Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I)” Sehemu ya Tano
Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Shetani Hajawahi Kuthubutu Kukiuka Mamlaka ya Muumba, na Kwa Sababu Hiyo, Vitu Vyote Vinaishi kwa Mpangilio
Mungu Pekee, Ambaye Anao Utambulisho wa Muumba, Anamiliki Mamlaka ya Kipekee
Utambulisho wa Muumba ni wa Kipekee, na Hufai Kufuata lile Wazo la Imani ya Kuabudu Miungu Wengi
Ingawaje Binadamu Amepotoka, Angali Anaishi Chini ya Ukuu wa Mamlaka ya Muumba
Mwenyezi Mungu anasema, Hili ni dondoo kutoka katika Kitabu cha Ayubu, na “yeye” katika maneno haya inaashiria Ayubu. Ingawaje imeandikwa kwa muhtasari, sentensi hii inaelezea masuala mengi. Inafafanua mabadilishano fulani kati ya Mungu na Shetani kwenye ulimwengu wa kiroho, na inatwambia kuwa kiini cha maneno ya Mungu kilikuwa Shetani. Pia inarekodi kile kilichozungumziwa mahususi na Mungu. Maneno ya Mungu yalikuwa amri na shurutisho kwa Shetani. Maelezo mahususi ya shurutisho hili ni kuhusiana na kuyaokoa maisha ya Ayubu na pale ambapo Mungu aliweka masharti namna ambavyo Shetani alifaa kumshughulikia Ayubu—Shetani alilazimika kuyaokoa maisha ya Ayubu. Kitu cha kwanza tunachojifunza kutoka kwenye sentensi hii ni kwamba matamshi haya yalitamkwa na Mungu kwa Shetani. Kulingana na maandishi ya asili ya Kitabu cha Ayubu, yanatwambia usuli wa matamshi kama hayo: Shetani alipenda kumshutumu Ayubu, na hivyo lazima angepokea huo mkataba wa Mungu kabla hajamtia majaribuni. Wakati alipokubali ombi la Shetani kumjaribu Ayubu, Mungu aliweza kumtajia Shetani sharti lifuatalo: “Tazama, yeye yuko katika mkono wako; lakini uuhifadhi uhai wake.” Ni nini asili ya maneno haya? Ni wazi kwamba ni amri, ni shurutisho. Baada ya kuelewa asili ya maneno haya, unafaa, bila shaka, pia kung’amua kwamba Aliyetoa shurutisho hili ni Mungu, na kwamba aliyepokea amri hii, na akaitii, ni Shetani. Sina haja ya kusema kwamba katika shurutisho hili, uhusiano kati ya Mungu na Shetani uko wazi kwa yeyote ambaye anasoma maneno haya. Bila shaka, huu ndio uhusiano kati ya Mungu na Shetani katika ulimwengu wa kiroho, na tofauti kati ya utambulisho na hadhi ya Mungu na Shetani, iliyoelezwa kwenye rekodi za mabadilishano ya mazungumzo ya Mungu na Shetani katika Maandiko, na, hadi leo, ni mfano mahususi na rekodi ya maandishi ambapo binadamu anaweza kujifunza tofauti kuu kati ya utambulisho na hadhi ya Mungu na Shetani. Wakati huu, lazima Niseme kwamba, rekodi ya maneno haya ni waraka muhimu sana katika ufahamu wa binadamu juu ya hadhi na utambulisho wa Mungu, na inatoa taarifa muhimu kwa maarifa ya mwanadamu kuhusu Mungu. Kupitia mabadilishano haya ya Mungu na Shetani katika ulimwengu wa kiroho, binadamu anaweza kuelewa dhana moja mahususi katika mamlaka ya Muumba. Maneno haya ni ushuhuda mwingine wa kuonyesha mamlaka ya kipekee ya Muumba.
Kwa nje, ni mabadilishano kati ya Yehova Mungu na Shetani. Hali yao halisi ni kwamba, mtazamo ambao Yehova Mungu anaongea, na nafasi ambayo Anazungumzia, ni ya juu zaidi kuliko ya Shetani. Hivyo ni kusema kwamba Yehova Mungu anamwamuru Shetani na sauti ya kushurutisha, na Anamwambia Shetani ni nini anafaa afanye na kile hafai kufanya, kwamba tayari Ayubu yu mikononi mwake, na yuko huru kumfanya Ayubu vyovyote atakavyo—lakini asiyachukue maisha ya Ayubu. Ujumbe hapa ni, ingawaje Ayubu alikuwa amewekwa kwenye mikono ya Shetani, maisha yake hayakuchukuliwa na Shetani; hakuna anayeweza kuchukua maisha ya Ayubu kutoka mikononi mwa Mungu isipokuwa Mungu amruhusu. Mtazamo wa Mungu unafafanuliwa waziwazi katika amri hii kwa Shetani, na amri hii pia inajionyesha na kufichua msimamo ambao Yehova Mungu anazungumza na Shetani. Katika haya, Yehova Mungu hashikilii tu hadhi ya Mungu aliyeumba nuru, na hewa, na vitu vyote na viumbe hai, au ya Mungu anayeshikilia ukuu juu ya vitu vyote na viumbe hai, lakini pia ya Mungu ambaye anaamuru mwanadamu, na kuamuru Jahanamu, Mungu ambaye anadhibiti maisha na kifo cha viumbe vyote hai. Katika ulimwengu wa kiroho, ni nani mbali na Mungu ambaye angethubutu kutoa shurutisho kama hilo kwa Shetani? Na ni kwa nini Mungu binafsi Alitoa shurutisho Lake kwa Shetani? Kwa sababu maisha ya binadamu, pamoja na yale ya Ayubu, yanadhibitiwa na Mungu. Mungu hakumruhusu Shetani kujeruhi au kuchukua maisha ya Ayubu, hivyo ni kusema kwamba kabla ya Mungu kumruhusu Shetani kumjaribu Ayubu, Mungu bado alikumbuka kutoa shurutisho maalum kama hilo, na kwa mara nyingine Akamwamuru Shetani asiyachukue maisha ya Ayubu. Shetani hajawahi kuthubutu kukiuka mamlaka ya Mungu, na, vilevile, amesikiliza kwa umakinifu siku zote na kutii shurutisho na amri mahususi za Mungu, asiwahi thubutu kuzivunja, na, bila shaka asithubutu kubadilisha kwa hiari shurutisho zozote za Mungu. Hiyo ndiyo mipaka ambayo Mungu amemwekea wazi Shetani, na hivyo Shetani hajawahi thubutu kuvuka mipaka hiyo. Huu si uwezo wa mamlaka ya Mungu? Je, huu si ushuhuda wa mamlaka ya Mungu? Wa namna ya kuwa mbele ya Mungu, na namna ya kumtazama Mungu, Shetani anao ung'amuzi bora zaidi kuliko mwanadamu, hivyo, katika ulimwengu wa kiroho, Shetani anaona hadhi na mamlaka ya Mungu vizuri sana, na anatambua sana ule uwezo wa mamlaka ya Mungu na kanuni zinazotilia mkazo kwenye mamlaka Yeye. Hathubutu, kamwe, kutozitilia maanani kanuni hizo, wala hathubutu kukiuka kanuni hizo kwa vyovyote vile, au kufanya chochote ambacho kinakiuka mamlaka ya Mungu, na hathubutu kukabiliana na hasira ya Mungu kwa njia yoyote. Ingawaje ni mwovu na mwenye kiburi kiasili, Shetani hajawahi kuthubutu kuvuka mipaka na viwango alivyowekewa na Mungu. Kwa miaka milioni, ametii kwa umakinifu mipaka hii, ametii kila amri na shurutisho lililotolewa na Mungu na hajawahi kuthubutu kukanyaga juu ya alama. Ingawaje ni mwenye kijicho, Shetani ni “mwerevu” zaidi kuliko mwanadamu aliyepotoka; anajua utambulisho wa Muumba, na anajua mipaka yake. Kutokana na vitendo vya Shetani vya kunyenyekea tunaweza kuona kwamba mamlaka na nguvu za Mungu ni maelekezo ya mbinguni ambayo hayawezi kukiukwa na Shetani, na kwamba yanatokana na upekee na mamlaka ya Mungu ndiposa viumbe vyote vinabadilika na kuzalisha katika njia ya mpangilio, kwamba mwanadamu anaweza kuishi na kuongezeka kupitia ndani ya mkondo ulioanzishwa na Mungu, huku hakuna mtu au kifaa kinachoweza kuuharibu mpango huu, na hakuna mtu au kifaa kinachoweza kubadilisha sheria hii—kwani vyote vinatoka kwenye mikono ya Muumba na kwenye mpangilio na mamlaka ya Muumba.
Tazama zaidi: Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I)” Sehemu ya Kwanza
Kujua zaidi: Chanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni