Neno la Mwenyezi Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote II Sehemu ya Tatu
Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II) Sehemu ya Tatu
Chakula na Kinywaji cha Kila Siku Ambavyo Mungu Anawatayarishia Wanadamu
Tulikuwa tumezungumza sasa hivi kuhusu sehemu ya mazingira ya jumla, yaani, hali zilizo muhimu kwa kuendelea kuishi kwa wanadamu ambazo Mungu aliwatayarishia wanadamu tangu Alipoumba ulimwengu. Tumezungumza sasa hivi kuhusu vitu vitano, na vitu hivi vitano ndivyo mazingira ya jumla. Tunachoenda kuzungumzia baada ya hapo kinahusiana kwa karibu na kila maisha ya wanadamu katika mwili. Ni hali muhimu inayolingana zaidi na inayokubaliana zaidi na maisha ya mtu katika mwili. Kitu hiki ni chakula.
Mungu alimuumba mwanadamu na akamweka ndani ya mazingira ya kuishi yanayofaa. Baadaye, mwanadamu alihitaji chakula na maji. Mwanadamu alikuwa na hitaji hilo, hivyo Mungu alimtengenezea mwanadamu matayarisho hayo. Kwa hiyo, kila hatua ya kazi ya Mungu na kila kitu Anachofanya sio maneno matupu tu, lakini vinafanyika kwa kweli. Je, chakula ni kitu ambacho watu hawawezi kukosa kuwa nacho katika maisha yao? Chakula ni muhimu zaidi kuliko hewa? Vyote ni muhimu kwa njia sawa, sivyo? Vyote ni hali na vitu muhimu kwa kuendelea kuishi kwa wanadamu na kuhifadhi mwendelezo wa maisha ya binadamu. Hewa ni muhimu zaidi au maji ni muhimu zaidi? Halijoto ni muhimu zaidi au chakula ni muhimu zaidi? Vyote ni muhimu. Watu hawawezi kuchagua kwa sababu hawawezi kuishi bila chochote kati ya hivyo vyote. Hili ni tatizo halisi, si kitu unachoweza kuchagua. Hujui, lakini Mungu anajua. Unapoviona vitu hivi, utahisi, "Siwezi kuishi bila chakula!" Lakini ungewekwa pale baada tu ya wewe kuumbwa, je, ungejua kwamba unahitaji chakula? Hungejua, lakini Mungu anajua. Ni wakati tu unapokuwa na njaa na kuona kuna matunda juu ya miti na nafaka juu ya ardhi ili uweze kula ndipo unatambua, "Ah, nahitaji chakula." Ni wakati tu unapokuwa na kiu na unataka kunywa maji ndipo utatambua, "Ninahitaji maji. Ninaweza kupata maji wapi?" Unaona chemchemi ya maji mbele yako, kisha unakunywa kutoka hapo. Unasema, "Kinywaji hiki kina ladha nzuri sana. Ni nini?" Ni maji, na Mungu alimtayarishia mwanadamu. Kuhusu chakula, haijalishi ikiwa wewe hula milo mitatu kwa siku, milo miwili kwa siku, au hata zaidi ya hiyo; kwa ufupi, chakula ni kitu ambacho wanadamu hawawezi kukosa kuwa nacho katika maisha yao ya kila siku. Ni mojawapo ya vitu muhimu vya kudumisha kuendelea kuishi kwa kawaida kwa mwili wa binadamu. Hivyo chakula hasa hutoka wapi? Kwanza, kinatoka ndani ya udongo. Udongo ulitayarishwa na Mungu kwa ajili ya wanadamu. Udongo unafaa kwa kuendelea kuishi kwa mimea mbalimbali, sio tu kwa ajili ya miti au nyasi. Mungu aliwatayarishia wanadamu mbegu za kila aina ya nafaka na vyakula mbalimbali, na vilevile udongo na ardhi vinavyofaa kwa watu kupanda, na hivyo kuwapa chakula. Kuna aina gani za chakula? Mnapaswa kulijua hili vizuri, sivyo? Kwanza, kuna aina mbalimbali za nafaka. Ni nini kinahusishwa katika nafaka. Ngano, mtama wa mkia wa mbweha, mtama wa proso, mchele…, inayokuwa na maganda. Mazao ya nafaka pia yametenganishwa katika aina nyingi mbalimbali. Kuna aina nyingi za mazao ya nafaka kutoka kusini mpaka kaskazini, kama vile shayiri, ngano, oti, na nafaka inayofanana na ngano. Aina mbalimbali zinafaa kukuzwa katika maeneo mbalimbali. Pia kuna aina mbalimbali za mchele. Kusini ina aina zake za mchele, iliyo ndefu zaidi na inawafaa watu kutoka kusini kwa sababu si ya kunata sana. Kwa vile hali ya nchi ni joto zaidi kusini, wanahitajika kula aina mbalimbali kama vile mchele wa indica. Hautakiwi kunata sana la sivyo hawataweza kula na watapoteza hamu yao ya kula. Mchele unaoliwa na watu wa kaskazini ni wa kunata zaidi. Kwa vile kaskazini huwa na baridi zaidi kila mara, wanahitajika kula mchele wa kunata zaidi. Kuongezea, kuna aina mbalimbali za maharagwe. Haya yanakuzwa juu ya ardhi. Pia kuna vile vinavyokuzwa chini ya ardhi, kama viazi, viazi vitamu, jimbi, na vinginevyo. Viazi huota kaskazini. Sifa ya viazi vya kaskazini ni nzuri sana. Watu wakikosa nafaka za kula, viazi vinaweza kuwa chakula kikuu cha mlo wao ili waweze kudumisha milo mitatu kwa siku. Viazi pia vinaweza kuwa ugavi wa chakula. Viazi vitamu si vizuri kama viazi kulingana na sifa, lakini bado vinaweza kutumiwa na watu kama chakula cha kudumisha milo yao mitatu kwa siku. Ikiwa nafaka hazipatikani, watu wanaweza kutumia viazi vitamu kujaza matumbo yao. Jimbi, ambalo mara nyingi huliwa na watu wa kusini, inaweza kutumiwa kwa njia hiyo, na pia inaweza kuwa chakula kikuu. Hizi ni aina mbalimbali za nafaka, muhimu kwa chakula cha watu cha kila siku. Watu hutumia nafaka mbalimbali kutengeneza nudo, mkate mdogo wa mviringo uliopikwa kwa mvuke, mchele, na nudo za mchele. Mungu ametoa aina hizi mbalimbali za nafaka kwa wanadamu kwa wingi. Kwa nini kuna aina nyingi sana? Makusudi ya Mungu yanaweza kupatikana humo: Kwa upande mmoja, ni kwa ajili ya kufaa aina mbalimbali za udongo na hali ya nchi kaskazini, kusini, mashariki, na magharibi; kwa upande mwingine, vijenzi na kadiri mbalimbali vya nafaka hizi vinakubaliana na vijenzi na kadiri mbalimbali vya mwili wa mwanadamu. Watu wanaweza tu kudumisha virutubishi na vijenzi mbalimbali vinavyohitajika kwa miili yao kwa kula nafaka hizi. Ingawa chakula cha kaskazini na chakula cha kusini ni tofauti, vina mifanano mingi kuliko tofauti. Vyakula hivi vyote vinaweza kuridhisha mahitaji ya kawaida ya mwili wa mwanadamu na vinaweza kudumisha kuendelea kuishi kwa kawaida kwa mwili wa mwanadamu. Hivyo, sababu ya aina zinazozalishwa katika maeneo mbalimbali kuwa nyingi mno ni kwamba mwili wa mwanadamu unahitaji kinachotolewa na vyakula hivyo. Wanahitaji kinachotolewa na vyakula mbalimbali vinavyokuzwa kutoka kwa udongo ili kudumisha kuendelea kuishi kwa kawaida kwa mwili wa mwanadamu na kutimiza maisha ya kawaida ya mwanadamu. Kwa ufupi, Mungu aliwafikiria sana wanadamu. Vyakula mbalimbali ambavyo Mungu aliwapa watu si vya kuchosha—ni vyenye maarifa mengi mno. Ikiwa watu wanataka kula nafaka wanaweza kula nafaka. Wengine huenda wakasema, "Sipendi kula nudo, ninataka kula mchele," na wanaweza kula mchele. Kuna aina nyingi za mchele—mchele mrefu, mchele mfupi, na yote inaweza kuridhisha ladha walizonazo watu. Kwa hiyo, watu wakila nafaka hizi—bora tu si wa kuchaguachagua kuhusu vyakula vyao—hawatakosa lishe na wanahakikishiwa kuishi kwa afya nzuri mpaka umri wa uzeeni. Hilo lilikuwa wazo la asili ambalo Mungu alikuwa nalo akilini Alipowapa wanadamu chakula. Mwili wa mwanadamu hauwezi kuishi bila vitu hivi—je, hiyo si kweli? Wanadamu hawawezi kutatua matatizo haya halisi, lakini Mungu alikuwa tayari ametayarisha na kulifikiria kabisa. Mungu alikuwa amewatayarishia wanadamu vitu zamani sana.
Mungu amempa mwanadamu zaidi ya vitu hivi tu—pia kuna mboga. Unapokula mchele, ikiwa mchele ndio kila kitu unachokula, huenda ukakosa lishe. Ikiwa kisha utakaranga kwa mafuta kidogo vyakula kadhaa kiasi kidogokidogo au uchanganye kachumbari ya kula na mlo huo, basi vitamini katika mboga hizo na kiasi kidogo cha vitu vya msingi au lishe zingine vitaweza kupeana mahitaji ya mwili wa mwanadamu kwa njia ya kawaida sana. Wakati watu hawali vyakula vikuu wanaweza pia kula matunda, sivyo? Wakati mwingine, watu wanapohitaji uowevu au lishe zingine au ladha tofauti, pia kuna mboga na matunda ya kuwapa vitu hivyo. Kwa vile udongo na hali ya nchi ya kaskazini, kusini, mashariki na magharibi ni tofauti, pia kuna aina mbalimbali za mboga na matunda. Kwa vile hali ya nchi ya kusini ni joto sana, matunda mengi na mboga ni vya aina ya kufanywa baridi vinavyoweza kusawazisha baridi na joto ndani ya miili ya watu wanapokula vitu hivyo. Kwa upande mwingine, kuna aina chache ya mboga na matunda kaskazini, lakini hata hivyo vinatosha kwa watu wa kaskazini kufurahia. Kwa hali yoyote, kwa sababu ya ustawi wa kijamii katika miaka ya hivi karibuni, kwa sababu ya kile kinachoitwa maendeleo ya kijamii, na vilevile maendeleo katika usafiri na mawasiliano vinavyounganisha kaskazini na kusini na mashariki na magharibi, watu walio kaskazini wanaweza pia kula matunda mengine, vitu vya sifa maalum vya mahali maalum au mboga kutoka kusini, hata katika mwaka mzima. Kwa njia hiyo, hata kama watu wanaweza kuridhisha hamu yao ya chakula na matamanio ya vitu vya mwili, miili yao bila kujua inapatwa na viwango mbalimbali vya madhara. Hii ni kwa sababu miongoni mwa vyakula ambavyo Mungu aliwatayarishia wanadamu, kuna vyakula na matunda na mboga vinavyofaa watu walio kusini, na vilevile vyakula na matunda na mboga vinavyofaa watu walio kaskazini. Yaani, ikiwa ulizaliwa kusini, kula vitu kutoka kusini kunakufaa wewe sana. Mungu alitayarisha vyakula hivi na matunda na mboga kwa sababu kusini ina hali ya nchi mahsusi. Kaskazini ina vyakula vinavyohitajika kwa miili ya watu walio kaskazini. Lakini kwa vile watu wana hamu ya chakula ya ulafi, wamefagiliwa bila kujua katika mkondo wa maendeleo ya kijamii, na kuwafanya kukiuka sheria hizi bila kujua. Ingawa watu wanahisi kwamba maisha yao sasa ni bora zaidi, maendeleo ya kijamii kama hayo huleta madhara ya kufichika kwa miili ya watu wengi zaidi. Hiki si kile ambacho Mungu anataka kuona na si kile ambacho Mungu alikusudia mwanzoni Alipoleta vitu vyote pamoja na vyakula hivi, matunda na mboga kwa wanadamu. Hii ilisababishwa na wanadamu kukiuka sheria ambazo Mungu aliweka.
Kuongezea, kile ambacho Mungu aliwapa wanadamu ni cha fahari na kingi, kila sehemu ikiwa na vitu maalum vya mahali maalum. Kwa mfano, sehemu nyingine zina utajiri wa tende nyekundu (zinazojulikana kwa kawaida kama jujubes), ilhali zingine zina utajiri wa jozi, karanga, au aina nyingine mbalimbali za njugu. Vitu hivi yakinifu vyote vinatoa lishe inayohitajika na mwili wa mwanadamu. Lakini Mungu huwapa wanadamu vitu kulingana na misimu na wakati, na pia anawapa kiasi sahihi kwa wakati sahihi. Wanadamu hutamani kujifurahisha kwa kimwili na ni walafi, hiyo inafanya kuwa rahisi kukiuka na kuharibu sheria za kawaida za ukuaji wa mwanadamu tangu Alipowaumba wanadamu. Kama mfano, hebu tutazame matunda ya cheri, ambazo kila mtu anapaswa kuzijua, sivyo? Hizo huvunwa karibu Juni. Kwa kawaida, hizo huisha kabla ya Agosti. Cheri huwa mbichi kwa miezi miwili pekee, lakini kupitia mbinu za kisayansi watu sasa wanaweza kurefusha muda huo mpaka miezi 12, hata mpaka msimu wa cheri wa mwaka unaofuata. Hiyo inamaanisha cheri zipo kwa mwaka mzima. Je, jambo hili ni la kawaida? (La.) Basi msimu bora zaidi wa kula cheri ni upi? Ni kipindi cha kuanzia Juni mpaka Agosti. Zaidi ya kikomo hiki, haijalishi utaziweka mbichi vipi, hazitakuwa na ladha sawa, wala sio kile ambacho mwili wa mwanadamu unahitaji. Mara tu tarehe ya kuisha kutumika inapopita, haijalishi ni vitu vipi vya kemikali unatumia, hutaweza kuzifanya ziwe kama zinavyokuwa wakati zinakuzwa kwa kawaida. Zaidi, madhara ambayo kemikali huleta kwa wanadamu ni kitu ambacho hakuna anayeweza kufanya chochote kuyaondoa au kuyabadilisha. Unaelewa, sivyo? Basi, ni nini ambacho soko la uchumi la wakati huu linawaletea watu? Maisha ya watu yanaonekana kuwa mazuri zaidi, usafiri katika pande zote umekuwa wa kufikika kwa urahisi sana, na watu wanaweza kula aina zote za matunda katika msimu wowote kati ya misimu minne ya mwaka. Watu wa kaskazini mara kwa mara huweza kula ndizi na chakula chochote, vitu maalum vya mahali maalum au matunda kutoka kusini. Lakini haya si maisha ambayo Mungu anataka kuwapa wanadamu. Soko hili la uchumi huleta manufaa fulani kwa maisha ya wanadamu lakini pia linaweza kuleta madhara. Kwa sababu ya wingi wa vyakula sokoni, watu wengi hula chochote, wao hula bika kufikiria. Jambo hili hukiuka sheria za asili na lina madhara kwa afya yao. Hivyo, soko la uchumi haliwezi kuletea watu furaha ya kweli. Unaelewa, sivyo? Hebu tazama. Si, zabibu huuzwa sokoni katika misimu yote minne ya mwaka? Zabibu kwa kweli huwa mbichi tu kwa muda wa kipindi kifupi sana baada ya kuchumwa. Ukiziweka mpaka Juni inayofuata, bado zinaweza kuitwa zabibu? Je, unaweza kuziita takataka? Hazitakosa tu vijenzi vya asili vya zabibu, lakini pia zina kemikali zaidi juu yake. Baada ya mwaka mmoja, hazijapoteza tu ubichi wake, lakini pia lishe zake zimepotea kitambo. Watu wanapokula zabibu, wanahisi: "Ninafurahi sana! Je, tungeweza kula zabibu wakati wa msimu huu miaka 30 iliyopita? Hungeweza kuzila hata kama ungetaka. Maisha ni mazuri jinsi gani wakati huu!" Je, hii ni furaha kweli? Ukipenda, unaweza kwenda kusoma juu ya zabibu zilizohifadhiwa kwa kemikali na uone hasa vijenzi vyake ni vipi na iwapo vijenzi hivi vinaweza kuleta manufaa yoyote kwa wanadamu. Katika Enzi ya Sheria. Waisraeli walipokuwa njiani baada ya kuondoka Misri, Mungu aliwapa kware na mana. Je, Mungu aliwaruhusu watu kuvihifadhi? (La.) Watu wengine walikuwa na fikira ndogo na waliogopa kwamba hakungekuwa na zaidi siku iliyofuata, hivyo walihifadhi nyingine. "Tuweke akiba iwapo tutahitaji baadaye!" Kisha nini kilifanyika? Kufikia siku iliyofuata ilikuwa imeoza. Mungu hakuwaruhusu kuweka nyingine kama akiba kwa sababu Mungu alikuwa amefanya matayarisho fulani, yaliyohakikisha hawangekufa kwa njaa. Wanadamu hawana hakika hiyo, wala hawana imani ya kweli kwa Mungu. Kila mara wanaweka nyengine kando kwa ajili ya baadaye na hawawezi kamwe kuona utunzi wote na mawazo yaliyo ndani ya kile ambacho Mungu amewatayarishia wanadamu. Kila mara hawawezi kuhisi hasa, kila mara wanakosa kumwamini Mungu, kila mara wanafikiria: "Matendo ya Mungu si ya kutegemewa! Nani anajua iwapo Mungu atawapa wanadamu au ni lini Atawapa! Ikiwa nina njaa sana na Mungu hanipi, basi si nitakufa njaa? Si nitakosa lishe?" Ona jinsi hakika ya mwanadamu ni ndogo sana!
Nafaka, matunda na mboga, na kila aina ya njugu vyote ni vyakula vya wala mboga. Hata kama ni vyakula vya wala mboga, vina lishe za kutosha kuridhisha mahitaji ya mwili wa mwanadamu. Kwa hali yoyote, Mungu hakusema: "Kuwapa wanadamu hiki kunatosha. Wanadamu wanaweza tu kula vitu hivi." Mungu hakuachia hapo na badala yake aliwatayarishia wanadamu vitu vyenye ladha nzuri zaidi. Vitu hivi ni gani? Ni aina mbalimbali ya nyama na samaki wengi wenu mnaweza kuona na kula kila siku. Kuna aina nyingi sana za nyama na samaki ambazo Mungu amemtayarishia mwanadamu. Samaki wote huishi majini; umbile asili la nyama yao ni tofauti na la nyama inayokuzwa juu ya ardhi na wanaweza kuwapa wanadamu lishe mbalimbali. Sifa za samaki zinaweza kubadilisha baridi na joto ndani ya mwili wa mwanadamu, kwa hiyo ni za manufaa makubwa sana kwa wanadamu. Lakini kilicho na ladha nzuri hakitakiwi kuliwa zaidi. Bado msemo ni huo huo: Mungu huwapa wanadamu kiasi sahihi kwa wakati sahihi, ili watu waweze kufurahia kwa kawaida na vizuri vitu hivi kulingana na msimu na wakati. Ndege wa kufugwa wanahusisha nini? Kuku, kware, njiwa, n.k. Watu wengi hula pia bata na bata bukini. Ingawa Mungu alifanya matayarisho, kwa watu waliochaguliwa na Mungu, bado Mungu aliwawekea masharti na alikuwa ameweka eneo fulani katika Enzi ya Sheria. Sasa eneo hili linatokana na kupendelea kwa mtu binafsi na ufahamu wa mtu binafsi. Aina hizi mbalimbali za nyama hupatia mwili wa mwanadamu lishe mbalimbali, zinazoweza kusheheneza protini na madini ya chuma, kusitawisha damu, kuimarisha misuli na mifupa, na kupeana nguvu zaidi. Haijalishi ni mbinu gani watu hutumia kupika na kula vitu hivyo, kwa ufupi, vitu hivi vinaweza kwa upande mmoja kuwasaidia watu kuendeleza ladha na hamu ya chakula, na kwa upande mwingine kuridhisha matumbo yao. Kitu cha muhimu zaidi ni kwamba zinaweza kupatia mwili wa mwanadamu mahitaji yao ya lishe ya kila siku. Hizi ndizo fikira ambazo Mungu alikuwa nazo Alipowatayarishia wanadamu chakula. Kuna vyakula vya wala mboga na pia nyama—je, hiyo si ya fahari na nyingi? Lakini watu wanapaswa kuelewa kusudi la asili la Mungu lilikuwa gani Mungu alipowatayarishia wanadamu vyakula vyote. Je, ilikuwa ni kuwaacha wanadamu wafurahie kwa ulafi vyakula hivi vya kimwili? Na je, watu wakijihusisha katika ridhaa hii ya kimwili? Je, hawapati lishe kupita kiasi? Je, lishe kupita kiasi haileti kila aina ya magonjwa kwa mwili wa mwanadamu? (Ndiyo.) Hiyo ndiyo maana Mungu hutoa kiasi sahihi kwa wakati sahihi na kuwaacha watu wafurahie vyakula mbalimbali kulingana na vipindi vya wakati na misimu. Kwa mfano, baada ya kuishi katika majira ya joto sana, watu watakusanya kiasi fulani cha joto, la kusababisha ukavu wa viini na unyevunyevu katika miili yao. Majira ya kupukutika kwa majani yakija, matunda ya aina nyingi sana yataiva, na watu watakapokula baadhi ya matunda unyevunyevu wao utaondolewa. Wakati huo huo, ng’ombe na kondoo watakuwa wamekua na kupata nguvu, ili watu wale nyama kiasi kama lishe. Baada ya kula aina mbalimbali za nyama, miili ya watu itakuwa na nguvu na joto la kuisaidia kustahimili baridi ya majira ya baridi, na kutokana na hayo wataweza kupita katika majira ya baridi kwa amani. Wakati upi wa kutayarisha vitu vipi kwa ajili ya wanadamu, na wakati upi wa kuacha vitu vipi vikue, vizae matunda na kuiva—yote haya yanadhibitiwa na kupangwa na Mungu kwa kupimwa kabisa. Hii ni mada kuhusu "jinsi Mungu alitayarisha chakula kilicho muhimu kwa maisha ya mwanadamu ya kila siku." Mbali na aina zote za chakula, Mungu pia huwapa wanadamu vyanzo vya maji. Watu huhitaji kunywa maji kiasi baada ya kula. Je, kula matunda tu kunatosha? Watu hawataweza kustahimili kula matunda pekee, licha ya hayo, huwa hakuna matunda katika misimu mingine. Hivyo tatizo la wanadamu la maji litawezaje kutatuliwa? Kwa Mungu kutayarisha vyanzo vingi vya maji juu ya ardhi na chini ya ardhi, ikiwemo maziwa, mito, na chemchemi. Vyanzo hivi vya maji vinaweza kunywewa maji katika hali ambazo hakuna kuchafuliwa kokote, au maendeleo ya wanadamu au uharibifu. Yaani, kuhusu vyanzo vya chakula kwa maisha ya miili ya wanadamu, Mungu amefanya matayarisho sahihi sana, yasiyo na hitilafu yoyote na ya kufaa sana, ili maisha ya watu yawe ya fahari na yenye wingi na yasiyokosa chochote. Hiki ni kitu ambacho watu wanaweza kuhisi na kuona.
Kuongezea, miongoni mwa vitu vyote, iwe ni wanyama, mimea, au kila aina ya nyasi, Mungu aliumba pia baadhi ya mimea ambayo ni muhimu kwa kutatua madhara au magonjwa kwa mwili wa mwanadamu. Utafanya nini, kwa mfano, ukichomeka? Je, unaweza kuosha kwa maji? Je, unaweza kutafuta kitambaa na kufunika mahali hapo? Huenda pakajaa usaha au kuambukizwa kwa njia hiyo. Utafanya nini, kwa mfano, ukiungua kwa bahati na moto au na maji moto? Unaweza kumimina maji juu yake? Kwa mfano, ukipata homa, upate mafua, upate majeraha kutokana na kazi ya viungo, maradhi ya tumbo kutokana na kula kitu kibaya, au kupata magonjwa fulani kwa sababu ya mienendo ya maisha au masuala ya hisia, kama vile magonjwa ya mishipa ya damu, hali za kisaikolojia au magonjwa ya ogani zilizo ndani ya mwili—kuna mimea inayolingana ya kutibu haya yote. Kuna mimea inayoendeleza mzunguko wa damu kuondoa ukwamaji, kutuliza maumivu, kukomesha kutokwa na damu, kutia ganzi, kuwasaidia watu kupata tena ngozi ya kawaida, kuondoa ukwamaji wa damu mwilini, na kuondoa sumu mwilini. Kwa ufupi, yote inaweza kutumiwa katika maisha ya kila siku. Ni ya kufaa watu na imetayarishwa na Mungu kwa ajili ya mwili wa mwanadamu iwapo inahitajika. Baadhi ya hiyo iliruhusiwa na Mungu kugunduliwa bila uangalifu na mwanadamu, ilhali mingine iligunduliwa kutoka kwa vitu fulani maalum au na watu fulani waliotayarishwa na Mungu. Baada ya ugunduzi wao, wanadamu wangeipitisha kwa wengine, na halafu watu wengi wangejua kuihusu. Kwa njia hii, uumbaji wa Mungu wa mimea hii unakuwa na thamani na maana. Kwa ufupi, vitu hivi vyote vinatoka kwa Mungu na vilitayarishwa na kupandwa Alipowaumbia wanadamu mazingira ya kuishi. Vitu hivi vyote ni muhimu sana. Je, fikira Zake Mungu zilifikiriwa vizuri sana kuliko za wanadamu? Unapoona yote ambayo Mungu amefanya, unaweza kuhisi upande wa Mungu wa vitendo? Mungu alifanya kazi katika siri. Kabla ya mwanadamu kuingia katika ulimwengu huu, kabla ya kukutana na wanadamu hawa, Mungu alikuwa tayari ameviumba vitu hivi vyote. Kila kitu alichofanya kilikuwa kwa ajili ya wanadamu, kwa ajili ya kuendelea kuishi kwao, na kwa ajili ya kufikiria juu ya kuwepo kwa wanadamu, ili wanadamu waweze kuishi kwa furaha katika ulimwengu huu yakinifu wa ufahari na wingi ambao Mungu aliwatayarishia, bila kuwa na wasiwasi kuhusu chakula au nguo, na bila kukosa chochote. Wanadamu wanaendelea kuzaa na kuendelea kuishi katika mazingira hayo.
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu
Yaliyopendekezwa: APP ya Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni