Jumapili, 21 Aprili 2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I Sehemu ya Nne


3) Mungu Atumia Upinde wa Mvua Kama Ishara ya Agano Lake na mwanadamu.
Mwa 9:11-13 Na nitaweka agano langu na ninyi, wala miili yote haitaondolewa tena na maji ya gharika; wala hakutakuwa na gharika tena kuiharibu dunia. Naye Mungu akasema, Hii ni alama ya agano ambayo naifanya kati ya Mimi na ninyi na viumbe vyote vyenye uhai vilivyo nanyi, kwa vizazi vya kudumu: naweka upinde wangu mawinguni, na utakuwa alama ya agano kati ya Mimi na dunia.
Kisha, hebu tuangalie sehemu hii ya maandiko kuhusu namna Mungu alivyounda upinde wa mvua kama ishara ya Agano lake na binadamu.
Watu wengi zaidi wanajua upinde wa mvua ni nini na wamesikia baadhi ya hadithi zinazohusiana na pinde za mvua. Kuhusiana na hadithi ile ya upinde wa mvua kwenye biblia, baadhi wa watu wanaisadiki, baadhi wanaichukulia tu kama hadithi ya kale, huku wengine hawaisadiki kamwe. Haijalishi ni nini, kila kitu kilichofanyika kuhusiana na upinde wa mvua ndicho kila kitu ambacho Mungu Alifanya hapo awali, na mambo yaliyofanyika katika mchakato huu wa usimamizi wa Mungu wa binadamu. Mambo haya yamerekodiwa vivyo hivyo kwenye Biblia. Rekodi hizi hazituambii chochote kuhusu hali ya Mungu ilivyokuwa wakati huo au nia zake nyuma ya maneno haya ambayo Mungu alisema. Zaidi, hakuna anayeweza kutambua ni nini Mungu alikuwa akihisi Aliposema maneno hayo. Hata hivyo, hali ya akili ya Mungu kuhusiana na hiki kitu chote inafichuliwa katikati ya mistari ya maandishi. Ni kana kwamba fikira zake wakati huo zinatoka kwenye ukurasa kupitia kila neno na kauli ya neno la Mungu.
Fikira za Mungu ni kile ambacho watu wanafaa kujali kuhusu na kile wanafaa kujaribu kujua zaidi. Hii ni kwa sababu fikira za Mungu zinahusiana kwa karibu na uelewa wa binadamu wa Mungu na uelewa wa binadamu wa Mungu ni kiungo muhimu sana kwa kuingia kwa binadamu katika maisha. Hivyo ni nini alichokuwa akifikiria Mungu wakati huo mambo haya yalipofanyika?
Hapo mwanzo, Mungu aliumba binadamu ambao katika macho Yake walikuwa wazuri sana na karibu na Yeye, lakini waliangamizwa na gharika baada ya kuasi dhidi Yake. Je, ilimwumiza Mungu kwamba binadamu kama hao walitoweka tu papo hapo hivyo? Bila shaka Aliumizwa! Kwa hivyo Maonyesho Yake ya maumivu haya yalikuwa nini? Ilirekodiwa vipi kwenye Biblia? Ilirekodiwa kwenye Biblia kama: "Na nitaweka agano langu na ninyi, wala miili yote haitaondolewa tena na maji ya gharika; wala hakutakuwa na gharika tena kuiharibu dunia." Sentensi hii rahisi inafichua fikira za Mungu. Kuangamizwa huku kwa ulimwengu kulimpa Yeye maumivu sana. Kwa maneno ya binadamu, Alikuwa na huzuni sana. Tunaweza kufikiria: Ni vipi ambavyo dunia iliyokuwa imejaa maisha inavyofanana baada ya kuangamizwa na gharika? Ni vipi ambavyo dunia iliyokuwa imejaa binadamu inavyofanana hivi sasa? Hakuna makazi ya binadamu, hakuna viumbe walio hai, maji kila mahali na machafuko kabisa juu ya maji. Hilo ndilo lililokuwa onyesho la kusudio la asili ya Mungu wakati alipoumba ulimwengu? Bila shaka la! Nia asilia ya Mungu ilikuwa ni kuyaona maisha katika maeneo yote, kuwaona wanadamu Aliowaumba wakimwabudu Yeye, si tu kwa Nuhu kuwa mtu pekee anayemwabudu, au kuwa wa pekee ambaye angejibu mwito Wake ili kukamilisha kile alichoaminiwa kufanya. Wakati binadamu walitoweka, Mungu hakuona kile alichonuia awali lakini kinyume cha mambo. Ni vipi ambavyo moyo Wake usingekuwa katika maumivu? Hivyo Alipokuwa akifichua tabia Yake na kuelezea hisia Zake, Mungu alifanya uamuzi. Ni aina gani ya uamuzi Alifanya? Kuunda uta mawinguni (kumbuka: upinde wa mvua tunaouona) kama agano na binadamu, ahadi kwamba Mungu hangemwangamiza mwanadamu kwa gharika tena. Wakati huohuo, ulikuwa pia ni kuwaambia watu kwamba Mungu aliwahi kuangamiza ulimwengu kwa gharika, kumfanya mwanadamu kukumbuka milele ni kwa nini Mungu alifanya kitu kama hicho.
Je, kuangamizwa kwa ulimwengu wakati huu kulikuwa ni jambo alilotaka Mungu? Bila shaka lilikuwa ni jambo asilotaka Mungu Huenda tukaweza kufikiria sehemu ndogo ya picha ile ya kusikitikia ya ulimwengu baada ya kuangamizwa kwa ulimwengu lakini hatuwezi kukaribia kufikiria namna hali ilivyokuwa wakati huo mbele ya macho ya Mungu. Tunaweza kusema kwamba, haijalishi kama ni watu wa sasa au wa wakati huo, hakuna yeyote anayeweza kufikiria au kutambua ni vipi Mungu alikuwa akihisi Aliposhuhudia tukio hilo, picha hiyo ya ulimwengu baada ya kuangamizwa kwake kwa gharika. Mungu alilazimishwa kufanya haya kutokana na kutotii kwa binadamu, lakini maumivu ambayo moyo wa Mungu ulipitia kutokana na maangamizo haya ya ulimwengu kwa gharika ni uhalisia ambao hakuna anayeweza kuufikiria au kuutambua. Ndiyo maana Mungu aliweka agano na mwanadamu, ambalo lilikuwa ni kuambia watu kukumbuka kwamba Mungu aliwahi kufanya kitu kama hiki, na kuapa kwamba Mungu asingewahi kuangamiza ulimwengu kwa njia hii tena. Katika agano hili, tunauona moyo wa Mungu—tunaona kwamba moyo wa Mungu ulikuwa katika maumivu Alipoangamiza binadamu hawa. Katika lugha ya binadamu, wakati Mungu aliangamiza mwanadamu na Akaona mwanadamu akitoweka, moyo Wake ulikuwa ukiomboleza na kuvuja damu. Je, hivyo sivyo tunavyoweza kuifafanua kwa njia bora zaidi? Maneno haya yanatumika na binadamu kuonyesha hisia za binadamu, lakini kwa sababu lugha ya binadamu inao ukosefu mwingi, kuitumia kufafanua hisia za Mungu hakuonekani kuwa mbaya sana kwangu Mimi, na wala si kubwa mno. Angaa inawapa uelewa sahihi kabisa, wa kufaa zaidi, wa hali ya Mungu ilivyokuwa wakati huo. Sasa mtafikiria nini mtakapouona upinde wa mvua tena? Angaa mtakumbuka namna ambavyo Mungu aliwahi kuwa katika huzuni kwa sababu ya kuangamiza ulimwengu kwa gharika. Mtakumbuka namna, hata kama Mungu aliuchukia ulimwengu huu na kudhalilisha binadamu hawa, Alipowaangamiza wanadamu Alioumba kwa mikono Yake mwenyewe, moyo Wake ulikuwa ukisononeka, ukipambana kuachilia, ukihisi kusita, na kuhisi vigumu kuvumilia mambo. Tulizo lake pekee lilikuwa katika familia ya wanane ya Nuhu. Ulikuwa ni ushirikiano wa Nuhu uliofanya jitihada Zake za kipekee za kuumba viumbe wote kuwa cha thamani. Kwa wakati ambao Mungu alikuwa akiteseka, hili ndilo jambo tu ambalo lingeweza kusawazisha maumivu Yake. Kuanzia hapo, Mungu aliweka matarajio Yake yote ya binadamu kwa familia ya Nuhu, akitumai kwamba wangeishi chini ya baraka Zake na si laana Yake, akitumai kwamba wasingewahi kumwona Mungu akiuangamiza ulimwengu kwa gharika na pia akitumai kwamba wasingeangamizwa.
Ni sehemu gani ya tabia ya Mungu tunayofaa kuelewa kutoka hapa? Mungu alikuwa amemdharau binadamu kwa sababu binadamu alikuwa na uadui na Yeye, lakini ndani ya moyo Wake, utunzaji Wake, kujali Kwake, na huruma Yake kwa binadamu vilibakia vilevile. Hata wakati alipowaangamiza wanadamu, moyo Wake hukubadilika. Wakati binadamu walikuwa wamejaa upotovu na kutotii Mungu hadi katika kiwango fulani, Mungu alilazimika, kwa sababu ya tabia Yake na kiini Chake, na kulingana na kanuni Zake, kuangamiza binadamu hao. Lakini kwa sababu ya kiini cha Mungu, bado Alisikitikia binadamu, hata Akataka kutumia njia mbalimbali za kuwakomboa wanadamu ili waweze kuendelea kuishi. Badala yake, binadamu alimpinga Mungu, akaendelea kutomtii Mungu, na kukataa kukubali wokovu wa Mungu, yaani, alikataa kukubali nia Zake nzuri. Haijalishi ni vipi Mungu aliwaita wao, aliwakumbusha, akawatosheleza haja zao, akawasaidia wao, au akawavumilia wao, binadamu hakutambua haya, wala hakutilia maanani. Katika maumivu Yake, Mungu bado hakusahau kumpa binadamu uvumilivu Wake wa kiwango cha juu zaidi, akisubiri binadamu kugeuka na kubadilika. Baada ya Yeye kufikia kikomo Chake, Alifanya kile Alicholazimika kufanya bila ya kusita. Kwa maneno mengine, kulikuwa na kipindi cha muda mahususi na mchakato kutoka pale ambapo Mungu alipanga kuangamiza wanadamu hadi katika mwanzo rasmi wa kazi Yake ya kuwaangamiza wanadamu. Mchakato huu ulikuwepo kwa kusudio la kumwezesha binadamu kugeuka, na ndio uliokuwa fursa ya mwisho ya Mungu kumpa binadamu. Hivyo ni nini ambacho Mungu alifanya kwenye kipindi hiki kabla ya kuangamiza wanadamu? Mungu alifanya kiwango kikubwa cha kazi ya kukumbusha na kazi ya kusihi. Haijalishi ni maumivu kiasi kipi na huzuni ambayo ilikuwa ndani ya moyo wa Mungu, Aliendelea kufanyisha zoezi utunzaji Wake, wasiwasi, na huruma nyingi juu ya binadamu. Tunaona nini kutoka kwa haya? Bila shaka, tunaona kwamba upendo wa Mungu kwa wanadamu ni wa kweli na si tu jambo ambalo Analizungumzia tu bila matendo. Ni jambo hakika, linaloweza kushikika na kutambulika, si bandia, halijatiwa najisi, halidanganyi wala halisingizii. Mungu kamwe hatumii uongo au kuunda taswira za bandia ili kufanya watu kuona kwamba Yeye anapendeka. Kamwe hatumii ushuhuda wa uongo ili kuwafanya kuona uzuri Wake, au kuringia uzuri wake na utakatifu Wake. Je, dhana hizi za tabia ya Mungu zinastahili upendo wa binadamu? Kwani nazo hazistahili kuabudiwa? Kwani nazo hazistahili kupendwa sana? Kwa sasa, Ningependa kuwauliza: Baada ya kuyasikia maneno haya, mnafikiri kwamba ukubwa wa Mungu ni tu maneno kwenye kipande cha karatasi? Je, uzuri wake Mungu ni maneno matupu tu? La! Bila shaka la! Mamlaka ya juu, ukubwa, utakatifu, uvumilivu, upendo, wa Mungu na kadhalika—dhana hizi zote mbalimbali za tabia ya Mungu na kiini chake zinaanza kutekelezwa kila wakati Anapoanza kazi Yake, zikiwa katika mapenzi Yake kwa binadamu, na pia zikitimizwa na kuonyeshwa kwa kila mtu. Licha ya kama umewahi kuzihisi awali, Mungu anamtunza kila mtu katika kila njia inayowezekana, kwa kutumia moyo Wake wa dhati, hekima, na mbinu mbalimbali ili kupashana mioyo ya kila mtu, na kuzindua roho ya kila mmoja. Huu ni ukweli usiopingika. Haijalishi ni watu wangapi wameketi hapa, kila mtu amekuwa na uzoefu tofauti na hisia tofauti kwa ustahimilivu, uvumilivu, na uzuri wake Mungu. Uzoefu huu wote wa Mungu na hisia hizi au utambuzi wa Yeye—kwa ufupi, mambo haya yote mazuri yanatoka kwa Mungu. Hivyo kwa kutangamanisha uzoefu wa kila mmoja na maarifa ya Mungu na kuziweka kwa pamoja na masomo yetu ya vifungu hivi vya Biblia leo, je sasa unao uelewa halisi na bora zaidi kumhusu Mungu?
Baada ya kuisoma hadithi hii na kuelewa baadhi ya tabia za Mungu zilizofichuliwa kupitia kwa hafla hii, ni aina gani mpya kabisa ya shukrani mliyo nayo kwa Mungu? Je, imewapa uelewa wa kina zaidi wa Mungu na moyo Wake? Mnahisi tofauti sasa mnapoiangalia hadithi ya Nuhu tena? Kulingana na maoni yenu, ingehitajika kufanya mawasiliano ya mistari hii ya Biblia? Kwa vile tumewasiliana kuihusu, mnafikiria kwamba ilihitajika? Ilihitajika, siyo? Ingawaje kile tulichosoma ni hadithi, ni rekodi ya kweli ya kazi ya Mungu ambayo aliwahi kuifanya. Nia yangu haikuwa kuwawezesha kufahamu maelezo ya hadithi hizi au mhusika huyu, wala haikuwa kwamba mweze kuenda kusomea kuhusu mhusika huyu, na bila shaka si eti mweze kurudi katika uchambuzi wa Biblia tena. Mnaelewa? Hivyo, hadithi hizi zimesaidia maarifa yenu ya Mungu? Hadithi hii imeongezea nini uelewa wenu wa Mungu? Twambie, kina kaka na kina dada kutoka makanisa ya Hong Kong. (Tuliona kwamba upendo wa Mungu ni kitu ambacho hakuna yeyote kati yetu binadamu potovu anamiliki.) Twambie, akina kaka na akina dada kutoka makanisa ya Korea. (Upendo wa Mungu kwa binadamu ni wa kweli. Upendo wa Mungu kwa binadamu unao tabia Yake na unabeba ukuu Wake, utakatifu, uongozi, na ustahimilivu Wake. Kupitia hadithi kama hii tunaweza kushukuru kwa njia bora zaidi kwamba vitu vyote hivi ni sehemu ya tabia ya Mungu, na kwamba inafaa sisi tujaribu kupata uelewa wa kina zaidi.) (Kupitia kwa mawasiliano ambayo tumetoka kuwa nayo, kwa upande mmoja Ninaweza kuona haki ya Mungu na tabia ya kitakatifu, na Ninaweza pia kuona wasiwasi alionao Mungu kwa mwanadamu, rehema za Mungu kwa mwanadamu, na kwamba kila kitu anachofanya Mungu na kila fikira na wazo Alilonalo linafichua upendo na kujali Kwake kwa binadamu.) (Uelewa wangu katika siku zilizopita ulikuwa kwamba Mungu alitumia gharika kuangamiza ulimwengu kwa sababu mwanadamu alikuwa amegeuka na kuwa mwovu kwa kiwango fulani, na ilikuwa ni kana kwamba Mungu aliangamiza binadamu hawa kwa sababu Aliuchukia. Ilikuwa tu baada ya Mungu kuzungumza kuhusu hadithi ya Nuhu leo na Akasema ya kwamba moyo wa Mungu ulikuwa unavuja ndipo Ninatambua kwamba Mungu alikuwa kwa hakika shingo upande kuachilia binadamu hawa. Ilikuwa tu ni kwa sababu mwanadamu alikuwa mtovu wa kusikia sana kiasi cha kwamba Mungu alikuwa hana chaguo lakini kumwangamiza. Kwa hakika, moyo wa Mungu wakati huo ulikuwa umesikitika sana. Kutokana na haya Ninaweza kuona katika tabia ya Mungu utunzaji na kujali Kwake kwa mwanadamu. Hili ni jambo ambalo Sikujua awali. Nilikuwa nikifikiri ilikuwa ni kwa sababu mwanadamu alikuwa mwovu sana, na hivyo Mungu akawaangamiza. Hivyo ndivyo uelewa wangu ulivyokuwa wa juujuu.) Vizuri sana! Mnaweza kwenda kwa kifuatacho. (Niliathiriwa sana baada ya kusikiliza. Nimeisoma Biblia kitambo, lakini sijawahi kuwa na uzoefu kama leo pale ambapo Mungu anachambua kwa njia ya moja kwa moja mambo haya ili tuweze kumjua Yeye. Kwa Mungu kutushika mkono kuweza kuona Biblia inanifanya nijue kwamba kiini cha Mungu kabla ya kupotoshwa kwa binadamu kilikuwa ni upendo na utunzaji kwa mwanadamu. Tangu wakati ule binadamu alipopotoka hadi katika siku za mwisho za sasa, ingawaje Mungu anayo tabia ya haki, upendo na utunzaji Wake unabakia vilevile, haubadiliki. Hii inaonyesha kwamba kiini cha upendo wa Mungu, kuanzia uumbaji hadi sasa, licha ya kama binadamu amepotoka, haubadiliki.) (Leo niliona kwamba kiini cha Mungu hakitabadilika kutokana na mabadiliko ya muda au mahali pa kazi Yake. Niliona pia kwamba, haijalishi kama Mungu anauumba ulimwengu au anauangamiza baada ya binadamu kupotoka, kila kitu Anachofanya kina maana na kinayo tabia Yake. Hivyo basi niliona kwamba upendo wa Mungu hauna kikomo na haupimiki, niliona pia, kama vile ambavyo wale kaka na dada wengine, utunzaji na rehema ya Mungu kwa mwanadamu wakati Alipouangamiza ulimwengu.) (Haya ni mambo kwa hakika sikuyajua kuhusu hapo awali. Baada ya kusikiliza leo, nahisi kwamba Mungu ni wa ajabu kwa kweli, wa kuaminika kwa kweli, anayestahili kusadikiwa, na kwamba kwa kweli Yupo. Ninaweza kutambua kwa dhati ndani ya moyo wangu kwamba tabia ya Mungu na upendo wa Mungu kwa kweli ni vitu vinavyoshikika. Hii ndiyo hisia niliyo nayo baada ya kusikiliza leo.) Safi kabisa! Yaonekana nyote mmechukua kile mlichosikia na kukitia moyoni.
Je, mmetambua ukweli fulani kutoka mistari yote ya Biblia, zikiwemo hadithi zote za Biblia tulizowasiliana leo? Je, Mungu amewahi kutumia lugha Yake mwenyewe ili kuelezea fikira Zake binafsi au kuelezea upendo na utunzaji Wake kwa binadamu? Kunayo rekodi ya Yeye kutumia lugha ya kawaida kutaja ni kiasi kipi ambacho Anajali na Anapenda mwanadamu? La! Je, si hayo ni kweli? Kunao wengi sana miongoni mwenu ambao wamesoma Biblia au vitabu vingine mbali na Biblia. Je, yupo yeyote kati yenu aliyeyaona maneno kama hayo? Jibu bila shaka ni la! Yaani, kwenye rekodi za Biblia, yakiwemo maneno ya Mungu au urekodi wa kazi Yake, Mungu hajawahi katika enzi yoyote au kipindi chochote kile kutumia mbinu Zake mwenyewe kufafanua hisia Zake au kuelezea upendo na utunzaji Wake kwa mwanadamu wala Mungu hajawahi kutumia matamshi au vitendo kufikisha hisia na mawazo Yake—Je, si hiyo ni ukweli? Kwa nini Ninasema hivyo? Kwa nini lazima Nitaje hii? Ni kwa sababu hii pia inayo uzuri wa Mungu na tabia Yake.

Chanzo: Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I (Sehemu ya Nne)



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni