Alhamisi, 16 Mei 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I) Sehemu ya Nne


Mamlaka ya Muumba Hayawekewi Mipaka ya Muda, Nafasi, au Jiografia, na Mamlaka ya Muumba Hayakadiriki
Hebu tutazame Mwanzo 22:17-18. Hili ni fungu jingine lililozungumziwa na Yehova Mungu, Alisema kwa Ibrahimu, "Kuwa katika kubariki nitakupa baraka, na katika kuzidisha uzao wako nitazidisha mithili ya nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa maadui zao; Na kupitia uzao wako kila taifa la dunia litabarikiwa; kwa kuwa umeitumikia sauti yangu." Yehova Mungu alimbariki Ibrahimu mara nyingi ili uzao wake uweze kuzidishwa—na kuzidishwa hadi kiwango gani? Hadi kiwango kilichozungumziwa katika Maandiko: "kama nyota za mbinguni na mchanga ulio pwani." Hii ni kusema kwamba Mungu alipenda kumpa Ibrahimu uzao uliokuwa mwingi kama nyota za mbinguni, na tele kama mchanga wa pwani. Mungu aliongea akitumia taswira, na kutoka kwenye taswira hii si vigumu kuona kwamba Mungu asingempa tu Ibrahimu uzao elfu moja, mbili, au hata elfu nyingi, lakini idadi isiyohesabika, iliyotosha kuwa uzao wa mataifa mengi ya dunia, kwani Mungu alimwahidi Ibrahimu kuwa atakuwa baba wa mataifa mengi. Na je, idadi hiyo iliamuliwa na binadamu au iliamuliwa na Mungu? Je, binadamu anaweza kudhibiti uzao kiasi gani atakaokuwa nao? Je, inategemea yeye? Haitegemei binadamu kujua kama atakuwa na uzao mbalimbali au la, sikwambii uzao mwingi kama "nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani." Ni nani asiyetamani uzao wake kuwa mwingi kama nyota? Kwa bahati mbaya mambo huwa hayaendi namna unavyotaka. Licha ya vile mwanadamu anaweza kuwa na mbinu au kuweza kufanya jambo fulani, haitegemei binadamu; hakuna anayeweza kusimama nje ya kile ambacho kimeamriwa na Mungu. Kiasi ambacho Atakuruhusu, hicho ndicho utakachokuwa nacho: Kama Mungu atakupa kidogo, basi hutawahi kuwa na kingi, na kama Mungu Atakupa kingi haina faida wewe kuchukia kingi hicho ulichonacho. Je, hayo si kweli? Haya yote yanategemea Mungu, si binadamu! Binadamu hutawaliwa na Mungu, na hakuna yule anayeachwa!
Wakati Mungu alisema "nitazidisha mithili," hili lilikuwa agano ambalo Mungu alianzisha na Ibrahimu, sawa na agano la upinde wa mvua, lingeweza kutimizwa milele hadi milele, na pia ilikuwa ahadi iliyotolewa na Mungu kwa Ibrahimu. Mungu pekee ndiye anayefuzu na kuweza kufanya ahadi hii kutimia. Bila kujali kama binadamu anaisadiki au la, bila kujali kama binadamu aikubali au la, na bila kujali namna binadamu anavyoitazama, na namna anavyoichukulia, haya yote yataweza kutimizwa, hadi mwisho wa maelezo ya agano hili, kulingana na matamshi yaliyotamkwa na Mungu. Matamshi ya Mungu hayatabadilishwa kwa sababu ya mabadiliko katika mapenzi au dhana za binadamu, na hayatabadilishwa kwa sababu ya mabadiliko ndani ya mtu yeyote, kitu au kifaa. Viumbe vyote vitaweza kutoweka lakini matamshi ya Mungu yatabaki milele hadi milele. Kinyume cha mambo ni, siku ambapo viumbe vyote vitatoweka ndiyo siku ile ile ambayo matamshi ya Mungu yataweza kutimizwa kabisa, kwani Yeye ndiye Muumba, na Anamiliki mamlaka ya Muumba, na nguvu za Muumba, na Anadhibiti vitu na viumbe vyote na nguvu zote za maisha; na Anaweza kusababisha kitu kutoka kule kusikokuwa na kitu, au kitu kuwa kile kisichokuwepo, na Anadhibiti mabadiliko ya viumbe vyote vilivyo na uhai na vile vilivyokufa, na kwa hivyo kwake Mungu, hakuna kinachokuwa rahisi kuliko kuzidisha uzao wa mtu. Haya yote yanaonekana ya kufikiria tu akilini mwa binadamu, sawa na hadithi za uwongo, lakini kwa Mungu, kile Anachoamua kufanya, na kuahidi kufanya, si cha kufikiria tu akilini wala si hadithi za uwongo. Badala yake ni hoja ambayo Mungu tayari ameiona, na ambayo kwa kweli itaweza kutimizwa. Je, unashukuru kuyasikia haya? Je, hoja hizi zinathibitisha kwamba uzao wa Ibrahimu ulikuwa mwingi? Na ulikuwa mwingi kiasi kipi? Mwingi kiasi cha "nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani" kama ilivyosemwa na Mungu? Je, uliweza kuenea kotekote katika mataifa na maeneo, kwenye kila sehemu ya ulimwengu? Na ni nini kilichotimiza hoja hii? Iliweza kutimizwa kutokana na mamlaka ya matamshi ya Mungu? Kwa miaka kadhaa ifikayo mamia au elfu baada ya matamshi ya Mungu kutamkwa, matamshi ya Mungu yaliendelea kutimizwa, na bila kusita yakaendelea kuwa hoja; huu ndio uwezo wa matamshi ya Mungu, na ithibati ya mamlaka ya Mungu. Wakati Mungu alipoumba viumbe vyote hapo mwanzo, Mungu alisema na hebu kuwe na nuru, na kukawa na nuru. Tokeo hili lilifanyika haraka sana, lilitimizwa kwa muda mfupi sana, na hakukuwa na kuchelewa kokote kuhusu kukamilika na kutimizwa kwake; athari za matamshi ya Mungu zilitokea papo hapo. Vyote vilikuwa onyesho la mamlaka ya Mungu, lakini wakati Mungu alipombariki Ibrahimu, Aliruhusu binadamu kuuona upande mwingine wa mamlaka ya Mungu, na Akaruhusu binadamu kuona mamlaka ya Muumba yasiyokadirika, na zaidi, Akaruhusu binadamu kuona upande halisi, bora zaidi wa mamlaka ya Muumba.
Punde tu matamshi ya Mungu yanapotamkwa, mamlaka ya Mungu yanachukua usukani wa kazi hii, na hoja iliyoahidiwa kwa kinywa cha Mungu kwa utaratibu huanza kugeuka na kuwa uhalisi. Miongoni mwa viumbe vyote, mabadiliko huanza kufanyika katika kila kitu kutokana na hayo, sawa na vile, kwenye mwanzo wa msimu wa mchipuko, nyasi hugeuka kuwa kijani, maua huchanua, macho ya maua yanachanua kutoka mitini, ndege wanaanza kuimba, nao batabukini wanaanza kurejea, nayo mashamba yanaanza kujaa watu…. Wakati wa msimu wa machipuko unapowadia viumbe vyote hupata nguvu, na hiki ndicho kitendo cha miujiza cha Muumba. Wakati Mungu anapokamilisha ahadi zake, viumbe vyote mbinguni na ardhini vinapata nguvu mpya na kubadilika kulingana na fikira za Mungu—na hakuna kiumbe ambacho kinaachwa. Wakati kujitolea au kuahidi kunapotamkwa kutoka kwa Mungu, viumbe vyote vinatimiza wajibu wake, na vinashughulikiwa kwa minajili ya kutimizwa kwake, na viumbe vyote vinaundwa na kupangiliwa chini ya utawala wa Mungu, na vinaendeleza wajibu wao maalum, na kuhudumu kazi zao husika. Haya ndiyo maonyesho ya mamlaka ya Muumba. Unaona nini katika mambo haya? Unajuaje mamlaka ya Mungu? Kunao upana wa mamlaka ya Mungu? Kuna kipimo cha muda? Je, inaweza kusemekana kuwa na kimo fulani, au urefu fulani? Je, inaweza kusemekana kuwa na ukubwa au nguvu fulani? Je, inaweza kupimwa kwa vipimo vya binadamu? Mamlaka ya Mungu hayawakiwaki yakizima, hayaji yakienda, na hakuna mtu anayeweza kupima namna ambavyo mamlaka Yake yalivyo makubwa. Haijalishi ni muda gani utakaopita, wakati Mungu anabariki mtu, baraka hizi zitaendelea kuwepo, na kuendelea kwake kutadhihirisha agano la mamlaka ya Mungu yasiyokadirika, na kutaruhusu mwanadamu kutazama kule kujitokeza upya kwa nguvu za maisha zisizozimika za Muumba, mara kwa mara. Kila onyesho la mamlaka Yake ni onyesho timilifu la maneno kutoka kwenye kinywa Chake, na linaonyeshwa kwa vitu vyote, na kwa mwanadamu. Zaidi ya hayo, kila kitu kinachokamilishwa na mamlaka Yake ni bora zaidi ya kulinganishwa, na hakina dosari kamwe. Yaweza kusemekana kwamba fikira Zake, matamshi Yake, mamlaka Yake, na kazi zote Anazozikamilisha, zote ni picha nzuri isiyolinganishwa, na kwa viumbe, lugha ya binadamu haiwezi kuelezea umuhimu na thamani yake. Mungu anapotoa ahadi kwa mtu, haijalishi kama ni kuhusiana na pale wanakoishi, au kile wanachofanya, asili yao kabla na baada ya kupata ahadi, au hata ni vipi ambavyo mageuzi makubwa yamekuwa makubwa katika harakati zao za kuishi kwenye mazingira yao—haya yote yanajulikana kwa Mungu kama sehemu ya nyuma ya mkono Wake. Haijalishi ni muda upi umepita baada ya matamshi ya Mungu kutamkwa, kwake Yeye, ni kama vile ndio mwanzo yametamkwa. Hivi ni kusema kwamba Mungu anazo nguvu, na Anayo mamlaka kama hayo, kiasi cha kwamba Anaweza kufuatilia, kudhibiti, na kutambua kila ahadi Anayotoa kwa mwanadamu, haijalishi ahadi hiyo ni nini, haijalishi ni muda gani itachukua kutimizwa kikamilifu, na, zaidi, haijalishi upana wa sehemu ambazo kukamilika huko kunagusia—kwa mfano, muda, jiografia, kabila, na kadhalika—ahadi hii itakamilishwa, na kutambuliwa, na, zaidi, kukamilishwa kwake na kutambuliwa kwake hakutahitaji jitihada Zake hata kidogo. Na haya yanathibitisha nini? Kwamba upana wa mamlaka ya Mungu na nguvu vinatosha kudhibiti ulimwengu mzima, na wanadamu wote. Mungu aliumba nuru, lakini hiyo haimaanishi kuwa Mungu anasimamia tu nuru, kwamba Yeye anasimamia maji tu kwa sababu Aliyaumba maji, na kwamba kila kitu kingine hakina uhusiano na Mungu. Je, hii siyo suitafahamu? Ingawaje baraka za Mungu kwa Ibrahimu zilikuwa zimefifia polepole kutoka kwenye kumbukumbu ya binadamu baada ya miaka mia kadhaa, kwake Mungu, ahadi hii ilibaki vilevile. Ilikuwa kwenye mchakato wa kukamilishwa, na haikuwahi kusitishwa. Binadamu hakuwahi kujua au kusikia namna ambavyo Mungu alisisitiza mamlaka Yake, namna ambavyo vitu vyote vilivyoundwa na kupangiliwa, na ni hadithi ngapi za ajabu zilifanyika miongoni mwa vitu vyote vya uumbaji wa Mungu kwenye kipindi hiki cha muda, lakini kila kipande kizuri cha onyesho la mamlaka ya Mungu na ufunuo wa matendo Yake vilipitishwa na kutukuzwa miongoni mwa viumbe vyote, viumbe vyote vilijitokeza na kuongea kuhusu vitendo vya kimiujiza vya Muumba, na kila mojawapo ya hadithi iliyosimuliwa sana kuhusu ukuu wa Muumba juu ya viumbe vyote itaweza kutangazwa na viumbe vyote daima dawamu. Mamlaka ambayo Mungu anatawala viumbe vyote, na nguvu za Mungu, vinaonyesha viumbe vyote kwamba Mungu anapatikana kila pahali wakati wote. Wakati unashuhudia upekee wa mamlaka na nguvu za Mungu, utaona kwamba Mungu anapatikana kila mahali na nyakati zote. Mamlaka na nguvu za Mungu haviwekewi mipaka ya muda, jiografia, nafasi, au mtu yeyote, jambo au kitu. Upana wa mamlaka na nguvu za Mungu unazidi mawazo ya binadamu; haufikiriki kwa binadamu, hauwaziki kwa binadamu, na hautawahi kujulikana na binadamu.
Baadhi ya watu wanapenda kujijazia na kujifikiria, lakini, mawazo ya binadamu yanaweza kufikia wapi? Yanaweza kuzidi ulimwengu huu? Je, mwanadamu ana uwezo wa kujijazia na kufikiria uhalali na usahihi wa mamlaka ya Mungu? Je, kule kujijazia na kujifikiria kwa binadamu kunaweza kuruhusu yeye kufikia maarifa ya mamlaka ya Mungu? Vinaweza kufanya binadamu kushukuru kwa kweli na kunyenyekea mbele ya mamlaka ya Mungu? Hoja zinathibitisha kwamba uingiliaji kati na kufikiria kwa binadamu ni zao tu la akili za binadamu, na hakutoi hata msaada kidogo au manufaa kidogo kwa maarifa ya binadamu kuhusu mamlaka ya Mungu. Baada ya kusoma makala ya kidhahania ya kisayansi, baadhi wanaweza kufikiria mwezi, na vile nyota zilivyo. Ilhali hii haimanishi kwamba binadamu anao ufahamu wowote wa mamlaka ya Mungu. Kufikiria kwa binadamu ni huku tu: kufikiria. Kuhusiana na hoja za mambo haya, hivi ni kusema kwamba, kwa kurejelea muunganiko wao kwa mamlaka ya Mungu, hana ung'amuzi wowote. Na je, ikiwa umeenda hadi mwezini? Je, hii inaonyesha kuwa unao ufahamu wa pande nyingi kuhusu mamlaka ya Mungu? Je, inaonyesha kwamba wewe unaweza kufikiria upana wa mamlaka na nguvu za Mungu? Kwa sababu huko kuingilia kati na kufikiria kwa mwanadamu hakuwezi kumruhusu kujua mamlaka ya Mungu, je, binadamu anafaa kufanya nini? Chaguo lenye hekima zaidi ni kutojijazia au kutojifikiria, ambapo ni kusema kwamba binadamu asiwahi kutegemea kufikiria na kutegemea uingiliaji kati inapohusu kujua mamlaka ya Mungu. Ni nini ambacho Ningependa kukwambia hapa? Maarifa ya mamlaka ya Mungu, nguvu za Mungu, utambulisho binafsi wa Mungu, na hali halisi ya Mungu haviwezi kutimizwa kwa kutegemea kufikiria kwako. Kwa vile huwezi kutegemea kufikiria ili kujua mamlaka ya Mungu, basi ni kwa njia gani unaweza kutimiza maarifa ya kweli ya mamlaka ya Mungu? Kwa kula na kunywa maneno ya Mungu, kupitia ushirika, na kupitia kwa uzoefu wa maneno ya Mungu, utaweza kuwa na hali halisi ya kujua kwa utaratibu na uthibitishaji wa mamlaka ya Mungu na hivyo basi utafaidi kuelewa kwa utaratibu na maarifa yaliyoongezeka. Hii ndiyo njia tu ya kutimiza maarifa ya mamlaka ya Mungu; hakuna njia za mkato. Kukuuliza kutofikiria si sawa na kukufanya uketi kimyakimya ukisubiri maangamizo, au kukusitisha dhidi ya kufanya kitu. Kutotumia akili zako kuwaza na kufikiria kunamaanisha kutotumia mantiki ya kujijazia, kutotumia maarifa kuchambua, kutotumia sayansi kama msingi, lakini badala yake kufurahia, kuhakikisha, na kuthibitisha kuwa Mungu unayemsadiki anayo mamlaka, kuthibitisha kwamba Yeye anashikilia ukuu juu ya hatima yako, na kwamba nguvu Zake nyakati zote zinathibitisha kuwa Yeye Mungu Mwenyewe ni wa kweli, kupitia kwa matamshi ya Mungu, kupitia ukweli, kupitia kwa kila kitu unachokabiliana nacho maishani. Hii ndiyo njia pekee ambayo mtu yeyote anaweza kutimiza ufahamu wa Mungu. Baadhi ya watu husema kwamba wangependa kupata njia rahisi ya kutimiza nia hii, lakini unaweza kufikiria kuhusu njia kama hiyo? Nakwambia, hakuna haja ya kufikiria: Hakuna njia nyingine! Njia ya pekee ni kujua kwa uangalifu na bila kusita na kuhakikisha kile Mungu anacho na alicho kupitia kwa kila neno Analolielezea na Analolifanya. Hii ndiyo njia pekee ya kujua Mungu. Kwani kile Mungu anacho na alicho, na kila kitu cha Mungu, si cha wazi na tupu—lakini cha kweli.
Hoja ya Udhibiti wa Muumba na Utawala Juu ya Vitu Vyote na Viumbe Vilivyo Hai Inazungumzia Uwepo wa Kweli wa Mamlaka ya Muumba
Vilevile, baraka za Yehova Mungu kwa Ayubu zimerekodiwa katika Kitabu cha Ayubu. Ni nini ambacho Mungu alimpa Ayubu? "Kwa hivyo Yehova akabariki mwisho wa baadaye wa Ayubu zaidi kuliko mwanzo wake: kwa sababu alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, na ngamia elfu sita, na elfu moja ya jozi za ng’ombe, na elfu moja ya punda wa kike" (Ayubu 42:12). Kutoka kwenye mtazamo wa binadamu, ni vitu gani alivyopewa Ayubu? Je, vilikuwa rasilimali ya binadamu? Akiwa na rasilimali hizi, je, Ayubu angeweza kuwa tajiri sana kwenye kipindi hicho? Na aliwezaje kumiliki rasilimali kama hizo? Ni nini kilisababisha utajiri wake? Bila shaka ilikuwa ni shukrani kwa baraka ya Mungu ambapo Ayubu alifanikiwa kumiliki. Namna ambavyo Ayubu alitazama rasilimali hizi, na vipi alivyochukulia baraka za Mungu, si jambo ambalo tutalizungumzia hapa. Tunapokuja katika baraka za Mungu watu wote hutamani, mchana na usiku, kubarikiwa na Mungu, ilhali binadamu hana udhibiti wowote kuhusiana na idadi ngapi ya rasilimali anaweza kufaidi katika maisha yake yote, au kama anaweza kupokea baraka kutoka kwa Mungu—na hii ni hoja isiyopingika! Mungu anayo mamlaka, na nguvu za kumpatia mwanadamu rasilimali yoyote, kumruhusu binadamu kupata tamko lolote la baraka, ilhali kuna kanuni ya baraka za Mungu. Ni aina gani ya watu ambao Mungu hubariki? Watu Anaowapenda, bila shaka! Ibrahimu na Ayubu walibarikiwa wote na Mungu, ilhali baraka walizopokea hazikuwa sawa. Mungu alibariki Ibrahimu kwa vizazi vingi kama mchanga na nyota. Wakati Mungu alipombariki Ibrahimu, Alisababisha vizazi vya mtu mmoja, taifa moja, kuwa na nguvu na ufanisi. Katika haya mamlaka ya Mungu yalitawala mwanadamu, ambaye alipumua pumzi za Mungu miongoni mwa viumbe vyote na viumbe vyenye uhai. Chini ya ukuu wa mamlaka ya Mungu, huyu mwanadamu aliweza kupenyeza na kuwepo kwa kasi, na ndani ya upana, ulioamuliwa na Mungu. Haswa, uwezo wa taifa hili, kima cha upanuzi, na matarajio ya maisha vyote vilikuwa sehemu ya mipangilio ya Mungu, na kanuni ya haya yote ilitokana kwa ujumla kwa ahadi ambazo Mungu alimpa Ibrahimu. Hivi ni kusema kwamba, licha ya hali zozote zile, ahadi za Mungu zingeendelea mbele bila kizuizi na kuweza kutambuliwa kulingana na uwepo wa mamlaka ya Mungu. Katika ahadi ambayo Mungu alimpa Ibrahimu, licha ya misukosuko ya ulimwengu, licha ya umri, licha ya majanga yanayovumiliwa na mwanadamu, vizazi vya Ibrahimu visingeweza kukabiliwa na hatari ya maangamizo, na taifa lao lisingefifia na kutokomea. Baraka ya Mungu kwa Ayubu, hata hivyo, ilimfanya kuwa tajiri wa kupindukia. Kile Mungu alichompa kilikuwa mseto wa viumbe hai, vinavyopumua, maelezo yake yalikuwa—idadi yao, kasi yao ya kuzaa, kima cha kuishi, kiwango cha mafuta kwenye viumbe hivyo, na kadhalika—vilidhibitiwa pia na Mungu. Ingawaje viumbe hivi hai havikumiliki uwezo wa kuongea, navyo pia vilikuwa sehemu ya mipangilio ya Muumba, na kanuni za mipangilio ya Mungu zilikuwa kulingana na baraka ambayo Mungu aliahidi Ayubu. Katika baraka ambazo Mungu alimpa Ibrahimu na Ayubu, ingawaje kile kilichokuwa kimeahidiwa kilikuwa tofauti, mamlaka ambayo Muumba alitumia kutawala viumbe vyote na viumbe vilivyo na uhai yalikuwa yale yale. Kila maelezo ya mamlaka na Nguvu za Mungu yameonyeshwa kwenye ahadi Zake tofauti na baraka zake kwa Ibrahimu na Ayubu, kwa mara nyingine zaonyesha binadamu kwamba mamlaka ya Mungu ni zaidi ya kufikiria kwa binadamu. Maelezo haya yanamwambia binadamu kwa mara nyingine kwamba kama angetaka kujua mamlaka ya Mungu, basi hii itawezekana tu kupitia kwa maneno ya Mungu na kuweza kupitia kazi ya Mungu.
Mamlaka ya Mungu ya ukuu juu ya viumbe vyote huruhusu binadamu kuweza kuona ukweli kwamba: Mamlaka ya Mungu hayapo tu katika matamshi "Mungu akasema, na Kuwepo na nuru, na kukawa na nuru, na, Kuwepo na anga, na kukawa na anga, na, Kuwepo na ardhi, na kukawa na ardhi," lakini, vilevile namna Alivyofanya nuru ile kuendelea kuwepo, kulizuia anga dhidi ya kutoweka na Akaiweka ardhi milele ikiwa kando na maji, pamoja na maelezo ya namna Alivyotawala na kusimamia viumbe: nuru, anga, na ardhi. Nini kingine unachoona katika baraka za Mungu kwa mwanadamu? Ni wazi, kwamba baada ya Mungu kuwabariki Ibrahimu na Ayubu, nyayo za Mungu hazikusita, kwani Alikuwa tu ameanza kuonyesha mamlaka Yake, na Alinuia kuhakikisha kwamba kila mojawapo ya matamshi Yake yangekuwa uhalisia, na kuhakikisha kuwa kila mojawapo ya maelezo ambayo Alizungumza yanatokea kuwa kweli, na kwa hivyo kwenye miaka iliyofuata, Aliendelea kufanya kila kitu Alichonuia. Kwa sababu Mungu anayo mamlaka, pengine inaonekana kwa binadamu kwamba Mungu huongea tu, na Hahitaji kuinua hata kidole chake ili mambo yote yaweze kutimizwa. Kufikiria hivyo, ni, lazima Niseme, mzaha! Kama utachukua mtazamo wa upande mmoja wa Mungu kuanzisha agano na binadamu kwa kutumia maneno, na ukamilishaji wa kila kitu na Mungu kwa kutumia maneno, na huwezi kuona ishara na hoja mbalimbali ambazo mamlaka ya Mungu yanatawala juu ya kila kitu, basi ufahamu wako kuhusiana na mamlaka ya Mungu ni mdogo mno na wa mzaha! Kama binadamu anafikiria Mungu kuwa hivyo, basi, lazima isemwe, maarifa ya binadamu kuhusu Mungu yameendeshwa hadi kwenye shimo la mwisho, na sasa yamefika mwisho wenyewe, kwani Yule Mungu ambaye binadamu anafikiria kuhusu ni mashine tu ya kutoa amri, na si Mungu anayemiliki mamlaka. Je, umeona nini kupitia kwenye mifano ya Ibrahimu na Ayubu? Je, umeuona upande halisia wa mamlaka na nguvu za Mungu? Baada ya Mungu kuwabariki Ibrahimu na Ayubu, Mungu hakubakia mahali Alipokuwa, wala Yeye kuwaweka wajumbe Wake kazini huku Akisubiri kuona matokeo yake yatakuwa yapi. Kinyume cha mambo ni kuwa, pindi Mungu alipotamka maneno Yake, akiongozwa na mamlaka ya Mungu, mambo yote yalianza kukubaliana na kazi ambayo Mungu alinuia kufanya, na kulikuwepo na watu waliokuwa wamejitayarisha, vitu, na vifaa ambavyo Mungu alihitaji. Hivi ni kusema kwamba, punde tu maneno hayo yalipotamkwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu, mamlaka ya Mungu yalianza kutumika kotekote kwenye ardhi nzima, na Akaweka wazi mkondo ili kuweza kukamilisha na kutimiza ahadi Alizotoa kwa Ibrahimu na Ayubu, huku Akifanya pia mipango na matayarisho yote kuhusiana na kila kitu kilichohitajika kwa kila awamu Aliyopanga kutekeleza. Kwa wakati huu, hakuwashawishi tu wafanyakazi Wake, lakini pia na viumbe vyote vilivyokuwa vimeumbwa na Yeye. Hivyo ni kusema kwamba upana ambao mamlaka ya Mungu yalitiliwa maanani haukujumuisha tu wajumbe, lakini, vilevile, vitu vyote, vilivyoshawishiwa ili kutii ile kazi ambayo Alinuia kukamilisha; hizi ndizo zilizokuwa tabia mahususi ambazo mamlaka ya Mungu yalitumiwa. Katika kufikiria kwako, baadhi ya watu wanaweza kuwa na ufahamu ufuatao kuhusiana na mamlaka ya Mungu: Mungu anayo mamlaka, na Mungu anao uwezo, na hivyo basi Mungu anahitaji kubaki katika mbingu ya tatu, au Anahitajika tu kubakia mahali maalum, na hahitajiki kufanya kazi yoyote fulani, na uzima wa kazi ya Mungu unakamilishwa katika fikira Zake. Baadhi wanaweza kusadiki kuwa, ingawaje Mungu alibariki Ibrahimu, Mungu hakuhitajika kufanya kitu chochote, na ilitosha kwake Yeye kutamka tu matamshi Yake. Je, hivi ndivyo ilivyofanyika kweli? Bila shaka la! Ingawaje Mungu anamiliki mamlaka na nguvu, mamlaka Yake ni ya kweli na halisia, si matupu. Uhalisi na ukweli wa mamlaka ya Mungu na nguvu hufichuliwa kwa utaratibu, kuwekwa ndani ya uumbaji Wake wa vitu vyote, na udhibiti wa vitu vyote, na katika mchakato ambao Anaongoza na kusimamia wanadamu. Kila mbinu, kila mtazamo na kila maelezo ya ukuu wa Mungu juu ya wanadamu na vitu vyote, na kazi yote ambayo Amekamilisha, vilevile ufahamu Wake kuhusu vitu vyovyote—vinathibitisha kwa kweli kwamba mamlaka na nguvu za Mungu si maneno matupu. Mamlaka na nguvu Zake vyote vinaonyeshwa na kufichuliwa kila mara, na katika mambo yote. Maonyesho haya na ufunuo vyote vinazungumzia uwepo wa kihalisia wa mamlaka ya Mungu, kwani Yeye ndiye anayetumia mamlaka na nguvu Zake kuendeleza kazi Yake, na kuamuru vitu vyote, na kutawala vitu vyote kila wakati, na nguvu na mamlaka Yake, vyote haviwezi kubadilishwa na malaika, au wajumbe wa Mungu. Mungu aliamua ni baraka gani Angempa Ibrahimu na Ayubu—uamuzi ulikuwa wa Mungu. Hata ingawaje wajumbe wa Mungu waliweza kumtembelea Ibrahimu na Ayubu wao binafsi, vitendo vyao vilikuwa kulingana na amri za Mungu, na kulingana na mamlaka ya Mungu, na pia walikuwa wakifuata ukuu wa Mungu. Ingawaje binadamu anawaona wajumbe wa Mungu wakimtembelea Ibrahimu, na hashuhudii Yehova Mungu binafsi akifanya chochote kwenye rekodi za Biblia, kwa hakika Yule Mmoja tu ambaye anatilia mkazo nguvu na mamlaka ni Mungu Mwenyewe, na hali hii haivumilii shaka yoyote kutoka kwa binadamu yeyote! Ingawaje umewaona malaika na wajumbe wakimiliki nguvu nyingi, na wametenda miujiza, au wamefanya baadhi ya mambo yaliyoagizwa na Mungu, vitendo vyao ni kwa minajili tu ya kukamilisha agizo la Mungu, na wala si tu kuonyesha mamlaka ya Mungu—kwani hakuna binadamu au kifaa kilicho na, au kinachomiliki, mamlaka ya Muumba ya kuumba vitu vyote na kutawala vitu vyote. Na kwa hivyo hakuna binadamu au kifaa chochote kinaweza kutumia au kuonyesha mamlaka ya Muumba.
Mamlaka ya Muumba Hayabadiliki na Hayakosewi
Ni nini umeona katika sehemu hizi tatu za maandiko? Je, umeona kuwa kuna kanuni ambayo Mungu hutumia mamlaka Yake? Kwa mfano, Mungu aliutumia upinde wa mvua kuanzisha agano na binadamu, ambapo Aliuweka upinde wa mvua katika mawingu ili kumwambia binadamu kuwa Yeye Hatawahi tena kutumia gharika kuangamiza ulimwengu. Je, upinde wa mvua tunaouona leo, bado ndio uleule uliozungumziwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu? Je, asili na maana yake vimebadilika? Bila shaka, havijabadilika. Mungu alitumia mamlaka Yake ili kutekeleza kitendo hiki, nalo agano Aliloanzisha na binadamu limeendelea hadi leo, na muda ambao agano hili litabadilishwa, bila shaka, ni uamuzi wa Mungu. Baada ya Mungu kutamka "Mimi nauweka upinde wangu wa mvua mawinguni," siku zote Mungu alifuata agano hili, Alilifuata hadi leo. Unaona nini katika haya? Ingawaje Mungu anayamiliki mamlaka na nguvu, Anayo bidii sana na Anafuata kanuni katika vitendo Vyake, na Anashikilia maneno Yake. Bidii Yake na kanuni za vitendo Vyake, vinaonyesha namna ambavyo Muumba asivyoweza kukosewa na namna ambavyo mamlaka ya Muumba yalivyo magumu kushindwa. Ingawaje Anamiliki mamlaka ya juu, na kila kitu kinatawaliwa na Yeye, na japokuwa Anazo nguvu za kutawala vitu vyote, Mungu hajawahi kuharibu mpango Wake au kutatiza mpangilio Wake mwenyewe, na kila wakati Anapotumia mamlaka Yake, ni kulingana na umakinifu unaohitajika kwenye kanuni Zake mwenyewe na hasa kwa kufuata kile kilichotamkwa kutoka kwenye kinywa Chake, na kufuata hatua na majukumu ya mpango Wake. Sina haja ya kusema kwamba kila kitu kinachotawaliwa na Mungu pia kinatii kanuni ambazo mamlaka ya Mungu yanatumika, na hakuna mwanadamu au kitu kisichojumuishwa kwenye mipangilio ya mamlaka Yake, wala hakuna anayeweza kubadilisha kanuni ambazo mamlaka Yake yanatumika. Kwenye macho ya Mungu, wale wanaobarikiwa hupokea utajiri mzuri unaoletwa na mamlaka Yake, na wale wanaolaaniwa hupokea adhabu yao kwa sababu ya mamlaka ya Mungu. Chini ya ukuu wa mamlaka ya Mungu, hakuna binadamu au kitu ambacho hakijumuishwi, kwenye utumiaji wa mamlaka Yake, wala hakuna kinachoweza kubadilisha kanuni hizi ambazo mamlaka Yake yanatumiwa. Mamlaka ya Muumba hayabadilishwi kwa mabadiliko ya aina yoyote ile, na, vilevile, kanuni ambazo mamlaka Yake yanatumiwa hazibadiliki kwa sababu yoyote ile. Mbingu na ardhi vyote vinaweza kupitia misukosuko mingi, lakini mamlaka ya Muumba hayatabadilika; vitu vyote vitatoweka, lakini mamlaka ya Muumba hayatawahi kutoweka. Hii ndiyo hali halisi ya mamlaka ya Muumba ambayo haibadiliki wala haikosewi, na huu ndio upekee wenyewe wa Muumba!
Maneno yaliyo hapa chini ni lazima katika kujua mamlaka ya Mungu, na maana yake yametolewa kwenye ushirika ulio hapa chini. Hebu tuendelee kuyasoma Maandiko.
4. Amri ya Mungu kwa Shetani
Ayubu 2:6 Naye Yehova akasema kwa Shetani, Tazama, yeye yuko katika mkono wako; lakini uuhifadhi uhai wake.
Shetani Hajawahi Kuthubutu Kukiuka Mamlaka ya Muumba, na Kwa Sababu Hiyo, Vitu Vyote Vinaishi kwa Mpangilio
Hili ni dondoo kutoka katika Kitabu cha Ayubu, na "yeye" katika maneno haya inaashiria Ayubu. Ingawaje imeandikwa kwa muhtasari, sentensi hii inaelezea masuala mengi. Inafafanua mabadilishano fulani kati ya Mungu na Shetani kwenye ulimwengu wa kiroho, na inatwambia kuwa kiini cha maneno ya Mungu kilikuwa Shetani. Pia inarekodi kile kilichozungumziwa mahususi na Mungu. Maneno ya Mungu yalikuwa amri na shurutisho kwa Shetani. Maelezo mahususi ya shurutisho hili ni kuhusiana na kuyaokoa maisha ya Ayubu na pale ambapo Mungu aliweka masharti namna ambavyo Shetani alifaa kumshughulikia Ayubu—Shetani alilazimika kuyaokoa maisha ya Ayubu. Kitu cha kwanza tunachojifunza kutoka kwenye sentensi hii ni kwamba matamshi haya yalitamkwa na Mungu kwa Shetani. Kulingana na maandishi ya asili ya Kitabu cha Ayubu, yanatwambia usuli wa matamshi kama hayo: Shetani alipenda kumshutumu Ayubu, na hivyo lazima angepokea huo mkataba wa Mungu kabla hajamtia majaribuni. Wakati alipokubali ombi la Shetani kumjaribu Ayubu, Mungu aliweza kumtajia Shetani sharti lifuatalo: "Tazama, yeye yuko katika mkono wako; lakini uuhifadhi uhai wake." Ni nini asili ya maneno haya? Ni wazi kwamba ni amri, ni shurutisho. Baada ya kuelewa asili ya maneno haya, unafaa, bila shaka, pia kung’amua kwamba Aliyetoa shurutisho hili ni Mungu, na kwamba aliyepokea amri hii, na akaitii, ni Shetani. Sina haja ya kusema kwamba katika shurutisho hili, uhusiano kati ya Mungu na Shetani uko wazi kwa yeyote ambaye anasoma maneno haya. Bila shaka, huu ndio uhusiano kati ya Mungu na Shetani katika ulimwengu wa kiroho, na tofauti kati ya utambulisho na hadhi ya Mungu na Shetani, iliyoelezwa kwenye rekodi za mabadilishano ya mazungumzo ya Mungu na Shetani katika Maandiko, na, hadi leo, ni mfano mahususi na rekodi ya maandishi ambapo binadamu anaweza kujifunza tofauti kuu kati ya utambulisho na hadhi ya Mungu na Shetani. Wakati huu, lazima Niseme kwamba, rekodi ya maneno haya ni waraka muhimu sana katika ufahamu wa binadamu juu ya hadhi na utambulisho wa Mungu, na inatoa taarifa muhimu kwa maarifa ya mwanadamu kuhusu Mungu. Kupitia mabadilishano haya ya Mungu na Shetani katika ulimwengu wa kiroho, binadamu anaweza kuelewa dhana moja mahususi katika mamlaka ya Muumba. Maneno haya ni ushuhuda mwingine wa kuonyesha mamlaka ya kipekee ya Muumba.
Kwa nje, ni mabadilishano kati ya Yehova Mungu na Shetani. Hali yao halisi ni kwamba, mtazamo ambao Yehova Mungu anaongea, na nafasi ambayo Anazungumzia, ni ya juu zaidi kuliko ya Shetani. Hivyo ni kusema kwamba Yehova Mungu anamwamuru Shetani na sauti ya kushurutisha, na Anamwambia Shetani ni nini anafaa afanye na kile hafai kufanya, kwamba tayari Ayubu yu mikononi mwake, na yuko huru kumfanya Ayubu vyovyote atakavyo—lakini asiyachukue maisha ya Ayubu. Ujumbe hapa ni, ingawaje Ayubu alikuwa amewekwa kwenye mikono ya Shetani, maisha yake hayakuchukuliwa na Shetani; hakuna anayeweza kuchukua maisha ya Ayubu kutoka mikononi mwa Mungu isipokuwa Mungu amruhusu. Mtazamo wa Mungu unafafanuliwa waziwazi katika amri hii kwa Shetani, na amri hii pia inajionyesha na kufichua msimamo ambao Yehova Mungu anazungumza na Shetani. Katika haya, Yehova Mungu hashikilii tu hadhi ya Mungu aliyeumba nuru, na hewa, na vitu vyote na viumbe hai, au ya Mungu anayeshikilia ukuu juu ya vitu vyote na viumbe hai, lakini pia ya Mungu ambaye anaamuru mwanadamu, na kuamuru Jahanamu, Mungu ambaye anadhibiti maisha na kifo cha viumbe vyote hai. Katika ulimwengu wa kiroho, ni nani mbali na Mungu ambaye angethubutu kutoa shurutisho kama hilo kwa Shetani? Na ni kwa nini Mungu binafsi Alitoa shurutisho Lake kwa Shetani? Kwa sababu maisha ya binadamu, pamoja na yale ya Ayubu, yanadhibitiwa na Mungu. Mungu hakumruhusu Shetani kujeruhi au kuchukua maisha ya Ayubu, hivyo ni kusema kwamba kabla ya Mungu kumruhusu Shetani kumjaribu Ayubu, Mungu bado alikumbuka kutoa shurutisho maalum kama hilo, na kwa mara nyingine Akamwamuru Shetani asiyachukue maisha ya Ayubu. Shetani hajawahi kuthubutu kukiuka mamlaka ya Mungu, na, vilevile, amesikiliza kwa umakinifu siku zote na kutii shurutisho na amri mahususi za Mungu, asiwahi thubutu kuzivunja, na, bila shaka asithubutu kubadilisha kwa hiari shurutisho zozote za Mungu. Hiyo ndiyo mipaka ambayo Mungu amemwekea wazi Shetani, na hivyo Shetani hajawahi thubutu kuvuka mipaka hiyo. Huu si uwezo wa mamlaka ya Mungu? Je, huu si ushuhuda wa mamlaka ya Mungu? Wa namna ya kuwa mbele ya Mungu, na namna ya kumtazama Mungu, Shetani anao ung'amuzi bora zaidi kuliko mwanadamu, hivyo, katika ulimwengu wa kiroho, Shetani anaona hadhi na mamlaka ya Mungu vizuri sana, na anatambua sana ule uwezo wa mamlaka ya Mungu na kanuni zinazotilia mkazo kwenye mamlaka Yeye. Hathubutu, kamwe, kutozitilia maanani kanuni hizo, wala hathubutu kukiuka kanuni hizo kwa vyovyote vile, au kufanya chochote ambacho kinakiuka mamlaka ya Mungu, na hathubutu kukabiliana na hasira ya Mungu kwa njia yoyote. Ingawaje ni mwovu na mwenye kiburi kiasili, Shetani hajawahi kuthubutu kuvuka mipaka na viwango alivyowekewa na Mungu. Kwa miaka milioni, ametii kwa umakinifu mipaka hii, ametii kila amri na shurutisho lililotolewa na Mungu na hajawahi kuthubutu kukanyaga juu ya alama. Ingawaje ni mwenye kijicho, Shetani ni "mwerevu" zaidi kuliko mwanadamu aliyepotoka; anajua utambulisho wa Muumba, na anajua mipaka yake. Kutokana na vitendo vya Shetani vya kunyenyekea tunaweza kuona kwamba mamlaka na nguvu za Mungu ni maelekezo ya mbinguni ambayo hayawezi kukiukwa na Shetani, na kwamba yanatokana na upekee na mamlaka ya Mungu ndiposa viumbe vyote vinabadilika na kuzalisha katika njia ya mpangilio, kwamba mwanadamu anaweza kuishi na kuongezeka kupitia ndani ya mkondo ulioanzishwa na Mungu, huku hakuna mtu au kifaa kinachoweza kuuharibu mpango huu, na hakuna mtu au kifaa kinachoweza kubadilisha sheria hii—kwani vyote vinatoka kwenye mikono ya Muumba na kwenye mpangilio na mamlaka ya Muumba.
Mungu Pekee, Ambaye Anao Utambulisho wa Muumba, Anamiliki Mamlaka ya Kipekee.
Ule utambulisho wa pekee wa Shetani umesababisha watu wengi kuonyesha shauku thabiti kwenye maonyesho yake ya dhana mbalimbali. Kunao hata watu wengi wajinga wanaosadiki kwamba, kama vile Mungu, Shetani anamiliki mamlaka, kwani shetani anaweza kuonyesha miujiza, na anaweza kufanya mambo ambayo mwanadamu hawezi kufanya. Kwa hivyo, mbali na kumwabudu Mungu, mwanadamu pia anahifadhi nafasi kwenye moyo wake, na hata humwabudu Shetani kama Mungu. Watu hawa wote ni wa kusikitikiwa na kuchukiwa. Ni wa kusikitikiwa kwa sababu ya kutojua kwao, na wa kuchukiwa kwa sababu ya hali yao ya uasi wa kidini na hali halisi ya maovu ya ndani kwa ndani. Wakati huu Nahisi kwamba ni muhimu niwafahamishe kuhusu maana ya mamlaka, yanaashiria nini, na yanawakilisha nini. Kwa mazungumzo ya jumla, Mungu Mwenyewe ni mamlaka, mamlaka Yake yaanashiria mamlaka ya juu na hali halisi ya Mungu, na mamlaka ya Mungu Mwenyewe yanawakilisha hadhi na utambulisho wa Mungu. Kwa hiyo, je, Shetani huthubutu kusema kwamba yeye ni Mungu? Je, Shetani huthubutu kusema kwamba aliumba viumbe vyote, na anashikilia ukuu juu ya viumbe vyote? Bila shaka la! Kwani hawezi kuumba viumbe vyote; mpaka leo, hajawahi kuumba chochote kilichoumbwa na Mungu, na hajawahi kuumba chochote kilicho na maisha. Kwa sababu hana mamlaka ya Mungu, hatawahi endapo itawezekana kumiliki hadhi na utambulisho wa Mungu, na hili linaamuliwa na hali yake halisi. Je, anazo nguvu sawa na Mungu? Bila shaka hana! Tunaita nini vitendo vya Shetani, na miujiza inayoonyeshwa na Shetani? Je, ni nguvu? Vitendo hivi vinaweza kuitwa mamlaka? Bila shaka la! Shetani huelekeza wimbi la maovu, na misukosuko, uharibifu, na kuchachawiza kila dhana ya kazi ya Mungu. Kwa miaka elfu kadhaa iliyopita, mbali na kupotosha na kunyanyasa mwanadamu, na kumjaribu na kumdanganya binadamu hadi kufikia kiwango cha uovu, na ukataaji wa Mungu, ili binadamu aweze kutembea kwenye bonde la kivuli cha mauti, je, Shetani amefanya chochote ambacho kinastahili hata kumbukumbu ndogo zaidi, pongezi au sherehe ndogo zaidi kutoka kwa binadamu? Kama Shetani angemiliki mamlaka na nguvu, je, binadamu angepotoshwa naye? Kama Shetani angemiliki mamlaka na nguvu, je, mwanadamu angepata madhara kutokana nayo? Kama Shetani angemiliki mamlaka na nguvu, je, mwanadamu angemwacha Mungu na kugeukia mauti? Kwa sababu Shetani hana mamlaka au nguvu, ni nini ambacho tunafaa kuhitimisha kuhusu hali halisi ya kila kitu anachofanya? Kunao wale wanaofafanua kila kitu ambacho Shetani hufanya kama ujanja mtupu, ilhali Nasadiki kwamba ufafanuzi kama huo haufai sana. Je, Matendo maovu ya kupotosha mwanadamu ni ujanja mtupu tu? Nguvu za maovu ambazo Shetani alimnyanyasia Ayubu, na tamanio lake kali la kumnyanyasa na kumpotosha, lisingewezekana kutimizwa kupitia kwa ujanja mtupu tu. Tukiangalia nyuma, tunaona kwamba, mara moja, kondoo na ng’ombe wa Ayubu walitawanyishwa kila pahali kotekote kwenye milima na vilima, walikuwa hawapo tena; kwa muda mfupi tu, utajiri mwingi wa Ayubu ukatoweka. Je, yawezekana kwamba haya yote yalitimizwa kupitia kwa ujanja mtupu tu? Asili ya yale yote ambayo Shetani hufanya yanalingana na kuingiliana na istilahi mbaya kama vile kudhoofisha, kukatiza, kuharibu, kudhuru, maovu, hali ya kuwa na kijicho, na giza, na kwa hivyo matukio haya yote ambayo si ya haki na ni maovu yanahusiana na kuunganika kwenye vitendo vya Shetani, na hayawezi kutenganishwa na ile hali halisi ya uovu wa Shetani. Haijalishi ni vipi ambavyo Shetani "alivyo na nguvu", haijalishi ni vipi Shetani alivyo mwenye kuthubutu na haijalishi ni vipi uwezo wake ulivyo mwingi katika kusababisha madhara, haijalishi ni vipi anavyotumia mbinu zenye mseto-mpana ambazo zinapotosha na kudanganya binadamu, haijalishi ni vipi alivyo mwerevu kupitia kwenye ujanja na njama zake ambazo anadhalilisha binadamu, haijalishi ni vipi anavyoweza kujibadilisha katika mfumo ule aliomo, hajawahi kuweza kuumba kiumbe chochote kimoja, hajawahi kuweza kuweka wazi sheria au kanuni za uwepo wa viumbe vyote, na hajawahi kutawala na kudhibiti kifaa chochote, kiwe ni chenye uhai au kisichokuwa na uhai. Kotekote kwenye upana mkubwa wa ulimwengu, hakuna hata mtu au kifaa kimoja kilichotokana na Shetani, au kilichopo kwa sababu ya Shetani; hakuna hata mtu au kifaa kimoja ambacho kimetawaliwa na Shetani, au kudhibitiwa na Shetani. Kinyume cha mambo ni kwamba, hana budi kuishi katika utawala wa Mungu lakini, vilevile, lazima atii shurutisho na amri zote za Mungu. Bila ruhusa ya Mungu, ni vigumu sana kwa Shetani kugusa hata tone la maji au chembechembe ya mchanga kwenye ardhi; bila ruhusa ya Mungu, Shetani hana hata hiari ya kusongea mchwa wanaojiendea zao kwenye ardhi—sikwambii hata mwanadamu, aliyeumbwa na Mungu. Kwenye macho ya Mungu, Shetani ni duni zaidi ya yungiyungi kwenye mlima, hadi kwenye ndege wanaopaa hewani, hadi kwenye samaki walio baharini, hadi kwenye funza kwenye juu ya nchi. Wajibu wake miongoni mwa viumbe vyote ni kuhudumia viumbe vyote, na kufanyia kazi mwanadamu, na kuhudumia kazi ya Mungu na mpango Wake wa usimamizi. Licha ya vile anavyoonea wenzake kijicho katika asili yake, na vile ambavyo hali yake halisi ya maovu ilivyo, kitu ambacho Shetani anaweza kufanya tu ni kuweza kukubaliana kwa wajibu kuhusiana na kazi yake: kuwa mwenye huduma kwa Mungu, na kuwa mjalizo kwa Mungu. Hiki ndicho kiini na nafasi ya Shetani. Hali yake halisi haijaungana na maisha, haijaungana na nguvu, haijaungana na mamlaka; ni kitu cha kuchezea tu kwenye mikono ya Mungu, mtambo tu kwenye huduma ya Mungu!
Baada ya kuelewa uso wa kweli wa Shetani, watu wengi bado wangali hawajaelewa ni nini maana ya mamlaka, hivyo basi wacha Mimi nikuelezee! Mamlaka yenyewe yanaweza kufafanuliwa kama nguvu za Mungu. Kwanza, inaweza kusemekana kwa uhakika kwamba mamlaka na nguvu vyote ni vizuri. Havina uunganisho wowote na kitu chochote kibaya, na havina uhusiano wowote na viumbe vyovyote vilivyoumbwa au vile ambavyo havikuumbwa. Nguvu za Mungu zinaweza kuumba viumbe vya mfumo wowote ulio na uzima na nguvu, na haya yote yanaamuliwa na uzima wa Mungu. Mungu ni uzima, kwa hivyo Yeye ndiye chanzo cha viumbe hai vyote. Vilevile, mamlaka ya Mungu yanaweza kufanya viumbe vyote kutii kila neno la Mungu, yaani kuumbika kulingana na matamshi yanayotoka kwenye kinywa cha Mungu, na kuishi na kuzaana kwa amri ya Mungu, ambapo baadaye Mungu anatawala na kuamuru viumbe vyote hai, na hakutakuwa na kupotoka kokote, daima dawamu. Hakuna mtu au kifaa kilicho na mambo haya; Muumba tu ndiye anayemiliki na aliye na nguvu kama hizo, na hivyo basi yanaitwa mamlaka. Huu ndio upekee wa Muumba. Kwa hivyo, haijalishi kama ni neno lenyewe "mamlaka" au hali halisi ya mamlaka haya, kila mojawapo linaweza tu kuhusishwa na Muumba kwa sababu ni ishara ya utambulisho na hali halisi ya kipekee ya Muumba; na inawakilisha utambulisho na hadhi ya Muumba, mbali na Muumba, hakuna mtu au kifaa kinachoweza kuhusishwa na neno "mamlaka" Huu ni ufasiri wa mamlaka ya kipekee ya Muumba.
Ingawaje Shetani alimwaangalia Ayubu kwa macho ya kutamani mali yake, bila ya ruhusa ya Mungu hakuthubutu kugusa hata unywele mmoja wa mwili wa Ayubu. Ingawaje ni mwenye uovu na unyama wa ndani, baada ya Mungu kutoa shurutisho Lake kwake, Shetani hakuwa na chaguo lakini kutii shurutisho la Mungu. Na kwa hivyo, hata ingawaje Shetani alionekana kana kwamba ameshikwa na kichaa sawa na mbwamwitu miongoni mwa kondoo alipomjia Ayubu, hakuthubutu kusahau mipaka aliyowekewa wazi na Mungu, hakuthubutu kukiuka shurutisho za Mungu, na kwa hayo yote, Shetani hakuthubutu kutoka kwenye kanuni ya maneno ya Mungu—je, hii si kweli? Kutokana na mtazamo huu wa maisha, tunaona kwamba Shetani hathubutu kuvunja matamshi yoyote yale ya Yehova Mungu. Kwake Shetani, kila neno kutoka kwenye kinywa cha Mungu ni shurutisho, na sheria ya kimbinguni, na maonyesho ya mamlaka ya Mungu—kwani nyuma ya kila neno la Mungu ni ile adhabu ya Mungu inayotokana na wale wanaokiuka shurutisho za Mungu, na wale wasiotii na wanaopinga sheria za kimbinguni. Shetani anajua wazi kwamba kama atakiuka shurutisho za Mungu, basi lazima akubali athari za kukiuka mamlaka ya Mungu na kupinga sheria za kimbinguni. Na sasa athari hizi ni zipi? Sina haja ya kusema kwamba, athari hizi bila shaka, ni adhabu kutoka kwa Mungu. Vitendo vya Shetani kwake Ayubu vilikuwa tu mfano mdogo wa yeye kumpotosha binadamu, na wakati ambapo Shetani alipokuwa akitekeleza vitendo hivi, ile mipaka ambayo Mungu Aliweka na amri Alizotoa kwake Shetani vilikuwa tu mfano mdogo wa kanuni zinazotokana na kila kitu anachofanya. Aidha, wajibu na nafasi ya Shetani katika suala hili ulikuwa tu mfano mdogo wa wajibu na nafasi yake katika kazi ya usimamizi wa Mungu, na utiifu kamili wa shetani kwa Mungu wakati alipomjaribu Ayubu, ulikuwa tu mfano mdogo wa namna ambavyo Shetani hakuthubutu kuweka hata upinzani mdogo kwa Mungu katika kazi ya usimamizi wa Mungu. Ni onyo gani ambalo mifano hii midogo inakupa? Miongoni mwa mambo yote, akiwemo Shetani, hakuna mtu au kitu kinachoweza kukiuka sheria na kanuni za mbinguni zilizowekwa wazi na Muumba, na hakuna mtu au kitu kinachothubutu kukiuka sheria na kanuni hizi za mbinguni, kwani hakuna mtu au kifaa kinaweza kubadilisha au kuepuka adhabu ambayo Mungu anawawekea wale wanaokosa kumtii. Ni Muumba tu anayeweza kuanzisha sheria na kanuni za kimbinguni, ni Muumba tu aliye na nguvu za kuanza kuzitekeleza na nguvu za Muumba ndizo haziwezi kukiukwa na mtu au kitu chochote. Haya ndiyo mamlaka ya kipekee ya Muumba, mamlaka haya yako juu zaidi miongoni mwa mambo yote, na kwa hivyo haiwezekani kusema kwamba "Mungu ndiye mkubwa zaidi naye Shetani ni nambari mbili." Isipokuwa Muumba anayemiliki mamlaka ya kipekee, hakuna Mungu mwengine.
Je, sasa unayo maarifa mapya kuhusu mamlaka ya Mungu? Kwanza, kunayo tofauti kati ya mamlaka ya Mungu yaliyotajwa hivi punde na nguvu za binadamu? Na tofauti ni nini? Baadhi ya wanadamu husema kwamba hakuna ulinganifu wowote kati ya haya mawili. Hayo ni kweli! Ingawaje watu husema kwamba hakuna ulinganisho kati ya haya mawili, kwenye fikira na dhana za binadamu, nguvu za binadamu mara nyingi zinadhaniwa kuwa mamlaka, huku haya mawili yakilinganishwa mara nyingi sako kwa bako. Ni nini kinachoendelea hapa? Je, watu hawafanyi kosa kubadilisha bila ya kuwa waangalifu kitu kimoja na kingine? Vitu hivi viwili havina uhusiano wowote na hakuna ulinganisho wowote kati yavyo, ilhali watu bado hawawezi kuelewa. Je, haya yatatuliwe vipi? Kama ungependa kwa kweli kupata suluhu, njia ya pekee ni kuelewa na kujua mamlaka ya kipekee ya Mungu. Baada ya kuelewa na kujua mamlaka ya Muumba, hutataja kwa mkupuo mmoja nguvu za binadamu na mamlaka ya Mungu.
Nguvu za binadamu zinarejelea nini? Kwa ufupi, ni uwezo au mbinu inayowezesha tabia potoshi, matamanio na malengo ya binadamu kuweza kupanuliwa au kutimizwa hadi kiwango cha juu zaidi. Je, haya yatumike kumaanisha mamlaka? Haijalishi ni vipi ambavyo malengo na matamanio ya binadamu yalivyo makubwa au yenye faida, mtu huyu hawezi kusemekana amemiliki mamlaka; kama amezidi sana, haya majivuno na ufanisi ni maonyesho tu ya upumbavu wa Shetani miongoni mwa binadamu, kama imezidi sana, ni upuzi ambao shetani anaendeleza kama babu yake mwenyewe ili kutimiza maono yake ya kuwa Mungu.
Unatazama vipi haswa mamlaka ya Mungu sasa? Kwa vile sasa maneno haya yamezungumziwa kwenye ushirika, unafaa kuwa na maarifa mapya kuhusu mamlaka ya Mungu. Na kwa hivyo Nakuuliza: Mamlaka ya Mungu yanaashiria nini? Je, yanaashiria ule utambulisho wa Mungu Mwenyewe? Je, yanaashiria nguvu za Mungu Mwenyewe? Je, yanaashiria hadhi ya kipekee ya Mungu Mwenyewe? Miongoni mwa mambo yote, ni katika kitu gani umeona mamlaka ya Mungu? Uliyaona vipi? Kwa mujibu wa ile misimu minne inayopitiwa na binadamu, je, mtu yeyote anaweza kubadilisha sheria ya mabadilishano kati ya machipuko, kiangazi, mapukutiko na kipupwe? Wakati wa machipuko, miti huweza kuchomoza na kuchanua; katika kiangazi, inafunikwa na majani; katika mapukutiko inazaa matunda na katika kipupwe majani yanaanguka. Je, yupo anayeweza kubadilisha sheria hii? Je, hii inaonyesha dhana moja ya mamlaka ya Mungu? Mungu alisema "Iwe Nuru," na ikawa nuru. Je, nuru hii ingali ipo? Nuru hii inakuwepo kwa ajili ya nini? Inakuwepo kwa sababu ya maneno ya Mungu, bila shaka, na kwa sababu ya mamlaka ya Mungu. Je, hewa iliyoumbwa na Mungu bado ipo? Je, hewa ambayo binadamu anapumua inatoka kwa Mungu? Je, kuna yeyote anayeweza kuchukua vitu vinavyotoka kwa Mungu? Je, kuna yeyote anayeweza kubadilisha hali yao halisi na kazi? Kuna yeyote anayeweza kutibua mpangilio wa usiku na mchana kama ulivyopangwa na Mungu, na sheria ya usiku na mchana kama ilivyoamrishwa na Mungu? Je, shetani anaweza kufanya kitu kama hicho? Hata kama hulali wakati wa usiku, na unachukulia usiku kuwa wakati wa mchana, basi bado ni wakati wa usiku; unaweza kubadilisha mazoea yako ya kila siku, lakini huwezi kubadilisha sheria ya mabadilishano kati ya usiku na mchana—na ukweli huu hauwezi kubadilishwa na mtu yeyote, au sio? Kuna yeyote anayeweza kumfanya simba kulima ardhi kama afanyavyo ng'ombe? Je, yupo yeyote anayeweza kubadilisha ndovu kuwa punda? Je, yupo anayeweza kubadilisha kuku akapaa hewani kama tai? Je, yupo anayeweza kumfanya mbwamwitu kula nyasi kama kondoo? Je, yupo anayeweza kumfanya samaki aliye majini kuishi kwenye ardhi kavu? Na kwa nini hamna? Kwa sababu Mungu aliwaamuru kuishi ndani ya maji, na kwa hivyo wanaishi ndani ya maji. Kwenye ardhi kavu hawataweza kuishi kwani watakufa; hawawezi kukiuka vipimo vya amri ya Mungu. Vitu vyote vina sheria na kipimo cha kuwepo kwao, na kila mojawapo kina silika zake binafsi. Haya yameamriwa na Muumba, na hayawezi kubadilishwa na kupitishwa na binadamu yeyote. Kwa mfano, simba siku zote ataishi jangwani, umbali fulani kutoka kwenye jumuia ya binadamu, na hatawahi kuwa mtulivu na mwaminifu kama vile ngo'mbe alivyo na anavyoishi na kumfanyia binadamu kazi. Ingawaje ndovu na punda ni wanyama, na wote wana miguu minne, na ni viumbe vinavyopumua hewa, ni aina tofauti, kwani waligawanywa kwenye aina tofauti na Mungu, kila mmoja wao anazo silika zake binafsi, na hivyo hawatawahi kubadilishana. Ingawaje kuku ana miguu miwili, na mbawa kama vile alivyo tai, hatawahi kuweza kupaa hewani; kama amejaribu sana anaweza tu kupaa hadi kwenye mti—na hili linaamuliwa na silika yake. Sina haja kusema, haya yote ni kwa sababu ya amri za mamlaka ya Mungu.
Katika maendeleo ya mwanadamu leo, sayansi ya mwanadamu inaweza kusemekana kwamba inanawiri, na mafanikio ya uchunguzi wa kisayansi wa binadamu unaweza kufafanuliwa kama wa kuvutia. Uwezo wa kibinadamu, lazima isemwe, unazidi kukua mkubwa zaidi, lakini kunao ushindi mmoja wa kisayansi ambao mwanadamu hajaweza kufanya: Mwanadamu ameunda ndege, vibebaji vya ndege, na hata bomu la atomiki, mwanadamu ameenda angani, ametembea mwezini, amevumbua Intaneti, na ameishi maisha ya kiwango cha juu ya teknolojia, ilhali mwanadamu hawezi kuumba kiumbe hai kinachopumua. Silika za kila kiumbe kilicho hai na sheria ambazo zinatawala kuishi kwake na mzunguko wa maisha na kifo wa kila kiumbe kilicho hai—vyote hivi haviwezekani na havidhibitiki na sayansi ya mwanadamu. Wakati huu, lazima isemekane kwamba haijalishi ni viwango gani vya juu zaidi vitakavyofikiwa na sayansi ya binadamu, haviwezi kulinganishwa na fikira zozote za Muumba na haiwezekani kutambua miujiza ya uumbaji wa Muumba na uwezo wa mamlaka Yake. Kunazo bahari nyingi sana juu ya nchi, ilhali hazijawahi kukiuka mipaka yao na kuja kwenye ardhi kwa nguvu, na hiyo ni kwa sababu Mungu aliwekea mipaka kila mojawapo ya bahari hizo; zilikaa popote pale Aliziamuru kukaa; na bila ya ruhusa ya Mungu haziwezi kusongasonga ovyo. Bila ya ruhusa ya Mungu, haziwezi kuingiliana, na zinaweza kusonga tu pale ambapo Mungu anasema hivyo, na pale ambapo zinaenda na kubakia ni suala na uamuzi wa mamlaka ya Mungu.
Ili kuweka wazi zaidi, "mamlaka ya Mungu" yanamaanisha kwamba ni wajibu wa Mungu. Mungu anayo haki ya kuamua namna ya kufanya kitu na kinafanywa kwa vyovyote vile Anavyopenda. Sheria ya vitu vyote ni wajibu wa Mungu, na wala si wajibu wa binadamu; na wala haiwezi kubadilishwa na binadamu. Haiwezi kusongeshwa kwa mapenzi ya binadamu, lakini inaweza badala yake kubadilishwa kwa fikira za Mungu, na hekima ya Mungu, na amri za Mungu, na hii ni kweli ambayo haiwezi kukataliwa na binadamu yeyote. Mbingu na nchi na viumbe vyote, ulimwengu, mbingu yenye nyota, misimu minne ya mwaka, ile inayoonekana na isiyoonekana kwa binadamu—yote haya yapo, yanafanya kazi, na kubadilika, bila ya kosa hata dogo, chini ya mamlaka ya Mungu, kulingana na shurutisho za Mungu, kulingana na amri za Mungu, na kulingana na sheria za mwanzo wa uumbaji. Si hata mtu mmoja au kifaa kimoja kinaweza kubadilisha sheria zao, au kubadilisha mkondo wa asili ambao sheria hizi zinafanya kazi; zilianza kutumika kwa sababu ya mamlaka ya Mungu, na zitaangamia kwa sababu ya mamlaka ya Mungu. Haya ndiyo mamlaka yenyewe ya Mungu. Sasa kwa sababu haya yote yamesemwa, je, unahisi kwamba mamlaka ya Mungu ni ishara ya utambulisho na ishara ya Mungu? Je, mamlaka ya Mungu yanaweza kumilikiwa na kiumbe chochote kilichoumbwa au ambacho hakijaumbwa? Yanaweza kuigwa, kughushiwa, au kubadilishwa na mtu yeyote, na kitu chochote, au kifaa chochote.
Utambulisho wa Muumba ni wa Kipekee, na Hufai Kufuata lile Wazo la Imani ya Kuabudu Miungu Wengi
Ingawaje mbinu na uwezo wa Shetani ni kubwa zaidi kuliko zile za binadamu, ingawaje anaweza kufanya mambo ambayo hayawezi kufanywa na binadamu, bila kujali kama waonea wivu au unatamani kile ambacho Shetani anafanya, bila kujali kama unachukia au unachukizwa na kile anachofanya, bila kujali kama unaweza au huwezi kuona hicho, bila kujali ni kiwango kipi ambacho Shetani anaweza kutimiza au ni watu wangapi anaweza kudanganya ili wakamwabudu na kumtolea kafara, na bila kujali ni vipi unavyomfafanua, haiwezekani wewe kusema kwamba Shetani anayo mamlaka na nguvu za Mungu. Unafaa kujua kwamba Mungu ni Mungu, tunaye Mungu mmoja tu, na zaidi ya yote unafaa kujua kwamba ni Mungu tu aliye na mamlaka, na kwamba Anazo nguvu za kudhibiti na kutawala viumbe vyote. Eti kwa sababu Shetani anao uwezo wa kudanganya watu, na anaweza kujifanya kuwa Mungu, na anaweza kuiga ishara na miujiza inayofanywa na Mungu, amefanya mambo sawa na yale ya Mungu, wewe unasadiki kimakosa kwamba Mungu si wa kipekee, kwamba tunayo miungu mingi, kwamba tofauti yao ni kule kuwa tu na mbinu nyingi au chache zaidi, na kwamba kunazo tofauti katika upana na nguvu zinazoonyeshwa. Unapima ukubwa wao katika mpangilio wa kuwasili kwao, na kulingana na umri wao, na unasadiki kwa njia isiyofaa kwamba kunayo miungu mingine mbali na Mungu, na unafikiri kwamba nguvu na mamlaka ya Mungu si ya kipekee. Kama unazo fikira kama hizo, kama hutambui upekee wa Mungu, husadiki ni Mungu pekee anayemiliki mamlaka na kama utatii tu imani ya kuabudu miungu wengi, basi Nasema kwamba wewe ni duni kabisa kuliko viumbe vyote, wewe ni mfano halisi na wa kweli wa Shetani, na wewe ni mtu kamili wa maovu! Je, unaelewa kile Ninachojaribu kufunza kwa kusema maneno haya? Haijalishi ni muda gani, mahali au maelezo ya ziada kuhusu wewe, haifai kuchanganya Mungu na mtu yeyote mwengine, kitu au kifaa. Haijalishi unavyohisi kwamba mamlaka ya Mungu na hali halisi ya Mungu Mwenyewe havijulikani wala kuweza kufikiwa, haijalishi ni kiwango kipi cha matendo na maneno ya Shetani yanavyokubaliana na utambuzi na kufikiria kwako, haijalishi ni vipi ambavyo mambo haya yanakutosheleza wewe, usiwe mjinga, usichanganye dhana hizi, usikatae uwepo wa Mungu, usikatae utambulisho na hadhi ya Mungu, usimsukume Mungu nje ya mlango na kumleta Shetani kuchukua nafasi ya "Mungu" aliye ndani ya moyo wako na kuwa Mungu wako. Sina shaka kwamba una uwezo wa kufikiria athari za kufanya hivyo!
Ingawaje Binadamu Amepotoka, Angali Anaishi Chini ya Ukuu wa Mamlaka ya Muumba
Shetani amekuwa akipotosha mwanadamu kwa maelfu ya miaka. Ameleta kiwango kisichosemezeka cha maovu, amedanganya vizazi baada ya vizazi, na ametenda uhalifu wa kuchukiza ulimwenguni. Amedhulumu binadamu, amedanganya binadamu, ameshawishi binadamu ili ampinge Mungu, na ametenda vitendo vya maovu ambavyo vimetatiza na kuharibu mpango wa Mungu mara kwa mara. Ilhali, chini ya mamlaka ya Mungu, viumbe vyote na viumbe vyenye uhai vinaendelea kutii kanuni na sheria zilizowekwa wazi na Mungu. Yakilinganishwa na mamlaka ya Mungu, asili ovu ya Shetani na kuenea kwake ni vitu vibaya mno, vinakera mno na ni vya kuleta aibu na ni vidogo mno na vinyonge. Hata ingawaje Shetani anatembea miongoni mwa viumbe vyote vilivyoumbwa na Mungu, hawezi kutekeleza mabadiliko madogo zaidi kwa watu, vitu, na vifaa vilivyoamriwa na Mungu. Miaka elfu kadhaa imepita, na mwanadamu angali anafurahia nuru na hewa aliyopewa na Mungu, angali anapumua pumzi iliyotolewa na Mungu Mwenyewe, angali anafurahia maua, ndege, samaki na wadudu walioumbwa na Mungu, na kufurahia viumbe vyote vilivyotolewa na Mungu; mchana na usiku zingali zinabadilishana nafasi zao bila kusita; hiyo misimu minne inabadilishana kama kawaida; nao batabukini wanaopaa wanaondoka msimu huu wa kipupwe, lakini bado watarudi kwenye msimu ujao wa machipuko; samaki ndani ya maji hawajawahi kuondoka kwenye mito, maziwa—maskani yao; wadudu aina ya nyenje kwenye mchanga wanaimba kwelikweli kwenye siku za kiangazi; nyenje kwenye nyasi wanaimba kwa sauti ya polepole huku wakikaribisha msimu wa mapukutiko, wale batabukini wanaanza kutembea kwa makundi, huku nao tai wanabakia pweke; fahari za simba wakijitosheleza wenyewe kwa kuwinda; nao kunguni wa kaskazini wa ulaya hawatoki kwenye nyasi na maua…. Kila aina ya kiumbe kilicho hai miongoni mwa viumbe vyote kinaondoka na kurudi, kisha kinaondoka tena, mabadiliko milioni yanafanyika kwa muda wa kufumba na kufumbua—lakini kile kisichobadilika ni silika zao na sheria za kusalia. Wanaishi katika ruzuku na kustawishwa na Mungu, na hakuna mtu anayeweza kubadilisha silika zao, na vilevile hakuna mtu yeyote anayeweza kukiuka sheria hizi za kuishi. Ingawaje mwanadamu, anayeishi miongoni mwa viumbe vyote amepotoka na kudanganywa na shetani, angali hawezi kupuuza maji yaliyoumbwa na Mungu, hewa iliyoumbwa na Mungu, na vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu, na binadamu angali bado anaishi na kuzaana kwenye anga hii iliyoumbwa na Mungu. Silika za mwanadamu zingali hazijabadilika. Binadamu angali anategemea macho yake kuona, masikio yake kusikia, ubongo wake kufikiria, moyo wake kuelewa, miguu na viganja vyake kutembea, mikono yake kufanya kazi, na kadhalika; silika zote ambazo Mungu alimpa binadamu ili aweze kukubali toleo la Mungu limebakia hivyo bila kubadilishwa, welekevu ambao binadamu alitumia kushirikiana na Mungu bado haujabadilika, welekevu wa mwanadamu wa kutenda wajibu wa kiumbe kilichoumbwa haujabadilishwa, mahitaji ya kiroho ya mwanadamu hayajabadilika, tamanio la mwanadamu kuweza kujua asili zake halijabadilika, hamu ya mwanadamu kuweza kuokolewa na Muumba haijabadilika. Hizi ndizo hali za sasa za mwanadamu, anayeishi katika mamlaka ya Mungu, na ambaye amevumilia maangamizo mabaya yaliyoletwa na Shetani. Ingawaje mwanadamu amepitia unyanyasaji wa Shetani, na yeye si Adamu na Hawa tena kutoka mwanzo wa uumbaji, badala yake amejaa mambo ambayo yana uadui na Mungu kama vile maarifa, fikira na kadhalika, na amejaa tabia ya kishetani iliyopotoka, kwenye macho ya Mungu, mwanadamu yungali bado mwanadamu yule yule Aliyemuumba. Mwanadamu angali anatawaliwa na kupangiwa na Mungu, na angali anaishi ndani ya mkondo uliowekwa wazi na Mungu, na kwa hivyo kwenye macho ya Mungu, mwanadamu ambaye amepotoshwa na Shetani amefunikwa tu na uchafu na tumbo linalonguruma, na miitikio ambayo ni ya kujikokota kidogo, kumbukumbu ambayo si nzuri kama ilivyokuwa, na mwenye umri ulioongezeka kidogo—lakini kazi na silika zote za binadamu bado hazijapata madhara kamwe. Huyu ndiye mwanadamu ambaye Mungu ananuia kuokoa. Mwanadamu huyu anahitaji tu kusikia mwito wa Muumba na kusikia sauti ya Muumba, naye atasimama wima na kukimbia kutafuta ni wapi sauti imetokea. Mwanadamu huyu lazima tu aweze kuona umbo la Muumba naye hatakuwa msikivu wa kila kitu kingine, ataacha kila kitu, ili kuweza kujitolea mwenyewe kwa Mungu, na hata atayatenga maisha yake kwa ajili Yake. Wakati moyo wa mwanadamu unapoelewa maneno hayo ya moyoni kutoka kwa Muumba, mwanadamu atakataa Shetani na atakuja upande wake Muumba; wakati mwanadamu atakuwa ametakasa kabisa uchafu kutoka kwenye mwili wake, na amepokea kwa mara nyingine toleo na ukuzaji kutoka kwa Muumba, basi kumbukumbu la mwanadamu litarejeshwa, na kwa wakati huu mwanadamu atakuwa amerejea kwa kweli katika utawala wa Muumba.
Desemba 14, 2013

Chanzo: Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu  (I) Sehemu ya Nne

Tufuate: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni