujiepusha Na Maovu Wanatazamiwa kwa Utunzwaji na Mungu, Huku Wale Walio Wajinga Wanaonekana kuwa Duni na Mungu
Katika Ayubu 42:7-9, Mungu Anasema kwamba Ayubu ni mtumishi Wake. Matumizi Yake ya neno “mtumishi” kumrejelea Ayubu yanaonyesha umuhimu wa Ayubu katika moyo Wake; ingawaje Mungu hakumwita Ayubu kitu chenye heshima zaidi, jina hili halikuwa na uamuzi wowote katika umuhimu wa Mungu ndani ya moyo wa Ayubu. “Mtumishi” hapa ni jina la lakabu la Mungu kwa Ayubu. Marejeleo mengi ya Mungu kwa “mtumishi wangu Ayubu” yanaonyesha ni vipi ambavyo Alipendezwa na Ayubu, ingawaje Mungu hakuongea kuhusu maana ya nyuma ya neno “Mtumishi,” ufafanuzi wa Mungu wa neno “mtumishi” unaweza kuonekana kupitia kwa maneno Yake katika kifungu hiki cha maandiko. Kwanza Mungu alimwambia Elifazi Mtemani: “Ghadhabu yangu inawaka dhidi yako, na dhidi ya hao marafiki zako wawili: kwa sababu nyinyi hamjasema kunihusu kile kilicho sawa, jinsi alivyofanya mtumishi wangu Ayubu.” Maneno haya ndiyo ya mara ya kwanza kwa Mungu kuambia watu waziwazi kwamba alikuwa amekubali yale yote yaliyokuwa yamesemwa na kufanywa na Ayubu baada ya majaribio ya Mungu kwake yeye, na ndiyo mara ya kwanza Alikuwa amethibitisha waziwazi ukweli na usahihi wa yale yote Ayubu alikuwa amefanya na kusema. Mungu alikuwa na ghadhabu kwake Elifazi na wengine kwa sababu ya mazungumzo yao yasiyokuwa sahihi na mabovu, kwa sababu, kama Ayubu wasingeweza kuona mwonekano wa Mungu au kusikia maneno aliyoongea katika maisha yao ilhali Ayubu alikuwa na maarifa sahihi Kumhusu Mungu, huku nao waliweza tu kukisia bila mpango kuhusu Mungu, kukiuka mapenzi ya Mungu na kujaribu uvumilivu wake kwa yote waliyoyafanya Kwa hivyo, wakati sawa na kukubali yote yalikuwa yamefanywa na kusemwa na Ayubu, Mungu alizidi kuongeza hasira zake kwa wale wengine, kwani ndani yao Hakuweza tu kuuona uhalisia wowote wa kumcha Mungu, lakini pia Hakusikia chochote cha kumcha Mungu kwa yale waliyoyasema. Na hivyo Mungu kwa kilichofuata Alisema madai yafuatayo kuwahusu. “Kwa hivyo sasa, jichukulieni ng’ombe wa kiume saba, na kondoo wa kiume saba, na muende kwake mtumishi wangu Ayubu, na mjitolee sadaka ya kuteketezwa; na mtumishi wangu Ayubu atawaombea: kwa kuwa yeye nitamkubali: nisije nikawatendea kulingana na makosa yenu.” Katika kifungu hiki Mungu anamwambia Elifazi na wengine kufanya jambo ambalo litakomboa dhambi zao, kwani upumbavu wao ulikuwa ni dhambi dhidi ya Yehova Mungu, na hivyo wangelazimika kutoa sadaka zilizoteketezwa ili kusuluhisha makosa yao. Sadaka zilizoteketezwa mara nyingi zinatolewa kwa Mungu, lakini kile kisicho cha kawaida kuhusu sadaka hizi zilizoteketezwa ni kwamba zilitolewa kwa Ayubu. Ayubu alikubaliwa na Mungu kwa sababu alikuwa nao ushuhuda kwa Mungu wakati wa majaribio yake. Rafiki hawa wa Ayubu, nao walifichuliwa katika kipindi kile cha majaribio yake, kwa sababu ya upumbavu wao, walishutumiwa na Mungu na wakachochea hasira ya Mungu, na wanafaa kuadhibiwa na Mungu—kuadhibiwa kwa kutoa sadaka zilizoteketezwa mbele ya Ayubu—na baadaye Ayubu aliwaombea wao ili kuiondoa ile adhabu na hasira ya Mungu kwao. Nia ya Mungu ilikuwa ni kuwaaibisha wao, kwani hawakuwa watu waliomcha Mungu na wa kujiepusha na maovu, na walikuwa wameshutumu uadilifu wa Ayubu. Kwa upande mmoja, Mungu alikuwa akiwaambia kwamba Hakukubali vitendo vyao lakini Alikubali pakubwa na Alifurahishwa na Ayubu; kwa upande mwingine, Mungu alikuwa akiwaambia kwamba kukubaliwa na Mungu kunampandisha daraja binadamu mbele ya Mungu, kwamba binadamu anachukiwa na Mungu kwa sababu ya upumbavu wake, na anamkosea Mungu kwa sababu ya hali hii, na anakuwa mdogo na mbaya mbele ya macho ya Mungu. Huu ndio ufafanuzi uliotolewa na Mungu kuhusu watu wa aina mbili, ni mielekeo ya Mungu kwa watu hawa wa aina mbili na ni ufafanuzi wa Mungu kuhusu thamani na hadhi ya watu wa aina hizi mbili. Ingawaje Mungu alimwita Ayubu mtumishi Wake, ndani ya macho ya Mungu huyu “mtumishi” alikuwa mpendwa Wake, na alipewa mamlaka ya kuwaombea wengine na kuwasamehe makosa yao. “Mtumishi huyu” aliweza kuongea moja kwa moja na Mungu na kuwa na mgusano wa moja kwa moja na Mungu, hadhi yake ilikuwa ya juu zaidi na ya heshima zaidi kuliko ya wale wengine. Haya ndiyo maana halisi ya neno “mtumishi” kama Mungu alivyoongea. Ayubu alipewa heshima hii maalum kwa sababu ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, na sababu iliyofanya wengine kutoitwa watumishi na Mungu ni kwa sababu hawakumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Mielekeo hii miwili tofauti na maalum ya Mungu ndiyo mielekeo yake kwa watu wa aina mbili: Wale wanaomcha Mungu na kujiepusha na maovu wanakubaliwa na Mungu, na wanaonekana wenye thamani mbele ya macho Yake, huku wale walio wapumbavu hawajamcha Mungu na hawawezi kujiepusha na maovu, na hawawezi kupokea kibali cha Mungu, mara nyingi wanachukiwa na kushutumiwa na Mungu, na ni wadogo mbele ya macho ya Mungu.
Mungu Anamtawaza Ayubu Mamlaka
Ayubu aliwaombea rafiki zake, na baadaye, kwa sababu ya maombi ya Ayubu, Mungu hakushughulika nao kama walivyostahili juu ya upumbavu wao—Hakuwaadhibu au kuchukua adhabu yoyote dhidi yao. Na sababu ilikuwa nini? Kwa sababu kulingana na wao maombi yanayohusu mtumishi wa Mungu, Ayubu, yalikuwa yamefikia masikio Yake; Mungu naye aliwasamehe kwa sababu Aliyakubali maombi ya Ayubu. Na tunaona nini katika haya? Wakati Mungu anapombariki mtu, Anampa tuzo nyingi, na si tu zile za kidunia: Mungu anawapa pia mamlaka, na Kuwaambia kuwa wanastahili kuwaombea wengine, naye Mungu husahau na kusamehe makosa ya hao watu kwa sababu Anayasikia maombi haya. Haya ndiyo mamlaka yenyewe ambayo Mungu alimpa Ayubu. Kupitia kwa maombi ya Ayubu kusitisha kushutumiwa kwao, Yehova Mungu aliwaletea aibu wale watu wapumbavu—ambayo, bila shaka, ndiyo iliyokuwa adhabu Yake maalum kwa Elifazi na wale wengine.
Ayubu Anabarikiwa kwa Mara Nyingine Tena na Mungu, na Hashtakiwi Tena na Shetani
Miongoni mwa matamko ya Yehova Mungu ni maneno kwamba “nyinyi hamkusema kunihusu kile kilicho sawa, kama alivyofanya mtumishi wangu Ayubu.” Ni nini kile ambacho Ayubu alikuwa amesema? Ni kile tulichozungumzia awali, pamoja na kile ambacho kurasa nyingi za maneno kwenye kitabu cha Ayubu ambacho Ayubu amerekodiwa kuwa alisema. Katika kurasa hizi nyingi za maneno, Ayubu hajawahi hata mara moja kuwa na malalamiko au mashaka yoyote kumhusu Mungu. Yeye anasubiria tu matokeo. Ni kusubiri huku ambako ndiko mwelekeo wake wa uaminifu, matokeo yake yakiwa, na kutokana na maneno aliyomwambia Mungu, Ayubu alikubaliwa na Mungu. Alipovumilia majaribio na kupata mateso ya Ugumu, Mungu alikuwa upande wake na ingawaje ugumu wake hukupunguzwa na uwepo wa Mungu, Mungu aliona kile Alichotaka kuona na kusikia kile Alichotaka kusikia. Kila mojawapo ya vitendo na maneno ya Ayubu kiliweza kufikia macho na masikio ya Mungu; Mungu alisikia na Akaona—na hii ni ukweli. Maarifa ya Ayubu kumhusu Mungu na fikira zake kumhusu Mungu katika moyo wake wakati huo, katika kipindi hicho, hazikuwa kwa hakika kama zile za watu wa leo, lakini katika muktadha wa wakati huo, Mungu aliweza kutambua bado kila kitu alichokuwa amesema, kwa sababu tabia yake na fikira zake ndani ya moyo wake, na kile alichokuwa ameelezea na kufichua, kilikuwa tosha kwa mahitaji Yake. Katika kipindi hiki cha wakati ambao Ayubu alipitia majaribio, yale ambayo alifikiria katika moyo wake na kuamua kufanya yaliweza kumwonyesha Mungu matokeo, yale ambayo yalimtosheleza Mungu, na baadaye Mungu akayaondoa majaribio ya Ayubu, Ayubu akaibuka kutoka kwenye matatizo yake, na majaribio yake yakawa yameondoka yasiwahi kumpata tena yeye. Kwa sababu Ayubu alikuwa tayari amepitia majaribio, na akawa amesimama imara katika majaribio haya, na akamshinda kabisa Shetani, Mungu alimpatia baraka ambazo kwa kweli alistahili. Kama ilivyorekodiwa katika Ayubu 42:10, 12, Ayubu alibarikiwa kwa mara nyingine tena, na akabarikiwa zaidi ya hata mara ya kwanza. Wakati huu Shetani alikuwa amejiondoa, na hakusema tena au kufanya chochote, na kutoka hapo kuenda mbele Ayubu hakuhitilafiana tena na Shetani au kushambulia Shetani, na Shetani hakutoa mashtaka tena dhidi ya baraka za Mungu kwa Ayubu.
Ayubu Aishi Nusu ya Mwisho ya Maisha Yake Katikati ya Baraka za Mungu
Ingawaje baraka Zake wakati huo zilikuwa tu zinajumuisha kondoo, ng’ombe, ngamia, na rasilimali za dunia, na kadhalika, baraka ambazo Mungu alitaka kumpa Ayubu katika moyo Wake zilikuwa mbali zaidi na hizi. Kwa wakati huo ziliporekodiwa, ni aina gani za ahadi za milele ambazo Mungu alipenda kumpa Ayubu? Katika baraka Zake kwa Ayubu, Mungu hakugusia au kutaja kuhusu mwisho wake, na haijalishi umuhimu au cheo ambacho Ayubu alishikilia ndani ya moyo wa Mungu, kwa ujumla Mungu alikuwa akimtambua katika baraka Zake. Mungu hakutangaza mwisho wa Ayubu. Hii inamaanisha nini? Wakati huo, wakati mpango wa Mungu ulikuwa bado haujafikia sehemu ya kutangaza mwisho wa binadamu, mpango huo ulikuwa bado uingie kwenye awamu ya mwisho ya kazi yake, Mungu hakutaja chochote kuhusu mwisho, huku akimpa binadamu baraka za rasilimali za dunia tu. Maana ya hii ni kwamba nusu ya mwisho ya maisha ya Ayubu ilipita katikati ya baraka za Mungu na hii ndiyo iliyomfanya kuwa tofauti na wale watu wengine—lakini kama wao alizeeka, na kama mtu yeyote yule wa kawaida siku ilifika ambapo aliuambia ulimwengu kwaheri. Na hivyo imerekodiwa kwamba “Kwa hivyo Ayubu akafariki, akiwa mzee na aliyejawa na siku” (Ayubu 42:17). Nini maana ya “akafariki … aliyejawa na siku” hapa? Katika enzi ya kabla Mungu kutangaza mwisho, Mungu alimwekea Ayubu matarajio ya maisha ambayo angeishi, na wakati umri huo ulipofikiwa Alimruhusu Ayubu kuondoka kiasili kutoka ulimwengu huu. Kutoka baraka ya pili ya Ayubu hadi kifo chake, Mungu hakuongezea ugumu wowote. Kwake Mungu, kifo cha Ayubu kilikuwa cha kiasili, na pia kilihitajika, kilikuwa kitu cha kawaida sana na wala si hukumu au shutuma. Alipokuwa hai, Ayubu alimwabudu na kumcha Mungu; kuhusiana na ni aina gani ya mwisho aliyokuwa nayo kufuatia kifo chake, Mungu hakusema chochote, wala kutoa maoni yoyote kuhusu hilo. Mungu ni mwenye busara katika kile Anachosema na kufanya, na maudhui na kanuni za maneno na vitendo vyake yanalingana na awamu ya kazi Yake na kipindi Anachofanyia kazi. Ni aina gani ya mwisho ambayo mtu kama Ayubu alikuwa nayo katika moyo wa Mungu? Je, Mungu alikuwa amefikia aina yoyote ya uamuzi katika moyo Wake? Bila shaka Alikuwa! Ni vile tu hili lilikuwa halijulikani kwa binadamu; Mungu hakutaka kumwambia binadamu wala Hakuwa na nia yoyote ya kumwambia binadamu. Na hivyo, kwa kuongea juujuu tu, Ayubu alikufa akiwa amejawa na siku, na hivyo ndivyo maisha ya Ayubu yalivyokuwa.
Gharama Iliyoishi kwa kudhihirishwa na Ayubu Wakati wa Maisha Yake
Je, Ayubu aliishi maisha ya thamani? Thamani yake ilikuwa wapi? Ni kwa nini inasemwa kwamba aliishi maisha yenye thamani? Kwa binadamu, thamani yake ilikuwa gani? Kutoka katika mtazamo wa binadamu, aliwawakilisha wanadamu ambao Mungu alitaka kuokoa, kwa kuwa na ushuhuda wa kipekee kwa Mungu mbele ya Shetani na watu wa ulimwengu. Alitimiza wajibu ambao ulistahili kutimizwa na kiumbe wa Mungu, na kuweka mfano halisi wa kuigwa, na kutenda kama kielelezo, kwa wale wote ambao Mungu angependa kuwaokoa, akiruhusu watu kuona kwamba inawezekana kabisa kushinda Shetani kwa kumtegemea Mungu. Nayo thamani yake kwa Mungu ilikuwa gani? Kwa Mungu, thamani ya maisha ya Ayubu ilikuwa ndani ya uwezo wake wa kumcha Mungu, kumwabudu Mungu, kutolea ushuhuda vitendo vya Mungu, na kusifu vitendo vya Mungu, kumpa Mungu tulizo na kitu cha kufurahia; kwa Mungu, thamani ya maisha ya Ayubu ilikuwa pia kwa namna ambavyo, kabla ya kifo chake, Ayubu alipitia majaribio na kushinda Shetani, na akawa na ushuhuda wa kipekee kwa Mungu mbele ya Shetani na watu wa ulimwengu, akimtukuza Mungu miongoni mwa wanadamu, akiutuliza moyo wa Mungu na kuruhusu moyo wa Mungu wenye hamu kuyaona matokeo, na kuliona tumaini. Ushuhuda wake uliweka mfano wa kufuatwa kutokana na uwezo wake wa kusimama imara katika ushuhuda wa Mungu, na kuweza kumwaibisha Shetani kwa niaba ya Mungu, katika kazi ya Mungu ya kuwasimamia wanadamu. Je, hii si thamani ya maisha ya Ayubu? Ayubu alileta tulizo kwa moyo wa Mungu, alimpa Mungu kionjo cha furaha ya kutukuzwa, na akaanzisha mwanzo mzuri kwa mpango wa usimamizi wa Mungu. Na kuanzia hapo kuenda mbele jina la Ayubu likawa ishara ya utukuzaji wa Mungu na ishara ya kushinda kwa wanadamu dhidi ya Shetani. Kile Ayubu aliishi kwa kudhihirisha wakati wa maisha yake na ushindi wake wa kipekee dhidi ya Shetani milele utabakia ukifurahiwa mno na Mungu na utimilifu wake, unyofu, na hali yake ya kumcha Mungu itaheshimiwa na kuigwa na vizazi vitakavyokuja. Milele atafurahiwa mno na Mungu kama johari lisilo na makosa, wala dosari, na pia ndivyo alivyo na thamani ya kuthaminiwa sana na binadamu!
Kisha, hebu tuangalie kazi ya Mungu wakati wa Enzi ya Sheria.
D. Taratibu za Enzi ya Sheria
Amri Kumi
Kanuni za Kujenga Madhabahu
Taratibu za Ushughulikiaji wa Watumishi
Taratibu za Wizi na Fidia
Kutimiza Mwaka wa Sabato na Karamu Tatu
Taratibu za Siku ya Sabato
Taratibu za Kutoa Sadaka
Sadaka zilizoteketezwa
Sadaka za Unga
Sadaka za Amani
Sadaka za Dhambi
Sadaka za Hatia
Taratibu za Sadaka za Kuhani (Aroni na Watoto Wake wa Kiume Waamrishwa Kutii)
Sadaka za Kuteketezwa na Kuhani
Sadaka za Unga na Kuhani
Sadaka za Dhambi na Kuhani
Sadaka za Hatia na Kuhani
Sadaka za Amani na Kuhani
Taratibu za Ulaji wa Sadaka na Kuhani
Wanyama Walio Halali na Wale Walio Haramu (Wale Wanaoweza na Wasioweza Kuliwa)
Taratibu za Utakasaji Wanawake Baada ya Kujifungua
Viwango vya Uchunguzi wa Ukoma
Taratibu kwa Wale Ambao Wameponywa Ukoma
Taratibu za Kuzitakasa Nyumba Zilizoambukizwa
taratibu za Wale Wanaougua Kisonono Kisicho cha Kawaida
Siku ya Upatanisho Wa Mungu na Binadamu Ambayo Lazima Iadhimishwe Mara Moja Kwa Mwaka
Sheria za Kuchinja Ng’ombe na Mbuzi
Kuzuiliwa kwa Mazoea Yafuatayo Yanayochukiza Ya Watu wa Mataifa (Si Kutenda Kujamiiana Kwa Maharimu, na Kadhalika)
Taratibu Ambazo Lazima Zifuatwe na Watu (“Mtakuwa watakatifu: kwani Mimi Yehova Mungu wenu ni mtakatifu.”)
Kutendewa kwa Wale Wanaotoa Kafara Watoto Wao kwa Molka
Taratibu za Adhabu ya Uhalifu wa Uasherati
Sheria Zinazofaa Kufuatiliwa na Kuhani (Sheria za Tabia Yao Ya Kila Siku, Sheria za Matumizi ya Mambo matakatifu, Sheria za Kutoa Sadaka na Kadhalika)
Karamu Zinazofaa Kufuatiliwa (siku ya Sabato, Pentekoste, Siku ya Upatanisho wa Mungu na Binadamu kwa Maisha ya Kifo cha Yesu, na Kadhalika)
Taratibu Nyingine (Kuteketezwa kwa Taa, Mwaka wa Jubilii, Ukombozi wa Ardhi, Ulaji wa Viapo, Utoaji wa Zaka, na Kadhalika)
Taratibu za Enzi ya Sheria ni Thibitisho la Kweli la Maelekezo ya Mungu kwa Wanadamu Wote
Hivyo, mmezisoma taratibu na kanuni hizi za Enzi ya Sheria, kweli? Je, taratibu hizi zinajumuisha mseto mpana? Kwanza, zinajumuisha Amri Kumi, na baadaye kuna taratibu za namna ya kujenga madhabahu, na kadhalika. Hizi zinafuatwa na taratibu za kuitimiza Sabato na kuzidumisha zile karamu tatu, na baadaye kuna taratibu za kutoa sadaka. Je, mnaona ni aina ngapi za sadaka ambazo zimo? Kunazo sadaka zilizoteketezwa, sadaka za unga, sadaka za amani, sadaka za dhambi, na kadhalika, ambazo zinafuatwa na taratibu za sadaka za kuhani, zikiwemo sadaka zilizoteketezwa na sadaka za unga zilizotolewa na Kuhani, na aina nyingine za sadaka. Taratibu za nane ni za ulaji wa sadaka na Kuhani, na kisha kunazo taratibu zinazofaa kudumishwa wakati wa maisha ya watu. Kunayo masharti ya vipengele vingi vya maisha ya watu, kama vile taratibu zinazotawala kile wanachoweza au wasichoweza kula, kwa utakasaji wa wanawake baada ya wao kujifungua, na kwa wale ambao wameponywa ugonjwa wa ukoma. Katika taratibu hizi, Mungu Anafikia hadi kiwango cha kuzungumzia kuhusu ugonjwa, na kunazo hata sheria za kuchinja kondoo na ng’ombe, na kadhalika. Kondoo na ng’ombe waliumbwa na Mungu, na unafaa kuwachinja hata hivyo Mungu anakuambia kufanya hivyo; kunayo, bila shaka, sababu ya maneno ya Mungu, na ni sahihi bila shaka kutenda kama inavyokaririwa na Mungu, na kwa hakika itakuwa ya manufaa kwa watu! Kunazo pia karamu na sheria za kufuatwa, kama vile siku ya Sabato, Pasaka, na zaidi—Mungu aliweza kuzungumzia yote haya. Hebu tuangalie zile za mwisho: taratibu nyingine—kuteketezwa kwa taa, mwaka wa Jubilii, ukombozi wa ardhi, ulaji wa viapo, utoaji wa zaka, na kadhalika. Je, hizi zinajumuisha mseto mpana? Kitu cha kwanza cha kuzungumziwa ni suala la sadaka la watu, kisha kunazo taratibu za wizi na fidia, na udumishaji wa siku ya Sabato…; kila mojawapo ya maelezo ya maisha yanahusishwa. Hivi ni kusema, wakati Mungu alianza kazi Yake rasmi ya mpango Wake wa usimamizi, Aliweka wazi taratibu nyingi ambazo zilifaa kufuatwa na binadamu. Taratibu hizi zilikuwa ili kumruhusu binadamu kuishi maisha ya kawaida ya binadamu hapa duniani, maisha ya kawaida ya binadamu ambayo hayajatenganishwa na Mungu na uongozi Wake. Mungu alimwambia binadamu kwanza namna ya kuunda madhabahu, namna ya kuyaunda madhabahu. Baada ya hapo, Alimwambia binadamu namna ya kutoa sadaka, na kuamuru namna ambavyo binadamu alifaa kuishi—kile alichofaa kutilia maanani katika maisha, kile alichofaa kutii, kile anachofaa na hafai kufanya. Kile Mungu alichoweka wazi kwa binadamu kilikuwa kinakubalika chote, na pamoja na tamaduni, taratibu, na kanuni hizi Aliwastanisha tabia ya watu, kuongoza maisha yao, kuongoza uanzishaji wao wa sheria za Mungu, kuwaongoza kuja mbele ya madhabahu ya Mungu, kuwaongoza katika kuishi maisha miongoni mwa mambo mengine yote ambayo Mungu alikuwa amemuumbia binadamu na yaliyomilikiwa na mpangilio na marudio ya mara kwa mara na ya kiasi. Kwanza Mungu alitumia taratibu na kanuni hizi rahisi kuweka vipimo kwa binadamu, ili hapa duniani binadamu aweze kuwa na maisha ya kawaida ya kumwabudu Mungu, aweze kuwa na maisha ya kawaida; hivi ndivyo yalivyo maudhui mahususi ya mwanzo wa mpango Wake wa usimamizi wa miaka elfu sita. Taratibu na sheria zinajumuisha maudhui mapana mno, yote ni maelezo ya mwongozo wa Mungu wa mwanadamu wakati wa Enzi ya Sheria, lazima yangekubaliwa na kuheshimiwa na watu waliokuwa wamekuja kabla ya Enzi ya Sheria, ni rekodi ya kazi iliyofanywa na Mungu katika Enzi ya Sheria, na ni ithibati ya kweli ya uongozi na mwongozo wa Mungu kwa wanadamu wote.
Wanadamu Hawatenganishwi Milele na Mafundisho na Matoleo ya Mungu
Katika taratibu hizi tunaona kwamba mwelekeo wa Mungu katika kazi Yake, katika usimamizi Wake, na kwa wanadamu ukiwa wa kumakinikia zaidi, wa ukweli, wa bidii, na wa kuwajibika. Anaifanya kazi ambayo lazima Afanye miongoni mwa wanadamu kulingana na hatua Zake, bila ya hitilafu hata kidogo, Akiongea maneno ambayo lazima aongee kwa wanadamu bila ya kosa au upungufu hata kidogo, Akimruhusu binadamu kuona kwamba hawezi kutenganishwa na uongozi wa Mungu, na Akimwonyesha namna ambavyo yale yote ambayo Mungu anafanya na kusema yalivyo muhimu kwa wanadamu. Licha ya kile ambacho binadamu alivyo katika enzi ijayo, kwa ufupi, wakati wa mwanzo kabisa—wakati wa Enzi ya Sheria—Mungu alifanya mambo haya rahisi. Kwa Mungu, dhana za watu kumhusu Mungu, ulimwengu na mwanadamu katika enzi hiyo zilikuwa za kidhahania na zisizoeleweka, na ingawaje walikuwa na fikra na nia fulani husika, zote zilikuwa hazina uwazi na si sahihi, na hivyo wanadamu walikuwa hawawezi kutenganishwa kutoka kwa mafundisho na matoleo ya Mungu kwao. Wanadamu wa mapema zaidi hawakujua chochote, na hivyo Mungu alilazimika kuanza kumfunza binadamu kutoka kwenye kanuni za juujuu na za kimsingi zaidi kwa minajili ya uwepo na taratibu zinazohitajika za kuishi, kutia moyoni mambo haya yote kwenye moyo wa binadamu kidogo kidogo, na kumpa binadamu uelewa wa Mungu kwa utaratibu, kutambua na kuelewa uongozi wa Mungu kwa utaratibu, na dhana ya kimsingi ya uhusiano kati ya binadamu na Mungu, kupitia kwa taratibu hizi na kupitia kwa sheria hizi, ambazo zilikuwa za maneno. Baada ya kutimiza athari hii, ndipo tu Mungu aliweza, kidogo kidogo, kufanya kazi ambayo Angeweza kufanya baadaye, na hivyo taratibu hizi na kazi iliyofanywa na Mungu kwenye Enzi ya Sheria zikawa ndiyo msingi wa kazi Yake ya kuwaokoa wanadamu na hatua ya kwanza ya kazi katika mpango wa usimamizi wa Mungu. Ingawaje, kabla ya kazi ya Enzi ya Sheria, Mungu alikuwa ameongea naye Adamu, Hawa, na babu zao, amri na mafunzo hayo hayakuwa ya hatua kwa hatua sana au mahususi ili kutolewa moja baada ya nyingine kwa mwanadamu, na hayakuwa yameandikwa, wala hayakuwa taratibu. Hii ni kwa sababu, kwa wakati huo, mpango wa Mungu haukuwa umeenda mbali kiasi hicho; na Mungu alipokuwa amemwongoza binadamu hadi katika hatua hii tu ndipo Alipoweza kuongea taratibu hizi za Enzi ya Sheria, na kuanza kumfanya binadamu kuzitekeleza. Ulikuwa ni mchakato unaohitajika, na matokeo yasingeweza kuepukika. Tamaduni na taratibu hizi rahisi zinaonyesha binadamu hatua za usimamizi wa kazi ya Mungu na hekima ya Mungu inayofichuliwa katika mpango Wake wa usimamizi. Mungu anayajua maudhui yapi na mbinu zipi za kutumia ili kuanza, mbinu zipi za kutumia kuendelea na mbinu zipi za kutumia kumaliza ili aweze kupata kundi la watu lililo na ushuhuda Kwake Yeye, Aweze kupata kundi la watu walio na akili sawa na Yake. Anajua kile kilicho ndani ya binadamu, na kujua kile kinachokosa kwa binadamu, Anajua kile anachofaa kutoa, na namna Anavyofaa kumwongoza binadamu, na pia ndivyo Anavyojua kile binadamu anafaa na hafai kufanya. Binadamu ni kama kikaragosi: Ingawaje hakuwa na uelewa wowote wa mapenzi ya Mungu, alilazimika kuongozwa na kazi ya Mungu ya usimamizi, hatua kwa hatua hadi leo. Hakukuwa na kutodhihirika kokote katika moyo wa Mungu kuhusu kile Alichofaa kufanya; katika moyo Wake kulikuwa na mpango wazi na kamilifu kabisa, na Alitekeleza kazi hiyo ambayo Yeye mwenyewe alitaka kufanya kulingana na hatua Zake na mpango Wake, Akiendelea mbele kutoka katika hali ya juujuu hadi ile hali ya ndani kabisa. Ingawaje Hakuwa ameonyesha kazi ambayo Alifaa kufanya baadaye, kazi Yake ya baadaye bado iliendelea kutekelezwa na kuendelea mbele kulingana kabisa na mpango Wake, ambayo ni maonyesho ya kile Mungu anacho na alicho, na pia ni mamlaka ya Mungu. Licha ya ni awamu gani ya mpango Wake wa usimamizi ambayo Anafanya, tabia Yake na kiini chake kinamwakilisha Yeye mwenyewe—na hakuna kosa katika haya. Licha ya enzi, au awamu ya kazi, aina ya watu ambao Mungu anapenda, aina ya watu ambao Anachukia, tabia Yake, na chote ambacho Anacho na alicho hakitawahi kubadilika. Ingawaje taratibu na kanuni hizi ambazo Mungu alianzisha katika kazi ya Enzi ya Sheria zinaonekana rahisi na za juujuu kwa watu wa leo, na Ingawaje ni rahisi kuelewa na kutimiza, ndani ya hizo kunayo bado hekima ya Mungu, na kunayo bado tabia ya Mungu na kile Anacho na alicho. Kwani ndani ya taratibu hizi zinazoonekana rahisi, uwajibikaji na utunzaji wa Mungu kwa wanadamu unaonyeshwa, na kiini kizuri cha fikira zake, kumruhusu binadamu kutambua kwa kweli ukweli kwamba Mungu anatawala mambo yote na mambo yote yanadhibitiwa kwa mkono Wake. Haijalishi ni kiwango kipi cha maarifa ambacho wanadamu watajifunza au nadhari au mafumbo mangapi wanaelewa, kwa Mungu hakuna chochote kati ya hivi ambavyo vinaweza kusawazisha toleo Lake kwa, na uongozi wa wanadamu; wanadamu milele hawatatenganishwa na mwongozo wa Mungu na kazi ya kibinafsi ya Mungu. Huu ndiyo uhusiano kati ya binadamu na Mungu usiotenganishwa. Licha ya kama Mungu anakupa amri, au taratibu, au Anakupa ukweli ili kuyaelewa mapenzi Yake, haijalishi ni nini Anachofanya, nia ya Mungu ni kumwongoza binadamu hadi katika siku nzuri ya kesho. Maneno yaliyotamkwa na Mungu na kazi Anayofanya ni ufunuo wa kipengele kimoja cha kiini Chake na vilevile ni ufunuo wa kipengele kimoja cha tabia Yake na hekima Yake, zote hizi ni hatua zisizozuilika katika mpango Wake wa usimamizi. Hili halifai kupuuzwa! Mapenzi ya Mungu yamo katika chochote Anachofanya; Mungu haogopi maoni yasiyo mahali pake wala haogopi dhana au fikira zozote za binadamu kuhusu Yeye. Yeye hufanya kazi Yake tu, na kuendeleza usimamizi Wake, kulingana na mpango Wake wa usimamizi, usiozuiliwa na mtu yeyote, suala lolote au kifaa chochote.
Sawa, ni hayo kwa leo. Tuonane wakati mwingine!

November 9, 2013

Chanzo: Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II Sehemu ya Saba

Soma Zaidi: Matamshi ya Mwenyezi Mungu


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni