Ijumaa, 31 Mei 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake"



Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake"

Mwenyezi Mungu anasema, “Hakuna mtu mbali na Yeye anayeweza kujua mawazo yetu yote, au kufahamu asili yetu na kiini chetu kwa dhahiri na ukamilifu, ama kuhukumu uasi na upotovu wa binadamu, ama kusema nasi na kufanya kazi kati yetu kama hivi kwa niaba ya Mungu aliye mbinguni. Hakuna mtu isipokuwa Yeye ambaye amepewa mamlaka, hekima, na heshima ya Mungu; tabia ya Mungu na kile Mungu Anacho na alicho yanatoka, kwa ukamilifu wao, ndani Yake. Hakuna mtu mbali na Yeye ambaye anaweza kutuonyesha njia na kutuletea mwangaza. Hakuna yeyote ila Yeye anayeweza kutufichulia siri ambazo Mungu hajatufunulia tangu uumbaji hadi leo.

Alhamisi, 30 Mei 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu II Sehemu ya Tatu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Uhuru: Awamu ya Tatu
Mwenyezi Mungu anasema, Baada ya mtu kupita utoto na wakati wake wa kubaleghe na kwa utaratibu bila kuzuilika kufikia ukomavu, hatua inayofuata ni kwake yeye kuuaga kabisa ule ujana wake, kuwaaga wazazi wake, na kukabiliana na barabara iliyo mbele yake akiwa mtu mzima huru. Wakati huo[c] lazima wakabiliane na watu, matukio na mambo yote ambayo mtu mzima lazima apitie, na kukabiliana na viungo mbalimbali katika msururu wa hatima yake. Hii ndiyo awamu ya tatu ambayo lazima mtu apitie.
1. Baada ya Kuwa Huru, Mtu Huanza Kupitia Ukuu wa Muumba
Kama kuzaliwa kwa mtu na kulelewa kwake ni "kipindi cha matayarisho" katika safari ya mtu maishani, kuweka lile jiwe la msingi katika hatima ya mtu, basi uhuru wa mtu ndio mazungumzo nafsi ya kufungua hatima ya maisha ya mtu.

Jumatano, 29 Mei 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II) Sehemu ya Pili

Maneno ya Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II) Sehemu ya Pili

Awamu Sita katika Maisha ya Binadamu
Katika mkondo wa maisha ya mtu, kila mtu hufikia kwenye misururu ya awamu muhimu. Hizi ni hatua za kimsingi zaidi, na muhimu zaidi, zinazoamua hatima ya maisha ya mtu. Kile kinachofuata ni ufafanuzi mfupi kuhusu mafanikio haya ambayo kila mtu lazima apitie kwenye mkondo wa maisha yake.
Kuzaliwa: Awamu ya Kwanza
Mahali ambapo mtu amezaliwa, amezaliwa katika familia ya aina gani, jinsia ya mtu, umbo la mtu, na wakati wa kuzaliwa: haya ndiyo maelezo ya awamu ya kwanza ya maisha ya binadamu.
Hakuna yeyote aliye na chaguo kuhusu sehemu hizi za awamu hii; zote ziliamuliwa kabla, mapema kabisa na Muumba.

Jumanne, 28 Mei 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu II Sehemu ya Kwanza

Leo tutaendelea na ushirika wetu kuhusu mada ya "Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee." Tayari tumekuwa na ushirika mara mbili katika mada hii, wa kwanza kuhusiana na mamlaka ya Mungu na wa pili kuhusiana na tabia ya haki ya Mungu. Baada ya kusikiliza ushirika huu mara mbili, je, mmepata ufahamu mpya wa utambulisho wa Mungu, hadhi, na hali halisi? Je, maono haya yamewasaidia kufikia maarifa mazito zaidi na uhakika wa ukweli kuuhusu uwepo wa Mungu? Leo Ninapanga kufafanua mada hii ya "Mamlaka ya Mungu."

Kuelewa Mamlaka ya Mungu Kutoka kwa Mitazamo Mikubwa na Midogo
Mamlaka ya Mungu ni ya kipekee. Ndiyo maonyesho ya sifa ya, na hali halisi maalum ya, utambulisho wa Mungu Mwenyewe. Hakuna kiumbe ambacho kiliumbwa wala kile ambacho hakikuumbwa kinachomiliki maonyesho ya sifa kama hizi na hali halisi maalum; Muumba tu ndiye anayemiliki aina hii ya mamlaka.

Jumatatu, 27 Mei 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemi ya Tatu



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemi ya Tatu

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”. Maudhui ya video hii: Uhuru: Awamu ya Tatu 1. Baada ya Kuwa Huru, Mtu Huanza Kupitia Ukuu wa Muumba 2. Kuwaacha Wazazi wa Mtu na Kuanza kwa Bidii Kuendeleza Wajibu Wako Kwenye Ukumbi wa Sanaa wa Maisha Ndoa: Awamu ya Nne 1. Mtu Hana Chaguo Kuhusu Ndoa 2. Ndoa Inazaliwa Kutokana na Hatima ya Wandani Wawili


Tazama Video: Neno la Mungu | “Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu

Kujua zaidi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Jumapili, 26 Mei 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Kuhusu Majina na Utambulisho" (Sehemu ya Kwanza)



Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Kuhusu Majina na Utambulisho" (Sehemu ya Kwanza)


Mwenyezi Mungu anasema, "Yesu aliwakilisha Roho wa Mungu, na Alikuwa Roho wa Mungu Akifanya kazi moja kwa moja. Alifanya kazi ya enzi mpya, kazi ambayo hakuna aliyekuwa amefanya mbeleni. Yeye Alifungua njia mpya, Alimwakilisha Yehova, na Alimwakilisha Mungu Mwenyewe. Ilhali kwa Petro, Paulo na Daudi, bila kujali walichoitwa, waliwakilisha tu utambulisho wa kiumbe wa Mungu, ama walitumwa na Yesu na Yehova.

Jumamosi, 25 Mei 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu Sehemu ya Tano


Aina Tano za Watu
Kwa sasa, Nitaacha ushirika wetu kuhusu tabia ya haki ya Mungu umalizikie hapo. Kinachofuata Nitaainisha wafuasi wa Mungu katika kategoria mbalimbali, kulingana na ufahamu wao wa Mungu na ufahamu wao na kile wamepitia kuhusiana na tabia ya haki Yake, ili muweze kujua awamu ambayo kwa sasa mnapatikana ndani pamoja na kimo chenu cha sasa. Kuhusiana na maarifa yao ya Mungu na ufahamu wao wa tabia Yake ya haki, awamu na kimo tofauti ambavyo watu huwa navyo vinaweza kugawanywa katika aina tano.

Ijumaa, 24 Mei 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu Sehemu ya Nne

Kutubu kwa Kweli Ndani ya Mioyo ya Waninawi Kunawapa Rehema ya Mungu na Kwabadilisha Hatima Zao Wenyewe

Je, kulikuwa na kuhitilafiana kokote kati ya mabadiliko ya moyo wa Mungu na hasira Yake? Bila shaka la! Hii ni kwa sababu uvumilivu wa Mungu kwa wakati ule ulikuwa na sababu yake. Je, sababu yake yaweza kuwa nini? Ni ile iliyotajwa kwenye Biblia: "Kila mtu aligeuka kutoka kwenye njia yake ya maovu" na "kuacha udhalimu uliokuwa mikononi mwake."

Alhamisi, 23 Mei 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu Sehemu ya Tatu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Binadamu Hupata Huruma na Uvumilivu wa Mungu Kupitia kwa Toba ya Dhati
Kinachofuata ni hadithi ya biblia ya "Wokovu wa Mungu kwa Ninawi."
Yona 1:1–2 Sasa neno la Yehova likaja kwa Yona mwana wa Amitai, likisema, Amka, nenda Ninawi, mji mkuu, na uipigie kelele, kwani uovu wao umeenda juu mbele yangu.
Yona 3 Neno lake Yehova likakuja kwake Yona kwa mara ya pili, likisema, Inuka, nenda Ninawi, mji huo mkuu; na uuhubirie mahubiri ninayokuambia. Kwa hivyo Yona akainuka, na kuenda Ninawi, kulingana na neno la Yehova. Sasa Ninawi ulikuwa mji mkuu wa safari ya siku tatu. Naye Yona akaanza kuingia ndani ya mji huo safari ya siku moja, na akatoa sauti kubwa, na kusema, Imebaki siku arobaini, na Ninawi utashindwa.

Jumatano, 22 Mei 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu Sehemu ya Pili


Ingawaje Hasira ya Mungu ni Fiche na Haijulikani kwa Binadamu, Haivumilii Kosa Lolote
Namna Mungu alivyoshughulikia binadamu wote wa ujinga na kutojua ulitokana kimsingi na huruma na uvumilivu. Hasira yake, kwa upande mwingine, imefichwa kwenye wingi mkubwa mno wa muda na wa mambo; haijulikani kwa binadamu. Kutokana na hayo, ni vigumu sana kwa binadamu kumwona Mungu akionyesha hasira Yake, na ni vigumu pia kuelewa hasira Yake. Kwa hivyo, binadamu huchukulia hasira ya Mungu kuwa ndogo.

Jumanne, 21 Mei 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu Sehemu ya Kwanza

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Kwa vile sasa mmesikiliza ushirika uliopita kuhusu mamlaka ya Mungu, Ninao ujasiri kwamba mmejihami vilivyo na mseto wa maneno kuhusu suala hili. Kiwango unachoweza kukubali, kufahamu, na kuelewa vyote hivi vinategemea na jitihada zipi utakazotumia. Ni tumaini Langu kwamba utaweza kutazamia suala hili kwa dhati; kwa vyovyote vile hufai kulishughulikia shingo upande! Sasa, je, kujua mamlaka ya Mungu ni sawa na kujua Mungu kwa uzima wake? Mtu anaweza kusema kwamba kujua mamlaka ya Mungu ndiyo mwanzo wa kumjua Mungu mwenyewe kwa upekee wake, na mtu anaweza kusema pia kwamba kuyajua mamlaka ya Mungu kunamaanisha kwamba mtu tayari ameingia kwenye lango kuu la kujua hali halisi ya ule upekee wa Mungu Mwenyewe. Ufahamu huu ni sehemu moja ya kumjua Mungu.

Jumatatu, 20 Mei 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu” Sehemu ya Kwanza


Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu” Sehemu ya Kwanza

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”. Maudhui ya video hii: Kwa Kupinga Mungu kwa Ukaidi, Binadamu Anaangamizwa na Hasira za Mungu Kupotoka kwa Sodoma: Kunakasirisha Binadamu, Kunaghadhibisha Mungu Sodoma Yaangamizwa kwa Kukosea Hasira za Mungu Baada ya Ukinzani wa Mara kwa Mara wa Sodoma na Ukatili Wao Dhidi Yake, Mungu Anaufuta Kabisa

Tazama zaidi: Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Pili
Kujua zaidi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Jumapili, 19 Mei 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Pili



Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Pili
Mwenyezi Mungu anasema, “Vitu vyote haviwezi kutenganishwa na kanuni ya Mungu, na hakuna mtu hata mmoja ambaye anaweza kujitenganisha kwenye kanuni Yake. Kupoteza kanuni Yake na kupoteza uangalizi wake kungekuwa na maana kwamba maisha ya watu, maisha ya watu katika mwili yangetoweka. Huu ndio umuhimu wa Mungu kuanzisha mazingira kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi.

Jumamosi, 18 Mei 2019

Neno la Mungu | “Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu”


Neno la Mungu | “Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu”
Mwenyezi Mungu anasema, “Vitendo vyote na matendo ya Shetani vinaonyeshwa kupitia kwa binadamu. Sasa vitendo vyote na matendo yote ya binadamu ni maonyesho ya Shetani na hivyo basi haviwezi kumwakilisha Mungu. Binadamu ni mfano halisi wa Shetani, na tabia ya mwanadamu haiwezi kuiwakilisha tabia ya Mungu. Baadhi ya wanadamu ni wenye tabia nzuri; Mungu anaweza kufanya baadhi ya kazi kupitia kwa tabia hiyo nayo kazi yao inatawaliwa na Roho Mtakatifu. Ilhali tabia yao haiwezi kumwakilisha Mungu.

Ijumaa, 17 Mei 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I) Sehemu ya Tano

Maneno yaliyo hapa chini ni lazima katika kujua mamlaka ya Mungu, na maana yake yametolewa kwenye ushirika ulio hapa chini. Hebu tuendelee kuyasoma Maandiko.

4. Amri ya Mungu kwa Shetani
Ayubu 2:6 Naye Yehova akasema kwa Shetani, Tazama, yeye yuko katika mkono wako; lakini uuhifadhi uhai wake.
Shetani Hajawahi Kuthubutu Kukiuka Mamlaka ya Muumba, na Kwa Sababu Hiyo, Vitu Vyote Vinaishi kwa Mpangilio

Alhamisi, 16 Mei 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I) Sehemu ya Nne


Mamlaka ya Muumba Hayawekewi Mipaka ya Muda, Nafasi, au Jiografia, na Mamlaka ya Muumba Hayakadiriki
Hebu tutazame Mwanzo 22:17-18. Hili ni fungu jingine lililozungumziwa na Yehova Mungu, Alisema kwa Ibrahimu, "Kuwa katika kubariki nitakupa baraka, na katika kuzidisha uzao wako nitazidisha mithili ya nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa maadui zao; Na kupitia uzao wako kila taifa la dunia litabarikiwa; kwa kuwa umeitumikia sauti yangu." Yehova Mungu alimbariki Ibrahimu mara nyingi ili uzao wake uweze kuzidishwa—na kuzidishwa hadi kiwango gani? Hadi kiwango kilichozungumziwa katika Maandiko: "kama nyota za mbinguni na mchanga ulio pwani."

Jumatano, 15 Mei 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I) Sehemu ya Tatu


2. Mungu Hutumia Matamshi Yake Kuanzisha Agano na Binadamu.
Mwa 9:11-13 Na nitaweka agano langu na ninyi, wala miili yote haitaondolewa tena na maji ya gharika; wala hakutakuwa na gharika tena kuiharibu dunia. Naye Mungu akasema, Hii ni alama ya agano ambayo naifanya kati ya Mimi na ninyi na viumbe vyote vyenye uhai vilivyo nanyi, kwa vizazi vya kudumu: naweka upinde wangu mawinguni, na utakuwa alama ya agano kati ya Mimi na dunia.

Jumanne, 14 Mei 2019

Neno la Mwenyezi Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I) Uendelezo wa Sehemu ya Pili

Neno la Mwenyezi Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu  (I) Uendelezo wa Sehemu ya Pili

Kwenye Siku ya Sita, Muumba Aongea, na Kila Aina ya Kiumbe Hai Akilini Mwake Chajitokeza, Kimoja Baada ya Kingine
Bila kuchoka, kazi ya Muumba ya kuumba viumbe vyote ilikuwa imeendelea kwa siku tano, na punde tu baada ya hapo ndipo Muumba alipokaribisha siku ya sita ya uumbaji Wake wa viumbe vyote. Siku hii ilikuwa mwanzo mwingine mpya, na siku nyingine isiyo ya kawaida. Nini, basi, kilikuwa mpango wa Muumba mkesha wa siku hii mpya?

Jumatatu, 13 Mei 2019

Neno la Mungu | “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” Sehemu ya Pili



Neno la Mungu | “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” Sehemu ya Pili

Mwenyezi Mungu anasema, “Hatua tatu za kazi ndizo kiini cha usimamizi mzima wa Mungu, na ndani yazo zimeelezwa tabia ya Mungu na kile Alicho. Wale wasiojua kuhusu hatua tatu za kazi ya Mungu hawana uwezo wa kutambua jinsi Mungu anavyoonyesha tabia Yake, wala hawajui hekima ya kazi ya Mungu, na wanasalia kutojua njia nyingi Anazomwokoa mwanadamu, na mapenzi Yake kwa wanadamu wote. Hatua tatu za kazi ndizo maonyesho kamili ya kazi ya kumwokoa mwanadamu.

Jumapili, 12 Mei 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I) Sehemu ya Pili


Kwenye Siku ya Nne, Misimu, Siku, na Miaka ya Mwanadamu Iliumbika Huku Mungu Akionyesha Mamlaka Yake kwa Mara Nyingine Tena
Muumba alitumia matamshi Yake kutimiza mpango Wake, na kwa njia hii Alipitisha siku tatu zake za kwanza kwenye mpango Wake. Kwenye siku hizi tatu, Mungu hakuonekana kushughulika kila pahali, au kujichosha Yeye Mwenyewe; kinyume cha mambo ni kwamba, Alikuwa na siku tatu za kwanza nzuri katika mpango Wake na Alitimiza utekelezaji mkubwa wa mabadiliko makubwa ya ulimwengu.

Jumamosi, 11 Mei 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I) Sehemu ya Kwanza

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Vikao vyangu mbalimbali vya ushirika vilivyopita vilikuwa vinahusu kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Baada ya kuvisikiliza vikao hivi vya ushirika, je, unahisi kuwa umefaidi na kupata ufahamu na maarifa kuhusu tabia ya Mungu? Ufahamu wako na maarifa ni mkubwa kiwango gani? Je, unaweza kuweka nambari katika kiwango hicho? Je, vikao hivi vya ushirika vilikupa ufahamu wa kina kuhusu Mungu? Inaweza kusemwa ufahamu huu ni maarifa ya kweli ya Mungu? Inaweza kusemwa kwamba maarifa na ufahamu huu wa Mungu ni maarifa ya hali halisi nzima ya Mungu, na kila kitu Anacho na alicho? La, bila shaka haiwezi kusemwa hivyo!

Ijumaa, 10 Mei 2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III (Sehemu ya Saba)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Sasa hebu tusome dondoo za maandiko zilizo hapa chini.
12. Maneno ya Bwana Yesu kwa Wanafunzi Wake Baada ya Kufufuka Kwake
Yohana 20:26-29 Na kufuatia siku nane tena wanafunzi wake walikuwa ndani, naye Tomaso alikuwa nao: kisha Yesu akaja, milango ikiwa imefungwa, na kusimama katikati, na kuema, Amani iwe nanyi. Kisha akasema kwa Tomaso, nyoosha kidole chako hapa, na uitazame mikono yangu, nyoosha mkono wako hapa, na uusongeshe mbavuni mwangu: na usiwe bila imani, ila mwenye imani.

Alhamisi, 9 Mei 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V Utakatifu wa Mungu II” Sehemu ya Nne



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V Utakatifu wa Mungu (II)” Sehemu ya Nne

Mwenyezi Mungu anasema, “Kuelewa kiini cha Mungu na kujua kiini cha Mungu kinapeana msaada usioweza kupimika kwa kuingia kwa watu katika maisha. Natumai kwamba hamtapuuza haya ama kuyaona kama mchezo; kwa sababu kumjua Mungu ni msingi muhimu na msingi wa imani ya mwanadamu kwa Mungu na ufuatiliaji wa mwanadamu wa ukweli na wokovu na kitu ambacho hakifai kuachiliwa.

Jumatano, 8 Mei 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Pili



Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Pili

Mwenyezi Mungu anasema, “Hakuna kizuizi chochote katika kazi Yake na kile Anachokifanya, na haitawekewa kizuizi chochote na binadamu yeyote, kitu chochote, au kifaa chochote, na haitakatizwa na nguvu zozote za kikatili. Katika kazi Yake mpya, Yeye ni Mfalme anayeshinda daima, na nguvu zozote za kikatili na uvumi wote na hoja za uwongo zote kutoka kwa mwanadamu zimekanyagiwa chini ya kibao Chake cha kuwekea miguu.

Jumanne, 7 Mei 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I” Sehemu ya Tatu



Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I” Sehemu ya Tatu
Mwenyezi Mungu anasema, “Katika moyo wa Nuhu na fahamu yake, uwepo wa Mungu ulikuwepo na bila shaka, na hivyo basi utiifu wake kwa Mungu ulikuwa haujatiwa doa wala toa na ungeweza kustahimili majaribio. Moyo wake ulikuwa safi na wazi kwa Mungu. Hakuhitaji maarifa ya mafundisho ya dini mengi mno ili kujishawishi kufuata kila neno la Mungu, wala hakuhitaji ukweli mwingi kuthibitisha uwepo wa Mungu, ili akubali kile Mungu alimwaminia na kuweza kufanya chochote kile ambacho Mungu angemruhusu kufanya.

Jumatatu, 6 Mei 2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III (Sehemu ya Sita)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

10. Hukumu ya Mafarisayo kwa Bwana Yesu.

Marko 3:21-22 Na wakati marafiki zake walisikia kuhusu hilo, walitoka kumshika: kwani walisema, Yeye si wa akili sawa. Nao waandishi waliokuja kutoka Yerusalemu walisema, Ana Beelzebubi, na kupitia mwana wa mfalme wa mapepo huwaondoa mapepo.
11. Mafarisayo Kukemewa na Bwana Yesu.
Mat 12:31-32 Ndiyo sababu nawaambieni, Wanadamu watasamehewa kila namna ya dhambi na kukufuru: lakini wanadamu hawatasamehewa kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu.

Jumapili, 5 Mei 2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III (Sehemu ya Tano)


Halafu, hebu tuangalie vifungu vifuatavyo katika maandiko.
9. Bwana Yesu Atenda Miujiza.
1) Bwana Yesu Awalisha Watu Elfu Tano.
Yohana 6:8-13 Mmoja wa wanafunzi wake, Andrea, ndugu yake Simoni Petro, akasema kwake, Kuna mvulana hapa, aliye na mikate mitano ya shayiri nao samaki wawili wadogo: lakini ni yapi miongoni mwa watu wengi? Naye Yesu akasema, Wafanye watu waketi chini. Na kulikuwa na nyasi nyingi pahali hapo. Kwa hivyo wanaume wakaketi chini, wakiwa idadi ya takribani elfu tano.

Jumamosi, 4 Mei 2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III (Sehemu ya Nne)


Halafu hebu tusome fahamu zifuatazo.
6. Ibada Mlimani
Sifa na Heri (Mat 5:3-12)
Chumvi na Nuru (Mt 5:13-16)
Sheria (Mat 5:17-20)
Kuhusu Hasira (Mat 5:21-26)
Kuhusu Uzinzi (Mat 5:27-30)

Ijumaa, 3 Mei 2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III Sehemu ya Tatu


Kifuatacho tutaangalia mfano uliozungumziwa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema.

3. Mfano wa Kondoo Aliyepotea
Mat 18:12-14 Mnafikiri vipi? Iwapo mtu ana kondoo mia moja, na mmoja wao apotee, je, hawaachi hao tisini na tisa, na kuenda milimani, na amtafute huyo ambaye amepotea? Na iwapo atampata, kweli nawaambia, anafurahi zaidi kwa sababu ya huyo kondoo, kuliko wao tisini na tisa ambao hawakupotea. Kwa namna hiyo siyo mapenzi ya Baba yenu ambaye yuko mbinguni, kuwa mmoja wa hawa wadogo aangamie.

Alhamisi, 2 Mei 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Kwanza



Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Kwanza

Mwenyezi Mungu anasema, “Unaona nini katika haya? Wakati Mungu alipofanya kazi katika ubinadamu, mbinu, maneno, na ukweli Wake mwingi vyote vilionyeshwa kwa njia ya kibinadamu. Lakini wakati uo huo tabia ya Mungu, kile Alicho nacho na kile Alicho, na mapenzi Yake vyote vilionyeshwa kwa watu kuweza kujua na kuvielewa. Kile walichojua na kuelewa kilikuwa hasa kiini Chake na Alicho nacho na kile Alicho, vyote ambavyo vinawakilisha utambulisho na hadhi ya asili ya Mungu Mwenyewe.

Jumatano, 1 Mei 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu III” Sehemu ya Pili


Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu (III)” Sehemu ya Pili

Mwenyezi Mungu anasema, “Zaidi ya mwanadamu kutafuta kwa tamaa umaarufu na faida, daima anaendelea kutekeleza uchunguzi wa sayansi na utafiti wa kina, kisha bila kikomo huridhisha mahitaji yake ya mwili na tamaa; yapi tena ni matokeo ya mwanadamu? Kwanza kabisa hakuna tena usawa wa ikolojia na, pamoja na hili, miili ya wanadamu yote imetiwa doa na kuharibiwa na mazingira ya hali hii, na magonjwa mbalimbali ya kuambukiza na mapigo kusambaa kila mahali. Hii ni hali ambayo mwanadamu sasa hawezi kudhibiti, sivyo?