Matamshi ya Mungu | “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” Sehemu ya Kwanza
Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Uzito wa Matokeo katika Mioyo ya Watu
Imani za Watu Haziwezi Kubadilishwa na Ukweli
Kunayo Maoni Mengi Yanayohusu Kiwango Ambacho Mungu Hutumia Kuasisi Matokeo ya Binadamu
Mwenyezi Mungu
anasema, Yaonekana mnavyo vitu katika mioyo yenu kuhusu njia mnayofaa kutembea na mmeimarisha uelewa na ung'amuzi mzuri kuhusu vitu hivyo. Lakini kama kila kitu mlichokisema kitaishia kuwa maneno matupu au uhalisia halisi inategemea ni nini mnatilia maanani katika mazoea yako ya kila siku. Mmepata mavuno kutoka kwenye dhana zote za ukweli kupitia miaka hii, kwenye falsafa na kwenye maudhui ya ukweli. Hii inathibitisha kwamba watu siku hizi wanatilia mkazo kule kutafuta ukweli. Na kutokana na hayo, kila dhana na kila kipengele cha ukweli kwa hakika kimeweka mizizi kwenye mioyo ya baadhi ya watu. Hata hivyo, ni nini hasa Ninachoogopa sana? Kwamba ingawa wahusika wa ukweli, na nadharia hizi, yameweza kunakili mizizi yao, maudhui halisi bado hayana uzito mkubwa katika mioyo yenu. Wakati mnapokumbana na masuala, mnapopitia majaribio, mnapopitia chaguo—mtaweza kwa kiwango kipi kutumia uhalisia wa ukweli huu vizuri? Je, haya yote yatawasaidia kupitia kwenye ugumu wenu na kuwafanya kuibuka kutoka kwenye majaribio yenu baada ya kutosheleza nia za Mungu? Je, mtasimama imara katika majaribio yenu na kushuhudia kwa sauti na waziwazi kwake Mungu? Je, mmewahi kuwa na kivutio katika masuala haya awali? Mniruhusu kuuliza: Katika mioyo yenu, kwenye fikira na tafakari zenu za kila siku, ni nini hicho ambacho ni muhimu sana kwenu? Mmewahi kuja kwenye hitimisho? Ni nini mnachosadiki kuwa kitu muhimu zaidi? Baadhi ya watu husema “ni kuweka ukweli katika matendo, bila shaka”; baadhi ya watu husema “bila shaka ni kulisoma neno la Mungu kila siku”; baadhi ya watu husema “ni kujiweka mbele ya Mungu na kuomba Mungu kila siku, bila shaka”; na kisha kunao wale wanaosema “bila shaka ni kutekeleza wajibu wangu kwa njia bora kila siku”; kunao baadhi ya watu pia ambao wanasema wanafikiria wakati wote tu kuhusu namna ya kumtosheleza Mungu, namna ya kumtii Yeye katika mambo yote, na namna ya kuchukua hatua kulingana na mapenzi Yake. Je, hivi ndivyo ilivyo? Je, hivi ndivyo kila kitu kinavyohitajika kufanywa? Kwa mfano, kunao baadhi wanaosema: “Mimi ninataka tu kumtii Mungu, lakini kitu kinapofanyika siwezi kumtii Yeye.” Baadhi ya watu husema: “Nataka tu kumtosheleza Mungu. Hata kama ningemtosheleza Yeye mara moja tu, hilo lingetosha, lakini sitoweza kumtosheleza Yeye.” Na baadhi ya watu husema: “Ninataka tu kumtii Mungu. Katika nyakati za majaribio nataka kunyenyekea katika mipango Yake, huku nikitii ukuu na mipangilio Yake, bila ya malalamiko au maombi yoyote. Ilhali karibu kila wakati ninashindwa kuwa mtiifu.” Baadhi ya watu wengine husema: “Ninapokabiliwa na uamuzi, siwezi kamwe kutia ukweli katika matendo. Siku zote nataka kutosheleza mwili, siku zote nataka kutosheleza matamanio yangu ya kibinafsi ninayojitakia.” Ni nini sababu ya haya? Kabla ya jaribio la Mungu kufika, je, mmewahi kujipa changamoto nyinyi wenyewe mara nyingi, na kujijaribu nyinyi wenyewe mara nyingi? Oneni kama kweli mnaweza kumtii Mungu, kuweza kwa kweli kumtosheleza Mungu, na kuwa na hakika kutomsaliti Mungu. Tazameni kama hamwezi kujitosheleza, kutojitosheleza matamanio yenu ya kibinafsi, lakini kumtosheleza Mungu tu, bila ya chaguo lenu la kibinafsi. Je, yupo aliye hivi? Kwa hakika, kunayo hoja moja tu ambayo imewekwa mbele ya macho yenu nyinyi wenyewe. Ni kile ambacho kila mmoja wenu anavutiwa nacho, kile ambacho mnachotaka kujua zaidi, na hilo ni suala la matokeo na hatima ya kila mmoja wenu. Huenda msitambue, lakini hili ni jambo ambalo hakuna anayeweza kulikataa. Ninajua kwamba kunao baadhi ya watu ambao, tunapokuja katika ukweli wa matokeo ya binadamu, ahadi ya Mungu kwa ubinadamu, na aina gani ya hatima ambayo Mungu ananuia kumleta binadamu katika, tayari wamefanyia uchunguzi neno la Mungu katika masuala haya mara kadhaa. Kisha kunao ambao kila mara wanalitafuta na kulifikiria kwenye akili zao, na bado hawapati matokeo, au pengine wanafikia katika hitimisho fulani isiyoeleweka. Hatimaye bado hawana hakika kuhusu ni aina gani ya matokeo yanayowasubiri. Wakati wa kuyakubali mawasiliano ya ukweli, wakati wa kuyakubali maisha ya kanisa, wakati wa kutenda wajibu wao, baadhi ya watu siku zote wanataka kujua jibu wazi kwa maswali yafuatayo: Matokeo yangu yatakuwa yapi? Ninaweza kutembelea njia hii hadi mwisho wake? Mwelekeo wa Mungu kwake binadamu ni upi? Baadhi ya watu huwa hata na wasiwasi: Nimefanya baadhi ya mambo siku zilizopita, nimesema baadhi ya mambo, sikumtii Mungu, nimefanya mambo fulani ambayo yamemsaliti Mungu, kulikuwa na masuala fulani ambapo sikumtosheleza Mungu, niliuumiza moyo wa Mungu, nilimfanya Mungu kunikasirikia, nilimfanya Mungu kunichukia na kuniona kwamba ninachukiza, hivyo basi pengine matokeo yangu hayajulikani. Ni haki kusema kwamba watu wengi zaidi wanahisi wasiwasi kuhusu matokeo yao wenyewe. Hakuna anayethubutu kusema: “Nahisi kwa uhakika wa asilimia mia moja kwamba nitaishi Ninao uhakika wa asilimia mia moja kwamba ninaweza kuzitosheleza nia za Mungu; mimi ni mtu anayefuata moyo wa Mungu; mimi ni mtu anayesifiwa na Mungu.” Baadhi ya watu hufikiria ni vigumu hasa kufuata njia ya Mungu, na kwamba kutia ukweli katika matendo ndilo jambo gumu zaidi la kufanya. Kwa hivyo, watu hawa hufikiria hawawezi kusaidika, na hawathubutu kuwa na matumaini ya kuwa na matokeo mazuri. Au pengine wanasadiki kwamba hawawezi kutosheleza nia za Mungu, na kuweza kuishi; na kwa sababu ya haya watasema kwamba hawana matokeo, na hawawezi kufikia hatima nzuri. Licha ya jinsi watu hufikiria, kila mmoja anastaajabu kuhusu matokeo yao mara nyingi. Kuhusu masuala ya siku zao za usoni, kuhusu maswali ya kile watakachopata wakati Mungu atakapomaliza kazi Yake, watu hawa siku zote wanapiga hesabu, siku zote wanapanga. Baadhi ya watu wanalipia bei mara dufu; baadhi ya watu wanaacha familia zao na kazi zao; baadhi ya watu wanakata tamaa katika ndoa zao; baadhi ya watu wanakubali bila kulalamika kutumia rasilmali kwa ajili ya Mungu; baadhi ya watu huacha nyumba zao ili kutenda wajibu wao; baadhi ya watu huchagua ugumu, na kuanza kufanya kazi ambazo ni chungu zaidi na zinachosha zaidi; baadhi ya watu huchagua kuutoa utajiri wao, kujitolea kila kitu chao; na bado baadhi ya watu huchagua kufuata ukweli na kufuatilia kumjua Mungu. Haijalishi namna mnavyochagua kutenda, namna mnavyotenda ndiyo muhimu zaidi? (Si muhimu.) Ni vipi tunavyoelezea kwamba si muhimu, basi? Kama namna hiyo si muhimu, basi ni nini muhimu? (Tabia nzuri kwa nje si wakilishi wa kutia ukweli katika matendo.) (Kile ambacho kila mmoja anafikiria si muhimu. Cha msingi hapa ni kama tumeweza kutia ukweli katika matendo, na kama tunampenda Mungu.) (Maangamizi ya wapinga Kristo na viongozi bandia hutusaidia kuelewa kwamba tabia ya nje si jambo muhimu zaidi. Kwa nje wanaonekana kuwa wamejinyima mengi, na wanaonekana kuwa radhi kulipa bei, lakini kwa kuchambua tunaweza kuona kwamba hawana moyo kabisa unaomcha Mungu; kwa mitazamo yote wanampinga Yeye. Siku zote wanasimama pamoja na Shetani katika nyakati za hatari, na kuingilia kazi ya Mungu. Hivyo basi, utiliaji maanani mkuu hapa ni upande gani tutasimama wakati ukiwadia, na mitazamo yetu.) Nyote mnaongea vyema, na yaonekana kwamba tayari mnao msingi wa uelewa wa na kiwango cha kuweza kutia ukweli wenu katika matendo, nia za Mungu, na kile Mungu anahitaji kutoka kwa binadamu. Kwamba mnaweza kuongea hivi ni jambo la kugusa kweli. Ingawa kuna maneno machache yasiyofaa hapa na pale, kauli zenu tayari zinakaribia ufafanuzi unaostahili ukweli Hii inathibitisha kwamba mmeimarisha uelewa wenu halisi wa watu matukio, na vifaa vilivyo karibu nanyi, mazingira yenu yote ambayo Mungu amepanga, na kila kitu mnachoweza kuona. Uelewa huu unakaribia ukweli. Hata ingawa kile mnachosema si pana kabisa, na maneno machache hayafai sana, uelewa wenu tayari unakaribia uhalisi wa ukweli. Kuwasikiliza mkiongea kwa njia hii kunanifanya Mimi kuhisi vizuri sana.
Tazama zaidi: Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni